Mafunzo CCP mhhh

Ngwini nadhani sasa umeelewa,habari ndio kwahiyo serikali haitoi tena pesa ya kujikimu?
ndugu yangu,au mnataka nikwambie nina m2 ambae ni recruits? Mimi mwenyewe nimefanya auditing ya mapato na ma2mizi ya polisi kwa mwaka wa fedha 2009/2010,so nina uhakika.
 
Sita inatosha mkuu, tatizo ni kuwa wanapopangiwa vituo vya kazi hawa jamaa wanasahaulika kabisa mpaka wanachaka nje ndani, hakuna refresher kozi wala upgrade! Hivyo anabaki kukariri yale aliyojifunza miaka nenda rudi. Kuwe na utaratibu wa ku -upgrade ili wawe conversant na mambo mapya yanayolikabili jeshi....Kingine kujuana kwingi ndani ya polisi, hupandishwi cheo mpaka kamishna ahongwe,,,na mpaka hongo imfikie kuna watu kibao hapo kati> sasa unategemea nini kama sio kukata tamaa na kuwa na hasira na waandamanaji wanaoandamana kwa amani kudai haki hata kama ni haki ya kumtetea askali mwenyewe!.
 
Mmh! Kumbe mume wangu alinidanganya mshahara wake, leo ndo leo atanieleza nyingine huwa anapeleka wapi
 
Muda huo unatosha sana kwa watu wenye mipango na uelewa mzuri. Tatizo la TZ, wengi wa wanaoenda kwenye mafunzo hayo hawana sifa zinazotakiwa na ndiyo maana tunaona kama muda hautoshi.
 
Kimsingi askari wengi waliopitia mafunzo wa hiyo miezi sita, hawana uelewa wa kutosha juu ya taaluma yao. Muda wa miezi sita ni mfupi sana kitu cha maana pale ni shotokulia vinginevyo ni utata mtupu. Fikiria askari wa mafunzo ya miezi sita kesho ndiyo trafiki, au kitengo cha upelelezi. Nafikiri hawa viongozi wa Jeshi la Polisi waliangalie jambo hili kwa kina maana inawezekana huu ni mzaha katika masuala nyeti na muhimu.

Ni kama wale waalimu wa miezi mi4.Then udaktari utakuwa mwaka1,sheria miezi6 nk.
 
Ni kama wale waalimu wa miezi mi4.Then udaktari utakuwa mwaka1,sheria miezi6 nk.
Arnold...hao matraffic wanashindwa uelewa hata na nadereva wa VETA na NIT...kwanza wengi hawajui hata clutch ipo wapi na alama za barabarani ni kama kichina kwao
 
Mafunzo ya miezi sita mpaka saba yanatosha. Nadhani hawa mabwana tokea recruit anaingia kuna programe ambayo imeandaliwa kiutalaamu. Miezi ya awali itakuwa ni kuwasltoa uraia, yaani ukakamavu baadae kidato kinaanza kama kawa. Mitaala ni lazima itakuwa inabadilika kulingana na wakati mfani sidhani kama maafande wa dep miaka ya 80 -90 kama walikuwa wanajivunza somo la haki za binadamu lakini siku hizi ni tumaini langu mtaala huo utakuwa umejumuishwa katika mafunzo yao ili kuweza kukidhi wakati na mambo mengine.
Mwisho kama utahitajika kwenda mafunzo ya ziada nionavyo ni lazima kuwe na refresh kozi mf. Traffic huwa kuna refresh kozi kwa ajili ya kuwaweka sawa hawa mabwana wasiliaibishe jeshi. Ni kama sisi tu mkuu unaweza kila siku kupewa mahubiri lakini mwisho wa siku ukafanya madudu. Mtazamo wangu muda huo ni muafaka kwani hakuna la ajabu sana katika nchi yetu ambalo litahitaji kuwaweka watu kwa muda huo.
Sio kweli mkubwa, hakuna cha kozi maalum wala nn hawa wanacheza kwata kisha darasani miezi sita wamemaliza, matrafiki nawaona wanateuliwa tu na kutolewa hakuna kozi wala mafunzo. Kama unabisha nitakupa ushahidi ukiuhitaji, polisi hovyo.
 
Arnold...hao matraffic wanashindwa uelewa hata na nadereva wa VETA na NIT...kwanza wengi hawajui hata clutch ipo wapi na alama za barabarani ni kama kichina kwao
Ni kweli matrafiki wengi hawajui kuendesha hata pikipiki sijui hii imekaaje
 
Sio kweli mkubwa, hakuna cha kozi maalum wala nn hawa wanacheza kwata kisha darasani miezi sita wamemaliza, matrafiki nawaona wanateuliwa tu na kutolewa hakuna kozi wala mafunzo. Kama unabisha nitakupa ushahidi ukiuhitaji, polisi hovyo.

tafadhali naomba prrof ya usemayo!
kila askari anayeteuliwa traffic anaenda mafunzo ya trafic either zenji ama ccp moshi...inapotokea ukakuta askari ambaye hajaenda mafuno hayo na anafanya kazi hiyo, mostly ni emergency case na whenever course hiyo itakapotangazwa ataenda...idadi ya askari ni ndogo kuliko mhitaji....
ongea FACTS sio ushabiki!!!!
 
Wadau naomba mchango wenu ..
Je muda wanaoutumia kutoa mafunzo ya askari polisi kwa miezi sita pale CCP unatosha?
-Lini utajifunza uraia na human rights
-Lini utajifunza Law
-Lini utajifunza ukakamavu
-lini utajifunza mbinu na medani za kijeshi za kukabiliana na adui na uhalifu?
-Lini unachunguzwa kama ukikabidhiwa silaha hutaleta nayo madhara?
-Kubwa zaidi ni lini utaenda field kupractise kazi yako before employment? au kujiunga CCP ni already employed
Nakumbuka walioenda National Service kwa mujibu wa Sheria ilikuwa mwaka mzima solid sasa hii ya polisi mhhhh
Hebu tuichambue hii kama ina tija!

Kungekuwa na muda wa kuwachambua namna hiyo tusingekuwa na mbunge kichaa tangu kuzaliwa kama Lusinde
 
tafadhali naomba prrof ya usemayo!
kila askari anayeteuliwa traffic anaenda mafunzo ya trafic either zenji ama ccp moshi...inapotokea ukakuta askari ambaye hajaenda mafuno hayo na anafanya kazi hiyo,
mostly ni emergency case na whenever course hiyo itakapotangazwa ataenda...idadi ya askari ni ndogo kuliko mhitaji....
ongea FACTS sio ushabiki!!!!
tunawajua waliokuwa sio traffic wakaloby na kuvishwa magawanda meupe bila kozi yoyote
 
Sita inatosha mkuu, tatizo ni kuwa wanapopangiwa vituo vya kazi hawa jamaa wanasahaulika kabisa mpaka wanachaka nje ndani, hakuna refresher kozi wala upgrade! Hivyo anabaki kukariri yale aliyojifunza miaka nenda rudi. Kuwe na utaratibu wa ku -upgrade ili wawe conversant na mambo mapya yanayolikabili jeshi....Kingine kujuana kwingi ndani ya polisi, hupandishwi cheo mpaka kamishna ahongwe,,,na mpaka hongo imfikie kuna watu kibao hapo kati> sasa unategemea nini kama sio kukata tamaa na kuwa na hasira na waandamanaji wanaoandamana kwa amani kudai haki hata kama ni haki ya kumtetea askali mwenyewe!.

Hapa unasema uongo, polisi huenda kozi mara kwa mara, na kila baada ya miaka 3 wanaenda kozi ili kupandishwa cheo. Polisi wapya hukaa chini ya uangalizi maalum kwa miaka miwili huku wakilala katika kambi maalum na kupewa mafunzo kama vile wako chuoni. Nadhani narturing yao ni nzuri tatizo ni anaye wa-nurture anauelewa wa aina gani.
 
Miezi miwili ya mwanzo ni kujifunza masomo ya darasani na ukakamavu.then miezi miwili inayofuata wanapelekwa porini kujifunza medani za kivita,miezi miwili ya mwisho wanapelekwa field.ukiangalia kwa makini,huo muda unatosha kabisa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom