Mafundi ni wasumbufu, ila hawa wa cherehani wamezidi!!

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,983
12,701
Ni mwezi wa tano sasa suti yangu haijakamilika, njoo kesho au wiki ijayo ndio jibu nililokuwa napewa kila nikimuona. Ilibidi niazime suti ya kaka wakati wa sherehe iliyokusudiwa niivae hiyo suti. Leo nimeenda kudai kitambaa changu na pesa yangu, nimepigwa na mshangao baada ya kuambiwa na msaidizi wa fundi kuwa suti ilikamilika muda mrefu, lakini ikauzwa..
 
umenikumbusha wimbo wa marijani Rajabu na Dar internatinal...... Dunia ya sasa imekwisha
hebu soma ubeti huu........

Fundi cherehani kaletewa kitambaa, mwenyewe ataka suruali 3
fundi akajibu ewala vimefika, kumbe mfukoni fundi kachacha
vitambaa kauza na pesa katia ndani, wiki iliyofuata mwenyewe afika
anauliza fundi wapi suruali zangu, fundi analia ooooohhhhhh
anaulizwa fundi walia nini, eeti anajibu oooohhhh vimeibiwa.

Pole mkuu katavi........ utapiga mguu hapo bila mafanikio labda umshitaki kama unauthibitisho
 
Asikwambie mtu kaka, mafundi wote waongo, matapeli utadhani walinyonyeshwa na mama mmoja! Si wa cherehani tu! Seremala, redio, simu wote wizi mtupu! Wananikera hao...!
 
Wanakera kwa kweli hawa mafundi...
 
Katavi umenikumbusha mbali sana, wasambaa wa pale mwenge kiboko!!

siku hizi mie na mchina tu!
 
Umenikumbusha kisa cha kweli cha marafiki wawili wakubwa, ambao wote walikuwa wanaishi shamba kila mmoja na kijiji chake na wanafanya kazi mjini. Mmoja alikuwa kinyozi, mwengine mshoni. Ilikuwa hivi:

Kinyozi alipeleka vitambaa kwa ajili ya nguo za siku kuu za watoto wake wawili, tangu mwezi wa kumi lakini mpaka siku ya tarehe 29 R'dhan, nguo zilikuwa bado.
"Wewe njoo kesho hata kama ni siku kuu zitakuwa tayari".
Na kweli siku ilofuata ilikuwa siku kuu, na kweli fundi alikuwepo. Alipofika akamkabidhi nguo za wanawe, na kwa kuaminiana kwao, wala kinyozi hakujishughulisha kufungua na kuangalia. Alipofika nyumbani, kumbe mzigo ule aliompa ulikuwa na vitambaa hata havijakatwa vya mtu mwengine. Ikambidi arejee mjini.

Huku nyuma, mshoni kwa kuwa alifanya vile kusudi ili kupata muda zaidi, mara tu alipoondoka rafiki yake, akatoa vitambaa, akaanza kushona, na chini ya saa moja nguo zikawa tayari. Kinyozi aliporejea, akiwa kahamaki kama mbogo, akamrushia vitambaa na kumwambia, "Najua nguo za wanangu hujazishona, lakini leo nitahakikisha unalala hospitali kwa kipigo nitachokupiga".

Samahani rafiki, si unajua tena, nilisahau nikakufungia nilichokufungia, ulipoondika ndio nikagundua kosa langu. Nguo zako ziko tayari. Siku kuu njema na watoto".
 
Katavi umenikumbusha mbali sana, wasambaa wa pale mwenge kiboko!! siku hizi mie na mchina tu!
heri yako maana mimi mchina lazima nitamrekebisha maana na uzee huu siwezi kuvaa ile style ya vijana-kata k, nijiishia kwenye jeans za mitumba tu. Kutukanana na mafundi wa kushona nilishachoka, na siwaamini kabisa! wengine i wa ujenzi anaweza akashika site tatu au nne kwa wakati mmoja kila wiki angalau siku tatu-nne antakwambia anaumwa, mara msiba yaani shida tupu.
 
dawa ya mafundi ni polisi tu, anawekwa ndani siku kazaa akitoka unamrudisha tena
 
umenikumbusha wimbo wa marijani Rajabu na Dar internatinal...... Dunia ya sasa imekwisha
hebu soma ubeti huu........

Fundi cherehani kaletewa kitambaa, mwenyewe ataka suruali 3
fundi akajibu ewala vimefika, kumbe mfukoni fundi kachacha
vitambaa kauza na pesa katia ndani, wiki iliyofuata mwenyewe afika
anauliza fundi wapi suruali zangu, fundi analia ooooohhhhhh
anaulizwa fundi walia nini, eeti anajibu oooohhhh vimeibiwa.

Pole mkuu katavi........ utapiga mguu hapo bila mafanikio labda umshitaki kama unauthibitisho

Nafikiria kumpeleka polisi.......!!!
 
Umenikumbusha kisa cha kweli cha marafiki wawili wakubwa, ambao wote walikuwa wanaishi shamba kila mmoja na kijiji chake na wanafanya kazi mjini. Mmoja alikuwa kinyozi, mwengine mshoni. Ilikuwa hivi:

Kinyozi alipeleka vitambaa kwa ajili ya nguo za siku kuu za watoto wake wawili, tangu mwezi wa kumi lakini mpaka siku ya tarehe 29 R'dhan, nguo zilikuwa bado.
"Wewe njoo kesho hata kama ni siku kuu zitakuwa tayari".
Na kweli siku ilofuata ilikuwa siku kuu, na kweli fundi alikuwepo. Alipofika akamkabidhi nguo za wanawe, na kwa kuaminiana kwao, wala kinyozi hakujishughulisha kufungua na kuangalia. Alipofika nyumbani, kumbe mzigo ule aliompa ulikuwa na vitambaa hata havijakatwa vya mtu mwengine. Ikambidi arejee mjini.

Huku nyuma, mshoni kwa kuwa alifanya vile kusudi ili kupata muda zaidi, mara tu alipoondoka rafiki yake, akatoa vitambaa, akaanza kushona, na chini ya saa moja nguo zikawa tayari. Kinyozi aliporejea, akiwa kahamaki kama mbogo, akamrushia vitambaa na kumwambia, "Najua nguo za wanangu hujazishona, lakini leo nitahakikisha unalala hospitali kwa kipigo nitachokupiga".

Samahani rafiki, si unajua tena, nilisahau nikakufungia nilichokufungia, ulipoondika ndio nikagundua kosa langu. Nguo zako ziko tayari. Siku kuu njema na watoto".
Ahahahaaah!!! Hii nayo kali...
 
heri yako maana mimi mchina lazima nitamrekebisha maana na uzee huu siwezi kuvaa ile style ya vijana-kata k, nijiishia kwenye jeans za mitumba tu. Kutukanana na mafundi wa kushona nilishachoka, na siwaamini kabisa! wengine i wa ujenzi anaweza akashika site tatu au nne kwa wakati mmoja kila wiki angalau siku tatu-nne antakwambia anaumwa, mara msiba yaani shida tupu.

Utingo umenikumbusha jamaa yangu aliyegombana na fundi mjenzi baada ya kumkuta anafanya kazi kwa mtu mwingi wakati alisma amekwenda hospitali kwa matibabu. mbaya zaidi pesa za matibabu alito jamaa yangu. Kaaaaazi kweli kweli
 
Ahahahaaah!!! Hii nayo kali...
Hiki kisa alinisimulia mtendwa - kinyozi - kwa bahati tu kwani nilikuwa na ninatafuta fundi cherahani. Nilipomtaja huyu ndipo kinyozi akanisimulia kisa kilichomfika yeye. Lakini alikuwa hajui bao la kisigino alilopigwa na rafiki yake.
 
Utingo umenikumbusha jamaa yangu aliyegombana na fundi mjenzi baada ya kumkuta anafanya kazi kwa mtu mwingi wakati alisma amekwenda hospitali kwa matibabu. mbaya zaidi pesa za matibabu alito jamaa yangu. Kaaaaazi kweli kweli

Visa vya mafundi haviishi. Mimi fundi mjenzi alikuja nyumbani asubuhi sana kiasi nilishangaa. aliweka mkoba wake wa zana akaaga anarudi nyumbani kunywa chai. Mpaka saa 3 hakutokea. Nikaamua kwenda sokoni kununua samaki. Huwezi kuamini, njiani nilikutana naye akiwa amepandia baiskeli yake na mkoba mwengine wa zana anaelekea kufanyakazi kwengine. Nilimzuwia na kumrudisha nyumbani.

Ndipo nilipoamini kuwa mafundi wajenzi wanaweza kuwa na mikoba mpka minne ya zana. Anakuja kukuwekea mkoba, kumbe anaenda kufanyakazi kwengie.
 
Mimi suti zangu huwa nashonea pale Magomeni Mapipa karibu na stendi ya daladala za kuelekea mjini kuna Waha wawili ni mafundi hasa na sijawahi kucheleweshewa suti yangu wala kutapeliwa hata mara moja.
 
Kaa na haohao, siku ukihama tu utajuta!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom