Mafisadi Watumia Weapons of Mass Destruction

Arafat

JF-Expert Member
Nov 17, 2009
2,581
758
Kuna wakati tulikwisha sema ya CCM na mafisadi wake lazima watatumia mbinu za kivita kuishambulia CDM na wanachama wake ilimradi kujiami, kama nilivyo bashiri awali kwamba uenda wakatumia Weapons of Mass destructive, yaani silaha ya kungamiza Jamii kwa ujumla, ndivyo walivyo fanya bila kujali hiyo silaha itammaliza nani na kumbakisha nani; silaha kama hizo alikuwa nazo Mzee Saadam Hussein zikisimamiwa na Chemical ALLY, mara nyingi ni silaha za chemikali au Atomiki ni silaha kama iliyopigwa Hiroshima Japan; Mafisadi wa CCM wametumia sehemu ya Mgawo wao wa Malipo ya DOWANS (Kumbukeni kuwa wanauhakika wa kupata hizo fedha kwahiyo wanaweza kufanya overdraft payments) kuwanunu Mashekh na kulete hoja tata katika jamii, kuwa kuwapinga Mafisadi ni kupingana na Dini ya Kiislam! Hii ni silaha hatari sana wametumia, kazi kwenu CDM, kaeni chini mtafakari kabla ya kuanza hatua nyingine.

Ushauri

Nashauri mara moja ianzishwe Operation sambaratisha Mafisadi, CDM wajitolee kuongoza Jamii katika Operation hiyo yafanyike Mambo yafuatayo

Zifanyike Midaharo kumi (10) Dar es Salaam yenye kichwa cha habari "Je Tanzania Kuna Udini?" au "Je Mafisadi wana dini" au "Mafisadi hawana Dini, dini yao ni Ufisadi wao, nasi dini yetu Umaskini wetu" au title yoyote inayofaha kuunganisha Jamii nzima kujadili na kuchangia maada kwa pamoja, midahalo mitatu ifanyike Mwaka huu (2011), Mitatu 2012, Mitatu 2013 na mmoja 2014 .
CDM wafanye Operation Sambaza Mafisadi katika mikutano mikubwa Saba kila Mwaka, Mikutano hiyo itumike kuelimisha jamii juu ya kuungana dhidi ya mafisadi bila kujali Fisadi ni rangi yako, dini yako, wala kabila lako; maana madhara yake hayachagui dini, kabila wala rangi. Mikutano hiyo ifanyike Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Singida, Tabora na Zanzibar.
Wabunge vijana wa CDM waelekeze nguvu kufungua Matawi ya Chama Zanzibar kwa wingi kwa kutumia nafasi yao ya Ujana na Mtandawo wa Vijana wenzao waliosoma nao kutoka Zanzibar
Dr. Slaa aombe kukuta na Mashekh wa Dar es Salaam katika mikutano ya ndani na kuwaeleza umuhimu wa kuunganisha nguvu na sala za watanzani bila kujali dini, kabila wala rangi dhidi ya kidhuluma kwa maana madhara ya dhuluma hayachagui rangi ya mtu, kabila lake wala dini yake; Laila Odinga alifanya vikao kadhaa na Wazee Kislaam wa Lamu na Mombasa na ndio kisa cha Balala Kujiunga na ODM, hii ilikuwa mara baada ya Kibaki kutangaza kuwa anasera ya kufuta sheria ya Ugaidi ili ku-win kura za waislaam, inasema katika vikao hivyo pamoja na mambo mengine Laila alikuwa anawaelezea wazee hao kuwa Sheria hiyo ilitungwa na Serikali ya Kibaki iweje leo iwe agenda ya kuombea kura! Au aliitunga kwasababu hiyo, aliwakumbusha wazee hao kuwa shida haina dini wala kabila.
CDM-CC ikutane kuangalia way-forward, itayarishwe mpango kabambe wa mkakati wa kuunganisha Jamii katika wakati huu tunapo taka kujikomboa.
 
Back
Top Bottom