Mafisadi watashinda! - A somber look

1. au tujiunge humo humo na kula nao "sahani moja".

2. Huko tunakokwenda neutrality is not an option!

3. Je tujiunge nao ili tuwabomoe kutoka "ndani"?[/QUOTE]

- Kwa maoni yangu haya matatu ndio solution, kama kweli unaielewa vizuri sana reality ya mazingira ya siasa yetu ya bongo sasa hivi, uwezekano wa kubadilishwa katiba ni very slim na bila katiba kubadilika mabadiliko ya jumla ni ndoto ya muda mrefu sana, bado tunasumbuliwa na ukabila, udini, undugu, kujuana, ndio maana ukimtoa Lowassa u-PM, bado atapokewa kishujaa jimboni kwake,

- Juzi nilikuwa naongea na kiongozi mmoja wa juu kutoka jimbo la Chenge, yaani mpaka unatamani kulia machozi ambavyo haelewi what is wrong with Chenge kwamba anaandamwa sana bila sababu! Sasa hebu mwambie Shukuru Kawambwa na Said Mwema kwamba Muungwana hafai, sijui itakuwaje, Tanzania tuna mengi sana ya ku-overcome kabla ya kufikia ufisadi, maana ni lazima uvuke haya ya udini, ukabila na kujuana ndio uweze kutokomeza ufisadi na mafisadi,

- Siku hizi bongo imezuka EPA mpya, nayo ni safari za nje zisizokwisha kwa viongozi na maofisa wa serikali, wakiongozwa na Muungwana mwenyewe, I mean this EPA is worse kuliko hata EPA yenyewe, leave alone ufisadi ndugu zangu tuna safari ndefu sana, dawa kwa maoni yangu ni kama principle ya kina Bush's Family, kutafuta hela kwanza and then kuingia siasa ukiwa huna njaa na kuwabadilikia humo humo ndani! Kkubali ukweli sio kushindwa ila ni kujipa nafasi ya kujipanga upya ili ushinde next time, kumbuka it is not how you fall, ila umeangukia wapi!

Otherwise, Mkulu MMJ you nailed it!

Respect.

FMES!
 
Hatimaye nimefikia hitimisho kuwa juhudi za kupambana na ufisadi nchini hazitofanikiwa na ya kuwa upepo wa ushindi unavuma kuelekeza merikebu za mafisadi kuelekea ushindi! Zaidi ya watu kulalamika pembeni na kuonesha kuchukizwa na ufisadi, himaya ya ufisadi itazidi kujikita na kupenya katika vyombo vingi zaidi kwani sasa hivi dalili zote zinaonesha ufisadi haufanywi na mtu mmoja bali umekuwa ni mtandao wa uhalifu ambao umeundwa na wasomi, wanasiasa, wafanyabiashara na watu wenye ushawishi mkubwa kwenye jamii.

Mwanzoni ilipotajwa kuwa ni Tanzanian Mafia nilidhani ni hyperbole lakini wiki hizi chache zilizopita na taarifa ambazo ninazipata hasa baada ya kuanza kuandika suala hili ni wazi kuwa ipo "familia ya kihalifu" ambayo imejipanga vilivyo na iko tayari kutumia nguvu zao zote kuzima juhudi zozote zile za kunyofoa meno yao kwenye migongo ya Watanzania.

Sitoshangaa joto linavyozidi kupanda waandishi mahiri wa uchunguzi wakajikuta wanashambuliwa na kitakachoelezewa kuwa ni "majambazi" na kwa mwendo huo kuleta hofu kubwa kwa waandishi na kuwalazimisha waoga kati yao kunywea na kuchukua upande wa familia hiyo.

Kama vile Jitu Kubwa linavyoshika kwa kuminya mkono wa mtoto mdogo na kumburuza ndivyo ufisadi utakavyoendelea kuburuza taifa na Watanzania wengi. Lengo kubwa ni kuhakikisha kuwa watawala wenye uwezo wa kifisadi wataendelea kutawala tena bila kuulizwa. Ufisadi utakaofunuliwa baadaye mwaka huu yawezekana ukawa ndiyo msumari wa mwisho kabisa utakaowafanya mafisadi kuja na silaha zao zote kuhakikisha Taifa zima linapiga magoti na kwa sauti kali kama ya wale nyani wa kwenye filamu ya Planet of the Apes watapiga ukelele "Bow"!

Kuelekea uchaguzi mkuu mwakani himaya hiyo imepanga sasa watu wapya kabisa kuanza kuingia katika safu za uongozi na hasa Bungeni ili hatimaye usalama wao uzidi kuhakikishwa. Kiwango kikubwa cha fedha kimeshatengwa kuhakikisha (na hili limeshasemwa na wengine) wabunge wote ambao wanapigia kelele ufisadi wanaaungushwa kwenye kura za maoni na watu wapya kuingia. Lengo la hilo ni kuhakikisha kuwa inapofika Bunge jipya ule upinzani ambao umekuwa ukisikika utakuwa umezimwa kwa kiasi cha kutosha na ukabakia kuwa ni upinzani wa magazetini.

Juhudi kubwa ya kujipanga huko sasa hivi ni kuelekea pia katika Mahakama za juu kitu ambacho kinafanywa kwa uangalifu mkubwa na tahadhari. Kwa macho ya uchunguzi tuangalie sana teuzi zinazokuja za Mahakama na kuzielewa vizuri.

Vyovyote vile ilivyo, naomba niwakatishe matumaini kabisa kuwa kufikiria kuwa "vita ya ufisadi ambayo bado inaendelea" kwa mujibu wa Mkuchika ni vita ambayo mafisadi watashinda. Watashinda kwa sababu kubwa tano.

a. Wamejipanga vizuri zaidi kuliko wanaopinga ufisadi (well organized). Wanaopinga ufisadi they are a fragmented bunch!

b. Wamewekeza fedha pale wanapokula na hawaoni haya kufanya hivyo (well funded). Wanaopinga ufisadi wanatumia maneno tu, wenye kuwekeza fedha wanaonekana wanataka kujitajirisha na wale ambao wanatumia fedha zao kupigana na ufisadi na wenyewe wanageuziwa kibano alimradi kuvuruga juhudi zao. Mtu mmoja (ambaye sistahili kufunga kamba za viatu vyake) ameniambia kwenye sakata hili la RA na RM nisichague upande kwa sababu nitaonekana nampendelea mmoja wao!

Yaani, mtu asichague upande kwa kuogopa kuonekana yuko upande mmoja. Ushauri wangu ni kuwa upande niliopo sihami, mtu anayetaka abadili yeye upande aje upande wangu, na ukija upande wangu wewe mwenzangu, ukiwa kinyume changu najua upande wako, neutrality is the position of the weak and the coward, I'm neither weak nor a coward!

Nawapongeza wale waliochagua upande mmoja kati ya hizi!

c. Wamejikita vizuri na kuwabana watawala na vyombo mbalimbali na hivyo kama utando wa buibui wanajua na wanaweza kujua chochote wanachotaka kujua (well connected). Wanaopinga ufisadi wachache walioko serikalini au madarakani wanafanya hivyo at their own risk hakuna wa kuwakinga na muda si mrefu wataanza kupukuchwa kama hindi.

d. Wanaogopesha; wanatumia serikali na vyombo vyake kuingiza hofu kwa watu wa kawaida kwa kauli za "kuvunjika kwa amani", "watachukuliwa hatua za kisheria", n.k (they command fear). Wanaopinga ufisadi bado hawajaanza kuleta itikadi ya matumaini na badala yake wamejikita na kupiga kambi kwenye mazungumzo ya ufisadi na kauli za dhidi ya CCM ambazo ni sawa (kwa maoni yangu) na mtu kuupuliza mbuyu, likianguka buyu moja anafikiri ni kwa sababu yake!!

e. Wako tayari kwenda umbali wowote ule kuhakikisha hawaondoki madarakani au mirija yao kukatwa (ready to sacrifice). Katika hili watawatoa sadaka wenzao wachache ili kutuliza munkari wa jamii lakini wakati huo huo wakiwapanga wengine.

Ninachosema kwa maneno mawili ni kuwa 'we are screwed!" (najua ni matatu!) hakuna matumaini, hakuna njia ya kutokea, na hakuna mashujaa wetu wa kutuongoza vitani. Tufike mahali aidha tusalimu amri, au tujiunge humo humo na kula nao "sahani moja". Tufike mahali aidha tuendelee kupiga kelele kwenye mtandao na kuibua mambo kadha wa kadha au tukubaliane kujiunga nao.

Huko tunakokwenda neutrality is not an option! Ni waoga na wasio na msimamo ndio watajifanya kuwa neutral wengine wetu itabidi tuchague upande au tukae kimya na kusubiri upande unaoshinda! aidha tuko kinyume na familia na himaya hii ya ufisadi (kwa vitendo siyo mawazo) au tuko sehemu ya familia hii na sisi tukipata nafasi tutakuwa hivyo hivyo!

Je kuna matumaini? Je, tuwaachie nchi kwani nasibu iko kinyume yetu? Je tukubali yaishe ili tuendelee kuzungumzia mambo mengine ya maendeleo? Je, Je tuwaachie nchi watawale wapendavyo!? Je tujiunga nao ili tuwabomoe kutoka "ndani"?
analysis nzuri !

Hata hivyo sina uhakika ni ushindi/mafanikio gani ambao ulitegemea hivi karibuni. Nadhani ni mapema mno tena sana, na hawa watu ili kuangushwa haitotokea ndani ya usiku mmoja, lakini ninachoweza kusema kazi ya kuufumua huu mtandano wa wahalifu imeshaanza lakini itachukua muda kuufumua wote. Akina zitto na dr slaa naweza kusema wamefanya waliyosema na kipande kilichobaki sasa ni kwetu sote.

Iwapo tunaamini elimu ( yaani ni uraia ) nayo itasaidia kuamsha akili za watz basi tukazane kuhimizana juu ya hilo. Hivyo ningependa nitofautiane na wewe kwamba mafisadi wanashinda. Hapana hawashindi isipokuwa wanajiweka vizuri, na huko kujiweka vizuri kwao inabidi "ITEGEMEE" kwa maana ya kwamba "WASIGEUKANE" na hiyo mipango yao iwe imesukwa "kweli kweli". Hata hivyo ninaamini there still will be a way through kuwaondoa.

No matter how difficult it is, i still see a shiny Tanzania within the next few years ! Yes i do, sio kwamba nasema tu, bali nuru ishaanza kuonekana angalau kupitia kwa watu wachache wenye uwezo wa kuthubutu kama wa akina Dr. Slaa ! Tusiangalie ni kiasi gani ya watu, wafanyabiashara, wanasiasa au mapadri wapo katika huo mtandao, BALI tuangalie Dr. Slaa wangapi tunaweza kuwa nao ili kulikomboa taifa !! Ukisema uuangalie huo mtandao, utaumiza kichwa bure !
*NB - kuna mafisadi nao washaanza kupiga kelele ili waonekane nao wanapinga ufisadi, yaani mafisadi washaanza kuingiza watu wao katika kundi safi ili kulidhoofisha. Wengi wa hawa ni wabunge, haina haja ya kuwataja nadhani wanafahamika !

Hakuna ugumu wowote katika kuubomoa huu mtandao, isipokuwa itahitaji muda na subira itahijika! Mambo ya Inside Information mkuu !

Kazi na Dawa wazee!
 
Last edited:
Mzee Mwanakijiji,

Lakini pia si kuna mipango imeandaliwa ya watu kulia wanaangushwa kwasababu ni wapinga ufisadi wakati wanajua sababu kubwa ni kushindwa kwao ku deliver waliyoahidi.

Mipango hiyo ni kuhakikisha kila atakayewapinga basi huyo anaunganishwa na mafisadi hata kama hana uhusiano na mafisadi.

Naamini mipango yote haitafanikiwa, hakuna ambaye ana mkataba na bunge, miaka mitano ikiisha kila mtu ana haki sawa ya kushiriki uchaguzi mahali popote.

Watu wanaanza kuzua mambo ya ajabu ajabu kupakazia watu wengine na kuwahusisha na vitendo ambavyo hata havipo, je huo sio ufisadi?

Kuna watu wanataka kutumia vita dhidi ya ufisadi kama mtaji wa kisiasa 2010. Nitaelewa kama mtu atasema yeye anafaa kwasababu amefanya A, B, C na pia amepigana na mafisadi. Lakini kuanza kusingizia kila anayeingia kwa mpambano kama ni fisadi, amepewa pesa na mafisadi nk. bila ushahidi wowote naamini huo ni ufisadi mkubwa sana.

Hii imetulia mzee, tatizo lipo hapo vita dhidi ya ufisadi imegeuka kuwa chaka la watu kuwamaliza wenzao ( risasi kidole ) Mtu akitaka kugombea mahala utaambiwa kutumwa na kambi ya fulani ( mafisadi ) kummaliza fulani kwa sababu eti yeye anapinga mafisadi!
 
Kama mafisadi watashinda, kwa nini bado uko hapa? Ukistaajabu haya ya wapiganaji vita dhidi ya ufisadi....
 
Mkjj kumbuka kwamba the only thing that can not change is the change itself. Mimi bado naamini vita hii mafisadi hawatashinda and for just one reason - Political dynamics. God forbid lakini say JK anavuta leo hii do you still think mambo yatabaki in the status quo???? Well huu ni mfano tu! Kumbuka pia hawa mafisadi hata wakishinda kwenye phase hii ya haka kavita things will never be the same as it is at the moment.

Mara zote mwisho wa vita huwa ni mwanzo wa vita nyingine. Jambo kubwa ni kuendeleza mapambano(alluta continua).
Hata hizi dalili za uhuru wa kuzungumza haya yote ni dalili za ushindi katika mapambano kumbukeni hatukuwa na hii hali tuliyo nayo sasa.(joy comes in morning)tuko gizani/usiku lakini asubuhi inakuja.
Tusikate tamaa ninaimani hili vuguvugu hatimaye litazaa matunda iko siku.
 
Mafisadi hawatashinda - the bright side.

Mwanakijiji, you could be right but only up to a point - ukweli ulio wazi ni kuwa tumewabana. Kama mfa maji, wanachofanya sasa hivi ni kutapatapa - hebu shuhudia mwenyewe vituko vyao kulingana na hizi habari chache kutoka sehemu mbali mbali.

1. Viongozi wa CCM mkoani Mbeya wamepinga makatibu kata waliompa kipigo Katibu wa CCM wilaya ya Kyela, Mwambanga kushitakiwa kwa kile walichodai kwamba hatua hiyo itakivuruga chama hicho kisiasa wilayani humo na mkoa kwa kuzingatia kuwa kipindi hiki ni cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwakani.
1. KATIBU Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba, amewaagiza makatibu wa CCM na jumuia zake ngazi za mikoa, kuandaa maandamano ya kumpongeza Rais Jakaya Kikwete na serikali, kwa kufanikiwa kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM, katika kipengele cha kupambana na rushwa.
3.Diwani mmoja wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, amekamatwa na kutupwa ndani wilayani Geita baada ya kukamatwa `laivu` akidaiwa kununua shahada za kupigia kura mitaani, jambo ambalo ni kinyume cha sheria za nchi.
4. John Malecela amewaeleza watu wa Busanda kuwa iwapo watamchagua mgombea wa CCM, basi serikali itawaletea umeme na kutenga maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo.

Ukisikia mafisadi kuchanganyikiwa ndiko huku na kamwe hatutakiwi kulegeza kibano kwa namna yoyote ile - hivi vitendo vinazidi kuwaumbua kwa kuzidi kuanika maovu yao. Mafisadi lazima wawe na muundo unaowaunganisha ambao ama ni chama, kundi, mtandao, umoja au jumuiya - huko ndiko kimbilio na maficho yao, nje ya hapo hawawezi kufanikiwa. Wananchi kwa ujumla wao wanaanza kuwaona kwa sura zao halisi na si kama zamani walipoweza kujificha nyuma ya slogans za aina ya amani, utulivu na mshikamano.

Lazima sasa tuelekeze nguvu zetu katika kufyeka hiki kichaka.Kila siku tunasonga mbele na kila hatua ni pigo kwa mafisadi kwa kuwa pole pole tunawavua nguo. Mpaka sasa tumefanikiwa kuwatoa kwenye suti zao na hivi sasa wameanza kugombania kipande cha kanga waweze kujisetiri kwa hatari ya kubaki uchi. Taratibu kanga inaanza kuchanika na muda si mrefu, kwa aibu, kila moja wao ataanza kutimua mbio kivyake akitafuta pa kujificha - uzuri ni kuwa kichaka chenyewe tuko kazini tunakifyeka kama kazi.
Hapana Mwanakijiji, hakika tutashinda​
Kimbilio la mafiasdi tusiliruhusu kuendelea kudumu
 
Mafisadi hawatashinda - the bright side.

Mwanakijiji, you could be right but only up to a point - ukweli ulio wazi ni kuwa tumewabana. Kama mfa maji, wanachofanya sasa hivi ni kutapatapa - hebu shuhudia mwenyewe vituko vyao kulingana na hizi habari chache kutoka sehemu mbali mbali.



Ukisikia mafisadi kuchanganyikiwa ndiko huku na kamwe hatutakiwi kulegeza kibano kwa namna yoyote ile - hivi vitendo vinazidi kuwaumbua kwa kuzidi kuanika maovu yao. Mafisadi lazima wawe na muundo unaowaunganisha ambao ama ni chama, kundi, mtandao, umoja au jumuiya - huko ndiko kimbilio na maficho yao, nje ya hapo hawawezi kufanikiwa. Wananchi kwa ujumla wao wanaanza kuwaona kwa sura zao halisi na si kama zamani walipoweza kujificha nyuma ya slogans za aina ya amani, utulivu na mshikamano.

Lazima sasa tuelekeze nguvu zetu katika kufyeka hiki kichaka.Kila siku tunasonga mbele na kila hatua ni pigo kwa mafisadi kwa kuwa pole pole tunawavua nguo. Mpaka sasa tumefanikiwa kuwatoa kwenye suti zao na hivi sasa wameanza kugombania kipande cha kanga waweze kujisetiri kwa hatari ya kubaki uchi. Taratibu kanga inaanza kuchanika na muda si mrefu, kwa aibu, kila moja wao ataanza kutimua mbio kivyake akitafuta pa kujificha - uzuri ni kuwa kichaka chenyewe tuko kazini tunakifyeka kama kazi.
Hapana Mwanakijiji, hakika tutashinda​

Kimbilio la mafiasdi tusiliruhusu kuendelea kudumu

I like this one! tutashindaje though wakati the odds are stacked against us.. nyie subirini ya kesho na keshokutwa...
 
Mkjj kumbuka kwamba the only thing that can not change is the change itself. Mimi bado naamini vita hii mafisadi hawatashinda and for just one reason - Political dynamics. God forbid lakini say JK anavuta leo hii do you still think mambo yatabaki in the status quo???? Well huu ni mfano tu! Kumbuka pia hawa mafisadi hata wakishinda kwenye phase hii ya haka kavita things will never be the same as it is at the moment.

Hypothetically thinking. if JK does not return to power, in whatever means, will the situation be any better?
 
Mkuu FMES na Mzee Mwanakijiji,

Alichokisema Mwanakijiji.....niliki-highlight karibu miaka miwili iliyopita. Napenda kusisitiza tena ni vema kujua unapigana na nani na unapigania nini (we must reach a point inabidi tu-itemise hivi vitu)........hapo kati kati tumekuwa na maendeleo mazuri kiasi......ila kwa sasa tumeanza kujichanganya tena sisi wenyewe kwa wenyewe.......kwa sababu za UBINAFSI, UNDUGU, UDINI, URAFIKI nk.....bila ya kuweka haya mambo pembeni trust me HAKUNA KUMKOMA NYANI GILADI.............

kuna kitu kinaitwa "BLACK CRAB SYNDROME" ndiyo inayotusulubu sasa hivi hapa JF na hata kwenye System i.e. Serikalini.

THE ONLY DAWA,
FIGHT FROM BOTH ANGLES i.e FROM INSIDE and FROM OUTSIDE.......somewhere we will have to put a STOP.(step by step)........and that will be the begining of a FUNDAMENTAL CHANGE WE CAN BUILD UPON
 
hii vita ni ngumu sana, lakini tutashinda tena kwa kishindo. Kazi kubwa ni kila mmoja kuchagua upande halafu kuanza kuelimisha wananchi ni nini madhara ya wizi wa fedha za kodi. Na ningeshauri kutoa elimu sana kwa watoto wa primary na secondary, kuonisha maisha na viwango vya elimu wanazopata kuwa vinasababishwa na vitendo vya ufisadi. Kuendelea kuweka wazi familia zilizofaidika na vitendo vya kifisadi na kuonyesha wazi tunawachukia kwa matendo yao, kutoa hawa watu kwenye kumbukumbu ya nembo ya utumishi wa umma na kuwaweka kama watu na familia hatari kwa ustawi wa jamii.

Ni lazima kuweka kumbukumbu na za matukio ya aibu yaliyofanywa na mafisadi kwa majina yao.
Vita hii sio rahisi ni ngumu ushindi sio mrahisi. Mafisadi watashindwa ila kabla ya ushindi kutachimbika.
Kuelimisha watanzania kuwa hatuna amani na neno hili amani ni silaha ya mafisadi. hakuna amani kwani wananchi wengi wanakufa kwa wizi na utendaji wa mafisadi.

Na tukumbuke kuwa Fisadi namba moja ni raisi wa nchi kwani ndiye analea mafisadi. Fisadi namba mbili ni bunge la taznania kwani linashangilia mafisadi. Fisadi namba tatu ni mahaka kwani haitoa hukumu zinazofaa kwenye kesi za kifisadi.

Raisi anamamlaka makubwa sana anaweza kupunguza au kumaliza mafisadi kama yeye sio mmoja wao. anawateua majaji, usalama wa taifa, mkuu wa polisi, mkuu wa majeshi.
Ukiangali kwa undani teuzi hizi ndizo zilizofanya ufisadi , wafanyabiashara walibeba tu mikoba ya ufisadi sasa watu wa kwanza kuwasulubisha lazima wawe wao, tukianzia na mkuu wa kaya.

Nitapigana na ufisadi kwa nguvu zangu zote na sasa naanzia na JK.
 
siwezi kuwasaliti watz kwa kujiunga nao...tutapigana mpaka tunaenda kaburini.mzee mwanakijiji aluta......cont
 
Asante MMK kwa analysis yako.
Lakini nadhani hakuna sababu ya kufa moyo, mafisadi wamejijenga kwa muda mrefu na wana mizizi mirefu sasa, ambayo unapoingoa pia inabidi ingooke na mimiea mingeine mizuri. Lakini tukubaliane kuwa japo mafanikio katika kupigana na ufisadi hayajaonekana lakini angalao sasa wanafahamu kuwa vita ipo dhidi yao, na hii ni hatua nzuri.

Watoto wa MBWA WAMEFUNGUKA (PASUKA) MACHO, sasa hawawezi tena kuendelea kulala!
 
In his book, man’s search for meaning, Viktor E. Frankly said, I quote
"Don't aim at success - the more you aim at it and make it a target, the more you are going to miss it. For success, like happiness, cannot be pursued; it must ensue, and it only does so as the unintended side-effect of one's personal dedication to a cause greater than oneself or
as the by-product of one's surrender to a person other than oneself. Happiness must happen, and the same holds for success: you have to let it happen by not
caring about it. I want you to listen to what your conscience commands you to do and go on to carry it out to the best of your knowledge. Then you will live
to see that in the long run - in the long run, I say! -success will follow you precisely because you had forgotten to think of it."
MMKJ, huyu shetani atashindwa ila ni vita ambayo siyo ya siku moja au wiki kadhaa kama tunavyofikiri.
Tukumbuke uhuru ulichukua muda mrefu kuudai na kuupata toka kwa wakoloni. Ingekuwaje wazee wale wangekata tamaa? Tunajua vuguvugu la kuudai lilianzaje? Naamini wema utaushinda uovu. Ni kweli kabisa umafia upo Tanzania na kwa bahati mbaya unawanufaisha baadhi ya watu wanaoufanya wakidhani wanalisaidia Taifa. Kuna siku ipo yaja tutaona mabadiliko ya kweli tusikatee tamaa
 
Ukiwa vitani hutakiwi kukata tamaa, kujua mbinu za adui yako ni success factor ya ushindi wako so Mwankijiji kama ushajua mbinu za hawa fisadi basi tujipange kutegua mitego yao nakuwashambulia zaidi.
 
It can be done! Play your part. Haya maneno ya miaka 48 iliyopita have more meaning today than at any other time.
 
Hypothetically thinking. if JK does not return to power, in whatever means, will the situation be any better?

It might push the leaders to be more aware of the people they lead. CCM never lost an election & no sitting president has ever lost a second term, if JK looses then that will be a big message sent by the people telling the leader that non of them are immune. Nadhani tatizo kubwa ni kwamba kuna baadhi ya viongozi wana jiona nothing can ever be done to them. If we do something to them then it will make them check their egos & inflated heads.
 
Back
Top Bottom