Mafisadi Wakamatwe!-wasiruhusiwe Kuligawa Taifa!

Chenge: Nimezushiwa

na Jane Kajoki, Bariadi

MBUNGE wa Bariadi Magharibi aliyejiuzulu uwaziri hivi karibuni kwa kashfa ya kukutwa na fedha zinazohusishwa na ufisadi, Andrew Chenge amewataka wananchi wa jimbo lake kuendelea kumwamini kwa kuwa yeye ni mtu safi na asiye na hatia yoyote kwani tuhuma dhidi yake ni za kuzushwa.
Mbali ya hilo, Chenge alisema alifikia uamuzi wa kujiuzulu wadhifa wa Waziri wa Miundombinu zaidi ya wiki mbili zilizopita si kwa sababu ya kukiri makosa, bali ili kutoa fursa kwa taasisi zinazochunguza kashfa yake kufanya kazi yake kwa uwazi.
Chenge ambaye jana alihutubia mikutano ya hadhara katika maeneo ya Bariadi Mjini, Ramadi, Nyakabimbi na Kapiwi, alisema wakazi wa Dar es Salaam ndio ambao wamekuwa wakimuona kuwa mtu asiyefaa kutokana na kubebeshwa tuhuma zisizo za ukweli, ikiwa ni pamoja na kuzushiwa kifo.
"Dar es Salaam wanasema sifai labda kwa sababu ya sura yangu...Pamoja na watu wa Dar es Salaam kupiga kelele kuwa sifai, naamini sina hatia yoyote, na ndiyo maana nilijiuzulu. Ninyi wakazi wa jimboni kwangu ndio mnajua kama sifai au nafaa.
"Haya mambo yaliyotokea ni ajali ya kisiasa. Ni mambo ya kupikwa na watu, lakini kwa tuhuma hizi wacha tuwape nafasi waendelee na uchunguzi. Sitakiwi kuzungumzia hilo kwa sasa, nimekuja nyumbani kuhimiza shughuli za maendeleo katika jimbo letu katika nyanja zote za barabara, elimu, afya na maji," alisema Chenge ambaye alivuta umati mkubwa wa wananchi waliokuwa wakimshangilia kila alipokuwa akihutubia.
Alisema pamoja na kujiuzulu uwaziri, aliahidi kuendelea kuwatumikia wananchi wa jimbo lake na akasema anaamini ifikapo mwaka 2010 atakuwa ametekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005-2010.
"Walio na ndoto za ubunge tukutane kwenye hoja za utekelezaji wa ilani mwaka 2010. Mmeona tulivyojenga shule za sekondari, barabara, mabwawa, visima, vituo vya afya vyote hivyo ni katika jimbo letu. Pamoja na habari ya kuzushiwa kifo, nawaomba mtulie, tushirikiane kwa kutembea kifua mbele kufanya kazi na kujiletea maendeleo," alisema Chenge ambaye anatembelea jimbo lake kwa mara ya kwanza tangu ajiuzulu.
Akiwa katika Kijiji cha Dutwa alisema alitaja vijisenti si kwa nia ya kukejeli bali akiwa na mtazamo wa Kisukuma ambao wao wanapoongelea ng'ombe 100 kwa mfano wanasema ‘vijing'ombe'.
Hii ni mara ya pili kwa Chenge kuzungumzia kauli yake ya vijisenti ambayo kwa kiwango kikubwa ndiyo inayoonekana kuwa iliyokuza tuhuma alizokuwa akihusishwa nazo.
Kwa mara ya kwanza, Chenge alizungumzia kauli yake hiyo jijini Dar es Salaam wakati alipofanya mahojiano kwa njia ya simu na gazeti hili, ambapo aliwaomba radhi Watanzania ambao walikwazika au kuumizwa na kauli yake hiyo ya vijisenti.
Alisema halikuwa lengo lake kuwakera wananchi kwa kauli hiyo iliyozua mjadala kiasi cha baadhi ya makundi ya watu wa kada tofauti kutoa maoni yao wakimtaka Rais Jakaya Kikwete amwajibishe.
"Mimi siyo Mzaramo. Hiki ni Kiswahili. Sisi wengine kule Usukumani kusema vijimambo, au vijisenti, vijitoto hivi ni kawaida kwa desturi zetu...ndiyo maana napenda kusema wazi kwamba iwapo kuna Watanzania niliwaumiza kwa kauli ile niliyoitoa kwa nia njema kabisa na wala si kwa lengo la kuwakejeli, naomba radhi kwa hilo," alisema Chenge wakati huo.
Tuhuma dhidi ya Chenge ziliandikwa kwa mara ya kwanza katika gazeti la The Guardian la nchini Uingereza likikariri taarifa kutoka Taasisi ya Uchunguzi wa Makosa Makubwa ya Jinai ya nchini humo (SFO).
Gazeti hilo liliandika kuwa, uchunguzi wa SFO uligundua akaunti moja inayohusishwa na Chenge ikiwa na zaidi ya dola za Marekani milioni moja iliyopo kwenye kisiwa cha Jersey.
Gazeti hilo liliandika kwamba, SFO ilikuwa ikitarajia kuanza upya kufanya uchunguzi kuhusu fedha hizo ili kuangalia iwapo zilikuwa na uhusiano na zile zinazoaminika kuwa zilitolewa kwa njia ya rushwa wakati Tanzania iliponunua rada ya kijeshi kutoka nchini humo kwa paundi milioni 28 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 70, mwaka 2002.
The Guardian katika habari yake hiyo liliripoti kuwa, taarifa hizo zinakuja ikiwa ni miaka mitatu sasa tangu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) kwa kushirikiana na SFO na taasisi za uchunguzi za Uswisi na Jersey zilipoanza kuchunguza kuhusu kashfa nzima ya ununuzi wa rada.
Gazeti hilo lilimkariri Waziri Chenge akikiri kwamba fedha hizo ni zake na akatumia fursa hiyo kukanusha kuwapo kwa uhusiano wowote kati ya fedha hizo na kashfa nzima ya ununuzi wa rada, uliofanywa wakati yeye akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
"Jambo la wazi linalotaka kuonekana hapa ni kwamba mimi nilipokea kwa lengo la kujinufaisha mwenyewe fedha za rushwa kutoka BAE. Huu ni uongo," alisema Chenge.
Aidha, gazeti hilo lilimkariri Chenge akisema kuwa, wakati rada hiyo ilipokuwa ikinunuliwa yeye alihusika kwa kiwango kidogo sana katika mchakato mzima, kwani jambo hilo lilishughulikiwa na wizara nyingine na uamuzi ukaidhinishwa na Baraza la Mawaziri.
Mbali ya hilo, gazeti hilo lilimkariri mwanasheria wa Chenge anayeishi Cleveland, Ohio, nchini Marekani, J Lewis Madorsky, akikanusha kwa niaba ya mteja wake huyo, kuwapo kwa uhusiano wowote kati ya fedha zake na tuhuma zozote.
"Wakati tukitambua kuwa masuala hayo yalitokea muda mrefu uliopita, tunaweza tu tukathibitisha kuwa, tuhuma zozote za ukiukwaji wa sheria, ukiukwaji wa maadili, kutenda isivyo sawa na mambo mengine ya hivyo dhidi ya mteja wetu ni mambo ambayo kimsingi tunayakanusha kwa nguvu kubwa," alisema mwanasheria huyo wa Chenge. Hata hivyo, gazeti hilo liliandika uchunguzi huo dhidi ya Chenge unamfanya yeye kuwa tu shahidi muhimu, kwani wanaielenga zaidi BAE ambayo inadaiwa ilimlipa wakala mmoja wa Tanzania mamilioni ya fedha ili kujenga ushawishi wa rada iliyokuwa ikiiuza kununuliwa. Wakala huyo ambaye amekuwa akitajwa kwa muda mrefu, na ambaye sasa anaaminika kukimbia nchini na kutafutwa na polisi wa kimataifa ni, Shailesh Vithlani.

Ndugu wana JF...Kama si kuwagawa wananchi.."Then kuwa mtu wa Dar es Salam, ama kuwa mtu wa Mara...Kuwa Mzaramo ama kuwa Msukuma"

Vinahusiana vipi na yeye kutuhumiwa na Taifa kuwa ni FISADI?

MWENYE JIBU NAOMBA ANIPE TAFADHALI!

NB: Je Muungwana anakubaliana na Chenge kuwa eti ni "Ajali ya Kisiasa?"

Na kama si hivyo..then mbona hakamatwi?

WAPI BALALI?
 
Chenge kadata. Kwani Kiswahili ni lugha ya Wazaramo peke yao? Na kama hujui Kiswahili basi hukustahili kuwa Waziri. Na hiyo Sheria amefundishwa Kisukuma? Labda kweli haelewi lolote zaidi ya Kisukuma ndio maana anasema hili swala hawezi kuliongelea halafu hapo hapo analielezea kama ni ajali ya Kisiasa. Labda haelewi lugha nyingine ndio maana anasaini mikataba mibovu. Anapata ujiko wa bure kwamba ni Harvard educated lawyer. Ukisema Harvard lawyer manake una JD ya miaka mitatu. Masters za Harvard zinatolewa kumi kwa senti kumi. Mpaka Sumaye nae anayo! Chenge hujui Kiswahili, tafadhali!
 
Chenge hajadata!

Ni victim wa "Defensive Mechanism!" Unajua sisi ni binadamu! Kujaribu kututaka sisi tuamini something tofauti na ukweli ambao uko wazi!

Kwenye "Defensive mechanism" ni sawa na mtoto anapokukania kuwa hajalamba sukari na wakati unaiona wazi wazi pembezoni mwa mdomo!

Huyu haja data wala nini.. ila anampango mahsusi wa kuwagawa wananchi ili arudi kwa rais na kumwambia kuwa bado ana support ya wananchi hivyo awe makini pale anapotaka kumshughulikia.

Kumtisha Mh Rais kuwa he's still powerfull!

Kujijenga upya ili kuendelea na madai kuwa yeye ni kipenzi cha wananchi na wala si fisadi!

Kwamba Mh Rais ampe muda wa kujisafisha ili iwe vigumu kwa yeye kuwajibishwa kwa kisingizio cha kinga ya wananchi na ubunge!

NASEMA HIVI... HAWA WATU WAKAMATWE MARA MOJA! WAHOJIWE, WAFUNGULIWE MASHTAKA..THEN WAFANYE MIKUTANO YA "KUJISAFISHA"
 
Kwa wale wasioamini mwisho wa mafisadi huu u karibu!

Matukio ya ufisadi, ubadhirifu wa mali yamewaamsha Watanzania

2008-05-12 08:59:11
Na Dunstan Bahai

``...Urithi wetu umegeuka kuwa mali ya wageni, na nyumba zetu kuwa mali ya makafiri. Tumekuwa yatima waliofiwa na baba, mama zetu wamekuwa kama wajane.

Tunakunywa maji yetu kwa fedha, kuni zetu twauziwa.

Watufuatao wako juu ya shingo zetu, tumechoka tusipate raha yoyote Baba zetu walitenda dhambi hata hawako, na sisi tumeyachukuwa maovu yao. Watumwa wanatutawala, hakuna mtu wa kutuokoa na mikono yao.

``Twapata chakula kwa kujihatarisha nafsi zetu, kwa sababu ya upanga wa nyikani. Ngozi zetu ni nyeusi kama tanuu, kwa sababu ya hali ya njaa ituteketezayo Wakuu hutungikwa kwa mikono yao, nyuso za wazee hazipewi heshima.

``... Wazee wameacha kwenda langoni, na vijana kwenda ngomani. Furaha ya mioyo yetu imekoma, michezo yetu imegeuka maombolezo.

``Mbona watusahau siku zote, na kutuacha muda huu mwingi. We Bwana, utugeuze kwako nasi tutageuka, zifanye mpya siku zetu kama siku za kale. Isipokuwa wewe umetukataa kabisa, nawe una hasira nyingi sana juu yetu,`` hayo ni baadhi maneno ya Bibilia yanayopatikana kwenye kitabu cha Maombolezo sura ya 5:1-22.

Nimelazimika kunukuu sehemu hiyo ya Biblia kama kitabu kitakatifu, kuonyesha maonyo yaliyotolewa wakati wa zamani na dhuluma iliyopo sasa duniani, hasa katika nchi maskini na zile zinazoendelea, dhuluma zinazofanywa na baadhi ya watawala wake.

Katika kipindi cha takribani miaka miwili na miezi minne hivi, Watanzania na Walimwengu kwa ujumla, wameshuhudia viongozi wa juu wa serikali ya awamu ya nne wanavyoachia nyadhifa zao.

Hatua hiyo ya viongozi kuachia nyadhifa zao haimaanishi wamehusika na tuhuma zinazoenezwa juu yao, bali ni ishara ya heshima na uwajibikaji.

Hatuwezi kuwahukumu viongozi hao kuwa `walivaa ngozi ya kondoo`, huku wakijijua ni `mbwa mwitu` bali walionyesha mfano mzuri wa kuwajibika ingawa wapo wengi wa aina hiyo wanaotakiwa kufuata nyayo zao.

Kuwajibika si dhambi, wala kuwajibika si aibu bali kama kiongozi, anazidi kujijengea heshima.

Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Mwesiga Baregu, anatanabaisha kwamba baada ya Tanzania kupata Uhuru, uongozi wa wakati huo ulikuwa ukitegemea Rais zaidi.

Hata hivyo, alikiri kuwa viongozi wa wakati huo walikuwa na maadili makubwa ikilinganishwa na wa sasa.

Alisema mtu mbadhirifu au aliyepatikana na rushwa, alikuwa hana nafasi wala sifa ya kuendelea kuwa kiongozi, kwani Rais, wakati huo hayati Mwalimu Julius Nyerere, hakusita kumchukulia hatua kali ikiwa ni pamoja na kumfukuza kazi moja kwa moja.

``Wakati huo ilikuwa amri moja tu kwa kiongozi asiye na maadili. Zamani kiongozi akiitwa Ikulu anatetemeka, anajua akirudi hana kazi, ni kiama kwake, lakini sasa hivi mambo tofauti.`` alisema.

Alisema kipindi cha awamu ya kwanza, kulikuwa na matukio mengi ya viongozi kujiuzulu, kufukuzwa na kustaafishwa kazi.

Miongoni mwa tukio la kujiuzulu kwa kuwajibika ni la aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, kutokana na makosa yaliyotokea katika wizara yake.

Katika serikali ya sasa viongozi wengine walioachia ngazi zao kwa uwajibikaji mapema mwaka huu ni aliyekuwa Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Nazir Karamagi, aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Ibrahim Msabaha na hivi karibuni aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Bw. Andrew Chenge.

Hata hivyo, aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Daud Balali, alifukuzwa kazi ingawa ni baada ya kumuandikia Rais kuwa ameamua kujiuzulu.

Uwajibikaji ni sehemu ya uadilifu, nidhamu na kujijengea heshima ndani ya familia ya anayewajibika, lakini zaidi nje ya familia yake na nje ya mipaka ya nchi, kwani kiongozi anaonyesha kujutia kilichotokea akiwa kiongozi katika eneo lake, lakini kujiuzulu kwa shinikizo la umma, hilo halimletei heshima kiongozi.

Kwa mujibu wa Profesa Baregu, kumekuwa na matukio mengi ya ubadhirifu, hali ambayo imewaudhi wananchi hadi kufikia umma huo kuchukia kudanganywa huku mali zao wakishuhudia zikiporwa.

Profesa Baregu alisema shinikizo la nguvu ya umma limechangia kuibuka kwa mambo mengi maovu.

Pia alivipongeza vyama vya upinzani hasa ushirika wa vyama vinne vya CHADEMA, CUF, TLP na NCCR-Mageuzi.

Alisema vyama hivyo kwa kushirikiana na umma wa Watanzania, waliweza kufanikiwa kuufikisha ujumbe, kilio chao cha kuporwa mali zao, na matokeo yalijidhihirisha na kwa upande mwingine serikali imeonyesha nia ya kushughulikia malalamiko hayo.

Hatua iliyofikiwa na serikali ya kuanika uozo uliojitokeza, ni hatua muhimu sana na ya kuungwa mkono na wananchi wengi, hicho ndicho kilichokuwa kikisubiriwa na umma wa Watanzania.

Aidha, hatua hiyo itairejesha heshima na imani ya Watanzania kwa uongozi wa Taifa na mihimili yote ya nchi.
Naye Askofu Mkuu Msaidizi wa Kanisa Katholiki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Methedius Kilaini, ameonyesha kukerwa na watu wanaohusika na ufisadi.

``Mimi simjui fisadi, lakini ninachukia sana hali hiyo. lakini nimeridhika jinsi suala hili lilivyoibuliwa, kwani haya mambo yalikuwepo tangu enzi za mababu, lakini, nani awe wa kwanza kumfunga paka kengele,`` alisema.

Aliwashauri Wabunge, kutokana na ujasiri wao kuliibua suala hili na kulizungumzia kwa kina, waendeleze jitihada hizo hadi mafisadi watakapojulikana na kufikishwa mahakamani, kwani huko wananchi watakapowajua na kupata haki yao.

Askofu Kilaini alikuwa akimaanisha, huwezi kumnyooshea mtu kidole kuwa ni fisadi, kwani wengi wanaamini viongozi wote waliojiuzulu ni mafisadi, la hasha, hao walifanya hivyo kama sehemu ya uwajibikaji, kwani tuhuma hizo zimeibuka wakati wao wakiwa ni viongozi wa maeneo yanayotuhumiwa.

Kwa maana hiyo, uchunguzi unaofanywa na serikali katika maeneo hayo wananchi wanaamini utawaibua mafisadi, pengine ni wale waliojiuzulu kwa heshima au wengine.

Inawezekana kabisa, Rais Kikwete ana dhamira ya kweli ya kuwaondolea umaskini na kero zote zinazowakabili wananchi, lakini wapo wanaokwenda kinyume na dhamira hiyo.

Hata hivyo kuna dalili yawezekana Rais Kikwete ameonyesha kukerwa na ufisadi pamoja na rushwa, ndiyo maana alishindwa kulitolea maamuzi suala hilo na badala yake ameviachia vyombo vya dola kulishughulikia, na Watanzania wanasubiri kwa hamu sana matokeo ya uchunguzi huo.

Kumekuwa na maoni mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na wananchi na viongozi wa dini, juu ya nini kifanyike kwa wale wote watakaobainika kuhusika na kupora mali za Watanzania.

Pia yapo maoni yaliyotolewa na Kamati Teule ya Bunge iliyokuwa ikiongozwa na Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, kuchunguza tuhuma za Richmond.

Baadhi ya maoni ya wananchi na viongozi wa dini ni serikali kuwachukulia hatua haraka wale wote wanaodhani ni mafisadi ikiwa ni pamoja na kufilisi mali zao.

Maoni hayo ni ya haraka sana, tunaamini hakuna mtu anayemfahamu fisadi, cha msingi ni wananchi kuwa na subira, kusubiri uchunguzi unaoendelea wa vyombo vya dola.

Cha msingi ni vyombo hivyo kufanyakazi yake kwa umakini na ukweli na uwazi ili Watanzania waendelee kujenga heshima kwa serikali yao ya awamu ya nne na hata Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ili suala hili lisiendelee kuwa mjadala, tena mjadala wa kutoaminiani, dhamana ya ukweli wa mambo yenyewe iko mikononi mwa vyombo vilivyoteuliwa na serikali katika kuchunguza masuala hayo.

Vyombo hivyo visipofanyakazi yake kwa makini na ukweli, viongozi waliojiuzulu nyadhifa zao hawatakwepa hasira za wananchi, na maisha yao yatakuwa juu ya mikono ya Watanzania.

Watanzania kama kawaida yao ni wapole, hivyo upole wao usichukuliwe kama ni mazuzu.

Tanzania ni yetu, hakuna mgeni atakayetutengenezea amani na utulivu, kwani suala hili likichukuliwa kwa jazba, urithi wa amani yetu utabakia kama historia, Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
  • SOURCE: Nipashe
 
Higlights zinakamilisha
 
Oooh Mi Msukuma wao Wazaramo!
Hawa wa Dar es Salam sisi wa Mara?
 
MKJJ na MKW kama nyie ni wazalendo naomba jibu hapa...Wakamatwe ama wasikamatwe?
Najua mlikuwa hamuamini kuwa Ballali alitakiwa akamatwe..Badala yake mkitaka apewe kinga...Vipi kuhusu wale wengine wanaoenda kuwagawa wananchi kwa misingi ya kikabila?
Wapewe kinga ama wakamatwe?
 
Wanaligawa Vipi Taifa Wakati Wao Ndio Viongozi Wa Taifa ? Kwa Sababu Wewe Ni Chadema Basi Chochote Kikisemwa Na Ccm Ni Kugawa Taifa , Kugawa Watu Sijui Udini Na Mambo Mengine Kama Hayo

Taifa Haliwezi Kugawa Kwa Mtindo Huo Na Tanzania Yote Ni Moja Kama Mtu Ana Malalamiko Yake Apeleka Katika Vyombo Vya Sheria Au Sehemu Husika Atasaidiwa Zaidi Katika Hilo Na Sio Kuwahukumu Watu Kwa Maneno Ya Vijiweni Kama Haya

Kwi kwi kwi...Mafisadi wa Taifa!
Hawa wakamatwe kabla ya kutuletea machafuko!
SERIKALI TUMESHAGUNDUA JANJA YENU..TOENI RIPOTI NA MAFISADI WAKAMATWE MARA MOJA!
 
labda wakamatane au vipi,sijui nani atakayeanza kumkamata mwenzake!
 
Mkapa awasha moto

na Salehe Mohamed

UAMUZI wa Rais mstaafu, Benjamin Mkapa kuanza kujibu tuhuma dhidi yake, umeibua malumbano ya hoja kutoka kwa wanasiasa kadhaa ambao wameeleza kushangazwa na majibu na hatua yake hiyo.
Miongoni mwa watu wa kwanza kutoa maoni yao kuhusu kauli hiyo ya Mkapa, ni Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro ambaye alikuwa mwanasiasa wa kwanza kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumrushia makombora ya tuhuma rais huyo mstaafu, akifanya hivyo ndani ya Bunge.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Kimaro alimtaka Mkapa kujibu tuhuma dhidi yake na kuacha kuwanyoshea kidole wengine kwa matatizo anayokabiliana nayo.
Katika kauli yake hiyo, Kimaro alisema alielekeza tuhuma kwa Mkapa si kwa sababu ya chuki au kwa kuwa alinyimwa nafasi yoyote ya kimadaraka serikalini kama alivyodai kiongozi huyo mstaafu, bali alifanya hivyo kutokana na kuwa na mapenzi ya dhati kwa taifa lake.
Alisema kuwa, alichokisema kilitokana na kuwa na moyo wa kuwaonya viongozi mbalimbali kutokana na kutumia madaraka yao vibaya na kwa masilahi binafsi.
Alisema ushahidi wa Mkapa kujihusisha na biashara akiwa Ikulu upo Mamlaka ya Usajili wa Leseni na Biashara (Brela), Tanesco na taasisi nyingine zinazohusika na mambo ya biashara, hivyo alichokisema si jambo la kutunga au kumzushia kiongozi huyo kwa sababu ya chuki binafsi au nyinginezo.
“Mimi sitarajii uongozi serikalini, nilishafanya kazi huko nikaamua niendelee na mambo mengine, nitakuwa muwazi siku zote… kamwe sitaki unafiki na yoyote anayefikiri nilifanya hivyo kwa ajili ya kumlenga Mkapa anakosea… nilifanya vile kwa sababu ya kuisimamia serikali na viongozi wengine wasielekee kule kusikofaa,” alisema Kimaro.
Alisema tabia ya viongozi kusema kuwa nchi ina amani, utulivu na rasilimali nyingi haina mantiki kwa wananchi, iwapo hawataona uwajibikaji wa viongozi na matumizi sahihi ya rasilimali zao katika jitihada za kuwakomboa katika lindi la umasikini.
Kimaro alisema hatarajii kufanya siasa za kumchafua mtu, bali anachokifanya hivi sasa ni kile alichotumwa na wananchi wake, hivyo si vema mtu kumhusisha na dhana mbaya dhidi ya viongozi anapotimiza wajibu wake aliotumwa na wapiga kura wake wenye kiu ya maendeleo.
Wakati wa kikao kilichopita, Bunge lilipokuwa likijadili Muswada wa Sheria ya Nishati, Kimaro alimtuhumu Mkapa kwa kutumia vibaya madaraka yake kujinufaisha wakati akiwa madarakani.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chacha Wangwe, alisema mtindo alioutumia Mkapa kujibu tuhuma zilizoelekezwa kwake unaweza kuzaa matatizo mengine na kusababisha malumbano yasiyokwisha.
Akitoa ushauri wake, Wangwe alisema kwa kuwa Mkapa anaonekana kuwa ameamua kuanza kujibu tuhuma hizo, anatakiwa kujitofautisha na watu wanaoonekana kujitafutia huruma kupitia kuwachafua watu wengine.
Alisema ili aaminike, Mkapa anapaswa kutoa utetezi wake chini ya kiapo cha mahakama kuhusu kutohusika kwake na ufisadi, ili kuwawezesha wapinzani na wananchi kufuatilia mali zake, badala ya kujitetea mkoani kwake.
Akizungumza na waandishi kuhusu utetezi wa Mkapa alioutoa mwishoni mwa wiki iliyopita, Wangwe alisema kuwa, kauli hiyo ya rais huyo mstaafu haina uzito wowote kwa Watanzania, bali kama kweli ana nia ya kusafisha jina lake akale kiapo mahakamani kuhusu kile anachokisema.
Alisema baada ya hapo, ufuate uchunguzi dhidi yake, ufanyike kulingana na kiapo hicho na kama atabainika kufanya biashara akiwa Ikulu, kiapo hicho kitumike kama ushahidi dhidi yake.
“Leo hii Mkapa hawezi kusema mambo kirahisi rahisi namna hii… anapaswa akale kiapo mahakamani na serikali ifanye uchunguzi juu ya kile alichokisema na kama itathibitika kuwa kafanya ufisadi akiwa madarakani, basi kiapo kile kiwe sehemu ya ushahidi,” alisema Wangwe.
Wangwe alisisitiza kuwa Mkapa hawezi kuepuka dhambi ya ufisadi, kwani wasaidizi wake wengi akiwemo aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wake, Andrew Chenge, wanakabiliwa na tuhuma za ufisadi na ni miongoni mwa watu waliokuwa wakimsaidia kugeuzageuza mikataba mbalimbali kwa lengo la kujinufaisha.
Alisema ni jambo lililo wazi kuwa Mkapa alikuwa akifanya biashara akiwa Ikulu na kibaya zaidi alikuwa akitumia anwani ya Ikulu kwa masilahi binafsi, jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya maadili ya watumishi wa umma na viongozi, lakini kwa sababu ya tamaa za madaraka aliamua kupindisha sheria hiyo.
Katika mtazamo mwingine, Wangwe aliliunganisha tukio la Mkapa kujitetea akiwa kijijini kwake na matukio yanayofanana na hayo yaliyopata kufanywa kwa nyakati tofauti na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na Chenge.
Wangwe aliutumia mlolongo huo wa matukio kuonya kuwa inaelekea nchi sasa inamezwa na ukabila kwani haiwezekani mtu atuhumiwe kitaifa, halafu atumie jukwaa la kijijini kujibu tuhuma hizo.
Alionya kuwa matukio hayo yanaipeleka nchi pabaya zaidi, kwani watu wanaotumiwa kwa ufisadi wameanza kugeuza ajenda hizo kwa ukabila kwa kukimbilia vijijini kwao kujitetea.
“Kila mtu hivi sasa anakimbilia jimboni au mkoani kwake kujisafisha, mara leo utasikia huyu yupo Monduli, kesho utasikia yule yupo Bariadi, hii ni hatari kwa maendeleo ya nchi kwani wanataka Watanzania wasahau kuhusiana na vita ya ufisadi na badala yake wajikite katika ukabila,” alisema Wangwe.
Aidha, alisema hoja ya Mkapa kuwa wanaomtuhumu hivi sasa wanafanya hivyo kwa husuda baada ya kuwanyima vyeo, haina maana kwani wanaopiga kelele hizo wengi wao ni wapinzani ambao kwa mfumo wa sasa wa utawala, hawawezi kujumuishwa serikalini.
Alisema kama Mkapa anao ushahidi wa kuombwa nafasi za uongozi na kambi ya upinzani, ajitokeze hadharani na kuwataja watu hao, ili hoja yake iweze kuwa na nguvu, kuliko anavyodai hivi sasa kuwa aliwanyima nafasi za uongozi na wanamuonea wivu.
Wangwe alisema Mkapa ni mmoja kati ya watu waliotajwa na wapinzani akituhumiwa kwa ufisadi kati ya viongozi wakubwa 11, lakini hajawahi hata siku moja kujitokeza na kukanusha jambo hilo au kwenda mahakamani kuwafungulia kesi wale wanaomhusisha na ufisadi. Alisema Mkapa alikingiwa kifua na baba wa taifa hayati Mwalimu Nyerere kuwa ni msafi na kweli alipoanza kazi miaka mitatu ya mwanzo, alikuwa akifanya kazi vizuri, lakini aligeuka mara baada ya kifo cha Nyerere na kuanza kuinadi nchi kama vile haina mwenyewe sambamba na kukithiri kwa rushwa na kufikia viwango vikubwa. Alisema katika kipindi cha miaka 17 iliyopita, rushwa kubwa imeimarika zaidi ambapo miaka mitano ya mwisho wa uongozi wa rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, ndipo ilipoanza na miaka yote kumi ya awamu ya tatu chini ya Mkapa rushwa iliimarika mara dufu na miaka miwili ya Rais Kikwete hali iliendelea kuwa ile ile.
 
Kikwete mchunge Mkapa

ban_tahariri.jpg

KAULI aliyoitoa Rais mstaafu, Benjamin Mkapa hivi karibuni kijijini kwake Masasi kuhusu tuhuma za ufisadi, kwa namna moja au nyingine zinaongeza idadi ya mitikisiko ndani ya Serikali ya Rais Jakaya Kikwete.
Madai ya Mkapa kwamba, anatuhumiwa kwa sababu tu ya kukataa kwake kuwapendelea baadhi ya watu waliotaka awape madaraka wakati akiwa rais, hayaingii akilini.
Kimsingi, hoja yake hiyo ya kuwageukia wengine na kuwanyoshea kidole, inaonyesha hulka ya siku zote ya Mkapa ya kuwapuuza na kuwadhalilisha watu wanaomnyoshea kidole yeye binafsi au baadhi ya waliokuwa wasaidizi wake.
Leo hii wakati akijua fika kwamba serikali imetangaza rasmi kuanza kumchunguza kutokana na kukabiliwa na tuhuma nzito za kutumia madaraka yake vibaya wakati akiwa Ikulu, ndipo anapoibuka na kutoa utetezi wa jumla jumla.
Kwa namna ya ajabu, badala ya kujibu hoja za msingi za namna anavyohusika katika mradi wa makaa ya mawe ya Kiwira au kuhusu Kampuni ya ANBEM, anaishia kutaja neno uongo kwa zaidi ya mara tatu kwa mfululizo.
Ukiyatafakari kwa makini maneno yake hayo, mara moja utaona dhahiri namna anavyojaribu kupotosha kwa lengo la kutafuta huruma ya wananchi ambao baadhi yao tayari wameshaanza kumwita fisadi.
Kwa upande wetu, kauli hiyo ya Mkapa inatukumbusha wajibu mmoja muhimu kwa serikali ambayo tayari imeshatangaza kumchunguza kiongozi huyo mstaafu.
Wito wetu kwa Kikwete ni kuwakumbusha tu kwamba utetezi huo wa awali wa Mkapa ambao yamkini unaweza ukafuatiwa na mwingine baada ya mwingine, haupaswi kuitoa nje ya mstari serikali kuendelea na uchunguzi wake.
Tunasema hivyo tukitambua kwamba, Mkapa anaweza akaifanya serikali ya sasa kuingia katika tanuri jingine la moto la kuyumba kama ilivyokwishatokea katika matukio mengine.
Kikwete anapaswa kutambua kuwa kuyumba huku kwa serikali ni dhahiri kumewapa watu kadhaa tukiwamo sisi, kusema bayana kuwa serikali imepwaya.
Tunaamini kuwa tangu aingie madarakani Desemba 21 mwaka 2005, akiwa mkuu wa dola, amejikuta akikabiliwa na mitikisiko mingi na isiyokwisha inayoiandama serikali yake.
Kikwete anatakiwa kufahamu kwamba, ingawa Mkapa sasa yuko nje ya serikali, kauli yake ya majuzi kwa namna moja au nyingine inainyoshea kidole serikali ya awamu ya nne.
Anaposema kwamba wanaomnyoshea kidole ni wale aliowanyima fursa wakati akiwa madarakani maana yake ni kwamba, hivi sasa watu hao wako serikalini na ndiyo maana wamepata mwanya wa kumtuhumu.
Kufikiria hivyo ni rahisi kabisa kwani, ni wazi kwamba kwa majibu yake ni kwamba walishindwa kufanya hivyo wakati wakiwa nje zama akiwa rais na sasa wanafanya hivyo wakiwa na mamlaka.
Ni ajabu kwamba anatoa tuhuma hizo tunazoziita za juu juu huku akijua kuwa miongoni mwa waliomtuhumu ni waandishi wa habari wasio wana CCM, wabunge kama Dk. Willibrod Slaa walio katika kambi ya upinzani, na Joseph Butiku mmoja wa viongozi wastaafu ambayo haiyumkiniki hakupata kufikiria kurudi serikalini baada ya kustaafu.
Kwa maneno rahisi, Mkapa ametoa majibu yasiyo ya kweli bali ameyatoa kwa malengo yake yakiwamo ya kuiyumbusha serikali kimsimamo, kuwayumbisha Watanzania na kutafuta huruma. Tunaamini iwapo kweli alikuwa akikusudia kuanza kujibu tuhuma hizo nzito dhidi yake basi angewaeleza Watanzania kwamba kumbukumbu za kiserikali zinazomtaja yeye na mkewe kuwa wamiliki wa kampuni ya Tanpower iliyonunua makaa ya Kiwira si za kweli bali ni za uongo. Alipaswa kuwaambia Watanzania kwamba, hakujapata kuwapo kwa kampuni yenye uhusiano na yeye iliyoundwa wakati akiwa Ikulu na ikapewa jina la Anbem na kumhusisha yeye moja kwa moja badala ya kubadili mwelekeo wa hoja za msingi.
 
Waraka mzito wa maaskofu kwa JK

na Kulwa Karedia

MAASKOFU wa makanisa kadhaa kupitia kile wanachokiita Ushirika wa Maaskofu Tanzania, wameandika waraka maalumu wenye ujumbe mkali na mzito kwa serikali, wakitaka kuchukuliwa kwa hatua kubwa ili kulinusuru taifa dhidi ya misukosuko linayokabiliana nayo.
Waraka huo wa maaskofu wanaofanya kazi chini ya uenyekiti wa mtu anayetajwa kuwa ni Askofu John Mwela, unaelezwa kuwa ni matokeo ya kikao cha pili cha kamati ya maaskofu hao kilichokutana Dodoma kwa siku nne kuanzia Mei 13 hadi 16 mwaka huu.
Kwa mujibu wa waraka huo wa maaskofu ambao Tanzania Daima imeusoma, pia kuchapwa katika baadhi ya magazeti jana, maaskofu hao wanaeleza kuguswa na matukio kadhaa wanayoyaelezea kuwa yaliyochangia kuliyumbisha taifa.
Miongoni mwa mambo yanayotajwa katika waraka huo wa kwanza wa aina yake, ni pamoja na ufisadi, mpasuko wa kisiasa Zanzibar, uwakilishi wa viti maalumu bungeni, migomo vyuoni na katika mashirika na tatizo la usafiri kwa wanafunzi wa mijini.
Wakirejea matukio ya siku za hivi karibuni, maaskofu hao wanasema kuwa yana sura nne, zikihusisha ubadhirifu wa fedha za Watanzania kupitia Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje katika Benki Kuu (EPA), Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge kuhusu Richmond, na kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na mawaziri wengine kadhaa.
Mawaziri waliojiuzulu wanaotajwa katika waraka huo ni pamoja na Dk. Ibrahim Msabaha, Nazir Karamagi na Andrew Chenge.
Maaskofu hao wanabainisha kuwa mwelekeo wa mambo hapa nchini unaonyesha kuwa serikali inahitaji msaada mkubwa katika kuweka hali sawa.
Wanasema kuwa matukio hayo ya ufisadi yamesababisha Watanzania wagawanyike katika makundi manne, ambayo hata hivyo hawataji chanzo chao cha utafiti kilichowawezesha kufikia katika mpangilio wao huo.
Kwa mtazamo wao, kundi linaloongoza ni lile linalojumuisha watu wanaofikia asilimia 60, wanaochukizwa na kuumizwa na viongozi na watu wachache waliojilimbikizia mali.
Kundi la pili wanalolitaja ni la watu wanaofikia asilimia 25, ambao wao ni wale wanaolia na kutoa hukumu yao kwa kulalamika wakiiona serikali kuwa iliyoshindwa kuwajibika.
Aidha, walilitaja kundi la tatu (asilimia 14.75) kuwa ni lile la watu wasioona shida yoyote, kwa maana wao wana kila kitu, huku kundi la nne na la mwisho likijumuisha watu wachache (asilimia 0.25) wanaomlilia Mungu aliponye taifa la Tanzania.
Kutokana na mambo hayo, maaskofu hao wanatamka kujifunga kuisaidia serikali na hususan Rais Kikwete, katika maeneo kadhaa, kwa kutoa ushauri katika masuala ya ufisadi, mabadiliko yanayohitajika katika kuandaa uchumi wenye nguvu, pamoja na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa 2010.
Aidha, ushauri wao huo unahusisha pia jinsi ya kufikia muafaka kati ya CCM na CUF huko Zanzibar, na kugusia njia ya kushughulikia migomo katika vyuo vikuu, mashirika ya umma na makampuni binafsi, pamoja na serikalini kwenyewe.
Kwa upande mwingine, wakati serikali imekuwa ikifikiria kuongeza idadi ya viti vya wabunge maalumu hadi kufikia asilimia 50 mwaka 2010, kwa lengo la kukuza ushiriki wa wanawake katika hatua za maamuzi, maaskofu hao wamelitaka Bunge kufuta mara moja sera ya uwakilishi bungeni kupitia utaratibu wa viti maalumu.
Kamati hiyo imesema iwapo Bunge halitachukua hatua hiyo, basi kanisa nalo litaomba viti saba vya uwakilishi, wakivigawa vitatu kwenda kwa makanisa ya kiprotestanti yaliyo chini ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), viwili Kanisa Katoliki chini ya TEC, na makanisa ya kipentekoste yapate kimoja na kimoja kingine kiende kwa makanisa yanayojitegemea.
Tamko la kamati hiyo, lililosainiwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Askofu Mwela na Katibu wake, Godfred Lema, linasema hatua yao hiyo imelenga kuboresha uwiano wa uwakilishi bungeni, tofauti na hali ilivyo sasa.
Katika hayo yote, maaskofu hao wamesema kuwa wapo tayari kusimama kidete kumsaidia Rais Jakaya Kikwete kutafuta suluhisho dhidi viongozi mafisadi ndani ya serikali.
Maaskofu hao wanasema wamejitoa kupambana na ufisadi kwa sababu hali hiyo imefika katika hatua mbaya, ambayo rais anapaswa kusaidiwa haraka, ili kupunguza hatari ya mgawanyiko ndani ya jamii.
“Tumekubaliana kusimama na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume na serikali zao kutafuta suluhisho la matukio haya, kwa sababu tunajua nchi ni ya Watanzania wa dini na rangi zote, hivyo sote tunawajibika mbele za Mungu kuitunza,” inasomeka sehemu ya waraka huo.
Wanasema kuwa wakati umefika kwa makanisa kujiingiza katika vita dhidi ya ufisadi, kwa sababu baadhi ya watu wanaoendeleza vitendo hivyo wamo ndani ya makanisa hayo.
“Wengi wa watu hawa wanaoitwa mafisadi wako katika makanisa yetu, hivyo tutatumia nguvu kutoka kwa Mungu ili kuwaumbua na kuwaongoza, kuwa mabadiliko haya yanahitajika katika kuandaa uchumi wenye nguvu,” inasomeka taarifa hiyo.
Sambamba na vita dhidi ya ufisadi, waraka huo unasema maaskofu hao wamekubaliana pia kushiriki kikamilifu katika maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Katika hili wanatoa ahadi ya kukutana na viongozi wa vyama vya siasa ili kushauriana kwa pamoja, mambo yanayohusu umoja wa kitaifa na masilahi yake. “Tutawaelekeza na kuwafundisha wale wanaowaongoza, umuhimu wa kutuunga mkono katika azima yetu. Tunaamini kwa kufanya hivi na kwa maelekezo haya sahihi ya Mungu, tutakuwa na umoja wa kitaifa, taifa lisilo na magonjwa kama vile malaria, ukimwi na vifo katika umri mdogo pamoja na kuondokana na umaskini na maisha duni,” inasomeka sehemu ya waraka huo. Katika sehemu moja ya waraka huo, maaskofu hao wanaandika kuwa wanasubiri kuundwa kwa kamati ya kudumu ya maaskofu, baada ya kufanyika kwa vikao vya makanisa yaliyo chini ya CCT, TEC na PCT.
 
Trully...Wasn't...Isn't by my self.
Thats for sure...

Slaa ataka Balali akamatwe

na Hellen Ngoromera

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa, alimtaka Kikwete kuamuru kukamatwa kwa Dalali na kuwekwa gerezani, hadi mahakama itakapotoa uamuzi kuhusu tuhuma za ubadhirifu wa fedha za serikali alizokutwa nazo.
Kwa upande mwingine, Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohamed, alisema kubainika kwa ubadhirifu ndani ya BoT kumedhihirisha kuwa maneno waliyoyasema wapinzani kuhusu suala hilo hayakuwa ya uzushi.
Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Dk. Slaa alisema hatua ya Rais Kikwete kutengua uteuzi wa Dk. Balali haitoshi.
Kwa mujibu wa Dk. Slaa, wakati walipoibua hoja hiyo, viongozi kadhaa wa serikali, waliwatukana na kusema inabidi sasa wasafishwe, kwani inaonekana walichokisema ni cha uhakika.
Aidha, alishangazwa na rais kuchukua muda mrefu kupata ukweli wa masuala hayo wakati wao walishayasema miezi minane iliyopita.
"Baada ya sisi kutoa hoja yetu rais alitutukana, aliwahi kusema kelele za mlango hazimnyimi mwenye nyumba usingizi…amechelewa kutoa majibu, hata hivyo hatua hiyo haitoshi, Balali amefanya kitu kibaya katika nchi na ni mwanzo wa matabaka.
"Mtu akiiba sh 5,000 anawekwa lupango hadi atakapopelekwa mahakamani na akiwa mgonjwa anakuwa chini ya ulinzi wa askari magereza kitandani lakini Balali anaachwa.
Nasisitiza akamatwe na kukaa gerezani hadi mahakama itakapotoa uamuzi wa suala lake, rais pia alitangazie taifa mara moja kukamatwa kwake kwa sababu pesa zilizoibwa ni zetu," alisema Dk. Slaa.
Akizungumzia kuhusu rais kuagiza Bodi ya Wakurugenzi ya BoT kukutana mara moja ili kujadili taarifa ya ukaguzi na kuchukua hatua zipasazo za kinidhamu dhidi ya maofisa wote wa benki walio chini ya mamlaka yake waliohusika na kusababisha hasara kwa taifa, Dk. Slaa alisisitiza kwa kumtaka rais kutowaachia watendaji wake kuchukua hatua dhidi ya Dk. Balali, bali yeye mwenyewe aelekeze hatua za kuchukua dhidi yake wka sababu ni yeye ndiye aliyemteua.
"Rais aelekeze hatua za kuchukua dhidi ya mapambano hayo ya wizi mkubwa, uzembe mkubwa na ubadhirifu mkubwa ambazo zimetokea, asijifiche kama mbuni, aelekeze hatua za kuchukua dhidi ya Dk. Balali," alisisitiza Dk. Slaa.
Alisema wamesubiri ukaguzi wa suala hilo kwa muda mrefu na matokeo yake kilichotolewa na serikali ni ukaguzi wa Hesabu za Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tu, ambayo alisema kuwa ni tone la maji katika bahari. Alimtaka rais kueleza fedha zilizochukuliwa katika kampuni mbalimbali ikiwemo Meremeta, Mwananchi Gold, Tan Gold na nyingine, zimekwenda wapi na zimetumikaje.
Akizungumzia kuhusu rais kumteua aliyekuwa Naibu Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu kuwa Gavana mpya wa BoT, Dk. Slaa alimpongeza na kumkaribisha BoT lakini alimtaka kutambua kuwa Benki Kuu ni chungu cha Watanzania wote, hivyo aitunze kama mboni ya jicho lake.
Kwa upande wake, Hamad Rashid aliipongeza hatua ya Rais Kikwete kufanya uamuzi huo.
Alimtaka Rais Kikwete kuyashughulikia maeneo mengine yasiyotajwa katika taarifa hiyo kama vile ujenzi wa Benki Kuu. Pia aliitaka serikali kutowabeza wapinzani, hasa wanapozungunza ndani ya Bunge kuhusu masuala mbalimbali, kwani wanachokuwa wanazungumza wanakuwa na uhakika nacho.
"Bunge ni chombo cha kutunga sheria, serikali isitubeze pale tunapozungumza jambo mahali pale, kwani sisi si watoto wadogo. Tunaomba pia ikitokea tumezungumza jambo tusiadhibiwe kabla uchunguzi haujakamilika," alisema.
Aliongeza kuwa kambi ya upinzani itaendelea kushirikiana na rais kufichua ufisadi, rushwa na ubadhirifu katika kusimamia matumizi mazuri ya rasilimali za nchi kama vile madini na nyinginezo.
Alimshauri rais kutafuta njia nyingine ya kushughulikia tatizo lililobainika kwa sababu kuna uwezekano mkubwa kuwa maagizo yake kwa vyombo kama Takukuru, Jeshi la Polisi na kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, yanaweza kuchukua muda mrefu kutekelezwa.
Pamoja na mambo mengine, kiongozi huyo wa kambi ya upinzani aliwataka wananchi kuwaunga mkono wapinzani kwa kuwaongezea nguvu za ziada ili kuwawezesha kufanya kazi kwa ari.
Ukaguzi huo wa hesabu katika akaunti ya malipo ya EPA ambao ulifanywa na wakaguzi wa Kampuni ya Ernst & Young kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, ulianza Septemba mwaka jana na kukamilika Desemba. Ripoti yake ilikabidhiwa kwa Rais Kikwete Januari 7, mwaka huu.
Katika taarifa hiyo, rais aliagiza Bodi ya Wakurugenzi ya BoT ikutane mara moja kujadili taarifa ya ukaguzi na kuchukua hatua zipasazo za kinidhamu dhidi ya maofisa wote wa benki hiyo walio chini ya mamlaka yake waliohusika na kusababisha hasara hiyo kwa taifa.
Aliamua pia shughuli za ulipaji wa madeni katika akaunti ya EPA zisimamishwe mara moja mpaka hapo taratibu za uhakiki na utaratibu mpya utakapotengenezwa. Rais pia amewaagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, kuchunguza na kuchukua hatua zipasazo za kisheria kwa makampuni na watu waliohusika na uhalifu huo. Amewataka pia wahakikishe fedha zilizolipwa isivyo halali zinarudishwa.
 
HII THREAD INAONYESHA WAZI KUWA KUNA BAADHI YA WANASIASA HUMO ccm AMBAO WANATAKA HAKI YA KISHERIA ICHUKUE MKONDO...Sasa sijui nini msimamo wao mara baada ya haya mambo ya kusafishana kuibuka humo chamani mwao!
Wanasiasa hao wanajua wazi kuwa sasa vita ya kukamata watuhumiwa ndani ya ccm haitawezekana tena!
 
Tulisha gawanyika siku nyingi na ndiyo maana CCM wameenda Dodoma kwenye NEC yao na kuamua kufa wote pamoja na kutuacha sisi huku .So are now 2 groups .
 
Tulisha gawanyika siku nyingi na ndiyo maana CCM wameenda Dodoma kwenye NEC yao na kuamua kufa wote pamoja na kutuacha sisi huku .So are now 2 groups .
Afadhali umesema wewe kiazi...Miye muhogo shida tupu.
Ila thread zote nilizoanzisha ni za kiutabiri unaoelekea kuwa wakweli...Hii thread niliiaanzisha kwasababu nilishasoma mipango yao ya mbele...Na mimi kwa uwezo wa Mungu nawazingira tu.
 
Muanzisha hii thread leo kaja na maada eti 'Lowassa angekuwa rais bora kabisa kuliko Magufuli'

muwe mnasimamia maamuzi na mitazamo yenu, mnakuwa na thamani zaidi

Fisadi anabaki kuwa fisadi haijalishi kaenda chama gani, yuko nje au jela, kama kaokoka na kujifanya malaika au la!!!

Fisadi ni identity hatakasikiki, wala kuosheka...wakiishafanya ufisadi kuna watu wanakufa kwa namna mbalimbali directly au indirectly! you can not reverse the damage done

Hata fisadi akaongea maneno matamu namna gani, au akaenda kukaa na watakatifu wa chadema! hata hawa watakatifu waliomuita kuja kunajisi ukuu wao bado haitamfanya fisadi kutakata!!

Vyama au mahali anapoenda na anapohamia havina mechanism ya kubadilisha moyo, damu na akili yake asiwe fisadi!

Lowassa ni fisadi sawa na walioko ccm, ambao for years wamejiwekea misingi ya unyonyaji, kuwa na biashara nzito na hawakutumika

Infact kisiasa Lowasa ni chadema, mirija, moyo na base zake zote za kupata hela ziko CCM inajulikana,

Lowasa na hao akina kikwete, mkapa, mwinyi , karamagi n.k wana biashara mbalimbali ambazo wako share

Leo anapokuja mwanachadema anatoa povu kana kwamba Lowasa alikufa akafufuka na akasahau na kuacha mambo yake ya kale unamwonea huruma!!

anapokuja ny.umb.u mmoja na kusema mbona hauyuko gerezani unacheka, kwani nani aliyesema ccm wasafi? hawa wote lao moja!!!!

endeleeni kusaga lami na ndala zenu zilizoisha

Lowasa kuwa Fisadi ni SI Unit, ni kama kuku KFC, au football barcelona, ni sawa na dhahabu barrick au ubongo wa lissu na sheria, Lowasa na ufisadi ni inseparable!!

Mengine yote semeni ila mtu huyu anapendeza sana kwa ID yake ya fisadi, imemvaa
 
Back
Top Bottom