Mafisadi Waachiwe!

Lusajo

JF-Expert Member
Feb 25, 2008
456
30
--------------------------------------------------------------------------------
(Mod's naomba muiache/muipe muda kabla ya kuichanganya na nyingine)
Nimeona niandike hii hapa inaweza kuwa njia ambayo itakuwa ni win win situation kati ya mafisadi (Wahujumu uchumi) na wananchi wa nchi niipendayo Tanzania. Mafisadi waachiwe/ wapewe adhabu ndogo.

Nimetoka kuangalia movie ya American Gangster ambayo muigizaji wake Frank Lucas (Denzel Washington) aliambiwa the only way atapata adhabu ndogo ya kifungo chake ni (ku-snitch) kutaja mali zake zoote popote pale zilipo, na pia kutaja pesa zake zoote popote pale zilipo duniani, akidanganya na asipotaja mali/cash zake zoote hata senti tano atakaa jela maisha yake yoote na pia akificha kutowaambia kuhusu mtu yeyote waliohusika naye kwenye deals alizokuwa akifanya na hapo pia hata kaa kuliona jua (Yaani atafungwa maisha.

Sasa nilichoona ni kwamba sidhani kama mafisadi (wahujumu uchumi) wanapenda kufungwa miaka mingi au hata kwenda jela, kwa hiyo Raisi/DPP/UWT/____ na wengine walioanza hii vita dhidi ya hao watu wakate nao dili kwamba mafisadi (wahujumu Uchumi) waredishe mali/pesa zoote labda waachiwe nyumba waliyokuwa nayo zamani hata 1 (warudisha nyumba na hela zoote ndani na nje ya Tanzania) yaani pesa/mali zoote bila kukosea hata moja, na ikigundulika kwamba kadanganya ndio adhabu yake iwe kali sana. Na hiyo dili ya kurudisha mali pia wahusishwe na ndugu zao woote waliofaidika na ufisadi, maana nimesikia wengine wajukuu zao wana mabilioni kwenye akaunti (sasa sijui wanakoishi miti inazaa mela?) na wengine wamewapa ndugu zao deals ambazo mishahara wanayolipwa ni ya ajabu kwenye nchi ambayo inaitwa masikini na iko "dunia ya tatu".

Na majengo pia yarudishwe kwa sababu hela waliyoiba ndio imewapa faida ya kuweza kununua hivyo vitu kwa hiyo mtu yeyote atakayekubaliana na hayo masharti ndio apewe miezi/miaka kadhaa Keko au aachiwe kutokana na makosa yake (kwa sababu hawakufanya ujambazi wa kushika silaha, kwamba wanaweza kuua mtu wakitoka) ingawa wamesababisha matatizo kwa njia moja au nyingine na pia wapewe probation ya kutokutoka nje ya nchi pamoja na kujihusisha na mambo fulani kwa muda fulani.

NB:
  1. Haya ni mawazo yangu tuu wanajamii mnaweza kuyakubali/kuyapinga/kuongezea au kupunguza kitu chochote unavyoona ni fit kwenye hili suala kwa sababu cha muhimu ni fedha/mali zirudi na hivyo vitu ndivyo vitakuwa njia nzuri ya kunegotiate nao, kwa sababu kuna maana gani kuwafunga miaka mingi na hela/mali yenyewe isiwe imerudishwa kwa ajili ya maendeleo ya wa-Tanzania?.
  2. Kama utaona nimetumia neno (Wahujumu wa Uchumi) kwenye mafisadi ili kosa lao lionekane ni kubwa zaidi ya sasa hivi wanavyoitwa mafisadi na nadhani adhabu ya muhujumu uchumi ni kubwa na kuna watu walisema haina mdhamana (yaani ukikaa ndani utakaa tu mpaka kesi iishe) tofauti na fisadi (whwrever this fisadi is!) =Thanks to Mzee Mwanakijiji on this one.
 
wazo zuri, ila wanatumia majina ya babu zao, wadogo za kzi kweli kweli,

nadhani tuzuie tu hela kwenda nje, maana hazimfaidishi mtanzania yeyote yule!

ndiyo hizo hizo zinarudi kwa jina la wawekezaji!
 
...prosecutors wengi wa States wanapenda kukata deals za namna hii na mara nyingi zina work kwa kuua mtandao na ku recover wanachotaka,maana sometimes haisaidii kumfungia mtu jela bora kupata ulichopoteza na kusambaratisha mtandao wa uhalifu....mara nyingi ,drugdealers,wallstreet,whitecollar criminals wanasambaratishwa kwa style hii,hata mafia walimalizwa kwa style hii...nafikiri inaweza kufanya kazi vizuri bongo lakini sijui watakohusika wataelewa seriousness ya hii kitu na kuanza kudanganya maana sijui kama wataamini na promise zitakuwa kept,honesty bado ni issue hata kwenye system,wengine watafikiri ni mitego tuu ya kuwaweka jela maisha na kutaifisha mali na maofisa wetu wanaweza wasi keep promise na kuwalinda waliosaidia...tujaribu lakini.
 
Saxby Chambliss............
 
Nadhani itakua vizuri kuwafunga na kuchukua malzoe ambazo zimepatikana kutokana na ufisadi huu. Nadhani kwa watu walosoma sheria kuna hukumu zinazo tolewa ili iwe mfano kwa watu wengine. Nadhani hili linahitajika sana sasa hivi. Kitu wanacho weza kupewa labda ni kupunguziwa hukumu kidogo labda iwe ya miaka nane hivi! Ila swala lakusema etiwarudishe tu pesa halafu waendezao, Hell NO!!! This is too much for African countries. Tuna mali nyingi sana na misaada minisana Tanzania nadhani kuliko nchi nyingine yeyote barani Afrika na bado masikini!!! Hiliswala linaniuma sana!!!
 
Mafisadi hawa watadanganya tu. Wanaijua Tanzania na uzembe wetu wa kutokufuatilia mambo kwa undani. Hebu angalia Mramba; nyumba yake moja yenye thamani kubwa sana (bilioni na ushee) imeandikishwa kwa jina la mtu mwingine kabisa. Bila soo la mahakama, hakuna mtu mwingine ambaye angejua kuwa ni ya Mramba.
 
Tatizo ni kuwa mazingira ya American Gangstar ni tofauti kidogo na mazingira halisi ya tanzania leo hii, achilia mbali mazingira ya Marekani. Yapo mambo yanayooneshwa kwenye hii filamu ambayo hapa Tanzania ni ndoto. Kikubwa ni kuwa wakati wamarekani ni honesty, sisi hapa ni waongo kupindukia, hvyo sidhani kama kuna atakayekubaliana na deal ya aina yoyote utakayomtajia
 
Deals? Why deals? Thats why we have DPPs and PCCB. We dont need no deals with these bastards. Jela watakwenda na fedha zetu watarudisha. Thats the best deal they will ever get.

Unajua hapa unapaswa kutofautisha mwizi anayeiba au anayefanya drug deals kama kwenye American Gangster bila kujulikana anapataje hela au anafanya deals gani, umtofautishe na mtu anayetumia madaraka vibaya na kuiba kodi za wavuja jasho. Mbinu wanazotumia viongozi wa serikali kuiba zinafahamika. Mbinu alizotumia Yona na Mramba kuiba zilikuwa zinafahamika hata kabla hawajatekeleza wizi wenyewe. Suala la Alex Stewart liliandikwa na kupigiwa kelele na wananchi. Suala la radar na ndege ya rais vilipigiwa kelele na wananchi wote. Hakuna kipya hapa. Hawa jamaa walikuwa wanatumia ubabe tu kuwaibia watanzania.

Why should we give em deals? Wizi mtupu!
 
Ndio maana niliandika kwamba inaweza kusaidia ili pesa/mali irudishwe, kwa sababu mali zao ndio zitakuwa dhamana yao na wakidanganya inaweza kugundulika kwa sababu sio kwamba UWT haijui jinsi mambo yanavyofanyika na ndugu zao hawajulikani, na hata kama hawatarudisha zoote hata wakirudisha zaidi ya asilimia sabini (70%) itakuwa ni afadhalii
 
Back
Top Bottom