Mafisadi vs wapiganaji

Should Seleli and Shelukindo divert to Chadema


  • Total voters
    49
  • Poll closed .

Geza Ulole

JF-Expert Member
Oct 31, 2009
59,185
79,366
Kutokana na tabia iliyojitokeza hivi karibuni wananchi kurubuniwa na fedha na kutowapigia kura wazalendo wa nchi hii wenye kusimamia maslahi ya walala hoi. Je mnaonaje kuhusu hii poll naomba tushirikiane kuwahimiza wapiganaji Seleli na Shelukindo waingie Chadema! Tunaweza sasa! Wapeni moyo wapiganaji, hebu fikiria Bunge linalokuja litakuwaje? kuna mtu atathubutu kukemea CCM ilhali ni Mbunge wa CCM? Hivi hii nchi inaenda wapi? Inahitajika busara ya wapiga kura kufahamu mustakabali wa nchi hii! Mbaya ni kwamba wana Kyela (wapiga kura wenye msimamo) wako wachache sana katika nchi hii! Shime jamani we need these people! Wakina Shibuda, Lembeli, Mpendazoe, Kimaro, Seleli, Shelukindo, Mwakyembe na Zitto ni muhimu wakati woote Bungeni kwa vile wamebarikiwa! How can a spoon-fed January Makamba beat Shelukindo? Hizo ni fitna jamani ni fitna za EL na RA! Jamani hii nchi haina wenyewe? by the way Mwakyembe unafanya nini CCM? au mtu wa usalama wewe? angalia nyakati safari hii watakuondoa kabisa hapa Duniani last time walikukosakosa, ukiongea tu bunge lijalo baba tutakusahau!

NOTE: halafu naomba moderator abadili neno save to serve! si unajua mambo ya kwenda shule za kata ungeli unanipiga chenga na neno representativeness to seats
 
Wanajamvi JF, tuunge mkono hiyo hoja pia tuwashawishe CHADEMA wampe Mpiganaji Mpendazoe, tiketi ya Jimbo la Segerea ili apambane na wakala wa Mafisadi Makongoro tuone kama mafisadi watafua dafu kwetu,
 
Wabaki hukohuko Deep Green hatuwataki:A S angry:
kaka siasa ni ku-reach out! It takes compromise watu kama wakina Mpendazoe, Kimaro, Seleli, Shelukindo, Mwakyembe, Zitto wanahitajika sana bungeni no matter what party they are! Hoja zao ni busara kubwa katika integrity ya serikali hii katika nchi hii ya Wadanganyika
 
We need them, for sure we need these guys kuongeza nguvu zaidi ili tuweze kuikomboa nchi toka kwa mafisadi. Tunazidiwa na nchi kibao sasa ambazo sisi tumezipa uhuru.

Sasa ni muda wa kufanya maamuzi magumu na yenye busara tosha kwa akina Shelukindo! wasisubiri mpaka jua lianze kuzama ndo waanze kutafuta kuni. Mapambano yaendelee, Selelii, Shelukindo, Shibuda, Kimaro hata mzee six njooni Chadema tumalizie kazi october.
 
Wanajamvi JF, tuunge mkono hiyo hoja pia tuwashawishe CHADEMA wampe Mpiganaji Mpendazoe, tiketi ya Jimbo la Segerea ili apambane na wakala wa Mafisadi Makongoro tuone kama mafisadi watafua dafu kwetu,


Kura ndio demokrasia ya kweli, hatuwezi kufanya hivyo CHADEMA. Ukishindwa kwa kura halali inabidi kukubali matokeo. Hatuchezi cheusi chekundu kama ndugu zetu Mafisadi CCM
 
Watoke huko waje Chadema na wengine pia il lile neno la Mwalimu kuwa upinzani wa kweli utatoka ndai ya CCM litimie. wasiogope maana kuogopa ni kusaliti maendeleo ya nchi yao. ni lazima kuwe na upinzani wenye nguvu. Wake up Tanzanians!
 
Minda acha kukata tamaa, vita bado mbichi kabisa, mapambano ndio yanaanza, vita ni vita tu!!
 
ndiyo, ,fisadi walishachukua nchi. Tunachotakiwa kufanya sasa ni kuwanyang'anya (kuirudisha nchi mikononi mwa watanzania!
 
kwenda chadema haiwezi kuwa suluhisho la muda mrefu...

maana hata kama wanarudi bungeni...wataishia kupiga domo tu mwisho kura zikipigwa CCM watashinda na miswada kupita kama kawa..

mi nadhani hawa jamaa wanaweza kuwa vocal sana tu kama watajiunga na asasi za kiraia na kupambana kutokea uraiani kwani tunahitaji watu wenye first hand experience ya uozo wa kwenye system kusaidia kwenye hizo asasi kimawazo nk...

lakini maamuzi yanabaki kwao...kweli wanataka kuwatumikia watanzania?????? au ni geresha tu kwa vile hawakuwa kambi ya lowasa???????
 
waje chadema.kama wabunge wachache waliokuwepo bunge lililopita waliweza kuitetemesha serikali je wakiwa mara mbili yake,si nchi itanyooka.hakuna kulala mpaka kieleweke.
 
..hivi kuna mtu bado anaota njozi kwamba kuna wapiganaji ndani ya CCM?

..Spika Sitta mliyedai ni kiongozi wa wapiganaji ndiyo huyo kajijengea Ofisi ya mamilioni ya fedha utadhani atakufa akiwa Spika.

..hivi mpiganaji wa kweli anayetetea maslahi ya walalahoi wa Tz anaweza kuwa anapenda makuu kama "mpiganaji" Samuel Sitta?
 
Inasikitisha kuwahimiza wapiganaji SELELI na SHELUKINDO, waingie chadema. Hata wakiingia chadema ni sawasawa wameruka mkojo wamekanyaga mavi, sii hoja kupiga kelele bungeni wakati kwenye majimbo yao wananchi hawawataki. Hakuna maendeleo yeyote walio leta zaidi ya kutafuta mtaji wa kisiasasa na kujitafutia umaarufu ili wananchi wawaonee huruma yakurudi majimboni, hizo nizilikua kelele tuu. Hata viongozi wa chadema ni mafisadi tuu, ufisadi upo kuanzia kwenye ukabila, mgao wa fedha za ruzukuu kwenye majimbo zote huliwa na FREEMAN MBOWE na DR.SLAA huku wengine wakisingizia wamekikopesha chama. Tatizo la nchi zetu za africa ufisadi nikitu cha kawaida, hata wewe tukikukabidhi urais ni yaleyale. Halafu mmekalia majungu na unafiki ya kusema watu wengine, kila kitu EL na RA!!! Mbona hamuwataji kina nyangumi??? Nchi hii inawenyewe na wananchi ndio wapiga kura na kuhusu MWAKYEMBE hii ni nchi ya amani, hakuna mtu atakayemuondoa mwenzake na wala hakuna aliyemkosakosa, huo ni ulikua unafiki wake wakujitafutia umaarufu na wapumbavu wakaamini.
 
Mimi nashangaa, NYINYI HAMNA KAZI YAKUFANYA??? Hakuna hadithi zingine zaidi ya ufisadi? Kilakukicha hadithi ni zilezile, hao mafisadi mnaowasema wamechukua nchi, mnataka nchi hii wakabidhiwe mafisimaji? Kwasababu kama serikali imechukuliwa na mafisadi hao mafisi maji mnaowataka wawekwe nchi hii siitakwisha kabisa! Mpaka wajaze matumbo yao sisi tutakua tumekufa, kila mtu anauchungu na nchi hii, nawapiga kura ndio wenye kuamua, mimi na wewe hatuna amri yakufanya chochote, nchi ni ya wa TANZANIA
 
Chakufurahisha zaidi ni kwamba wabunge hawa wametupwa nje, kwanza hawakubaliki kwenye majimbo yao, wameangushwa kwenye kura za maoni, na si ajabu kwa SHELUKINDO kuangushwa na JANUARY MAKAMBA, kwani shelukindo kawa nani? Kama hakufanya maendeleo kwenye jimbo lake, mlitegemea wananchi watamchagua? Msimpambe mtu amaye hakubaliki na msijifanye mnajua wakati hamjui, mzee kama SHELUKINDO ameshapitwa na wakati, hana jipya mshaurini avae kikoi na alee wajukuu nyumbani.
 
Kupambana na ufisadi ni jukumu la watu wote, hata hawa walioanzisha kupambana na ufisadi, wote ni wa CCM, lakini kupambana na ufisadi lazima mwenyewe uwe msafi. Hata hao wanafiki wa upinzani wamedandia hoja tuu. Kuna mkubwa wao fisadi mkubwa SAMWEL SITTA kajenga ofisi ya mamilioni ya fedha utadhani atakua spika milele. Kajikodishia nyumba ya mamilioni ya hela. Na kujinunulia ma fenicha ya mamilioni, je huo sio ufisadi??? Halafu mtu kama huyo anajiita mpiganaji wa ufisadi, kweli mtu kama huyo anatetea maslahi ya walalahoi watanzania? Kwakweli huyo mtu ni hatari, na ni mnafiki mkubwa.
 
Back
Top Bottom