Mafisadi CCM sasa wakalia kuti kavu; JK alikwepa mtafaruku, kupisha upepo mbaya

Muda ulishafika siku nyingi. Tatizo ni kukosekana mwenyekiti makini na mwenye ujasiri wa kutoa maamuzi magumu, siyo huyu ambaye naye ananuka ufisadi kuliko hata watuhumiwa.

Rais msanii mwenye uwezo wa kuigiza jinsi ya kukasirika na kucheka kwa wakati mmoja.

 
nape mbona kimya, mbona hajatuletea maamuzi ya nec ya ccm maake alisema ndiye source. Au wamemvua/amejitoa/amezira
reginamduma wewe ni mchokozi, swali lako ni wazi umeamua kumkebehi nape, uyu dogo hakuwajua kuwa ccm magamba walimgeuza kond...........m, maana alikuwa na thamani sana alipokuwa akitumiwa na sasa yeye na chiligati wanajiandaa kwenda kujibu tuhuma za kumchafua lowasa (richmond) na pia chenge, mzee visenti ktk kamati yao ya ati ya nidhamu, sjui ni nani ananidhamu uko ccm, duh vibaka kwa usanii, watajiju na tabia zao za wizi, hawa wezi tu, na ccm wakidondoka ndo watajua vibaka huwa wanafanywaje uswahilini, log off
 
Nape mbona kimya, mbona hajatuletea maamuzi ya NEC ya CCM maake alisema ndiye source. au wamemvua/amejitoa/amezira

Naskia yuko arusha anapiga kampeni za chini kwa chini ili magamba waweze kuibuka kidedea kwenye zile kata zilizoachwa wazi baada ya madiwani wake kutemwa na chadema na nasikia ana ulinzi wa wa hali ya juu unaosimamiwa na kamanda wa polisi wilaya bwana zuberi,makamanda mlioko arusha tujuzeni
 
Bila wananchi kuingia barabarani,tutaendelea kudhalauliwa na kuonekana wasindikizaji wa mafisadi katika nchi hii.
 
28 NOVEMBER 2011



*Mkakati wa kuwamaliza kidiplomasia yatajwa
*JK alikwepa mtafaruku,kupisha upepo mbaya


Na Mwandishi Wetu

SIKU tatu baada ya kumalizika kwa vikao vya juu vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma wiki iliyopita, upepo mbaya umeanza
kuwaelekea watuhumiwa wa ufisadia ndani ya chama hicho wanaotakiwa kujivua magamba kwa kutafakari wenyewe tuhuma zao kabla ya kuondolewa kwa nguvu.

Hali hiyo inatokana na siri nzito kutoka ndani ya vikao hivyo kueleza kuwa mbinu iliyotumiwa na Mwenyekiti wa chama hicho Rais Jakaya Kikwete, kurudisha suala hilo kuamuliwa na Kamati ya Maadili kisha kuwasilisha maamuzi yake kwa Kamati Kuu unalenga kuwamaliza kabisa watuhumiwa hao.

Imeelezwa kuwa syahili hiyo mpya iliyotumika mjini Dodoma haikulenga kufuta mchakato wa kuwaondoa watuhumiwa haoa kama ilivyodaiwa bali ulilenga kuepusha malumbano ndani ya kikao baada ya kubainika kundi hilo kuandaa watu wao kuwatetea kwanguvu kubwa na kuwa tayari hata kuchafua hali ya hewa.

Taarifa zilizoifikia Majira juzi na jana, vinaeleza kuwa baada ya kundi hilo kudaiwa kuwa na wafuasi wengi ndani ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), washauri wa masuala ya kisiasa ndani ya CCM walitaka Kamati ya Maadili imalize suala hilo kukwepa mjadala mzito kutokana na wahusika kuwa na kundi kubwa la kuwatetea.

"Kilichotakiwa watu waelewe tangu mwanzo ni kwamba CCM kama chama ni wajanja kuliko kundi la mafisadi, wale jamaa walijiandaa na wana wafuasi na kundi kubwa ndani ya NEC, kuwamaliza mle ni tatizo kubwa.

"Njia pekee wa kuwamaliza ni kuwaachia Kamati ya Maadili ambako mle kuna wajumbe wachache na wenye msimamo thabiti na wanaoijua vizuri chama, kama mnafikiri kujivua gamba imefikia mwisho subirini mtaona matokeo, Kamati inakwenda kumaliza kila kitu,"kilisema chanzo chetu.

Taarifa hizo zilieleza kuwa Rais Kikwete baada ya kuona hali halisi na kupewa taarifa za siri za jinsi kundi hilo ilivyojipanga kupambana kufa na kupona alishauriwa na wakongwe mbalimbali wa kisiasa kumaliza suala hilo kwa njia ya diplomasia na kwamba hakuna atayelaumiwa.

"Kamati ya Maadili ikishamaliza itawasilisha maamuzi yake ambayo kwa lugha ya diplomasia ya chama huitwa mapendekezo, Kamati Kuu itabariki maamuzi hayo na hapo ndio mwisho wa hatua hiyo watafuata wengine," kilisema chanzo chetu ndani ya CCM.

Majira ilipomtafuta Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Bw. Nape Nnauye, kuthubitisha taarifa hizo alisema yupo kwenye kikao na kuahidi kutoa ufafanuzi baada ya kumaliza. Hata hivyo hadi tunakwenda mtamboni kiongozi huyo hakuweza kuzungumzia suala hilo kwa maeleoz kuwa bado anaendelea na kikao.

Wajumbe wa Kamati ya Maadili ya CCM ni Mwenyekiti wa Taif Rais Jakaya Kikwete, Makamu Bara Bw. Pius Msekwa, Amani Karume, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balosi Seif Iddi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Katibu Mkuu Wilson Mukama, Naibu Katibu Mkuu Bara Bw. John Chiligati, Vuai Ali Vuai.


Kwa mujibu wa taratibu za CCM Kamati ya Maadili inaweza kuchukua hatua moja kwa moja au kutoa mapendekezo kwa Kamati Kuu (CC) ambayo pia wajumbe wake karibu wote wanaingia pia kuyabariki.

Katika kikao cha NEC cha wiki iliyopita Waziri Mkuu aliyejizulu Bw. Edward Lowassa, alilalamika kuchafuliwa huku Waziri Mkuu Mstaafu Bw. Frederick Sumate, alitaka majibu ya sababu zinazofanya wanaochafua Bw. Lowassa kutochukuliwa hatua kama hana kosa.

Suala la kujivua gamba ndani ya CCM imeleta mwamko mpya wa kimtazama ndani ya CCM huku kundi moja linalojipambanua kuwa na msimamo wa kimaadili ikielezwa kuusimami na upande wa pili ukieleza kuwa ni mchakato unaokivuruga chama hicho kwa madai kuwa hakuna ushaidi wa magamba yanayotakiwa kuvuliwa.



Mimi tokea juzi nawaambia vijana humu ndani lowassa kishaelekezwa kibla kwa kamati kuu kufanikiwa kupata kibali cha nec suala hilo likamalizwe cc,watu wamekazania kushangilia "lowasa kasema alipiga simu" "lowasa kasema alipiga simu!",hivi mnafikiri jk alikua mjinga kuivunjilia mbali kamati kuu ile ya mwanzo na kuunda mpya?!!!angalieni kwenye kamati kuu mpya mle mtu wa lowassa ukiacha anna makinda ambae hata hivyo hatabiriki ni nani?
Lowassa is a disaster na wazee wa ccm akiwemo mkapa na mwinyi wameshauri awekwe kando kwa maslahi ya taifa,suala la ushahidi kwenye vikao vya chama huwa halipo zaidi huwa zinatumika taarifa za "kiintelijensia" ambazo lowassa alikua akilia lia siku ile kumkumbusha jk kwamba mkapa angsikiliza taarifa za kiintelijensia jk asingekuwa amekaa pale kwenye kile kiti siku ile hivyo na yeye alikua kama anambembeleza jk akumbuke kumuonea huruma kwa kuzipuuza taarifa za "kiintelijensia" lakini bahati mbaya jazba ikamshika akafika mbali zaidi kwa kumtishia mwenyekiti na simu aliyopiga!hapo ndio alipokoroga mambo zaidi na wafuasi wake wa karibu toka siku ile kwenye vikao vyao wamekua wakimlaumu kwa hilo na kumwambia litamgharimu zaidi!

sasa haya magazeti ambayo wahariri wake wamekuwa wakilipwa mishahara na lowassa apart from mishahara ya waajiri wao kila mwezi yanang'ang'aniza tuamini eti lowassa aliibuka kidedea kwa kusema alipiga simu tu na bahati mbaya watz wengi maisha yetu yanaendeshwa na magazeti tokea hawa jamaa wa mtandao waichukue hii nchi basi kila mtu lowassa msafi lowasa msafi kasafishwa na sabuni gani mpaka atakate ghafla kiasi hicho!
 
......mkuu, upepo ni huu huu, leo na kesho, kama ni mbaya utaendelea kuwa hivyo na kama ni mzuri basi ni kinyume chake!!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom