Mafisadi CCM sasa wakalia kuti kavu; JK alikwepa mtafaruku, kupisha upepo mbaya

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
28 NOVEMBER 2011

Mkakati wa kuwamaliza kidiplomasia yatajwa

JK alikwepa mtafaruku,kupisha upepo mbaya

Na Mwandishi Wetu

SIKU tatu baada ya kumalizika kwa vikao vya juu vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma wiki iliyopita, upepo mbaya umeanza kuwaelekea watuhumiwa wa ufisadia ndani ya chama hicho wanaotakiwa kujivua magamba kwa kutafakari wenyewe tuhuma zao kabla ya kuondolewa kwa nguvu.

Hali hiyo inatokana na siri nzito kutoka ndani ya vikao hivyo kueleza kuwa mbinu iliyotumiwa na Mwenyekiti wa chama hicho Rais Jakaya Kikwete, kurudisha suala hilo kuamuliwa na Kamati ya Maadili kisha kuwasilisha maamuzi yake kwa Kamati Kuu unalenga kuwamaliza kabisa watuhumiwa hao.

Imeelezwa kuwa syahili hiyo mpya iliyotumika mjini Dodoma haikulenga kufuta mchakato wa kuwaondoa watuhumiwa haoa kama ilivyodaiwa bali ulilenga kuepusha malumbano ndani ya kikao baada ya kubainika kundi hilo kuandaa watu wao kuwatetea kwanguvu kubwa na kuwa tayari hata kuchafua hali ya hewa.

Taarifa zilizoifikia Majira juzi na jana, vinaeleza kuwa baada ya kundi hilo kudaiwa kuwa na wafuasi wengi ndani ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), washauri wa masuala ya kisiasa ndani ya CCM walitaka Kamati ya Maadili imalize suala hilo kukwepa mjadala mzito kutokana na wahusika kuwa na kundi kubwa la kuwatetea.

"Kilichotakiwa watu waelewe tangu mwanzo ni kwamba CCM kama chama ni wajanja kuliko kundi la mafisadi, wale jamaa walijiandaa na wana wafuasi na kundi kubwa ndani ya NEC, kuwamaliza mle ni tatizo kubwa.

"Njia pekee wa kuwamaliza ni kuwaachia Kamati ya Maadili ambako mle kuna wajumbe wachache na wenye msimamo thabiti na wanaoijua vizuri chama, kama mnafikiri kujivua gamba imefikia mwisho subirini mtaona matokeo, Kamati inakwenda kumaliza kila kitu,"kilisema chanzo chetu.

Taarifa hizo zilieleza kuwa Rais Kikwete baada ya kuona hali halisi na kupewa taarifa za siri za jinsi kundi hilo ilivyojipanga kupambana kufa na kupona alishauriwa na wakongwe mbalimbali wa kisiasa kumaliza suala hilo kwa njia ya diplomasia na kwamba hakuna atayelaumiwa.

"Kamati ya Maadili ikishamaliza itawasilisha maamuzi yake ambayo kwa lugha ya diplomasia ya chama huitwa mapendekezo, Kamati Kuu itabariki maamuzi hayo na hapo ndio mwisho wa hatua hiyo watafuata wengine," kilisema chanzo chetu ndani ya CCM.

Majira ilipomtafuta Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Bw. Nape Nnauye, kuthubitisha taarifa hizo alisema yupo kwenye kikao na kuahidi kutoa ufafanuzi baada ya kumaliza. Hata hivyo hadi tunakwenda mtamboni kiongozi huyo hakuweza kuzungumzia suala hilo kwa maeleoz kuwa bado anaendelea na kikao.

Wajumbe wa Kamati ya Maadili ya CCM ni Mwenyekiti wa Taif Rais Jakaya Kikwete, Makamu Bara Bw. Pius Msekwa, Amani Karume, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balosi Seif Iddi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Katibu Mkuu Wilson Mukama, Naibu Katibu Mkuu Bara Bw. John Chiligati, Vuai Ali Vuai.


Kwa mujibu wa taratibu za CCM Kamati ya Maadili inaweza kuchukua hatua moja kwa moja au kutoa mapendekezo kwa Kamati Kuu (CC) ambayo pia wajumbe wake karibu wote wanaingia pia kuyabariki.

Katika kikao cha NEC cha wiki iliyopita Waziri Mkuu aliyejizulu Bw. Edward Lowassa, alilalamika kuchafuliwa huku Waziri Mkuu Mstaafu Bw. Frederick Sumate, alitaka majibu ya sababu zinazofanya wanaochafua Bw. Lowassa kutochukuliwa hatua kama hana kosa.

Suala la kujivua gamba ndani ya CCM imeleta mwamko mpya wa kimtazama ndani ya CCM huku kundi moja linalojipambanua kuwa na msimamo wa kimaadili ikielezwa kuusimami na upande wa pili ukieleza kuwa ni mchakato unaokivuruga chama hicho kwa madai kuwa hakuna ushaidi wa magamba yanayotakiwa kuvuliwa.
 
Andrew Chenge siyo mjumbe wa kamati ya maadili? Atajihukumu mwenyewe?
 
hakuna lolote hapa kiboko yao chadema tu. mwambie mtu ukweli ili umuweke huru.
 
Hivi hii picha<ya kujivua gamba>mbona imekuwa ndefu kama isidingo?Haina mwisho?
 
Nape mbona kimya, mbona hajatuletea maamuzi ya NEC ya CCM maake alisema ndiye source. au wamemvua/amejitoa/amezira
 
Hatua za nidhamu sasa kumgeukia Nape. EL & Chenge watasafishwa watakuwa wasafiiiiiiiiiiiiiiiii (ndani ya CCM)
Hiyo ndio CCM, Nape simwoni sikuizi JF...


Il Gambino.
 
Porojo hizi jamani zimechosha...tuanze porojo za waluguru walima viazi, wakaguru walima mahindi, wahehe walima mahindi etc
 
Hiyo ni ZE COMEDI TU,hakuna mwenye uwezo wa kumhukumu mwenzie,na mfano hai ni hivi juzi wakati kikao kikiendelea,EL amenukuliwa akimwambia JK juu ya tuhuma zake zilizotaka kuibuliwa na kina D.Mwakawago na JK kuokolewa na uncle Ben na akakumbusha kuwa aliwahi kumwambia kuvunja mkataba wa Richmond bado JK alikataa,sasa kwa hayo tuliyoyasikia na mengine ambayo bado yamefunikwa kuhusu JK na wengineo,mnadhani ni nani anaweza kuibuka na kumhukumu mwenzake?

Hiyo ni sawa na FUTUHI au OK(original komedi).CCM ni ya kusafishwa na wananchi pindi waliowengi watakapobaini uchafu wa chama hiki na ufisadi inaoulea kila siku bila kujali unavyoitafuna nchi katika kila sector.
 
Kwa style hii du Patamu,Kama Movie hii ikichezwa na vyema,na hakika CCM watajipanua kuanza kuaminika tena kuwa kumbe hakuna Mwanachama aliyejuu kuliko chama.Ili waanzie hapo kutambua kuwa Wananchi siku hizi wanjua nazi ni nazi na sio kuwa nazi ni dafu.

Wasieneshe tena michezo ya kutizama upepo wa Wananchi utesemaje waendeshe chama chao kwa misingi ya HAKI NA UKWELI NA SIO MAIGIZO.

Zama za kirusi [Putin] kwa Tanzania zimekwisha zamani,siasa za wazee wa zamani waliosoma Russia [USSR] na China,siasa za baadhi ya Watu wachache ndani ya Nchi kuunda kakindu cha Watu wachache na kujiita wao ndio Nchi na kila kitu wao ndio wanajua hayo yanafanyika huko Russia na China,na sio Tanzania.

Nyerere kama Muungwana alikopi kweli baadhi ya mifumo ya uko lakini alipoona baadhi ya mikakati yake inapingana na utu wa binadamu akaachana nayo.Kama Mwalimu Nyerere angengania basi leo Tanzania angeitawala mpaka anakufa kitandani.

CCM wafike sehemu waachane na mbinu chafu dunia imeshakuwa ndogo kwa kuwa technlojia imeshazaa upataiakanaji wa taarifa sahihi na wakati sahihi mara moja na kwa kasi ya ajabu.Hivyo kuendeleza siasa za kinafki na uongo wa ghilba kwa watu wenye taifa lenye umri wa miaka hamsini ni aibu.Sisi tulio vijana tutakopi ujinga mara dufu kuliko ujinga wenu,hivyo tutahatarisha Taifa ambalo nyie wanaccm mnaishi ninyi, mama,baba, watoto na dada zenu.
 
28 NOVEMBER 2011


kama mnafikiri kujivua gamba imefikia mwisho subirini mtaona matokeo, Kamati inakwenda kumaliza kila kitu,

Hii episode ya kuvuana magamba.....ikimalizika itakuja episode gani vile?
Nauliza hili kwa sababu kuwatoa magamba wachache hakutamaliza tatizo la ufisadi na uozo chamani wala serikalini.
Tunachotaka wananchi ni kumalizika kwa ufisadi wote! Tunataka haki na fursa sawa kufaidi rasilimali zetu. Haijalishi ni chama gani
wala ni watu gani.Hivi leo tumeambiwa wabunge washajiongezea maposho kwa zaidi ya 150%! Inahuu?
 
Hawa jamaa hakuna lolote ni njia ya kusahaulisha wananchi kuhusu maandamano yetu ya katiba. Huuu ujinga wao wamalize huko huko sisi tunataka ku-exercise nguvu ya umma.
 
Mimi ni msafiri bado nipo njiani....! sijui lini nitafika ooooh!, naulizia watu kule ninakokwenda......! naambiwa bado ni mbali! sijui lini nitafika oooo!
 
Muda wa maamuzi magumu kwa chama umefika. Nadhani anaye jiona fisadi aachie ngazi mapema
Muda ulishafika siku nyingi. Tatizo ni kukosekana mwenyekiti makini na mwenye ujasiri wa kutoa maamuzi magumu, siyo huyu ambaye naye ananuka ufisadi kuliko hata watuhumiwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom