Mafia: Tumeibeba sana CCM sasa tutaiacha rasmi

Omari Kimbau alispend close to 300 million kutaka kuchukua kisiwa cha mafia lakini mwishowe hata baba yake alishindwa kumsaidia

hapo nazungumzia baba yake wa kuunganisha...yaani YUSUPH MAKAMBA ambaye dada yake aliolewa na dedi yake KIMBAU

wana Mafia waliuliza kama Makamba aliweza kumtafutia JIMBO mwanae January iweje leo ashindwe kumtafutia mwanae mwingine huyu Omari jimbo huko kwa wasambaa wenzie?

Omari alitembeza hongo mpaka kwa CCM Mkoa lakini mwishowe Mbunge wetu aliye na elimu ya darasa la 7 alishinda hands down lakini ukweli usiopingika kuwa the REAL mbunge wa Mafia anajulikana japo watu wa kisiwa cha Mafia hawalijui hilo lakini aliyeanzisha thread nadhani naye anajua ni nani hasa mbunge wa Mafia

CUF wako strong sana na hapo ndio mtajua kuwa machinery ya CCM Pwani ilipiga akili na kuondoa upuuzi aliokuwa anuleta yule Msambaa kutakakuwachagulia mbunge kwani wananchi walishaapa kuwa OMARI KIBAU akipitishwa then NGANGARI haoooo wanalichukua jimbo!

By the way kuna taarika kuwa tangu Mungu auombe dunia Mafia haina ma university graduates wasiozidi 15 na kati ya hao mmoja alitaka kugombea ubunge toka ulaya lakini akachanganyikiwa akili waliobaki ndio huyo wa sasa .

Kuhusu maendeleo sioni kipya Mafia kwanza wametengwa ki jiografia na maana bora wangekuwa part of znz wangepelekewa mawili matatu...lakini ukeli ni kuwa gato jipya linajengwa pale Kilindoni na uwanja wa ndege uko kwenye mchakato wa millenium challenge account na bila kusahau asasi mbali mbali za maendeleo zinajitahidi lakini mie naona asasi inayofanya la maana kisiwani ni hao waliojenga shule ya sekondari ya Bweni

otherwise bara bara mbovu, umeme ni wa jenereta, in short hakuna kinachoendelea kule kisiwani na wenye kuendeleza Mafia ndio hao wameenda kufungua bar kama akina Omari kimbao na hiyo baar yake ya MAFIAN...na ushahidi wa kuuza pobe huu hapa:

OmarKimbausMafianHeinekenParty.jpg
[/IMG]

Halafu mnashangaaa iweje Omari na Kinje hawazungumzi?

Ukweli ni kuwa hata huyo Bwana Mkubwa aliyekuwa ana mbankroll Omari Kimbau naye alishamchoka baada kuona maneno mengi na hakuna linalofanyika na mwishowe Omari aliamua kuridi where he is more comfortable badala ya kuendelea kusaidia maendeleo kisiwani pale

Nadhani tutamwona tena uchaguzi ukikaribia
 
Tunasikitika sana kutamka haya lakini imefika wakati wa kusema. Kisiwa cha Mafia tumekua wanachama na wapenzi wa ccm, na tumekuwa tukiichagua wakati wote wa uhai wake. Pamoja na chama hiki kukipenda na kuendelea kukiunga mkono, hali imekuwa tofauti na matarajio yetu kwa nusu karne sasa. Kisiwa hichi kimekosa barabara nzuri, hakuna kiwanja cha ndege bora, usafiri wa majini sio wa kuridhisha, hakuna shule bora, zilizopo zote ni za kidato cha nne, hospitali mbaya, hata sekta ya uvuvi nayo imesahaulika. Pamoja na hayo yote, kisiwa cha mafia tumesahaulika hata kwenye kugawa keki ya taifa, kwani hakuna kiongozi aliyewahi kuteuliwa nafasi yeyote ile kama ya ukurugenzi, U-DC, RC, hata makatibu wa chama ngazi yoyote ile tangu uhuru mpaka sasa, si kama mafia hakuna walio na sifa zinazofanana na wateule tuliowahi kuwa nao au tulio nao, ila ni kutokana na kudharauliwa na viongozi wote waliowahi kutawala nchi hii, pia kutokana na upole wetu na kutoonyesha kuleta upinzani kwa chama hiki.
Nadhani sasa umefika wakati wa kujibu mapigo kwa vitendo kwa ccm kwamba, dharau na hila zote tulizovumilia sasa inatosha. Tumetengwa vya kutosha, tumebaguliwa inatosha, hali tulikuwa nayo inasikitisha. Kama ccm si mshirika wetu wa dhati na kweli, ni muda sasa wa kujivua kutoka kwao. Haiwezekani wilaya ya mafia pamoja na kuwa na idara ya maji tangu kuanzishwa kwake, ni kijiji kkimoja tu ndicho chenye maji yanayozalishwa na idara hiyo, ni vijiji viwili tu ndivyo vyenye umeme tangu uunganishwe miaka ya sabini. Zao la nazi tunalotegemea limesahaulika, hakuna kiwanda cha kusindika mafuta ya nazi sasa, hakuna soko la uhakika, hakuna usafiri wa uhakika wa kusafirishia nazi hizo, hakuna anayeshughulikia hilo, hakuna hata ahadi juu ya hilo.
Hayo machache, nitaleta zaidi.
Tatizo lenu watu wa pwani mnapenda vya bure, acheni uvivu nyie, jishughulisheni na mazao mengine sio kusubiri nazi kila mwaka. Huo umeme unao utaka ni kwaajili ya nini? friji zenyewe mbili mafia nzima.
 
matusi ya nini ndugu yangu?
 
Tatizo lenu watu wa pwani mnapenda vya bure, acheni uvivu nyie, jishughulisheni na mazao mengine sio kusubiri nazi kila mwaka. Huo umeme unao utaka ni kwaajili ya nini? friji zenyewe mbili mafia nzima.

Mbona unapayuka ndugu, inaonyesha hujui unachokizungumza! Sasa umeme na fridge kinaanza nini? Poor thinking!
 
Maendeleo ya Mafia yyataletwa na Wafia wenyewe, Tuache mawazo ya kujitenga na mengine kama hayo, tunatakiwa tutangulize kuweza zaidi ya kkushindwa!
Wasomi na wanaharakati wanaotoka mafia wanatakiwa waone umuhimu na opportunities zilizopo mafia na kurudi kuendeleza na kuleta mabadiliko. Pia kuna umuhim wa kuangali upya namna ya kuchagua wawakilishi wetu, kwani sidhani kwa hali ya sasa italeta mabadiliko tunayoyazungumza
 
Tunasikitika sana kutamka haya lakini imefika wakati wa kusema. Kisiwa cha Mafia tumekua wanachama na wapenzi wa ccm, na tumekuwa tukiichagua wakati wote wa uhai wake. Pamoja na chama hiki kukipenda na kuendelea kukiunga mkono, hali imekuwa tofauti na matarajio yetu kwa nusu karne sasa. Kisiwa hichi kimekosa barabara nzuri, hakuna kiwanja cha ndege bora, usafiri wa majini sio wa kuridhisha, hakuna shule bora, zilizopo zote ni za kidato cha nne, hospitali mbaya, hata sekta ya uvuvi nayo imesahaulika. Pamoja na hayo yote, kisiwa cha mafia tumesahaulika hata kwenye kugawa keki ya taifa, kwani hakuna kiongozi aliyewahi kuteuliwa nafasi yeyote ile kama ya ukurugenzi, U-DC, RC, hata makatibu wa chama ngazi yoyote ile tangu uhuru mpaka sasa, si kama mafia hakuna walio na sifa zinazofanana na wateule tuliowahi kuwa nao au tulio nao, ila ni kutokana na kudharauliwa na viongozi wote waliowahi kutawala nchi hii, pia kutokana na upole wetu na kutoonyesha kuleta upinzani kwa chama hiki.
Nadhani sasa umefika wakati wa kujibu mapigo kwa vitendo kwa ccm kwamba, dharau na hila zote tulizovumilia sasa inatosha. Tumetengwa vya kutosha, tumebaguliwa inatosha, hali tulikuwa nayo inasikitisha. Kama ccm si mshirika wetu wa dhati na kweli, ni muda sasa wa kujivua kutoka kwao. Haiwezekani wilaya ya mafia pamoja na kuwa na idara ya maji tangu kuanzishwa kwake, ni kijiji kkimoja tu ndicho chenye maji yanayozalishwa na idara hiyo, ni vijiji viwili tu ndivyo vyenye umeme tangu uunganishwe miaka ya sabini. Zao la nazi tunalotegemea limesahaulika, hakuna kiwanda cha kusindika mafuta ya nazi sasa, hakuna soko la uhakika, hakuna usafiri wa uhakika wa kusafirishia nazi hizo, hakuna anayeshughulikia hilo, hakuna hata ahadi juu ya hilo.
Hayo machache, nitaleta zaidi.

Mmezungukwa na bahari lakini wanaofaidi samaki ni akina EL na Kinana ambao wamepaki mimeli kwenye pwani yenu huku wakiondosha mitani ya samaki na nyie mkiambulia sifuri.....
 
Huyu Omr nahisi akili yake ni seasonal...wewe unadhani watu wanahitaji umeme ili wamiliki friji tu? Wewe ni perculiar ccm type,njoo kwetu usome kazi za umeme,ukifaulu utapewa hata masters,Mafia is exploited enough,huu ni mda wa mapinduzi achanane ni mafisadi mtakuja kuumia hata maji msipate tena hata tone,au mnasubiri mkamliwe mpaka damu?
 
Wewe ndio huijui Mafia. Kwa nini Bulji amepata ubunge tena Mafia kama sio Gati na Uwanja wa ndege tena kwa ahadi kuwa airport itapeleka barabar ya lami mpaka Utende!!!?? Mbona nyumba za barabarani kwenda Utende zote zimepigwa alama kwamba zitafisdiwa kwa ajili ya Barabara ya Lami kwenda Utende?
Gati tayari mmeshaanza jengewa na karibu litamalizika, au unataka niaattach picha hapa?

aliekwambia buji kapata ubunge kihalali nani?ccm haikushinda ialeshinda ni mgombea wa CUF upo?hilo gati limechelewwa kuja watu washachoka halijaja wakati muafaka.kwa hiyo ccm sorry.hizo x toka zimewekwa hamna kinachoendelea hapo kilindoni hakuna fidia wala barabara
 
Unaweza kuthibitisha ni mwananchi gani aliyelipwa fidia ya nyumba yake kwa upanuzi wa barabar? Waweza kunitajia hiyo pesa ipo kwenye bajeti ya serikari ipi? Na ahadi ilitolewa wakati gani? Au na wewe unataka kusema hujui janja ya ccm kupata kura? Unakumbuka mbunge kimbau aliahidi kujenga bara bara kwa mchanga kutoka Ulaya, ilijengwa? Hizo ni siasa tu. Kwani kutiwa X nyumba za kando kando ya bara bara ndio kujengwa barbara? Angalia ilani ya ccm 2005- 2010 ilisema waislamu watapatiwa mahakama ya kadhi, ipo wapi? Pia ilisema kila wilaya itajengewa chuo cha veta, muda umepita, mafia kipo wapi? Balleni? Kilindoni? Chole? Malimbani? Utende? Au kirongwe na jojo?

Duh hapo kwenye red ... kweli mabomba nchi nzima yatatoa maziwa...hivi kweli mbunge anaawaambia hivyo nanyi mnasadiki...MAFIA mnahitaji kupata kikombe...tupeni ccm kapuni.
 
aliekwambia buji kapata ubunge kihalali nani?ccm haikushinda ialeshinda ni mgombea wa CUF upo?hilo gati limechelewwa kuja watu washachoka halijaja wakati muafaka.kwa hiyo ccm sorry.hizo x toka zimewekwa hamna kinachoendelea hapo kilindoni hakuna fidia wala barabara

Jamaa huyu hakubaliki kabisa huku Mafia, kwasababu hakuna anachofanya zaidi ya uswahili tu, mambo yake yakimasihara na uesharati. Sasa ndio ametoa mpya baada ya kuoa mtoto mdogo na kuitelekeza familia yake! Watu walipiga kelele sana juu ya kashfa yake ya kutumia vyeti vya kaka yake kupatia uongozi chama kikasema kwamba hayo yangetekelezwa kwa kutorudisha jina lake kwenye uchaguz wa 2010. Hayo hayakutekelezwa kwakuwa wale wanaonufaika na Rasilimali za Mafia wanampenda kutokana na udhaifu wake wa kiuongozi
 
Duh hapo kwenye red ... kweli mabomba nchi nzima yatatoa maziwa...hivi kweli mbunge anaawaambia hivyo nanyi mnasadiki...MAFIA mnahitaji kupata kikombe...tupeni ccm kapuni.

Mkuu alivyotoa ahadi hiyo ndipo watu walipostuka, wakampiga chini, akaleta mtoto wake pia wakampiga chini
 
na kuna hili la hivi karibuni ni kielelezo tosha kwamba, wafanya maamuziserikalini wamechoka akili kabisa! Mwekezaji amepewa kujenga sehem ya chanzo cha maji, ambapo ndipo idara ya maji inapotoa maji yake
 
bw mzizi, hapo umenigusa kidogo.inamaana wametoa pale bondeni kwa mkuu wa wilaya.? ni muwekezaji anae wekeza nini?
 
bw mzizi, hapo umenigusa kidogo.inamaana wametoa pale bondeni kwa mkuu wa wilaya.? ni muwekezaji anae wekeza nini?

Kizimkazi, kuna mkaburu kapewa ajenge hoteli ya kitalii pale, sasa sijui maji yakipotea tutayapata kutoka wapi ukizingatia hichi ni kisiwa
 
Kizimkazi, kuna mkaburu kapewa ajenge hoteli ya kitalii pale, sasa sijui maji yakipotea tutayapata kutoka wapi ukizingatia hichi ni kisiwa

Bw mzizi, ahsante kwa kutujuza mimi nilikuwa sinalo hilo,ila mafia mmbunge tuliyenaye ni mbumbumbu,ki upeo hata uwezo wa akili yake,analaghai kwa salam alykum na kujifanya muungwana. sasa maji yale pale hayatoshi hospitali, hayatoshi majengo wala kurungeni na msitu ndio huo tu unaotegemewa kutunza maji.sijui anawapigania watu gani.labda kila mtu awe na kisima chake sasa. nyundo uko wapi bw ulisema utagombea au umeogopa muhali? mzizi itabidi uni pm
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom