Mafanikio ya wanaume hupimwaje?

Kwa karne hii kumpata mwenza ambaye ni free-from malalamiko inabidi usugue goti sana,
Somo zuri.
 
Mkuu, somo zuri. Hiyo picha uliyotumia ni ya ndoa changa. Ukiweza kupata picha ya watu haohao baada ya kuwa kwenye ndoa miaka kumi hutaamini unachokiona.
 
Ni kweli kabisa huyu ni confirmed mzinifu lol....partner wake alikuwa Minister I think, kwasasa amebadilisha channel, anakitu kipya ambaye alikuwa ni Journalist.

Wafaransa ni watu ambao hawaamini sana mambo ya marriage, thats my point of view.

mhhhhhhhhhh
 
Mkuu, somo zuri. Hiyo picha uliyotumia ni ya ndoa changa. Ukiweza kupata picha ya watu haohao baada ya kuwa kwenye ndoa miaka kumi hutaamini unachokiona.
gmosha48 somo hili nimewalenga zaidi wanandoa wachanga na wale wanaoelekea kwenye ndoa..........
Wale ambao tayari wako kwenye ndoa na miaka imeshasonga 10+ linawahusu kwa ajili ya kuboresha tu ndoa zao.
Niliona ni vyema kutumia picha hiyo ili kupromoti ndoa kwa vijana....
Mie nishajizeekea zangu na mama Ngina na sasa tunalishana ugoro hapa tukisogeza siku zetu za kuelekea ukingoni.....LOL
old-african-american-couple-in-bed2.jpg
 
young-ethnic-couple-by-table-eating-breakfast-thumb10718814.jpg

Mke anapomjali na kumkubali mume humuongezea kujiamini…

Mahusiano kati ya mume na mke nyumbani huweza kumfanya mume afanikiwe kwenye shughuli zake au aanguke.

Kwa nini?

Ni kwamba, mtu ambaye anakataliwa na mtu au watu wanaomhusu huwa anakosa kujiamini, huwa anafikia mahali ambapo hujichukia hata yeye mwenyewe. Mke anapomkosoa mume, anapomlalamikia kila mara na kuwa na ghubu, bila kujali kama mume huyo amekosa au hapana, mume hufikia mahali huanza kujitilia mashaka kama kweli ana uwezo wa kufanya mambo, kama kweli ana thamani anayodhani kuwa anayo.

Kujiuliza huku mara nyingi kuna maana ya mwanaume kuanza kupoteza kujiamini na hata kuanza kuwa na uhusiano mbaya na watu anaohusiana nao mahali pengine kama kazini. Unaweza kumgundua mtu ambaye ana mke mlalamikaji, mkosoaji na mwenye ghubu kwa kuangalia jinsi anavyojitathmini. Kama mke ni mkosoaji na mwenye ghubu kwa mumewe ni lazima mume atakosa kujiamini katika kufanya mambo yake mengi, ni lazima ataanza kuwa na uhusiano mbaya na watu wengine kutokana na hukohuko kutojiamini kwake ambako kumesababishwa na ghubu na kukosoa kwingi kwa mkewe.

Mwanaume ambaye ana mke mkosoaji na mwenye ghubu hutokea kutowapenda watu wengine na kukosoa wengine inatokea kuwa sehemu muhimu kwa maisha yake, anatokea kuwa na hasira za karibukaribu na ni vigumu sana kwa mtu wa aina hii kuelewana na watu.

Baadhi ya makampuni huko Marekani, kabla hayajampandisha mtumishi wake cheo, humchunguza mke wa mtumishi. Hawachunguzi kama ni mzuri wa sura au kama anajua mapenzi au kupika vizuri. Mara zote huchunguza kama mwanamke huwa anampa mumewe moyo, kama hamkosoi na kumlalamikia na kama hana ghubu. Wanapogundua kwamba mke wa mtumishi siyo mkosoaji wala mwenye kulalamika-lalamika humpa cheo mtumishi kwa imani kwamba atakuwa ni mtu mwenye kujiamini.

Lakini wanapogundua kwamba mke ni mwenye kukosoa, mwenye ghubu na mlalamikaji, kamwe hawampi mtumishi cheo, kwa sababu wanaamini kwamba, mtumishi huyo hawezi kuwa makini, atakuwa hajiamini.

Nakubaliana na wewe mtambuzi kwenye hii mada yako. Mafanikio ya mume kazini na kwingineko kwa sehemu kubwa kuna changiwa na +ve support toka kwa mkewe.

Mfano wa wazi ni chunguza ndoa nyingi sana ambazo mume ni mlevi kupindukia, utagundua kuwa mkewe huko nyumbani mambo hayaendi vzr, ni mkosoaji, mgomvi na mlalamishi na hivyo kumfanya mume anakosa kujiamini na kuamua kupitia bar kupiga pombe kupunguza mawazo na kujijengea ujasiri wa kurudi nyumbani! Jambo hili huchangia kupunguza kujiamini na kushuka kwa perfomance ya kazi ofisini na kuleta umaskini ndani ya familia. Nahisi pia, hata saa nyingine sababu moja wapo ya mwanaume kuwa na nyumba ndogo ni kuwa na mwanamke mlalamishi, mkosoaji, mwenye ghubu asiye na support kwa mumewe!
 
young-ethnic-couple-by-table-eating-breakfast-thumb10718814.jpg

Mke anapomjali na kumkubali mume humuongezea kujiamini…

Mahusiano kati ya mume na mke nyumbani huweza kumfanya mume afanikiwe kwenye shughuli zake au aanguke.

Kwa nini?

Ni kwamba, mtu ambaye anakataliwa na mtu au watu wanaomhusu huwa anakosa kujiamini, huwa anafikia mahali ambapo hujichukia hata yeye mwenyewe. Mke anapomkosoa mume, anapomlalamikia kila mara na kuwa na ghubu, bila kujali kama mume huyo amekosa au hapana, mume hufikia mahali huanza kujitilia mashaka kama kweli ana uwezo wa kufanya mambo, kama kweli ana thamani anayodhani kuwa anayo.

Kujiuliza huku mara nyingi kuna maana ya mwanaume kuanza kupoteza kujiamini na hata kuanza kuwa na uhusiano mbaya na watu anaohusiana nao mahali pengine kama kazini. Unaweza kumgundua mtu ambaye ana mke mlalamikaji, mkosoaji na mwenye ghubu kwa kuangalia jinsi anavyojitathmini. Kama mke ni mkosoaji na mwenye ghubu kwa mumewe ni lazima mume atakosa kujiamini katika kufanya mambo yake mengi, ni lazima ataanza kuwa na uhusiano mbaya na watu wengine kutokana na hukohuko kutojiamini kwake ambako kumesababishwa na ghubu na kukosoa kwingi kwa mkewe.

Mwanaume ambaye ana mke mkosoaji na mwenye ghubu hutokea kutowapenda watu wengine na kukosoa wengine inatokea kuwa sehemu muhimu kwa maisha yake, anatokea kuwa na hasira za karibukaribu na ni vigumu sana kwa mtu wa aina hii kuelewana na watu.

Baadhi ya makampuni huko Marekani, kabla hayajampandisha mtumishi wake cheo, humchunguza mke wa mtumishi. Hawachunguzi kama ni mzuri wa sura au kama anajua mapenzi au kupika vizuri. Mara zote huchunguza kama mwanamke huwa anampa mumewe moyo, kama hamkosoi na kumlalamikia na kama hana ghubu. Wanapogundua kwamba mke wa mtumishi siyo mkosoaji wala mwenye kulalamika-lalamika humpa cheo mtumishi kwa imani kwamba atakuwa ni mtu mwenye kujiamini.

Lakini wanapogundua kwamba mke ni mwenye kukosoa, mwenye ghubu na mlalamikaji, kamwe hawampi mtumishi cheo, kwa sababu wanaamini kwamba, mtumishi huyo hawezi kuwa makini, atakuwa hajiamini.

kwa upande wangu mie mafanikio ya mwanaume nayapima kwa anavyoweza tafuta hela nyingi kuliko uwezo wangu wakutumia pesa zake na kuzimalioza...yaani hata nikitumiaje siwezi kuzimaliza....
 
babu Mtambuzi nice somo, believe me! i hope hubby wangu YM atapita huku aone, kuwa hata yeye hatakiwi kuwa na gubu lol!
 
Last edited by a moderator:
In no particular order
  1. money
  2. providing/caring for wife + children
  3. calm under pressure + emergencies
  4. balancing work and family life
 
Hakuna kampuni inayomchunguza mke, hiyo itakuwa highly illegal na lawsuits lazima zitafuata.
 
hiyo picha imenivutia hivi hayo mambo bado yapo karne hii kwa wanandoa wenye watoto au hata ambao hawajazawadiwa watoto.
 
Asnam mimi na mama Ngina siku moja moja huwa tunakumbushia hayo maloveee na tuna watoto watatu mpaka sasa tukielekea kutimiza miaka kumi ya kuishi pamoja.........
thumb_COLOURBOX4246788.jpg
 
Back
Top Bottom