Mafanikio ya serikali ya CCM chini ya Kikwete, DETAILED!

ADHA+YA+MAJI.JPG
 
KWA KWELI CCM imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutekeleza mema katika miaka 25. Ninarudia tena ku
waomba watanzania tumpe kura za ndio Mgombea wetu kipenzi cha watu Mhe. JAKAYA MRISHO
KIKWETE tarehe 31 Oktoba 2010.

Wahi ukamwone Daktari, nina wasiwasi na kichwa chako kama kina uwezo wa kupembua mambo vizuri. Lakini sijui, ikiwa una uwezo wa kukaa ktk PC na kupost hapa mawazo utakuwa mzima, ila huna uwezo wa kuunganisha au kuhusianisha mambo.
Siku hizi hata ukienda kijijini ukitaja tu neno "LOWASA" hata katoto kadogo kanajua umeshachafua hewa, hakuna jema hapo. Sasa wewe, hivi umeshawahi kusikia hili neno "lowasa" toka uzaliwe? yawezekana bado, basi niombe nikujuze linamaanisha nini, na huyo JK unayemtaja kuwa ni 'kipenzi' au mpenzi analielewa vipi hili neno.
 
TULIAHIDI KUENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA
Ujenzi wa miradi 15 ya barabara kwa kiwango cha lami yenye jumla ya urefu wa

Km. 1,398.6 imekamilishwa katika kipindi cha 2005 - 2010 huku ujenzi ambao
unaendelea ukiwa ni wa miradi 29 ya barabara zenye jumla ya Km. 2,536.4
 
Hiyo picha hapo juu haina uhusiano wowote na Tanzania, CCM ili ahidi KUKUZA NA KUBORESHA SEKTA YA AFYA
Kutoka mwaka 2005 hadi 2009,jumla ya zahanati 464,vituo vya afya 98

na nyumba za waganga 394 zilijengwa.Zahanati 1,037,vituo vya afya 285 na hospitali 112 zimekarabatiwa.
Vifo vya watoto wachanga vimepungua hadi kufikia 58 kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa hai mwaka 2009/2010.
 
MWAKA 2000 -2004 Vs 2005-2009

Unga 460 Vs 1000 = 217%
Mchele 600 Vs 1200 = 200%
Sukari 760/kg Vs 1600/kg = 210%
Mkate 250 Vs 700 = 280%
Maharagwe 360/kg Vs 1000/kg = 277%
Mafuta ya taa 450/lt Vs 1050/lt = 233%
Mafuta ya uto 178/lt Vs 720/lt = 404%
Nazi 100 Vs 550 = 550%
Mchicha/tembele 50 Vs 150 = 300%
 
TULIAHIDI KUENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA
Ujenzi wa miradi 15 ya barabara kwa kiwango cha lami yenye jumla ya urefu wa

Km. 1,398.6 imekamilishwa katika kipindi cha 2005 - 2010 huku ujenzi ambao
unaendelea ukiwa ni wa miradi 29 ya barabara zenye jumla ya Km. 2,536.4

huwa nazunguka sana nchi hii kwenye shughuli zangu za kutafuta riziki sio kuomba riziki naomba nieleweke vizuri hapo. Hizo barabara za lami za umbali huo unaotaja ziko nchi gani? kama ile ndefu aliyoiacha Mkapa (MZ -DM)n mpaka leo haijaisha, hizo zilizokamilika kwanini hamzitaji kwa majina.

Tusiongea kiushabiki kusifu pasipo sifa. Napenda sana nisome tumefanya hili mpaka hapa tumekwama hapa, hiyo ndiyo hoja. lakini kusema tumejaribu hilo haliniingii akilini kwani kuongoza nchi sio kufanya majaribio. experiments zinafnywa na wanasayansi wakifanikiwa wanatoa taarifa kwa utekelzaji rasmi.

naipenda tanzania. nawapenda watanzania. mimi ni mtanzania halisi
 
Kumbe kweli tunaona. Wiki iliyopita nilikwenda kijijini kwetu mpaka leo barabara inayotumika ni ile ambayo mkoloni alipitisha grader, ever hakuna ofisa wa wizara hiyo aliyetembelea eneo hilo kuona hali ya barabara. Barabara wanazosema waheshimiwa niyingi ni zile alizojenga mwingereza na sio mpya, wanazungumzia kuziba mashimo au kukarabati kama zile za Mandela na Morogoro, upuuzi tu. Kuwadanganya wajinga.

Hakuna barabara yoyote ambayo awamu ya nne wanaweza kujisifia, ni porojo tu.
 
heri yako ndugu umenena, juzi kati JK anajivunia daraja la umoja, kajenga yeye?
Sijui alijisikiaje wakati akipita kule Namtumbo na Nanyumbu jinsi hali ilivyo mbaya
 
Hiyo picha hapo juu haina uhusiano wowote na Tanzania, CCM ili ahidi KUKUZA NA KUBORESHA SEKTA YA AFYA
Kutoka mwaka 2005 hadi 2009,jumla ya zahanati 464,vituo vya afya 98

na nyumba za waganga 394 zilijengwa.Zahanati 1,037,vituo vya afya 285 na hospitali 112 zimekarabatiwa.
Vifo vya watoto wachanga vimepungua hadi kufikia 58 kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa hai mwaka 2009/2010.

Mkuu mbona tunadanganyana, nyumba za waganga hazina vyoo ambazo hata mbunge mmoja wa CCM hawezi kukubali kuenda kuishi kwenye nyumba kama hiyo.

Zahanati hazina dawa, hazina vitanda na hazina wauguzi, ukiangalia wodi za wajawazito unaweza kushangaa wanajipanga kama vile wanataka kuingia kwenye public toilet.

Unahakika vifo vya watoto wachanga vimepungua? takwimu hizo amekupa nani? mbona hujazungumzia kina mama wanaokufa, hujazungumzia wagonjwa wanaofia hospitali kwa magonjwa yanayoweza kutibika.

Mkuu lazima tuipende Tanzania na watanzania, si vizuri kuwaongopea watu.
 
Duh!
huu ujumbe ktk picha ni mzito..umekamilika
JK si akubali tu abwage manyanga..hakuna lolote alilofanya zaidi ya kugumisha maisha
 
We Acha tu, thread yako imetulia sana. Hongera.

Naomba tuwaambie vijijini mwetu hali halisi. Wasidanganyike na kofia za CCM. Wazipokee na kura kwa Chadema.
 
CCM ieleze mafanikio ya miaka 49 - Askofu

Thursday, 23 September 2010
Na Wilhelm Mulinda, Mwanza

ASKOFU wa Kanisa la Free Pentecostal nchini (FPCT) jijini Mwanza, Bw. Omas Hulilo amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinatakiwa kuwaambia wananchi mafanikio ambayo kimefikia miaka 49 ambayo kimekaa madarakani badala ya kuendelea kutoa ahadi katika kampeni zake za uchaguzi mkuu mwaka huu.

Akizungumza na Majira jijini hapa jana, Bw. Hulilo alisema kuwa baada ya CCM kuwaambia wananchi mafanikio yake kwa kipindi ambacho imekaa madarakani, ndipo inatakiwa kuwaomba wananchi waendelee kuichagua ili kukamilisha vipaumbele vyake ilivyobakiza katika maendeleo nchini.

"Sisi wapinzani (protestants) wa mafundisho ya Roma kuhusiana na Yesu Kristo tunaona kwamba kuna upotoshaji ndani ya CCM kuhusu masuala ya Richmond pamoja na ufisadi wote kwa ujumla ulivyoshughulikiwa.

"Tunaona kuwa maadili hayakufuatwa, hali ambayo imetuudhi viongozi wa madhehebu ya kiprotestant na hata madhehebu mengine ya kikiristo kwa ujumla japo hayataki kusema wazi," alisema Askofu huyo.

Alisema kuwa vyama vya upinzani ambavyo havijapata nafasi ya kuongoza, ndivyo vinatakiwa kutoa ahadi na kuwathibitishia wananchi bila kuacha shaka lolote ni kwa namna gani vinaweza kutekeleza wanayoahidi kwenye kampeni zao.

Pia Askofu huyo alisema kuwa ni makosa kwa serikali kudai kuwa inatenganisha masuala ya dini na siasa, kwani hali hiyo inaweza kufanya waumini wazuri wa dini kuingia kwenye siasa na kutokuwa tena na uadilifu kwa kujihusisha na vitendo viovu, ukiwamo ufisadi kutokana na kukosa hofu ya kumuogopa Mungu.

Alisema kuwa wao bado wanaunga mkono wabunge mbalimbali wa bunge lililopita akiwemo aliyekuwa Mbunge wa Nzega (CCM), Bw. Lucas Selelii pamoja na wabunge waliotoka katika vyama vya upinzani kwa kuonesha uzalendo katika kukemea uovu huo ambao umejikita katika misingi ya ubinafsi na uroho.

Alisema kuwa madhehebu hayo ya kipentekoste yako tayari kuungana na mtu yeyote ambaye anasimamia haki ya wanyonge na kupiga vita ufisadi na vitendo vingine vyote vinavyoashiria dhuluma kwa umma.

mwisho...

SOURCE GAZETI LA MAJIRA
 
Ni kweli kabisa, maana sasa inaonekana wanatoa ahadi kama vile wanatafututa kutwaa dola kwa mara ya kwanza.
 
Maji+1%5B1%5D.jpg

MAJI BWERERE

MAISHA+BORA.jpg

MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA YAMEWEZEKANA

HURUMA.jpg

USHAHIDI WA MAISHA BORA UNAONEKANA HATA KWA WATOTO WADOGO

ADHA+YA+MAJI.JPG

YOU SEE, TATIZO LA MAJI MIJINI NA VIJIJINI LIMEPATIWA UFUMBUZI WA KUDUMU

USAFIRI+WA+WANAFUNZI.jpg

TATIZO LA USAFIRI KWA WANAFUNZI MIJINI LIMEMALIZWA.MNATAKA MAISHA BORA YAPI ZAIDI YA HAYA?

POLISI+MSIMBAZI.jpg

MNAONA?POLISI WENYE MAKAZI DUNI SASA WANA SWIMMING POOL HAPO MSIMBAZI POLICE FLATS.MAISHA BORA KWA POLISI YAMEPELEKEA WAACHE KUDAI RUSHWA NA KUBAMBIKIZA KESI KWA WALALAHOI

MATREKTA+KILIMO+KWANZA.JPG

BARABARA ZETU NI MARIDADI.TUMELETEWA MATREKTA MENGI MNO KWA KILIMO KWANZA HADI INABIDI YAFANYE KAZI YA KUVUTA MALORI.EBO!KWANI CHA AJABU NINI TREKTA KUVUTA LORI?NI FERI ZA NCHI KAVU HIZO

MATOPE.JPG

CHAGUA KIKWETE NA CCM KWA BARABARA BORA.NA 2010-2015 BARABARA KAMA HIYO HAPO JUU ZITAKUWA UPGRADED TO FLYOVER.
 
Back
Top Bottom