Mafanikio ya serikali ya AWAMU YA NNE katika MAPINDUZI YA KILIMO

kwa muda wa miaka nyingi tumekua tukisikia serikali ikizungumza kilimo kwanza,ukimwuuliza mwananchi maana yake ni nini wengine wasema ni powertiler wengine ruzuku wengine hata wanayaita landcruiser new model kilimo kwanza,sishangai kwani wakala wengi wamechakachua mpaka haieleweki inamaanisha nini,kuna usemi unasema sera nzuri inatungwa tanzania inasomwa uganda na kutekelezwa kenya.tukirudi kwenye sera ya kilimo kwanza kwa mtazamo wa haraka tunazungumzia mkulima kubadilika kutoka kilimo cha jadi na kwenda kilimo cha kisasa cha kuzalisha gunia 40 kwa eka moja kama nchi zilizo endelea,sasa serikali yetu inadhani inaweza kumbadilisha mkulima huyu bila kurudi kwenye misingi kuu ya kilimo,kwanza ni kujua hali ya watu wako kua ni masikini mbegu ya 45000 kwa eka mbolea 120000,hatoweza na serikali haitoweza kutoa ruzuku milele huo niukweli,pili tuweze kuzalisha mbegu bora hapa nchini na kwa bei nafu tuepukane na uagizaji wa mbegu nje,ni aibu kwa nchi kama yetu eti asilimia 85 ya mahindi ya mbegu inatoka nje,tuhakikishe kila kata au wilaya yenye mito inatenga eneo la ku zalisha mbegu,tuinunue upya kiwanda cha mbolea na kuiboresha na hatimae wananchi masikini watapa mbegu na mbolea kwa bei nafuu,tunao wehu wanaodhani uchumi unaweza kukua bila mikakati ya dhati tumeishi kwa miaka mamia na kilimo cha jadi bila mabadiliko,tunafuga kwa kuzurura huku tunataka kubadilika tunadhani kutenga eneo la wakulima na wafugaji tumebadilika vita vya wakulima na wafugaji vitaongezeka kama hatutaki kujifunza kwa dhati kutoka nchi zilizo endelea leo hii marekani kwa siku moja wanachinja n'gombe laki moja na je wanapatikana kwa kuzurura,unamkuta mfugaji katoka katesh leo yuko anakimbizwa kwenye mpaka wa malawi na haelewi amefika mwisho wa tanzania ana mifugu hata familia yake haiwasaidii watoto hawaendi shule yeye amezeeka kwa kuzurura.tunahitaji serikali iliyo serious kama heart attack,badala ya kuongeza wizara tupunguze.mfano kuna hajagani ya kua na wizara ya ardhi na makazi,na ya kilimo.na mifugo.na huku huwezi kulima na kufuga bila ardhi hii ingekua wizara ya ardhi kisha ingekua na katibu wakuu wa tatu makazi,kilimo,mifigo.kama mtu ana ardhi ya kulima au kufuga au ya mkazi na hatumii wizara hiyo inaweza kua na mamlaka ya kuomba hati hiyo ifutwe na apewe anayeweza kutumia.
 
Zifuatazo ni juhudi zimezofanywa na serikali hii ya awamu ya nne chini ya Rais shupavu Mh.Jakaya Kikwete katika kuleta mapinduzi ya kilimo Tanzania.

Lengo la kwanza: Kuweka misingi ya mapinduzi ya kilimo (Ibara ya 30-33)
UTEKELEZAJI: Kwa kutambua nafasi maalumu ya kimkakati ya sekta ya kilimo katika kukuza uchumi na kupunguza umasikini ,serikali iliyo chini ya chama cha mapinduzi imefanya yafuatayo:
1) Kutayarisha na kuanza utekelezaji wa programu ya kuendeleza sekta ya kilimo (ASDP). Programu hii sasa imehuishwa na kufanyiwa marekebisho na kuiwezesha Nchi yetu kutia saini makubaliano ya programu kabambe ya kuendeleza sekta ya kilimo barani Afrika (COMPREHENCIVE AFRICAN AGRICULTURE DEVELOPMENT PROGRAMME (CAADP)
2) Kutayarisha azma ya kilimo kwanza ambayo kwa sasa imekuwa ni ya mfano duniani.
3) Kuanzisha dirisha la mikopo ya kilimo katika benki ya rasilimali (TIB)
4) Kuanzisha mchakato wa kuanzisha benki ya kilimo.
5) Kuanzisha mfumo wa kutoa ruzuku ya pembejeo kwa kutumia vocha
6) Kufanyika kwa mikutano minne kati ya waziri mkuu na wadau wa sekta ya kilimo kuhusu mifugo, uvuvi na utafiti.

LENGO LA PILI: KUBUNI MPANGO KABAMBE WA KUENEZA MATUMIZI YA PLAU NA ZANA ZA KISASA ZA KILIMO.(Ibara ya 31(b)

UTEKELEZAJI:
1. Matumizi ya majembe ya kukokotwa na ng'ombe yameongezeka kutoka 585240 mwaka 2005/2006 hadi kufikia 819360 mwa ka 2009/2010.

2. Jumla ya matrekta 1737 yaliingizwa nchini yakiwemo makubwa 362 na madogo (power tillers)1379 kwa kipindi cha kuanzia 2006 hadi 2009.
3. Mfuko wa pembejeo za kilimo umeongeza utoaji wa mikopo ya pembejeo za kilimo kutoka shilingi 4.9 mwaka 2005/2006 hadi shilingi bilioni 8.0 mwaka 2009/2010. Kwa wale wenye akili timamu naamini tumeona kuwa ni kwa kiasi gani serikali hii imefanya kazi juu ya suala hili.

Karibuni tujadili bila jazba, matusi wala kejeli

Sisi tunataka kuona tu bei ya unga na mchele ikishuka mengine tunalima na kufuga sisi nyie aliyelima mara ya mwisho hapo Magogoni ni Mchonga naye alisia ulezi
 
Back
Top Bottom