maendeleo yatakuja siku tutakapoachana na hii dhana!

LATTICE BOND

JF-Expert Member
May 30, 2011
219
48
1. Siku tutakapoacha kupanga maendeleo yetu kwa kutegemea misaada ndipo tutakapoondokana na umaskini!
2. Siku tutakapoacha kutembeza bakuli kuomba misaada ndipo tutakapopata demokrasia na maendeleo ya kweli!
3. Siku viongozi wetu watakapofanya maamuzi kwa kuzingatia kumbukumbu wanayotaka kuacha kwa Watanzania ndipo maendeleo yataanza kupatikana!
4. Siku viongozi wetu wakiacha tabia ya kufikiria familia zao pekee katika maendeleo ndipo nchi itakapoanza kupata maendeleo!
Tafadhali panga orodha ya mambo unayofikiri yakiacha kufanyika ndipo tutapata maendeleo. THINK OF THE ROOT FACTS NOT IMMEDEATE FACTS!
 
pia tutakapo amua kuacha mahubiri ya amani na kuvamia ikuru na kumtoa mbayuwayu,
 
Viongozi wanaoishi kwa kufuata demokrasia ya kweli, ndio wanaoleta maendeleo, Viongozi waache ubinafsi, waache kutumia rasilimali za nchi kwa manufaa yao na familia zao, wanaifanya nchi hii kama shamba lao.
 
Na shaka kweli, bila kipigo watu hao watazidi kuiyumbisha nchi, wapewe kichapo cha kweli kweli, maana kama kuongea, watu wameshaongea sana, wanasikiliza sikio la kulia, linatokea sikio la kushoto, hawataki kubadilika seriously, wakielezwa mapungufu yao, wanateteana, washushiwe kipigo tu, mpaka watikiswe ndio wanalegeza jeuri zao kidogo tena sana, sasa hivi bora wapewe kichapo cha kweli, kama ni wastaarabu na wanaipenda nchi, wameshindwa kuiendesha, waachie madaraka kwa amani, sio mpaka wakurupushwe lakini kama hawataki, watolewe madarakani kwa nguvu, hatutasonga tukiwaacha waendelee kuiuza nchi.
 
1. Siku tutakapoacha kupanga maendeleo yetu kwa kutegemea misaada ndipo tutakapoondokana na umaskini!
2. Siku tutakapoacha kutembeza bakuli kuomba misaada ndipo tutakapopata demokrasia na maendeleo ya kweli!
3. Siku viongozi wetu watakapofanya maamuzi kwa kuzingatia kumbukumbu wanayotaka kuacha kwa Watanzania ndipo maendeleo yataanza kupatikana!
4. Siku viongozi wetu wakiacha tabia ya kufikiria familia zao pekee katika maendeleo ndipo nchi itakapoanza kupata maendeleo!
Tafadhali panga orodha ya mambo unayofikiri yakiacha kufanyika ndipo tutapata maendeleo. THINK OF THE ROOT FACTS NOT IMMEDEATE FACTS!

Pamoja na orodha yote itakayowekwa hapa mimi nasema mandeleo yatakuja pale tu CCM itapoondolewa madarakani.
 
Maendeleo yatakuja tu mpaka tutakomwagana vinyesi kwa sababu kila mmoja atakuwa na heshima
 
Tutafanikiwa kupata maendeleo endapo tutapata kiongozi mkali kwa stail ya dikteta ambae ataogopwa na kila mtu, atakaye zuia ufisadi mikataba isiyo na tija kwa nchi yetu, na kusimamia rasilimali na maliasili zetu. kuachana na mawazo kuwa nchi hii haiwezi kuendelea bila ccm, pia ccm kuacha tabia ya kubeza mawazo ma mipango inayopendekezwa na vyama vya upinzani.
 
Back
Top Bottom