Maendeleo bila ya kiswahili

Che Kalizozele

JF-Expert Member
Jul 20, 2008
777
49
Katika kipindi kile palipokuwa na mjadala mkubwa kuhusu Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia toka elimu ya msingi mpaka chuo kikuu,binafsi nilikuwa napinga kwa nguvu zote huku nikiamini kwamba elimu yetu itashuka sana kama Kiswahili itakuwa ndo lugha ya kufundishia.Lakini kwa sasa nina mtazamo mwingine na ninafikiria imefika wakati kulijadiri suala hili kwa kina huku tukijaribu kuangalia kwa makini faida na hasara zake.Najua sisi watanzania tu waoga wa mijadala,lakini kwa sasa hatuna jinsi kwani hata hili la muungano bado halijaisha
Kama binadamu wa kawaida yapo mambo ninayoamini kama ambavyo wewe yapo unayamini kwayo.Kwa sasa ninaamini kama kweli tunataka kuendelea,maendeleo yale ya kweli,basi kuna haja ya Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia kuanzia shule ya msingi mpaka chuo kikuu.Kwa sababu zifuatazo

Uzalendo wa kweli. Naamini kwa sasa tunakosa wazalendo wa kweli na kama wapo basi ni wachache hivyo katu hawawezi kutosheleza mahitaji.Pia ninaamini nchi bila ya wazalendo haiwezi kufika popote kimaendeleo,na hili liko wazi katika nchi yetu,watu wanaongelea au kutanguliza umimi na usisi mbele huku nchi ikiendelea kuteketea,hivyo uzalendo ni suala la muhimu sana kwa ajili ya maendeleo ya nchi.Najua unajiuliza,Kiswahili na uzalendo wapi na wapi?Uwezi kuwa mzalendo kama haujui wewe ni nani na unatoka wapi.Kwa sisi waafrika ni lazima ujue mila na desturi zako na pia ni lazima uwajue wale waliosababisha taifa hili likafikia hapa lilipo,ujue walipatia wapi na walikosea wapi katika falsafa zao za kulijenga taifa lako.Haya yote yatakuwa ndoto kama utofundishwa kwa lugha mama ya taifa lako.Kiingereza katu hakiwezi kutuonesha thamani na uzuri wa mila na desturi zetu zaidi ya kuziteketeza kila siku moja baada ya nyingine kwa kisingizio cha mila potofu.Mie tangu kuzaliwa kwangu sijawahi kuona kitu ambacho ni kibaya kwa 100%,lakini mila zetu zinaonekana mbaya sana tena zinaonekana hazifai hata kidogo.hivyo badala ya kuzifanyia marekebisho ili ziendane na wakati uliopo na teknolojia iliyopo,tunakubali ziteketezwe mbele ya macho yetu.kiswahili kina uwezo wa kutuonesha asili yetu,historia yetu,mila na desturi zetu,thamani yake na nafasi yake katika jamii ya zamani na ya sasa.


Fikra sahihi uja kwa lugha sahihi.Sisi wote tunafikiria kiingereza,hatuwezi kuliona hilo kwa sababu sote ni waathirika,kwa sababu hatufikiri kwa lugha sahihi katu hatuwezi kuja nafikra sahihi kwa maendeleo yetu.Tumeathirika kiasi cha kudharau hata wazee wetu siku hizi eti kwa sababu tu hawajawahi kuingia darasani.Tumeathirika kiasi cha kushindwa kutofautisha kati ya msomi na kiingereza,tumeathirika kiasi cha hata cha kutokuthamini vya kwetu wenyewe na hata fikra zetu wenyewe.Mpaka sasa bado tunaamini mtaalam wa kweli ni lazima atoke nje ya nchi,sie wenyewe hatuwezi,kwa sababu tumeshaaminishwa hivyo.Kitu hakiwi kizuri mpaka umekilinganisha na cha kizungu.hivi wewe haujiulizi ni kwa nini matumizi ya misemo na nahau yanapungua siku hadi siku,huku falsafa mbalimbali zilizotolewa kwa Kiswahili na wataalamu na viongozi wetu zikikosa nguvu siku hadi siku? hebu angalia signature za wanaJF halafu utaniambia.ulishawahi kujiuliza ni kwa nini nchi karibia zote zilizoendelea zinafundia kwa lugha mama ya nchi zao,au unafikiri imetokea kwa bahati mbaya.


Kiingereza kimeshindwa kutupatia wataalam wa kweli.Navyofahamu mimi,mtaalamu siku zote ni chanzo cha utatuzi wa matatizo.lakini hebu angalia wataalamu wetu na elimu yetu ya simbi ya chuo kikuu iliyoambatana na fikra za kifisadi.Ukweli ni kwamba wengi wetu tunakariri tu na wala hatujui wala kuzielewa falfasafa zilizobebwa katika masomo tuanayofundishwa huku tukiamini kufaulu ndo suluhisho la matatizo.Na hapo ndo utakaposhangaa,mtu na daraja la kwanza,mkabizi kitengo sasa!Wengi hatuelewi tunachofundishwa,na kama unabisha nenda kawaulize walimu,na kama haujui tatizo ni nini basi leo jua tatizo ni lugha.


Umoja na utaifa wetu.Kiswahili kitaongeza umoja miongoni mwetu zaidi ya ilivyo sasa.Kila mtu atajivunia utaifa wake.Na kama vile haitoshi,Kiswahili pia kitapunguza idadi ya wataalam wanaotokomea nchi za nje kwa kuamini kuwa lugha aliyofundishiwa itampa tabu kufanya kazi sehemu zingine zaidi ya Tanzania


Najua kuna wengi wanaokubali kuna haja ya kubadilisha lugha ya kufundishia,lakini wanakatishwa tamaa na ugumu na gharama za kulifanikisha zoezi hili,kumbuka hakuna kisichowezekana chini ya jua,tunachohitaji ni dhamira ya kweli tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom