Maelfu kusota pasaka na Babu

Monasha

JF-Expert Member
Apr 2, 2011
561
421
ZAIDI ya wagonjwa na ndugu 3,000 watalazimika kusherehekea Mateso, Kufa na Kufufuka kwa Yesu Kristo (PASAKA) na Mchungaji Ambilikile Masapila, wakisubiri
kupata kikombe atakapoanza huduma Jumanne ijayo.

Wananchi hao wamefikia hatua ya kukaa katika Kijiji cha Samunge Wilayani Ngorongoro(kwetu) baada ya kushindwa kumfikia 'Babu' kabla ya sikukuu hiyo kuanza leo.
Ni wazi kuwa pasaka itawakuta watu hawa kwani Babu hataweza kumaliza msururu wa magari unaofikia kilomita 25 kabla sikukuu haijaanza.

Ilielezwa kuwa wagonjwa ambao hawatafanikiwa kupata kikombe hicho kati ya jana na leo watalazimika kusubiri hadi sikukuu hizo zipite kwa kuwa Babu alishatangaza mapema kupumzika siku hizo.
“Ukweli ni kwamba hakuna mgonjwa hata mmoja atakayerudi nyumbani baada ya kufika Samunge baada ya babu kusitisha tiba hiyo kusherehekea Siku ya PASAKA.

Naamini wote waliofika hapa watalazimika kusubiri hadi Jumanne ijayo atakaporudi kazini babu,” alisema Bw. Abdulrahman kutoka Samunge.

Alisema msururu wa magari bado unaongezeka licha ya serikali kutoa taarifu kuzuia wagonjwa na wasindikizaji kutosafiri tena kuelekea Samunge kutokana na Babu kupanga kupumzika.

Mkuu wa Wilaya Bunda mkoani Mara, Bw. Francis Issack, alisema jana kuwa tangu juzi wameanza kuzuia magari yasiende kwa Mchungaji Masapila kutokana na msongamano.

“Juzi kulikuwa na gari kadhaa tulizizuia na hata jana hakuna ruhusa ya gari kuelekea huko,” alisema Bw. Issack.

Hata hivyo habari kutoka Babati na Arusha mjini zinaeleza kuwa bado watu walikuwa njiani kuelekea Samunge licha ya agizo hilo la serikali.

Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Bw. Elias Lali, alisema hali bado ni mbaya na uwezekano wa babu kumaliza idadi ya wagonjwa waliofurika katika kijiji hicho kabla ya Siku ya Ijumaa Kuu ni ndogo.

Alisema kuna uwezekano mkubwa wa wagonjwa hao kushirikiana na Babu kula sikuu ya PASAKA wakisubiri tiba baada ya mapumziko hayo.

"Ndiyo kwanza naelekea huko lakini nikuhakikishie ndugu yangu, uwezekano wa mchungaji kumaliza idadi kubwa ya wagonjwa waliofurika huko kwa muda huu uliobaki ni ngumu.Labda watalazimika kula siku hizo na babu huku wakisubiria siku hizo zifika wapate tiba ndio waondoke,” alisema.

Hata hivyo serikali ndio inayolaumiwa kwa kushindwa kudhibiti mapema idadi ya watu kwa kuwa Mchungaji Masapila alitoa ratiba ya kupumzika PASAKA muda mrefu.

Baadhi ya wananchi Mkoani Mara na Babati walidai baadhi ya watendaji wa serikali wameshiriki kuongeza adha kwa wagonjwa kwa kutoa vibali na kuwaruhusu kuanza safari badala ya kuchukua hatua mapema kulingana na tangazo la Babu.

Katika hatua nyingine wagaonwja hao na ndugu zao wanakabiliwa na hali ugumu ya maisha kutokana na bei za vyakula na bidhaa zingine kuendelea kupaa kwa zaidi ya mara mbili.

Habari zilizolifikia gazeti hili zilieleza kuwa chakula cha bei ya chini ambacho ni ugali ama wali maharage inauzwa kati ya sh 2,500 na 3,500.Maji ya kunywa nusu lita inauzwa sh. 1,000 huku lita moja ikiuzwa sh. 2,000.Mafuta ya petroli pia imepaa hadi kufikia sh 6,000 na 8,000 kwa lita moja.

Gharama nyingine ambazo hazikuwepo siku za nyuma pia zimepanda kutokana bei ya awali huku gharama ya kuchaji simu moja ni kati ya sh 1000 na 1500.


Haya wana jamii kuna una ndugu yako aliyeenda kwa Babu basi uwe tayari kumsubiri kwani babu ndo kwanza anapumzika.
Ataanza kutoa tena huduma Jumanne ijayo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom