Maelezo ya Wizara ya Elimu kuhusu mchakato wa kurekebisha matokeo ya Kidato cha 4

NasDaz,

..asante kwa majibu yako.

..I hope Kitila Mkumbo na Kichuguu watapata nafasi kusoma post yako na kutoa maoni yake.

..mimi nashangaa kusoma kwamba waalimu wa shule mbalimbali walikuwa hawana taarifa kwamba NECTA wamebadili viwango vya ufaulu. imebainishwa kwamba NECTA wanapofanya uamuzi kama huo wizara huwa wanashirikishwa.

..mimi nina swali moja kwako: according to Kitila Mkumbo viwango vipya vya madaraja vilijaribiwa kwa watahiniwa wa 2011 na necta hawakuona matokeo mabaya. sasa kama taarifa hizo ni za kweli, bado unafikiri kilichowafelisha watahiniwa wa 2011 ni viwango vipya vya madaraja??

..It will also be interesting to know nini kilitokea NECTA na WIZARANI baada ya kupatikana matokeo mabaya kiasi hiki.
JokaKuu,
Nimemsoma Kitila Mkumbo, na kwa hakika nimemuelewa vizuri sana! Aidha, sina shaka kwamba baada ya mfumo huo mpya kujaribiwa matokeo ya 2010 & 2011, the margin btn the two systems was found to be narrow! Technically, matokeo ya hiyo margin inaweza kuwa very right. If so, then why wasting time na suala la kutumia viwango vya zamani ikiwa diffrerence yenyewe ni ndogo sana!

But if we raise the concern above (with RED), what if I raise another concern kwamba kulikuwa na maana gani basi ya kutumia mfumo mpya if there's insignificant difference between the TWO systems? Si tuendelee tu na mfumo wa zamani ikiwa hamna tofauti kubwa!!! How does it sound?

Anyway, in short, alichoongea Kitila Mkumbo, mathematically kipo right lakini kimsingi yupo general sana! Hapa kuna sababu kuu mbili za msingi ambazo zimewafanya waone hamna tofauti yoyote! Sababu ya kwanza, population ya wale wanaopata Div IV na ZERO, na sababu ya pili ni Uhalisia wa hizo zinazoitwa Div Four!

Tuanze na sababu hii ya pili coz' ipo wazi kabisa!

JokaKuu, ukipata muda jaribu kupitia matokeo hayo na mkazo uweke kwa wale tulioambiwa wamepata Division Four, ambao kimsingi nao ni wengi sana....I guess, they consitute the largest population! Ukichunguza kwa makini, wengi wa hawa waliopata Div IV wamepata Div Four MBAYA....wengi wamepata Div Four kuanzia Point 30 na kuendelea! Hii maana yake ni kwamba, wengi wao wana angalau "F" tatu! Na kama mtu ana ma-F yote hayo, basi obvious, hata D zenyewe ni za kuvutavuta! Unaweza kuta wengi wao ni wale ambao wana D za 30-40!! Hii maana yake ni kwamba, hata ukitumia system ya zamani ya D ni 21-40, bado hawa watakuwa na D zile zile!

Kwa upande mwingine, kwavile waliweza kupata angalau 4 D's; maana yake ni kwamba wanajiweza weza kidogo to the point kwamba si ajabu hata zile F zao zina kaunafuu! Which means, kama ni kweli viwango vilivyotumika ni vipya, basi ajabu hawa walikuwa na F za(say) 22-29 ambazo ukizileta kwenye OLD system, zinabadilika na kuwa D!

So, what's the NET OUTCOME? Mtu kama huyo bado atakuwa na ile ile Div Four, lakini wakati awali alikuwa na Division IV Point 31, hivi sasa atakuwa na Div IV Point 28! Vipi, nimeeleweka? Kama ndiyo, sasa tuhitimishe! Huyu mtu bado ana Div IV kama mara ya kwanza tofauti iliyopo ni kwamba Div Four ya sasa itakuwa ime-improve tofauti na ile ya zamani...lakini zote ni FOUR! So, ukifanya analysis yako kwa kuangalia Div Four as a whole, utaishia na jibu la DR. Kitila Mkumbo! Difference, haitaonekana BUT when you EXTRACT hizo Div Four, tofauti itaonekana!

Tukirudi kwa wale waliofaulu(Div I,II,III) kutakuwa na the same movement! Lakini tofauti na hao wa juu, movement kwenye kundi hili itakuwa na COMPLETE POSITIVE EFFECT especially kwa wale waliopata B's! Ukiangalia zile takwimu ambazo nilizotoa, utagundua kwamba Div I zilishuka sana na ku-boost watu waliopata Div II ! Hii maana yake ni kwamba hawa walikuwa na vi-C's ambavyo hatimae vikatengeneza hizo Div II! So, kwa kuangalia the same concept, hawa wana uwezo mkubwa na si ajabu C zao zilikuwa ni zile ambazo under normal condition zingekuwa B's na hivyo kuingia kwenye kundi la wale wenye Div I. Aidha, wale waliopata B's na A's ni wale wakali zaidi ambao under normal condition hizo B's zingekuwa ndo A's na kuwapeleka kwenye Division I za Point 7 ambazo kimsingi in 2012 zipo adimu ile mbaya!

Lakini, kwa bahati mbaya kabisa, population hii ya Div I, II, III ni ndogo sana compared na ile ya Div IV na ZERO! So, hata kama kutakuwa na hiyo improvement, kisha ukataka kulinganisha system mpya na miaka ya nyuma, bado utapata jibu kama alilotoa Dr. Kitila Mkumbo! Ingawaje movement kwenye Category hii inaweza kuwa from One Grade to another (say from Div II to Div I, or From Div I ya kawaida to Div I pt 7) bado net effect itakuwa insignificant coz' hii population ndogo itakuwa imemezwa na population kubwa iliyopata Div IV na ZERO na hivyo hapawezi kuonekana tofauti kubwa! Hoja hii ya mwisho, ndiyo inayojibu sababu ya pili ya kwanini hapaonekani tofauti kubwa system hiyo inapojaribiwa kwenye matokeo ya miaka ya nyuma!

Summary ya yote hayo ni kwamba, ikiwa utachanganya wote kwenye kapu moja kisha ukataka kutafuta tofauti, hakika hutaiona na kama utaiona basi itakuwa ndogo! Lakini kama utaamua kufanya case to case basis, lazima tofauti itaonekana!

Ni matumaini yangu kwamba nimeeleweka!
 
Last edited by a moderator:
Mfumo wa ufaulu wa maksi chini ya 50% ndio chanzo cha ufaulu mdogo. Kama viwango vinashushwa uwezo utapungua wa kusoma.
Awali nilidhani tatizo ni la usahihishaji, kumbe sivyo!
Elimu imewekwa sana maji ladha yake imechachuka.
 
Sawa kabisa hayo yote yatafanyika ila wasiwasi wangu ni mwelekeo wa elimu kwa ss unayumbaa!!...actually underperformance
 
NasDaz,

..asante kwa maelezo yako.

..now the question comes: what do we do next year? Or, next 5 years??
 
watu makini hawapimwi kwa mwonekano wa mavazi sura au vyama wanavyotoka,. mustakabali wa Taifa pia haupimwi kwa rasilimali asili zilizopo. vipimo hivi huweza toa matokeo yasiyo sahihi. nionavyo mimi umakini wa watu na taifa huweza kupimwa kwa namna watu wanavyojadiliana na mipango, yao. ndio kusema ukitaka kujua upuuzi wa mtu, anangilia jinsi anavyojenga, na kutetea hoja.
 
Kweli matokeo haya sisi wazazi yametusikitisha sana tumelia pamoja na watoto wetu,kwakweli haya ya kusema mnafuta matokeo ni sawa na safari ya bulicheka ya kukata kuti wakati umelikalia, mlikuwa wapi kabla ya kutangaza kwa Matokeo, kwa kweli tumeumia sana wazazi pamoja na wanafunzi,nimeamini Lukuvi na wenzake kweli ni janga la kitaifa, kuwa na viongozi shule sifuli ni matatizo makubwa, mawazo yao hakuna tofauti na kuku anaangalia pale anapo kula chakula. waswahili wanasema,tembea uone kweli duniani kuna maajabu.uzembe na uelewa wa viongozi wetu ndiyo umetufikisha hapa tulipo.
 
NasDaz,

..asante kwa maelezo yako.

..now the question comes: what do we do next year? Or, next 5 years??
The answer is simple! Kwanza kabisa panahitajika COMMITMENT toka kwa pande zote! Ninaposema pande zote ni kwamba toka Serikalini, Waalimu, Wazazi na Wanafunzi! Tunaweza kuwa na shule bora kabisa in terms of facilities na walimu wanaweza kuwa wanapata benefits bora kabisa! Lakini kama wazazi na wanafunzi hawapo committed, bado ni kazi bure! Kwa mazingira haya haya mabovu yaliyopo hivi sasa, kama wazazi na wanafunzi wanakuwa committed, ufaulu unaweza kuongezeka kwa kiwango cha ajabu kabisa! Nitakupa mifano miwili!

Binafsi O-Level nimesoma St. Anthony's Secondary School! Wakati ule St Anthony's ilikuwa ni among of best schools. Lakini trust me, tulikuwa na waalimu wa hovyo sana! Nakumbuka tulikuwa na mwalimu wa Geography akiitwa Mrs. Mkini! Huyu Mwalimu alikuwa mbovu sijapata kuona! Tulikuwa na mwalimu wa Hesabu Mrs. Mbwana! Hesabu zenyewe hajui! Tulikuwa na Mwalimu wa Biology Mrs. Adam, ni aibu tupu! Lakini ajabu ni kwamba wanafunzi walikuwa wanafaulu sana! WHY? Tulikuwa so committed!

Kwa upande wa pili, turudi Jitegemee Secondary pale JKT Kurasini! Ile shule asikuambie mtu! Jamaa wana kila kitu pale ndani!! Wakati nipo St Anthony's nilikuwa natumia sana notice zao, manake zilikuwa bomba ile! Lakini pamoja na yote hayo, Jitegemee ni one of the worst schools in the country! Ni jambo la kawaida sana pale kukuta kuna Four zaidi ya 400 na Zero zaidi ya 200! Sijaangalia matokeo yao 2012, lakini najua ni dhahama tupu! Kwanini? Coz' wanafunzi hawapo committed na wala wazazi inaelekea hawajali kinachoendelea kwa watoto wao! Nakumbuka enzi zetu tulikuwa tunatembea na Tape(audio tapes) mifukoni zenye instruments(beats) peke yake! Ikifika wakati wa Break tunaenda Jitegemee kushindana ku-rap na madogo wa pale! Sasa hapo unafikiri kuna kitu kweli hapo?!

A-level nilikuwa Tambaza! Kama ujuavyo, shule za serikali ndo hivyo tena, hadi kwa Tution! Trust me, wanafunzi wa Ilboru na Mzumbe walikuwa hawataki kuchanganyika na sisi kupiga tution; walikuwa wanadai sisi ni mabishoo, hatupo serious!! Kuna washikaji zangu walikuwa wanakaa hostel pale Tambaza! Ajabu ni kwamba, ilikuwa kila tukifika asubuhi wanatupigia story za mademu(machangu doa) wa mitaa ya Ubalozi!!ul Just imagine, wakati ule tulikuwa wadogo tu, lakini washikaji usiku kazi yao ilikuwa ni kwenda kupiga machangu doa! What do you expect? Nikirudi mitaa ya home, nakumbuka ucku tulikuwa tunajisomea pale DSA(TIA)! Ajabu ni kwamba, kulikuwa na washikaji fulani hivi toka Ilboru! Kama ilivyo wa kule kwenye tuition, hao nao walikuwa vilevile! Hawa walikuwa wanakuja pale saa 4 ucku wakati sie wengine ndo tunatoka! Tulikuwa sifahamu wanatoka saa ngapi hadi siku moja ndo nikakutana nao alfajiri! Hapo unaweza kuona ni namna gani wengine wapo committed na wengine wasivyo committed kiasi kwamba hata matokeo miongoni mwao yalivyo tofauti! Na hili suala la commitment ndilo linalo-define kwamba why the same school, the same class from the same locality, wengine wanapiga sana paper, na wengine wanafeli sana paper ile ile! hapa ni suala la COMMITMENT tu, mengine ziada! Unaweza kuwa na best schools in terms of teachers, libraries, laboratories, and whatever....but if no commitment from both sides, ni sawa na hakuna! Hili watu hatutaki kuliona kwavile waTanzania tumezoea kulalamika na kulaumu huku tukiwa hatutaki kujichunguza! Watu wanasahau kwamba zamani walikuwa wanasoma chini ya miembe kile kilichoitwa elimu ya watu wazima, na baada ya hapo wanatoka huku wakijua kusoma, kuandika na kuhesabu! Lakini sasa, mwanafunzi hata baada ya miaka saba darasani, lakini wengine wanatoka wakiwa hawajui kusoma wala kuandika!

Baada ya hilo la commitment kutoka kwa wanafunzi na wazazi, commitment nyingine hapa ni kutoka kwa walimu! Ni kweli maslahi ya walimu ni madogo sana; lakini mtu aniambie ni kada gani serikalini yenye maslahi makubwa ukiacha ile ya watawala na watendaji wakuu wenyewe? Mwalimu mwenye Shahada leo hii anapata mshahara unaofanana fanana na graduates wengine! manake watu wanavyoongea utafikiri labda Mchumi mwenye shahada(first entry) anapata milioni moja na mwalimu mwenye shahada anapata laki 2 wakati wote hawa wanapata somewhere above 530,000 but less than 600,000/=!! So, hata kama mwalimu leo hii atalipwa sh.2m lakini hana commitment, bado ni kazi bure! Commitment haitokani na mshahara mkubwa bali inatokana na kujitambua kwamba kwanini upo mahali husika!

Kama nilivyozumngumza hapo awali, kundi lingine linalotakiwa kuwa committed ni serikali! Hapa lazima watekeleze wajibu wao! Watekeleze wajibu wao sio tu wa ku-recruit walimu bali walimu bora! Watimize wajibu wao wa kutoa maslahi bora kwa walimu, wajibu wa kutoa vitendea kazi bora na mengine sawa na hayo!!

Jambo la mwisho dogo ni kwetu sie wananchi tuache kuwadekeza walimu! Walimu hawajali coz' wanafahamu kwamba hata wakiharibu, watatetewa tu na wananchi kwa kauli zetu za "serikali haiwajali walimu" as if kuna kada nyingine inayojaliwa! Walimu nao ni sehemu ya tatizo lakini kila cku tunawatetea! Wananchi wanazunguka pamoja na walimu mitaani wakati wa kazi, matokeo yakija kuwa mabovu tunailalamikia serikali! Tuache kuona kwamba walimu kuingia darasani na kufundisha is just a favor; hii sio favor bali ni wajibu wao and they're being paid for it! Miaka nenda rudi serikali haiwajali walimu lakini miaka nenda rudi form six graduates wanaenda Ualimu tena wengine wakiwa wamepata pass nzuri tu; sasa wanaenda kufanya nini kule?! Lazima wananchi tupunguze ku-side upande wa walimu na hatimae watagundua kwamba wao kuingia darasani na kufundisha sio favor kwa wananchi/serikali bali ni wajibu wao!

Hayo yote yakitimia, basi hata kama utaweka kiwango cha ufaulu ni marks 70, watu watafaulu tu kinyume chake ndiyo hayo yaliyotokea! just COMMITMENT kila upande na sio serikalini peke yake! Lakini committment ya kwanza kabisa inatakiwa kutoka kwa wazazi na wanafunzi, lakini kwavile wakati mwingine wanafunzi wanakuwa ni watoto wasiojitambua basi hapa wazazi wanatakiwa ku-bear responsibility! Wazazi waache kuona kwamba wajibu wao unaishia kwenye kutoa vitendea kazi na nauli ya kwenda na kurudi shule bila kujali ikiwa huko shule kwenyewe wameenda au hapana!
 
useless people where are we taking this country we need people who are upright to lead this country we are tired of these crooks, Let the go to hell, Politics and education can never walk together, Let the experts do there work Lukuvi is a stdr 7 so he cant know the negative impact this will have of the future generation
Wewe ni mtu wa mfumo....... unafurahi ukiona watoto wa wenzako wanakuwa vibaka kwa kazi mlizozifanya na NDalichako wako!
Waziri alishaagiza. very clear! tunasubiri matokeo mapya. Acheni kuhujumu nchi hii!
 
WEWE ACHA KULAUMU SHULE ZA SERIKALI! WATU WOTE HAO WANAOIHUJUMU ELIMU YA TZ(NECTA) WOTE WATOKEA KATIKA SHULE ZA SERIKALI. KINACHOFANYIKA SASA AKINA DR NDALICHAKO WANAFANYIA WATU KAZI....BRIBED BY PRIVATE SCHOOLS OWNERS... ILI WAZIFELISHE SHULE ZA SERIKALI NA KUZIPSISHA ZA PRIVATE KWA SABABU YA RUSHWA! HILI LINAJULIKANWA NA KILA MTU BALI WATANZANIA WANAKUFA NA KAMBA SHINGONI TU BILA KUSEMA!
Mfumo.....at work men!
 
kweli matokeo haya sisi wazazi yametusikitisha sana tumelia pamoja na watoto wetu,kwakweli haya ya kusema mnafuta matokeo ni sawa na safari ya bulicheka ya kukata kuti wakati umelikalia, mlikuwa wapi kabla ya kutangaza kwa matokeo, kwa kweli tumeumia sana wazazi pamoja na wanafunzi,nimeamini lukuvi na wenzake kweli ni janga la kitaifa, kuwa na viongozi shule sifuli ni matatizo makubwa, mawazo yao hakuna tofauti na kuku anaangalia pale anapo kula chakula. Waswahili wanasema,tembea uone kweli duniani kuna maajabu.uzembe na uelewa wa viongozi wetu ndiyo umetufikisha hapa tulipo.
kama kawaida yenu watu wa mfumo...hamuoni chanzo cha tatizo bali matokeo yake... Kwani lukuvi yuko kwenye secretatieti ya necta? Mbonda ndalichako na mukandala, na necta yao hamuwasemi? Si hawa ambao wameiharibu elimu ya tanzania.... Mnajua wanatumikia parokia ndio maana hamuwagusi sio?
 
Mfumo wa ufaulu wa maksi chini ya 50% ndio chanzo cha ufaulu mdogo. Kama viwango vinashushwa uwezo utapungua wa kusoma.
Awali nilidhani tatizo ni la usahihishaji, kumbe sivyo!
Elimu imewekwa sana maji ladha yake imechachuka.

Ni kweli mkuu. Kwakuwa unga ni kidogo basi tunajaribu kuongeza maji ili tupate ugali wa kutosha!

kama kawaida yenu watu wa mfumo...hamuoni chanzo cha tatizo bali matokeo yake... Kwani lukuvi yuko kwenye secretatieti ya necta? Mbonda ndalichako na mukandala, na necta yao hamuwasemi? Si hawa ambao wameiharibu elimu ya tanzania.... Mnajua wanatumikia parokia ndio maana hamuwagusi sio?

Siamini sana kwamba lazima kila msafara wa mamba kenge nao wawepo ila kwa ushauri wa bure ukiona uzi kama huu unachangiwa na wenye akili si lazima sana ukaleta pumba zako humu ndio maana wengi wanakupuuza na hawakujibu.

Wakuu haya matokeo yanatoka lini sasa maana tumeambiwa hawasahihishi upya ila wanapanga tu. Hivi karibuni ya kuyatangaza ni lini?
 
wewe acha kulaumu shule za serikali! Watu wote hao wanaoihujumu elimu ya tz(necta) wote watokea katika shule za serikali. Kinachofanyika sasa akina dr ndalichako wanafanyia watu kazi....bribed by private schools owners... Ili wazifelishe shule za serikali na kuzipsisha za private kwa sababu ya rushwa! Hili linajulikanwa na kila mtu bali watanzania wanakufa na kamba shingoni tu bila kusema!
Mfumo.....at work men!

ndugu umechemka kweli na tatizo siyo wewe ila hufahamu jinsi necta inavyofanya kazi,wanaoharibu ni ni wana siasa na hasa wa ccm
 
Serikali kupitia Wizara ya Elimu kwa kauli hiyo inasema uthamani wa matokeo ushushwe ili ufaulu uwe na taswira nzuri na si uhalisia wa ubora wa kipimo cha mtihani.

Si kosa la serikali ni kosa la walioiweka serikali madarakani. Waziri Kawambwa ni mtoto wa nasaba ya Kikwete; tafuta ufaulu wao kwenye mitihani utajiridhisha walioiweka serikali hii madarakani wametuua bila kututazama.

TAFAKARI CHUKUA HATUA.
o
Good point....safari bado tunayo japo tunakaribia na mwisho wake 2015. Ukweli dv 3/4"zitaongezeka na ndo hao wataenda ualimu-walimu watakao fundisha kwa viwango vya chini- na waitimu wasio jua haki zao-hivyo sism kuendelea kutawala kwa support yawasiojitambua.
 
Back
Top Bottom