Maelezo ya Wizara ya Elimu kuhusu mchakato wa kurekebisha matokeo ya Kidato cha 4

useless people where are we taking this country we need people who are upright to lead this country we are tired of these crooks, Let the go to hell, Politics and education can never walk together, Let the experts do there work Lukuvi is a stdr 7 so he cant know the negative impact this will have of the future generation

tunduruboy,

Wewe ndiyo useless person!Your broken English reveals and tell the true inside of you. Sijui kiwango chako cha elimu, na wewe ulipata daraja gani F4 yako,ninachotaka kukuambia ni kwamba ulichoongea ni pumba na hakina mantiki.
Tangazo la Wizara ya Elimu liko wazi kabisa kwamba wanatekeleza agizo la Serikali kukingana na maelekezo ya Tume ya PM kuwa LAZIMA MCHAKATO WA MATOKEO YA F4 MWAKA 2012 UFANANE NA MICHAKATO YA MIAKA YA NYUMA(GRADING PROCESS) AMBAO UMEKUWA UKITUMIKA TANGU MWAKA 1973. SINA HAKIKA KAMA ULIKUWA UMESHAZALIWA!

Sasa kama utaratibu wa Grading umekuwa ukitumika kwa miaka yote tangu 1973,utaratibu ambao hata mimi umeweza kunifikisha hapa nilipo na elimu yangu nzuri kabisa ambayo nina hakika hata tukiingia darasani leo ninatoka na flying colours. Iweje vijana,watoto na wadogo zetu leo wafelishwe kwa kutumia utaratibu mpya baada ya miaka 40?????!!!!

Umesema 'politics and education can never walk together'!!Seems you don't know what you're talking. SERA ZA ELIMU MAHALI POPOTE DUNIANI ZINAHUSISHA SIASA KWA MAANA WANAOTUNGA SERA NI HAOHAO WANASIASA(WABUNGE) WALIOCHAGULIWA NA WANANCHI WENYEWE. So, you can never separate politics and education. Never!

Acheni NECTA wafanye kazi yao kulingana na maelekezo ya Tume na Serikali halafu tuone sasa matokeo yatabakia vilevile au kutakuwa na mabadiliko. Kama mwanafunzi wa kidato cha 4 mwaka 2011 alipata D kwa kupata alama 30% kwa utaratibu wa (D:alama 21-40) kwa utaratibu ulokuwa unatumika tangu 1973 lakini mwanafunzi wa kidato cha 4 mwaka 2012 aliyepata 30% apate F(F:alama 0-34)???
 
Watanzania tunahaki ya kujua kilicho sababisha Baraza la Mitihani kuachana na mfumo uliokuwa unatumika toka 1973... Sababu za kurejea mfumo huo zinajulikana kuwa ni kuongezeka kwa kasi watahiniwa waliofeli! Je nini kilisababisha Baraza kubadili mfumo?...
Tusifanye mchezo katika elimu hata kidogo, hapa ndipo ambapo Taifa linazalisha madaktari, mainjinia, marubani, manahodha, wapiganaji, wanasiasa, waalimu aitha vipanga ama vilaza!...Kama Taifa, maendeleo yetu yatategemea na uwezo wa Rasilimaliwatu tuliowaandaa...
Kwa upande wa pili wa shilingi; Tunaweza kuendelea kutawaliwa kiakili na kimwili kwa kukosa maarifa! Kwa kukosa maarifa tunajikuta RASILIMALI zetu hazitusaidii bali zinawanufaisha mabeberu plus makuwadi wachache... nina mashaka na huu mkakati unaoendelea kama kweli unaangalia maslahi mapana ya Taifa letu, na si mbinu za kutufanya duni na kuendelea kutawaliwa kwa miongo mingine mingi ijayo...
Mkuu hoja yako ni ya msingi sana. Lakini kabla ya kujua hilo uliwahi kujiuliza ni kwanini matokeo ya CSEE 2012 kwa mara ya kwanza katika historia ya uanzishwaji wa Baraza la Mitihani na tokea Dr. J. Ndalichako aingie madarakani, hakutangaza yeye bali alitangaza Waziri wa Elimu Dr Kawambwa mwenyewe.

Wa-TZ tukiendelea kuchanganya siasa mpaka kwenye mambo nyeti ya kitaalamu kama Elimu tumekwisha.
 
mkuu LUKUVI katoa tamko kama serikali, suala la kupitia upya mtokeo ni limekuja baada ya wataalam kukaa ni kufikia muafaka huo, unaweza kujifanya na kiingereza chako, lakini kumbe hujui hata kinachoendelea

Shida kubwa inayoangamiza taifa letu ni kufanya kila kitu siasa, kila kitu serkali inachofanya ni kuhakikisha wananchi hawachukii, hata kama sio swala la siasa. Baraza la mitihani liko chini wizara ya elimu sasa kwakuwa sura kufeli kwa watoto sehemu ilichangiwa na serikali kwa kutoa elimu duni! alafu sasa mzigo wanawatwisha baraza la mitihani heti walibadirosha viwango!!

Haya mambo yanapatiana Tanzania tu! Kwani matokeo hayawezi kutangazwa mpaka yapitie wizarani, kwanza serikali illizika ndo waliyatangaza. Lakini yakuona wananchi wamechukia ndo waamua kuyachakachua ili wapiga kura wafurahi.

Mambo ya kuwa ni mapendekezo ya tume kuna walakini.
 
Wizara ya Elimu watafute underline cause ambayo wanajua kuwa ni mitaala mibovu, walimu wasio na uwezo, mazingira mabovu na kukabiliana athari hasi za utandawazi kwa wanafunzi si standardization wala kusahihisha mitihani upya na masuala yafanywe na wataalamu si wanasiasa.

wakati wanaangaika kuchakata matokeo ya form four ya form six yapo njiani sijui nayo yataingia kwenye uchakataji huu ili kuwafurahisha wananchi kwa ufaulu wa juu wakati ni changa
 
Hivi kwa nini usitumie kiswahili?....kiingereza hiki ndicho ulichotumia kujibu mitihani 2012....? hata Le Mutuz hawez ongea hiv...kibovu sana...pu...mb....a.fu

Kiingereza ni lugha ya pili, tatu au hata ya nne kwa baadhi ya watu. Ni sawa na ww Mmakonde ukajifunza Kigogo, huwezi kukosa makosa ktk matumizi. Mwenziyo amejitahidi kukitumia we unamtukana badala ya kumkosoa pale ww unapoona amekosea..., hatuwezi kufika popote maana mvunja nchi ni mwananchi!
 
Mwaka huu tutayabadilisha sawa lakini tatizo halijatatuliwa je, tutayabadilisha kila mwaka kwa kua mumeshindwa kutatua matatizo ya walimu ambacho ndio chanzo cha watoto kufeli kila mwaka?
 
Its a Hypocrite country,, hata kama wakirekebisha,, ila wajue kuna maisha ya wanafunzi yameharibika,,wachache wamejiua,, na wengi there state of mind its disrupted,,

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
NasDaz,

..asante kwa majibu yako.

..I hope Kitila Mkumbo na Kichuguu watapata nafasi kusoma post yako na kutoa maoni yake.

..mimi nashangaa kusoma kwamba waalimu wa shule mbalimbali walikuwa hawana taarifa kwamba NECTA wamebadili viwango vya ufaulu. imebainishwa kwamba NECTA wanapofanya uamuzi kama huo wizara huwa wanashirikishwa.

..mimi nina swali moja kwako: according to Kitila Mkumbo viwango vipya vya madaraja vilijaribiwa kwa watahiniwa wa 2011 na necta hawakuona matokeo mabaya. sasa kama taarifa hizo ni za kweli, bado unafikiri kilichowafelisha watahiniwa wa 2011 ni viwango vipya vya madaraja??

..It will also be interesting to know nini kilitokea NECTA na WIZARANI baada ya kupatikana matokeo mabaya kiasi hiki.

Kama nilivyoeleza kwenye makala yangu kwenye Raia Mwema, hakuna kigeni katika hili. Serikali inafanya propaganda katika jambo kubwa kama hili. Kila kitu kinajulikana na kilijulikana serikali, kwa sababu hakuna wanachoweza kufanya NECTA bila serikali kujua. Kumbuka NECTA ni moja ya vyombo vinavyoangaliwa sana na usalama wa taifa kwa sababu nzuri kabisa. Sasa watanzania tumezoea kudanganywa na kudanganyika. Kinachofanyika ni kujaribu kufukia takataka ndani ya carpet na kujidanganya kwamba takataka hizo hazipo!!
 
mbona Lukuvi mwenyewe hamtaji yeye digree zake za wapi? Mrema je mwenye digree ya kuangua maembe ha-ha-ha!
 
Katika hili mimi msimamo wangu upo clear….kimsingi unategemea sana na FACTS zinazotengeneza sakata hili! Kwa bahati mbaya kabisa, hakuna ambae ametamka bayana kuhusu hivyo viwango vya 2012 na vya miaka ya nyuma!

Naamini umenifuatilia kwenye posts zangu nyingi kwenye sakata hili. Mara kwa mara nimekuwa niki-refer taarifa ambayo ipo kwenye page ya facebook ambayo inadai ni official page ya NECTA ingawaje ukiangalia vizuri unakuta ni kama vile official page ya HakiElimu or someone else! Taarifa ile inadai kwamba Serikali imetoa viwango vipya ambavyo vitaanza kutumika 2013 ambapo, badala ya F kuanzia 0-20, kuanzia 2013 F itaanzia 0-34! Aidha, badala ya D kuanzia 21-40, mitihani kuanzia 2013 D itaanzia 35-44! Aidha, kwa mujibu wa Raia Mwema, wao wanadai viwango hivyo vipya ni kama ifuatavyo:
A = 85%-100% ....B = 65%-84% ....C = 50%-64% ....D = 35%-49% ....F = 0%-34%

Wakati viwango vya zamani ni hivi hapa chini:
A = 81%-100% ....B = 61%-80% ...C = 41%-60% ....D = 21%-40% ....F = 0%-20%.
Hapa chini, ni baadhi ya aya za habari hiyo kutoka gazeti la Raia Mwema.

Ni katika mazingira hayo taarifa ya mabadiliko katika utaratibu wa muda mrefu wa gredi za ushindi inakuwa habari kubwa. Alama zinazofahamika kwa muda mrefu ni A- alama 81 hadi 100; B- alama 61 hadi 80; C-alama 41 hadi 60; D- alama 21 hadi 40 na F- alama 0 hadi 20.

Kwamba alama hizo zimekuwa zikibadilishwa na Baraza la Mitihani (NECTA) katika kile kinachojulikana kuwa ni standardisation ni taarifa iliyowatisha wengi. Ni hali iliyowaathiri kwa aina ya pekee watahiniwa wa mwaka 2012, hata kama kwa miaka karibu mitano ya nyuma matokeo ya kidato cha nne, na hata ya kidato cha sita, yamekuwa yakionyesha kuserereka kuelekea chini.

Vyanzo kadhaa vya habari vinasema alama hizo sasa ziko katika makundi ya A-alama 85 hadi 100; B-alama 65 hadi 84; C-alama 50 hadi 64; D-alama 35 hadi 49 na F alama 0 hadi 34

Hivyo basi, mimi hoja yangu inasimama pale pale kwamba...ikiwa ni kweli kwamba viwango vipya vilipaswa kutumika 2013 na badala yake Baraza wakavitumia 2012; hili jambo si sahihi na haijalishi ni wakati gani Wizara walifahamu jambo hilo!

Hapa chini, ni kauli kuhusu Mkuu wa Shule wa Azania kutoka kwenye gazeti hilo hilo la Raia Mwema!

Mkuu wa Shule ya Sekondari Azania, Dar es Saalam, Bernard Ngozye, anasema matokeo hayo mabaya yaliwashangaza wadau wa elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam kiasi cha wao kukutana na kuhoji Baraza la Mitihani kujua chanzo ni nini. Anasema Machi mwaka huu walikutana na maofisa wa Baraza la Mitihani na ndipo hapo walipoambiwa kwamba Baraza lilirekebisha gredi, taarifa hiyo wakiisikia kwa mara ya kwanza.
Anasema Machi mwaka huu walikutana na maofisa wa Baraza la Mitihani na ndipo hapo walipoambiwa kwamba Baraza lilirekebisha gredi, taarifa hiyo wakiisikia kwa mara ya kwanza.

Aidha, gazeti lilimuhoji Mwalimu mwingine wa Shule ya Sekondari Kiteketeke iliyopo Newala. Hii ndo kauli ya Mwalimu huyo(Mkuu wa Shule):

“Walikuja hapa wenzenu. Niliwaambia haya haya. Mmoja baadaye akaniuliza kama nilikuwa ninajua kwamba gredi za Baraza ziko juu, nikasema hapana,” anasema Fredy John, Mkuu wa Shule ya Sekondari Chitekete, Newala, Mtwara, ambayo ni kati ya shule 10 zilizofanya vibaya zaidi kitaifa.

Hao hao Raia Mwema wakiongea na Mkuu wa Shule mwingine, Mkuu huyo anasema:

"Hapana. Hatujui kama kuna mabadiliko hayo ya alama za madaraja ya ufaulu. Wakibadili si lazima walimu na wanafunzi wawe na taarifa? Haya mabadiliko hayapo," alisema Magesa, ambae ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Mukituntu; Ukerewe Mwanza!

Hapa maana yake ni nini? Kumbe mabadiliko muhimu kama hayo ni lazima shule zifahamu na bila shaka ndio maana Mr. Magese ame-conclude kwamba no such changes coz’ hawana taarifa yoyote kama hiyo!

Kwamba shule zetu zina matatizo ya Waalimu, si jambo geni hata kidogo! Hoja kwamba shule zetu hazina maabala; kwangu si hoja coz’ masomo ya Art na Biashara hayahitaji Maabara na bado ufaulu wao ni mdogo! Kwamba shule za serikali zina matatizo lukuki; ni chizi tu ambae anaweza kukataa ukweli huo! Hata hivyo, ngoja tuone kauli ya Mwalimu mwingine ambae alihojiwa na Raia Mwema:

“Nami matokeo haya yamenishangaza sana. Shule yangu haina matatizo ya walimu, maabara wala maktaba, lakini imefanya vibaya tofauti na matarajio yetu,” anasema Sid Moir, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Katoke Lweru, Muleba, Kagera.

For more, link hii hapa: Raia Mwema - Siri ya waliofeli kidato cha nne 2012 nje nje

So what was so special in 2012? Anyway, ngoja tuchukue baadhi ya shule za mfano ambazo wadau wengi wanazifahamu.....kimsingi, nimeangalia zile maarufu na zenye kufaulisha kulingana na kundi husika!

Ukitaka kufanya Statistical/Mathematical Analysis, matokeo hayo yatakuwa kama ifuatavyo. Matokeo haya ni for three consecutive years, 2012, 2011 and 2010:
Div IDiv IIDiv III Div IVFLD TOTALPSD(I,II,III) Div IV+FLD %PSD %FLD
Marian Girls 42 36 8 2 0 88 86 2 97.7 2.3
73 30 10 1 0 114 113 1 99.1 0.9
75 4 2 0 0 101 101 0 100 0.0
Feza Boys 48 12 8 1 0 69 68 1 98.6 1.4
44 8 4 0 0 56 56 0 100 0.0
60 16 7 1 0 84 83 1 98.8 1.2
St Anthony’s 10 36 60 126 1 233 106 127 45.5 54.5
21 50 78 85 0 234 149 85 63.7 36.3
49 71 88 33 0 241 208 33 86.3 13.7
Kirinjiko 2 20 62 45 0 129 84 45 65.1 34.9
8 25 33 49 0 115 66 49 57.4 42.6
11 36 59 45 1 152 106 46 69.7 30.3
Mzumbe 32 35 16 16 3 102 83 19 81.4 18.6
63 28 14 6 0 111 105 6 94.6 5.4
60 20 10 11 1 102 90 12 88.2 11.8
Ilboru Sec. 20 38 30 27 0 115 88 27 76.5 23.5
40 23 24 14 1 102 87 15 85.3 14.7
48 12 19 11 0 90 79 11 87.8 12.2
Azania 14 47 57 137 180 435 118 317 27.1 72.9
48 34 66 138 71 357 148 209 41.5 58.5
56 62 122 207 159 606 240 366 39.6 60.4
Kibaha 26 41 25 13 2 107 92 15 86.0 14.0
59 22 15 8 0 104 96 8 92.3 7.7
53 18 21 14 0 106 92 14 86.8 13.2

KEY: PSD = PASSED
FLD = FAILED
FIRST ROW for each School= 2012 RESULTS
SECOND ROW for each School= 2011 RESULTS
THIRD ROW For each School = 2010 RESULTS

Aidha, kwenye mchanganuo huo hapo juu, Division IV na Zero zote kwangu ni FAILURE tu!

Kimsingi nimeamua kuyaweka kwa staili hiyo ili kujibu yale madai kwamba matokeo yamekuwa yakishuka mwaka hadi mwaka! Ukiangalia takwimu hizo, jibu ni KWELI matokeo yamekuwa yakishuka mwaka hadi mwaka. Lakini hata hivyo, hatuna budi kuangalia ushukaji huo umekaaje! UKichukua wakali wa serikali hapo juu, utakuta the theory prove TRUE only for ILBORU ambao mwaka 2010 walifeli 12.2% na mwaka 2011 walifeli 14.7%. Hata hivyo, pakatokea STEEP GRAPHICAL FAILURE in 2012 tofauti na ile ya 2011 taking 2010 as a benchmark! Hali kadhalika, Kibaha, Azania na Mzumbe kulikuwa na improvement ukiangalia matokeo ya 2011 kwa kulinganisha na yale ya 2010. Pamoja na yote hayo, bado nako pakatoea STEEP GRAPHICAL FAILURE kwa mwaka 2012 kuliko mwaka wowote ule huku kukiwa na almost DOUBLING kwenye failure ukichukua takwimu za 2011 na zile za 2012! WHY? Uhaba wa Walimu? Madawati? Mahabara? Nini hasa? Kama hizo ndizo sababu; ina maana uhaba huo umeibuka 2012?!

Turudi kwa shule za binafsi.
Ukiondoa Kirinjiko ambao wanaonekana wame-improve 2012 as compared to 2011; wengine wote wanaonekana wameharibu zaidi! Feza Boys from 0.0% to 1.4% wakati Marian Girls from 0.9% to 2.3%! S.t Anthony's Sec hali ndio mbaya zaidi! Percentage Failure ime-shoot from 36.3% in 2011 to 54.5% in 2012! What's wrong na kwenye hizi shule? Nako kuna uhaba wa Walimu? Madawati?Mahabara? Tatizo nini?!

Do these two categories share COMMON problems/challenges?! If not, what type of agent that drove all these categories to the current position (in 2012) as compared to years before?!

Generally speaking, hapa KUNA KITU! Suala la kujiuliza, ni nini hasa hicho kitu?! Ikiwa uhaba nilioutaja hapo juu do not seem to prove TRUE to both categories, so kwanini nisishawishike kwamba tatizo la msingi la 2012 sio lile tulilozoea kulisikia year after year? Ikiwa 2012 watu wamezungumzia suala la Madaraja Mapya, nina sababu gani za msingi za kutokubali hoja hiyo?! It's only GRADE RANGES ndiyo inayoonekana ku-prove TRUE in both categories na kinyume chake ni kuleta ILLOGICAL ASSUMPTIONS!

Na kwa hakika, matokeo haya yana-reflect madai ya kwamba viwango vilivyotumika sio vile vilivyozoeleka! With EXCEPTION of Feza Boys, shule zote hapo juu ufaulu wa Daraja la Kwanza umeshuka sana almost by half kwa kila shule! Did it happen by CONCIDENCE? No, I Don't Think so!

Sasa turudi kujichunguza wenyewe!! Nashawishika kuamini kwamba ni idadi ndogo sana ya wale watoto waliomaliza kidato cha nne mwaka jana ambao wanaingia sehemu kama JF! Hata hivyo, sina shaka hata kidogo kwamba humu jamvini kuna Wanafunzi wengi sana wa elimu ya juu!

Mathalani, wakati nipo SUA, grade zetu zilikuwa hivi:
71-100=A, 65-69=B+, 60-64=B, 50-59=C, 40-49=D, 0-39= E
Kwavile inasemekana kwamba Baraza walitumia viwango vipya bila wadau kufahamu; tu-assume SUA nao wanaamua kutumia viwango vipya bila wanafunzi kufahamu na kuwa kama ifuatavyo!
75-100=A, 70-74=B+, 64-69=B, 55-63=C, 46-54=D, 0-45=E

Tuseme paper imekuja, mwisho wa siku umepata 52! Hapo unapumua na kujiona umepata C (50-59)! Matokeo yanatoka kwenye notice board, unakuta umewekewa D (46-54)! Ukihoji, unaambiwa madaraja yamebadilishwa!! Tuwe wakweli, hivi huko vyuoni kweli kungekalika?! Yaani uambiwe from nowhere kwamba Madaraja yamebadilika; ya mwaka huu ni tofauti na ya mwaka jana!! The same situation iwe pia kwenye vyuo vyote nchini!

Let's be sincere here! Hivi kama ni kweli madaraja yaliyotumika ni tofauti na yale ya kila mwaka; halafu tu-assume the same SCANERIO inatokea upande wa Elimu ya Juu halafu utafiti ufanyike na kugundua kwamba tatizo ni viwango vipya ambavyo vilitumika kinyemela kisha serikali ikaamua viwango vya zamani vitumike hadi pale wadau watakapokuwa well informed.....hivi criticism hizi tunazoziona leo hii hapa bado zingekuwepo? Au kwavile wale watoto hawana wa kuwasemea ndio maana tunakata shauri la kuwala nyama mbichi kwa uzembe wa Baraza na Wizara? NO, tuache ubinafsi wa kujiona kwavile tumeshavuka mto, basi haya hayatuhusu! Hakika, tutafute pengine pa kuisulubu serikali lakini hapa sio pahala muafaka!

Aidha, lazima tukumbuke kwamba hawa madogo ndo kwanza wameanza safari! Matokeo haya ndiyo ambayo kesho na keshokutwa yatakayotumika ku-determine their future! Ni matokeo haya haya ambayo wengine yatatumika kama Competitive Edge/ Leverage katika ku-apply international Scholarships!! Tuseme mtu amepata 83; hii maana yake ni kwamba, kwa viwango vya kawaida, huyu mtu angekuwa na "A" lakini kwa viwango hivyo vipya, atakuwa amepata "B" na hivyo ku-minimize his/her competitive edge!!

What do I say about hivyo viwango vipya? Binafsi, sina tatizo na viwango vipya hata kidogo! And in fact, ilikuwa ni utani kwenye elimu kudai kwamba aliyepata 22% nae amefaulu! Haya yalikuwa masihara kwenye mustakabali wa elimu! Hata hivyo, ninachopinga mimi ni utumikaji wa viwango vipya kinyemela(kama ni kweli).Hili kwa hakika halikubaliki! Tutafute pa kuisurubu serikali lakini sio katika hili la kuamuru kutumika kwa viwango vya zamani PROVIDED ni kweli viwango vilivyotumika ni vipya! Nitakuja hapa kuungana na wote wanaopinga STANDARDIZATION IF and only IF itakuja kuthibitika kwamba madai ya kutumika kwa viwango vipya 2012 yalikuwa ni MADAI YA UONGO! Kinyume chake, matokeo lazima yarekebishwe na wahusika waliofanya mambo sensitive kama haya kinyemela wanapaswa kuondoka na si lazima wasubiri kuondoshwa!

c.c Kichuguu
Kitila Mkumbo,

..naomba kama una nafasi utusaidie kujibu maswali ambayo NasDaz ame-raise ktk posting niliyo-quote hapo juu.
 
Last edited by a moderator:
mkuu LUKUVI katoa tamko kama serikali, suala la kupitia upya mtokeo ni limekuja baada ya wataalam kukaa ni kufikia muafaka huo, unaweza kujifanya na kiingereza chako, lakini kumbe hujui hata kinachoendelea

Mkuu naomba unisaidie kuelewa hapa kwa kiswahili, kuna utaalamu gani wa kupitia upya mtihani unaoweza kumfanya mtoto aliyefeli kwa vigezo vilivowekwa na afaulu kwa vigezo hivyo hivyo na mtihani huo huo aliofanya?. Lugha pia hata kama ni kiswahili inatusumbua baadhi yetu ambao vidato vimetupita, "kupitia upya" kama watalaamu walivyokutana wanataka tuelewe nini, ni mtaalamu gani mwenye uwezo huo wa kupitia, bila kuchakachua na yaendane na matakwa ya kitaalama? Bila kujali kama ni Lukuvi amesema kwa niaba ya serikali, au kama ni kwa niaba ya "watalaamu", kitendo hiki cha kuboresha matokeo ili kuridhisha wazazi wa watoto waamini kuwa watoto wao wanafanya vizuri.

Kwa watu wa kawaida wa mtaani kama mimi, tunaona kuwa ni kama mchezo wa kuhamisha goli ili mshambuiliaji mzembe afunge. Kuchakachua matokeo ya uchaguzi labda kunaweza.......lakini kuchakachua hata matokeo ya mtihani wa kitaaluma? kidogo hapo mkuu inaleta mashaka kuhusu utaalamu wa wataalamu.
 
Mkuu hoja yako ni ya msingi sana. Lakini kabla ya kujua hilo uliwahi kujiuliza ni kwanini matokeo ya CSEE 2012 kwa mara ya kwanza katika historia ya uanzishwaji wa Baraza la Mitihani na tokea Dr. J. Ndalichako aingie madarakani, hakutangaza yeye bali alitangaza Waziri wa Elimu Dr Kawambwa mwenyewe.

Wa-TZ tukiendelea kuchanganya siasa mpaka kwenye mambo nyeti ya kitaalamu kama Elimu tumekwisha.
Siasa kama kansa mkuu...imeshatuingia sana... Why Waziri ?...
 
mkuu LUKUVI katoa tamko kama serikali, suala la kupitia upya mtokeo ni limekuja baada ya wataalam kukaa ni kufikia muafaka huo, unaweza kujifanya na kiingereza chako, lakini kumbe hujui hata kinachoendelea

uko sawa ndugu serikali imefanya kitu kizuri sema kuna mijitu mingne wao kila kitu kibaya kwao
 
tunduruboy,

Wewe ndiyo useless person!Your broken English reveals and tell the true inside of you. Sijui kiwango chako cha elimu, na wewe ulipata daraja gani F4 yako,ninachotaka kukuambia ni kwamba ulichoongea ni pumba na hakina mantiki.
Tangazo la Wizara ya Elimu liko wazi kabisa kwamba wanatekeleza agizo la Serikali kukingana na maelekezo ya Tume ya PM kuwa LAZIMA MCHAKATO WA MATOKEO YA F4 MWAKA 2012 UFANANE NA MICHAKATO YA MIAKA YA NYUMA(GRADING PROCESS) AMBAO UMEKUWA UKITUMIKA TANGU MWAKA 1973. SINA HAKIKA KAMA ULIKUWA UMESHAZALIWA!

Sasa kama utaratibu wa Grading umekuwa ukitumika kwa miaka yote tangu 1973,utaratibu ambao hata mimi umeweza kunifikisha hapa nilipo na elimu yangu nzuri kabisa ambayo nina hakika hata tukiingia darasani leo ninatoka na flying colours. Iweje vijana,watoto na wadogo zetu leo wafelishwe kwa kutumia utaratibu mpya baada ya miaka 40?????!!!!

Umesema 'politics and education can never walk together'!!Seems you don't know what you're talking. SERA ZA ELIMU MAHALI POPOTE DUNIANI ZINAHUSISHA SIASA KWA MAANA WANAOTUNGA SERA NI HAOHAO WANASIASA(WABUNGE) WALIOCHAGULIWA NA WANANCHI WENYEWE. So, you can never separate politics and education. Never!

Acheni NECTA wafanye kazi yao kulingana na maelekezo ya Tume na Serikali halafu tuone sasa matokeo yatabakia vilevile au kutakuwa na mabadiliko. Kama mwanafunzi wa kidato cha 4 mwaka 2011 alipata D kwa kupata alama 30% kwa utaratibu wa (D:alama 21-40) kwa utaratibu ulokuwa unatumika tangu 1973 lakini mwanafunzi wa kidato cha 4 mwaka 2012 aliyepata 30% apate F(F:alama 0-34)???

ahsante
 
Mkuu NasDaz hongera kwa uchambuzi mzuri, sema kuna mijitu humu ambayo kazi yao ni ubishi tu. Acha madogo wapate haki yao.
 
Last edited by a moderator:
Hoja ya msingi ni kuwa serikali ilijua lini haya mambo? Taarifa ya habari ITV jana makamanda wamesema kuwa wanao ushahidi kuwa mabadiliko hayo ni maelekezo ya Wizara. Kama hilo ni kweli, kwa nini Serikali ikubali kubadili? Kwa hiyo ni muhimu madogo wapate haki yao lakini waliosababisha sintofahamu hiyo nao wapate haki zaidi
 
Hoja ya msingi ni kuwa serikali ilijua lini haya mambo? Taarifa ya habari ITV jana makamanda wamesema kuwa wanao ushahidi kuwa mabadiliko hayo ni maelekezo ya Wizara. Kama hilo ni kweli, kwa nini Serikali ikubali kubadili? Kwa hiyo ni muhimu madogo wapate haki yao lakini waliosababisha sintofahamu hiyo nao wapate haki zaidi
Hili ndilo jambo la msingi sana ambalo watu wenye hekima wanapaswa kuliunga mkono kwa 100%. Period.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom