Maelezo ya Ndulu (BOT) yamemfutia tuhuma

Prodigal Son

JF-Expert Member
Dec 9, 2009
1,067
696
Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, amesema mpango wa wizara kutoa ripoti ya uchunguzi wa uamuzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kutumia zaidi ya Sh. bilioni 2.5 kujenga nyumba mbili za vigogo wake, hauna tija tena kwa vile wasiwasi uliojitokeza kuhusu suala hilo, umefafanuliwa vema na Gavana wa BoT, Profesa Beno Ndulu.

Mkulo alisema hayo alipotakiwa na Nipashe kueleza lini serikali itatoa ripoti ya uchunguzi wa suala hilo.

"Tulimwambia (Gavana) atoe ufafanuzi. Baada ya kutoa ufafanuzi vizuri, tumeona hakuna tija tena kutoa hiyo ripoti. nadhani alieleza vizuri tu, unaweza kupata hiyo ripoti kwa Gavana," alisema Waziri Mkulo.

Awali, Waziri Mkulo alieleza kushtushwa na taarifa za BoT kutumia zaidi ya Sh bilioni moja kujenga upya nyumba ya Ndulu na kuahidi kuwa wizara yake ingefanya uchunguzi kuona uhalali wa matumizi hayo na kuweka mambo hadharani.

Waziri Mkulo alipata kukaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa pamoja na kushtushwa na taarifa hizo, jambo hilo ni kubwa na linahitaji umuhimu wa kipekee kuchunguzwa ili walipakodi wajue ukweli wa matumizi ya fedha wanazoilipa serikali.

Akitoa ufafanuzi huo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Profesa Ndulu alikanusha kukarabatiwa na
ilimwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuteua mthamini huru ambaye atachunguza na kupitia taratibu na hesabu zilizotumika katika ujenzi wa nyumba hizo.


CHANZO: NIPASHE
 
Hii kali ya mwaka! Hiyo ripoti si ndo ingetujulisha kama maelezo ni ya kweli au sivyo, watu washamzima huyu Mkulo.

Kuanzia leo watuhumiwa wote wawe wanajieleza tu, hakuna haja ya upelelezi wowote!
 
hahaaaaaa,this country is full of jokes.Hakuna kitu serious tunaweza fanyiwa na viongozi wetu!
 
Niliwahi kusema katika thread za nyuma kuwa Mkulo ni msanii hatafanya lolote na nadhani mnaona maelezo yake. Hawa jamaa sijui hawajui linalolalamikiwa au wanajifanya hawasikii. Ishu ni gharama za nyumba ya gavana kuwa sawa na $1.2 Million halafu mnaenda kumuomba msaada marekani na uingereza wakati nyumba za magavana wao ni half the value ya nyumba ya Ben Ndulu.

Serikali ya JK naona inakosa mwelekeo kabisa na tunaloose hope wananchi nao kwani wamezika Richmond, sasa nyumba ya gavana, unadhani kesi nyengine kama RADA, Twin Tower na nyengine wanafanya nini cha maana zaidi ya hadaa tupu. Kwakweli JK ana hatari asichaguliwe tena kwa kasi hii sijui mie sitampa kura yangu wacha nitafute wa kumpa nimeshatoa imani nae hamna kitu hapa.
 
Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, amesema mpango wa wizara kutoa ripoti ya uchunguzi wa uamuzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kutumia zaidi ya Sh. bilioni 2.5 kujenga nyumba mbili za vigogo wake, hauna tija tena kwa vile wasiwasi uliojitokeza kuhusu suala hilo, umefafanuliwa vema na Gavana wa BoT, Profesa Beno Ndulu.
CHANZO: NIPASHE


Mungu wangu we! :( Sasa walipa kodi wa Tanzania hawana haki ya kuisoma ripoti hiyo!?
 
Duh..hawa ndio wasomi wetu tunaowategemea kutupeleka karne ya 21...hawa washenzi hawa...ufafanuzi my ass...the people want economic and social justification of spending bilions to build 4 houses. Things like; Why this was done, Who is responsible, What legal actions should be taken against those who misused our tax money, What can be done to stop this from happening again...etc...yeye anakuja kutuma ufafanuzi.

Huyu Mkullo anaishi Tanzania hii hii au kuna Tanzania nyingine jamani?
 
Mungu wangu we! :( Sasa walipa kodi wa Tanzania hawana haki ya kuisoma ripoti hiyo!?


Mkuu, Uchaguzi unakaribia

hatutakiwi hatakidogo kutoa habari amabzo zitawachanganya wapiga kura, kelele za ufisadi zimekwisha sasa mikakati tutarudije madarakani kwa kishindo, la msingi wananchi wameshasahau Ndulu aliongea nini,Tanzania hii hii wapo watu wanatumia pesa za walipa kodi na kuishi kama vile wako peponi (mfano huyo ndulu na watenda kazi wake ) ili khali wanaolipa kodi wanaishi kama ndo wako motoni vile.

Maendeleo ya nchi yanaletwa kwa watu kulipa kodi sasa kama kodi wanakushanya then wanatumia kama tayari tumeshaendelea na hawataki kulizwa ni jukumu letu sie tunaolipa kodi tuwahukumu Kivipi? ni swali la kujiuliza mie na wewe
 
Stuka! Chukua hatua, mwezi wa kumi haupo mbali. Hakikisha wewe na wote walio katika
nymba yako na walio kijijini kwako wanafanya maamuzi sahihi. No mkuloz.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom