mkuu unaweza kuunganisha hizi dot hapa hadi zikaungana? sijapata uhusiano hapo !! msaada plsYapata siku 3 baada ya gongo la mboto kulipuka,hatimaye mmiliki wa dowans ajitokeza hadharani.
KUNANI BONGO??
wanataka kurudi nini?Taarifa nilizozipata hivi punde zinadai kuwa "mwizi huyu" aliyeingia leo toka Oman ni mzaliwa wa Zanzibar aliyenusurika ktk mapinduzi ya Zanzibar na kukimbilia Oman. Ujio wa leo na kuongea na waandishi wa habari umekuwa ni wakushitukiza sana. Bado tuna muda wa kutosha kumuuliza maswali yanayotukera, na akileta ujinga, nguvu ya Umma itabidi imeshukie, kama vyombo husika vitasita kufanya hivyo, ama kwa kumuogopa au kwa kutojua vifanye nini. Uwezo wa nguvu ya Umma tunao, Sababu tunazo, na nia ya kumwadabisha "dhurumati" huyu tunayo. Tunataka dunia ielewe kuwa Tanzania ya jana sio ya leo ktk mambo ya mzaha kama huu.
Nijuavyo huyu alishawahi kuikana iweje leo awe mmiliki.
Nijuavyo mie huyu bwana kawekeza kwenye kiwanda cha kuchambua pamba lakini kikitumika pia ku-finance mambo ya dini fulani.
Hili kanyaboya coz mmiliki wa Dowans twamjua ni RA. Je, wamemwuliza ilikuwaje wakatoa PoA yenye mamlaka kubwa kiasi hicho kwa RA wakati si mwanahisa wala mkurugenzi wa Dowans.
Tatizo waandishi wetu wengi wanaenda kwenye press conference pasi maandalizi
Magreat Thinkers mbona mnashindwa kutoa maoni yenu kuna kitu kipo nyuma ya pazia.............?
Mtu yeyote akitaja neno Dowans basi waliopo karibu watakunja nyuso zao na kusema kila aina ya ubaya kwa kampuni ya dowans. Nafahamu kuwa mchakato wake haukuwa wa wazi lakini swali je hayo makampuni mengine ya kufua umeme kama IPTL, SONGAS na mengineyo yalifuata taratibu zote za kisheria bila kuhusisha ruswa kwenye mikataba yao na Tanesco? Ikiwa hivyo basi tuna haki ya kuisakama Dowans na wale wote wanaohusika kwa namna moja au nyingine na Dowans. Lakini ikiwa makampuni mengine yaliyosalia ukiitowa Dowans pia na yenyewe yamejaa usanii na mikataba yake haikuwa na tija na iliingiwa kwa hila basi sisi "Watanzania" ni wanafiki! Wanafiki na tuna sababu za nyuma ya pazia kuisakama Dowans!
Kuna habari nimepata kuzisikia kuwa Dowans ndio kampuni pekee inayochaji "capacity charges" kuliko makampuni mengine Dowans wanalipwa 152 mil per day, Songas over 250 mil per day na IPTL kwenye 300 mil per day.
Nadhani imefika wakati tujaribu kutafuta ukweli na kuyachambua makampuni yote yanayofua umeme tusiwe waitikia kiitikio "kolasi" na pili tuache unafiki kama kuna makampuni zaidi ya moja yanayohusika na hila basi yakemewe yote kwa nguvu zote yasishambuliwe makampuni baadhi kwa sababu ya hila na chuki binafsi huku mengine yakiendelea kutunyonya.
Kabla ya kuwakilisha na kukaribisha hoja napenda kukoselewa na kuelimishwa hayo ni maoni yangu binafsi na figures nilizotoa ni just round figures sina source ikiwa kuna mtu ana source itakuwa kafanya jambo la maana akituletea source ya charges zinazolipwa na Tanesco kwa makampuni husika.
Nawakilisha.....