Maelezo ya Bajeti Kivuli

Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,019
2,923
Kutoka Zitto na Demokrasia

Katika mjadala unaoendelea Bungeni kuhusu Bajeti, baadhi ya wabunge wameeleza kwamba Bajeti Kivuli haikuonyesha vyanzo vya mapato na hivyo kuita ni vyanzo sifuri. Ukweli ni kwamba tumeweka vyanzo vya mapato ya ndani kwa ujumla bila kuainisha mapato ya kikodi ni ngapi, mapato yasiyo ya kikodi ni ngapi na mapato ya Halmashauri ni kiasi gani. Hivyo tunakiri kosa hili na tumechukua hatua ya kuainisha mapato hayo Kama inavyoonekana kwenye jedwali hili hapa chini.

MAPATO
SHILINGI MILIONI
AMapato ya ndani
11,889,078
i)mapato ya kodi (TRA)
10,232,539​
ii)Mapato yasiyo ya kodi
1,163,533​
BMapato ya Halmashauri
493,006​
Mapato haya yamo ndani ya Hotuba ya Bajeti Mbadala lakini kwa makosa ya kihariri hayakuonyeshwa kwenye jedwali na hivyo kuleta usumbufu kwa Wabunge na Watanzania wengine waliopata fursa ya kusoma Hotuba yetu. Tunaomba radhi kwa usumbufu. Nawashukuru walioona tatizo hili na hii inaonyesha kuwa wabunge wanasoma kwa makini Bajeti ya Upinzani.
Ninawatakia mjadala mwema wa Bajeti.
Kabwe Zuberi Zitto,Mb
Waziri wa Fedha na Uchumi Kivuli
19.06.2012
 
Hii budget ya kivuli mliyooandaa ina maana kambi rasmi ya upinzani bungeni haikukaa na kuipitia na hakuna hata mbunge mmoja aliyoona hilo kosa? si unaona wabunge magamba walivotumia kosa hilo kuwadharau hadi wanaiita budget giza? kuweni makini msianze kutuaibisha!!
 
Back
Top Bottom