Maelezo binafsi ya mgombea wa CCM jimbo la Igunga Dk. Kafumu

Mkuu mleta thread ni vyema umeleta CV ya mgombea wa CCM.
Sijajua nia yako kama ni kumjenga au kumbomoa.
Ninaomba uturushie za wagombea wote wa ubunge Igunga ili wana JF wazichambue zote kwa pamoja.
Ninawasilisha.
 
Hawajadanganya, ila wamemrembea kwa kuipaka mafuta ili inoge......hata hivyo magamba hawashindwi kufanya chochote pale wanapotaka<br />
kitu chao kitimie....unaweza kuta yote yaliyomo kwenye cv hiyo ni 0 tu ndiyo ya kweli na mengine yote ni magumashi

Sasa kama wamedanganya litakuwa kosa la nani? Tofauti ya kuremba na kudanganya iko wapi?
 
Mkuu mleta thread ni vyema umeleta CV ya mgombea wa CCM.
Sijajua nia yako kama ni kumjenga au kumbomoa.
Ninaomba uturushie za wagombea wote wa ubunge Igunga ili wana JF wazichambue zote kwa pamoja.
Ninawasilisha.

Hawezi kuleta na za wengine kwa sababu hazifiki hata robo ukurasa. Ha ha ha ha haaa
 
Duh mkuu Kafumu umetishaje, yaani kwa CV hiyo unapata kura kiulainiii kama unanawaaa. Sasa ngoja tuone CV ya mgombea wa MAGWANDA, yaani haifiki hata robo ya ukurasa.

A well educated person and of learned calibre with high intergrity coupled with sound and tranquil mind can't, I repeat can not VIE to become a CCM member let alone an MP. He can neither become a staunch supporter nor tout for magambas' ukereketwa unless he's looking which side of of his slice is buttered. He's among magambas (fisadis). By the way, can Kafumu pass a corruption litmus test? I doubt...

So mrani, focus your mind on fundamental things which magamba have (and are still failing) failed to deliver!
Wacha ushabiki wa kiswahili.
 
Kwenye hiyo CV naona hakuna chochote kimesaidia taifa hili katika sekta ya madini kama walivyoamu kuipamba.
Kwangu mimi Mfwatiliaji, and as far as my contry is concerned, this is as good as nothing!!
Samahani Kafumu (Ph. D) lakini huo ndiyo ukweli!!
 
Good yaani safi!

Tupatie Vyuo alivyosoma na pia tupe ushiriki wake katika mikaba feki ya Madini, hasa ule wa Karamagi, Buhemba - Meremeta, Nyamongo na ule wa Nzega.

Tunasubiri maana haiwezekani kawepo wizara ya Madini msomi alafu tumeendelea kuibiwa na hata kuingizwa mikataba mibovu kila kukicha.
 
Elimu ni chombo tu kinachokupa mwanga wa kwenda kuitumikia jamii yako. ukitaka kuangalia uwezo wa mtu pamoja na elimu ya darasani
angalia sana sana kitu kinaitwa accomplishment hapo ndio utajua uwezo wa mhusika ktk kuitumikia jamii yake ambapo ndio lengo la elimu.

Inatia aibu kwa mtu kama huyu mwenye elimu kama hii kuwa na almost zero accomplishment kwani mambo yote anayodai kuwa ni
accomplishment yangeweza kufanywa na mtu hata wa darasa la saba kama mimi. Kutoa michango, kuchimba kisima na kadhalika. Ungete
gemea kwa mtu mwenye kiwango kama cha kwake uone mambo makubwa yenye ku involve creativity ya nguvu ambayo imetulea faida
kadhaa au imetatua matatizo makubwa yanayoikabili nchi yetu.

Je elimu yake ilitusaidiaje watanzania ktk kuakikisha mikataba ya madini inainufaisha nchi yetu zaidi na mikataba yote fake ambayo kila mtanzania ana ilalamikia haipewi nafasi ?? badala ya kutuambia umechimba kisima au kuanzisha saccos msomi mzima accomplishment sentesi 6 tu ni AIBU KUBWA KWA TAIFA.
 
Kule Korogwe Vijijini mganga wa miti shamba Maji marefu alimuondoa kiurahisi kabisa Profesa Mndolwa;

Mbeya Mjini
kijana Mbilinyi alimdondosha Mpesya mwenye elimu kubwa;

Ludewa Profesa Mwalyosi aling'olewa na mtu ambaye hana elimu hata nusu aliyonayo;

Mahenge
pia Profesa Birhan Mahenge akapoteza kiurahisi kabisa kwa mtu ambaye kielimu kamfunika mno;

Tabora Dr James Nsekela
hajarudi bungeni baada ya kubwagwa kwenye kura za maoni;

Kule Rungwe Magharibi kama sio mizengwe basi Profesa Mwakyusa leo hii asingekuwepo bungeni!

Hiyo ni baadhi tu ya mifano mingi kuwa ELIMU sio ndiyo kila kitu kwenye chaguzi za Tanzania!
 
Sasa kama wamedanganya litakuwa kosa la nani? Tofauti ya kuremba na kudanganya iko wapi?
Unauliza jibu kwani hujui? kosa ni la magamba na wewe ukiwepo.......alafu mkuu utakuwa mtetezi wa magamba hadi lini? zinduka mkuu!
 
Cv ina makosa mengi sana,idadi ya watoto haiendani na mchanganuo wake,halafu anasema alikuwa mhadhiri tokea mwaka 1978 na hapohapo amegraduate 1983????alikuwa mhadhiri kabla ya kugraduate?

Kama anashindwa kuihariri cv yake mwenyewe je atawezaje kusoma mikataba ya kurasa 100 na zaidi?no wonder tunaibiwa kwenye madini kutokana na watu kama hawa. Ningekuwa ndo nashortlist wagombea ningempiga chini.
 
Cv ina makosa mengi sana,idadi ya watoto haiendani na mchanganuo wake,halafu anasema alikuwa mhadhiri tokea mwaka 1978 na hapohapo amegraduate 1983????alikuwa mhadhiri kabla ya kugraduate?kama anashindwa kuihariri cv yake mwenyewe je atawezaje kusoma mikataba ya kurasa 100 na zaidi?no wonder tunaibiwa kwenye madini kutokana na watu kama hawa.
Ningekuwa ndo nashortlist wagombea ningempiga chini.

asante sana mkuu, no wonder why mikataba yote fake ya madini ikapita chini ya usimamizi wake. msomi mzima unafanya blanda za kijinga
namna hii ktk CV kitu amabcho ndio kinakuelezea who you are? kama anashindwa kujumlisha idadi ya watoto aliokuwa nao anawezaje kusoma
statistics za mineral resources.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Acha kudanganya watu wewe. Tunahitaji wasomi kama hawa kwenye siasa ili kusaidia kuharakisha maendeleo.
Unajuwa wewe kichwani ni emty kabisa, hivi unajuwa kwamba Bill Gates hajamaliza chuo kikuu? makaratasi ya mtu sisi yanatusaidia nini? yeye kama ni mtaalamu wa madini akae huko kwenye taaluma yake, why siasa/ ubunge?

We have long way to go.
 
"Nimesimamia marekebisho ya sheria ya Madini ya mwaka 1998 ili kupata sheria ya mwaka 2010. Sheria mpya inahakikisha kwamba:-
(i) Serikali na Wananchi wanashiriki zaidi katika uwekezaji madini kwa kupata hisa kwenye migodi.
(ii) Wananchi wanaoishi kwenye maeneo ya migodi wanafidiwa vizuri, kujengewa makazi mazuri na kushiriki kwenye mradi husika.
(iii) Kampuni kulipa kodi na mrahaba kwa viwango vya juu zaidi.
(iv) Wachimbaji wadogo wanatengewa maeneo yao, kupewa leseni zenye muda mrefu ili waweze kupata mitaji kutoka kwenye taasisi za fedha;na
(v) Viwanda vya uongezaji thamani ya madini vinajengwa hapa nchini ili kuongeza ajira na kukuza uchuni; na
(vi)Madini ya vito (Almasi, Tanzanite, Ruby na mengineyo) yanachimbwa na Watanzania tu."

Yaani sijaona cha kujivunia hapo ukilinganisha na taarifa za karibuni kwamba hata Airtel wana wazidi
barrick kwenye kulipa kodi
 
Siku zote huwa napenda kuona wabunge wakiwa ni watu makini, maana kosa moja linaweza kuligharimu taifa kama tulivyoona kwenye issue ya madini ingawa imenisikitisha kuwa kumbe hata hayu hawezi kukwepa lawama.
Hoja yangu ianzie kwenye idadi ya watoto alionao. Ukiangalia kwenye highlights zangu juu, amesema ana watoto 5 lakini ukijumlisha mchanganuo alioutoa unaleta watotot 6, Sasa je tuamini lipi? Je huyu ni mtu makini kweli?

Upande wa elimu anasema hivi *Shahada ya Uzamili ya Madini-BSc (Geology)-1995
Inaelekea huyu mkubwa hajui kuwa kuna tofauti kati ya shahada ya uzamili (Msc) na Bachelor of Science (Bsc) Sasa sijui hapo alimaanaisha kuwa ni Bachelor au Masters maana maelezo ni Masters lakini abbreviation ni Bachelor. Je huyu ni mtu makini kweli?
Anyway wana Igunga ndo wataamua kama wanataka mbunge makini au ili mradi mbunge

Dah,mkuu uko makini sana katika kuchambua!
Sikuliona hilo,ila linadhihirisha jinsi wizara ya nishati na madini isivokuwa
na watu makini,...

Afu amesema kawezesha migodi kutoa kodi kubwa nchini,sijui anaongelea migodi ipi sasa?
maana juzi tu tuliona mgodi atleast ulio ingia kwenye 15 bora ya walipa kodi ni ule
mdogo kabisa wa tabora
 
"Nimesimamia marekebisho ya sheria ya Madini ya mwaka 1998 ili kupata sheria ya mwaka 2010".

chadema, hiyo ndio nyundo ya uhakika ya kummalizia kafumu igunga amewapeni yeye mwenyewe haya kazi kwenu.
 

NDOA:

Nina mke na watoto watano ambao kati yao watatu ni Madaktari wa binadamu, wengine wawili bado wanasomea Udaktari wa Binadamu na mmoja anasoma Stashahada ya Ufamasia.


5 JUMLA 3+2+1=6




ELIMU
*Shahada ya kwanza ya Madini- BSc (Geology)-1983
*Stashahada ya Elimu-PGD (Education)-1987
*Shahada ya Uzamili ya Madini-BSc (Geology)-1995
*Stashahada ya Utafutaji Madini-PGD (Mineral Exploration)-1991
* Sahahada ya Uzamivu ya Madini-Ph.D (Geology)-2000


HUDUMA KWA UMMA WA TANZANIA
*NikiwaMjumbe wa Bodi ya Makandarasi (2006-2011) nimesimamia kuandikisha makandarasi nchini wanaotoa huduma za ujenzi kwenye sekta ya barabara na majengo na nikiwa mjumbe wa Bodi ya Chuo Kikuu cha Dodoma (2009-2011) nilishiriki katika usimamizi wa chuo hicho ili kutoa viajana wasomi bora wa kulitumikia Taifa la Tanzania.

na sehemi ya madini je

in the highlights...AND THEN kweli usijue watoto wako!!!!! watano (5) JUMLA 3+2+1=6
 
kwahii CV bora akawe lecturer tu UDOM ataleta mchango zaidi kwa taifa kuliko kwenda kupiga meza Mjengoni
 
Nimependa tu apo kwenye watoto watano halafu wote ni Madaktari!
Kuhusu mkataba wa Buzwagi wa miaka 90 najua umehusika na elimu yako haijakusaidia kitu imekuwa kama punda kabeba mzigo wa vitabu
 
HUDUMA KWA JAMII (2005-2011)
(i) kujenga Misikiti miwili katika Kata ya Itumga, kutoa vitabu vya rejea na kiada kwa shule kumi za sekondari wilaya ya Igunga:- Itimba, Igunga, Mwamashimba, Mwisi,Mwanzugi, Igurubi, Manshiku, Simbo na Nanga.
(ii) Kufadhili vikundi vya kina mama, Kata ya Itumba, Kwaya za Madhehebu ya Kikristo Igunga mjini na Mwanzugi.
(iii) Nikiwa mwanachama wa Igunga SACCOS nimekisaidia chama changu kwa ushauri wa kitaalam na kutoa ada na hisa na michango yangu kwa wakati.
(v) Nikiwa mlezi wa Vijana Kata za Mwamashimba na Itumba nilifadhili vifaa vya michezo (mipira, jezi na kombe) na kuendesha ligi ya mpira wa miguu katika kata hizo mwaka 2009-2010.
(vi) Nilitoa mchango wa sh. 800,000 kuchangia ujenzi wa visima virefu viwili Kata ya Itumbi.
.

Ngoja na mie nianze kuiweka vizuri CV yangu kwenye wa HUDUMA ZA JAMII, kutoa ni moyo, na kila aliye nacho anawajibu wa kibinadamu kushare na jamii yake.

By the way, Ipo Baraka Katika Kutoa.
 
Inabidi ni changie juu ya hili, kwa taarifa yenu igunga Dr kafumu anakubalika saaaana tena sana, mtasema mengi but ukweli ndo huo na hata chadema wanajua hilo, mtaishia kunawa igunga!! Huwa mnadai Cv za watu leo hii yamewashinda hamtaki tena,, duh kweli watanzania tunaelekea kubaya!! Let's wait and see!! Nawakilisha!
 
Back
Top Bottom