Madudu Ya Ekelege Wa TBS Yametambaa Hadi UK!

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Taarifa hii imetumwa kwenye Mjengwablog.com na Mtanzania aliye UK.

Mwenyekiti,

Hapa UK kuna kampuni moja mimi nasema ni ya kitapeli kwani bila shaka imeanzishwa na wakubwa fulani kwa manufaa yao na vijana wao wanaoishi hapa uk. Hii kampuni inajiita WTM UTILITY SEVICES LTD (TBS no: TZS 698.2003) hawa ukitaka kusafirisha gari kuja bongo wanasema lazima walikague ubora wake , lakini kitu cha ajabu hakuna ukaguzi huo unaofanyika.

Wewe unawapigia simu una gari, kasha una wafaksia kadi ya gari wanakuandikia certificate au kama una haraka unakutana nao mitaani maeneo ya east . Hapo wanakundikia hapo hapo!Kwa kweli inakera .

Watu wana tengenezeana michongo na Serikali haipati kitu. Sijui hao watu wa TBS waliowapa kibali cha shughuli hiyo kama wana jua chochote? Nadhani na wao wana fungu lao. Naomba wahusika wizarani wachunguze suala hili, basi kama kuna ulazima wa ukaguzi ufanyike nyumbani angalau walala hoi nao watapata ajira na Serikali itaambulia, na si pesa si kidogo. Mwenyekiti, nawasilisha.

Shukrani
Whistleblower

UK
 
Hili limedhihirishwa na wajumbe wa kamati ya Bunge pia kwani walipokwenda Hong Kong nao waliuziwa cheti feki cha TBS; Na hapo ndipo ambapo nimekuwa na tatizo idogo na balozi zetu kwani tuliweza sana ku link mambo na balozi zetu huko nje ili kuweka mambo sawa na kupunguza ufisadi ila tatizo nchi bwana kila mtu na lwake, watu wamejigawia vyao wao ndio kila kitu utawaambia nini.Hii Tanzania ina matatizo.
 
Ekelege@ work lol.......... Jana amewakimbia waandishi wa habari. They should keep in mind that 'Peace of this nation is very fragile'
 
Vicent Nyerere jana alimwaga ***** juu ya hawa wahuni wa inspection ya magari
 
Kama gari lina MOT wanataka kibali gani kingine. UK magari yote yenye umri zaidi ya miaka 3 yanakaguliwa ubora kila mwaka na kupewa utambulisho (MOT). Sasa hapo wabongo wanakagua nini?
 
Back
Top Bottom