Madudu na utapeli wa nacte kwa wanachuo..

emmagaja

Member
Feb 9, 2011
22
3
Baraza la Taifa la elimu ya ufundi(NACTE) limesababisha wanafunzi wengi waliohitimu diploma waliopeleka vyeti vyao kusajiliwa il kuweza kufanya udahili kwa mfumo wa pamoja(CAS) kushindwa kuomba nafasi ya kujiunga vyuo vikuu..wanafunzi hao walipeleka vyeti vyao pamoja na kulipa Tsh 20000 kama ada ya kusajiliwa toka mwezi 4 mwaka 2012 lakin wameshindwa kushughulikiwa..mpaka kufikia leo tarehe 4 Julai 2012 ambao ndo muda wa mwisho kwa tcu kupokea maombi ndo wamewajulisha baadhi ya wanafunzi huku namba nyingine hazifanyi kazi..wanafunzi wanaomba wanaoisimamia NACTE kuichunguza kwan inarudisha nyuma jitihada ya wanafunzi kujiendeleza za kielimu.
 
Back
Top Bottom