Madiwani watano wa CHADEMA Moshi watuhumiwa kwa vitendo vya rushwa

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,887
3,412
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) mkoa wa Kilimanjaro imeingia katika malumbano na Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini, Philemon Ndesamburo.

Malumbano hayo yanatokana na taarifa zilizozagaa kuwa Takukuru wamepelekewa majina ya madiwani watano wa Chadema wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Habari hizo zinadai kuwa madiwani hao wamekuwa wakishinikiza kutolewa kwa vibali vya ujenzi na kuruhusu ujenzi holela na ukarabati wa majengo chakavu ndani ya mji huo.

Hata hivyo Katibu wa mbunge huyo, Basil Lema alipoulizwa jana, alikiri kupewa taarifa ya Takukuru kupelekewa majina lakini anashangaa taasisi hiyo kutochukua hatua.

"Mimi na mheshimiwa Ndesamburo tulikwenda kuonana na kamanda wa Takukuru juu ya jambo hilo ambalo kimsingi linakipaka matope chama bila sababu," alisema Lema.

Lema alisema katika mazungumzo yao, Lema alimkariri Kamanda huyo akikiri kuwa na majina ya madiwani hao na kwamba wanatuhumiwa kushinikiza utoaji wa vibali vya ujenzi.

"Hoja ya Ndesamburo ni kuwa mwenye mamlaka kisheria kutoa vibali ni mkurugenzi kwa hiyo mwisho wa siku kama vipo vibali jambo hilo linarudi kwa mkurugenzi," alisema.

Lema alisema anaongea kwa niaba ya mbunge huyo, alisema kama wapo madiwani wanaotuhumiwa katika kashfa hiyo washtakiwe kama watu binafsi bila kuhusisha chama.

Hata hivyo kamanda wa Takukuru, Lawrence Swema alipohojiwa jana alisema hajawahi kupokea majina ya madiwani hao licha ya kumtaka Ndesamburo ampelekee majina hayo.

Swema alisema tangu Ndesamburo na Lema wafike ofisini kwake na kuwataka walete ushahidi wa majengo yaliyotolewa vibali, hadi jana walikuwa hawajarudi ofisini kwake.

Lema alipoulizwa kwa mara ya pili kuhusu msimamo huo wa Takukuru, alisema wao hawakwenda kupeleka majina bali kupata ufafanuzi wa kuwapo kwa majina hayo.

CHANZO: Mwananchi
 
Mlitegemea nini kutoka kwa wachagga? tazama TRA ilivyo, wanakula rushwa waziwazi, lakini kwa kuwa majority ni wao kwa wao, wanalindana.
 
Mbona habari inasema takukuru wanamajina ya hao madiwani, kamanda wao amehojiwa anasema anasubiri majina kutoka kwa mbunge! Hapo pana kaudaku flani. Inaonekana kuna habari za zilizomfikia mbunge kuhusisha madiwani na alipoenda kuuliza takukuru wakawa hawana habari. Hence the story is not valid!
 
Kama wamekula rushwa au kupindisha haki kwa namna yoyote, TAKUKURU panawastahili!
 
halaf mods muache mambo ya ajabu,nimekuwa mtu wakwanza kukomenti hapa,lakini cha ajabu post yangu mmeiondoa kwa sababu zisizo na kichwa wala miguu.
Na hii sio mara yakwanza,kiukweli mnazingua.
 
Mlitegemea nini kutoka kwa wachagga? tazama TRA ilivyo, wanakula rushwa waziwazi, lakini kwa kuwa majority ni wao kwa wao, wanalindana.

wewe ndiye zomba kweli. Ukabila unahusiana nini na habari hii? Au ukisikia Moshi tu moto unakuunguza!
 
halaf mods muache mambo ya ajabu,nimekuwa mtu wakwanza kukomenti hapa,lakini cha ajabu post yangu mmeiondoa kwa sababu zisizo na kichwa wala miguu.
Na hii sio mara yakwanza,kiukweli mnazingua.

Mkuu, mbona hata thread haioneshi kwamba kuna post iliyofutwa!? Na kama imefutwa si uipost tena? Au ulitaka tu uonekane ni wakwanza ku post?
 
Hivi kama sio kuchafuana mbona mbunge wenu juz alikamatwa na sio kuzushiwa kashfa, mi'najua mtuhumiwa wa rushwa anakamatwa na kuwepo chini ya ulinzi mpaka mashtaka yake yanaposomwa, na nyiemalimbuken hii nchi mpaka sasa ishauzwa kwa wekezaji tena kwa bei ya kutupa je ni wachaga wameiuza?, tena kuna fununu mkepa anamiliki migodi kibao hapa nchini jaman huko sindio kujilimbikizia mali.
 
mkuu zomba unamajina yao?? Hebu tuwekee maana mwananchi hawajataja.
 
Last edited by a moderator:
Muulize Ndesamburo.

Kuna zaidi ya Mchagga diwani wa Moshi
? kwi kwi kwi teh teh teh.

Meya wa manispaa ya Moshi diwani wa kata ya Bomambuzi Mh.Jaffery Michael (chadema) ni mpare,Diwani wa kata ya Pasua Mh.Mkalakala (chadema) ni msambaa,diwani wa kata ya Bondeni Mh.Abdulrahaman Sharriff (chadema) ana asili ya Asia,diwani wa kata ya Kaloleni Mh.Michael Mwita (ccm) ni Mkurya,kwa nini unatuandama sana wachagga,hujui tukigoma kufanya biashara nchi wote mtakufa kwa njaa na serikali itakosa kodi?
 
Na wale wanatuhumiwa kuchukuwa rushwa, mbona huwataji? Labda walevi na wala nguruwe wa nchi nzima wataacha, biashara yenu kubwa ni pombe na nguruwe.

Tufe njaa kwani nyie ndio miungu mnaotoa rizki za watu?
 
mkuu huo si mtiririko wa hoja wewe umesema hakuna diwani wa cdm manispaa ya moshi ambaye si mchaga,umetajiwa hapo meya wa moshi ambaye pia ni diwani ni mpare,sasa basi ungetueleza hii inakuwaje wakati wewe umeshatueleza awali, zaidi ya hapo na wewe ni mpiga mipasho tu kama nape
 
Mie nakwambia hakuna, ukiona hao unaowasema wote wana mzazi mmoja wa kichagga kama si hivyo na wao wameshakuwa zaidi ya wachagga. Hiyo ya kuwa hao wote sijui wapare sijui wahindi, mimi hainiingii akilini kabisa. Kitaifa tu, mmeshasema mnataka Nchi yenu ya Kaskazini, sasa hapo hapo kwenu aje mgeni awe kiongozi wenu? hunambii hata kidogo.
 
Back
Top Bottom