Madiwani waliotimuliwa Chadema Arusha waomba radhi, Napendekeza wasamehewe

Haha wanaomba msamaha baada ya mtoto wa mkulima kwenda Arusha
Kuna mmoja wao niliongea nae siku moja akaniambia hata Mh. Pinda na Mh. Zitto wameuafiki mwafaka kuwa uko safi....nikamuuliza je chama kina semaje na wewe uligombea udiwani kupitia Pinda au Zitto.....
 
Wawaambie wafute kes kwanza ndio wakazungumze.na wakishafuta tu cdm iwaambie mazoo chapeni mwendo walarushwa wakubwa na nimafedhuli sana hao jamaa,hukumu yalema walichinja na kunywa kwa macho yangu,hawa wametusumbua sanaa wakirud cdm makamanda walio kufa tar5 mwez wa kwanza watafufuka na watapinga vikali na sinto kiamin tena cdm nauchungu nahawajamaa sanaa.siwalipenda pesasa?watuache tukae bila madiwani bana yani!
 
Kushindwa mahakamamni kwa Lema kumechangiwa sana na madiwani hawa kwani ni waasi nalazimika kuamini kwamba wakati wa kesi hiyo walishiriki kuihujumu chadema chini chini kwa kuwa Lema alikuwa mwiba kwao katika suala la Arusha sasa wanarudi na kuomba radhi pengine wanafahamu kuwa rufaa ya Lema hatashinda.

Chadema mkitaka kupoteza umaarufu Arusha warudishe hawa waasi.

Mgogoro huu wa madiwani umerudisha nyuma wajibu wao kwa wananchi kupitia chadema hawafai hata kidogo.

Kama wana uhakika wa kurudi kwenye udiwani kupitia chama chochote sio lazima warudi CDM vyama viko vingi

Baada tu ya hawa jamaa kungolewa John na Mallah kwa pamoja walisema ametuondoa lakini na yeye ataondolewa ubunge... kwa kuwa kipindi hicho hata kesi ilikuwa haijaanza kwa kweli sikuya tilia maanani.....
 
Hatutaki huo msamaha wao wameturudisha nyuma sana ungekuta MEYA ni wa CDM muda huu wanakumbuka shuka kumekucha walitaka kupimana ubavu na nguvu ya UMMA kwanza wana umri mkubwa wangekuwa vijana tungesema hawajakomaa sisi ile mizee ya nini sisi.
 
Mtu mwenye akili ataoanisha haya matukio na kuyaweka pamoja: Milya, Lowassa kutoa neno kesho, madiwani kuomba msamaha! Mpango wa kuhakikisha ngome ya CHDM Arusha inavunjwa kama si kubomolewa ndo huo unakaribia kupata jibu. Haya yote haiwezekani yakaja mara moja na yanaonekana kuiinua CDM, hapa CDM wajiandae kuanguka chali kama watadanganyika. Binafsi nasema hakuna chochote hapo, waachwe waendelee kujipanga hakuna msamaha
 
hatuwahitaji kwa sasa waende tu CCM aliyeamua kulima hapaswi nkutizama nyuma mwendo mdundo mapambano yanaendelea nawashauri viongozi wa CDM hawa hawatufai wametuhujumu vya kutosha
 
Walikuwa wanatingisha kiberiti wakakuta kimejaa hahahaha.... wabongo wanasema imekula kwao hiyo!!
 
arusha hatuwaitaji mawakala wa mafisadi..wamesaidia sana kumuangusha mh Lema ktk kesi iweje leo watake kurudi? dr slaa mkiwarudisha awa jiandae kuangukia pua ktk uchaguzi kama ukirudiwa!
 
Ninaunga mkono, kusamehe ni sheria mojawapo ya Mungu. Wasamehewe kwa vile wametambua kosa walilolifanya na unafiki wao. Watakuwa watendaji wazuri na wawakilishi wema wa wananchi.

Hapana, kwa walichoonyesha ni watu wenye kuendekeza maslahi binafsi zaidi. Wasamehewe lakini wapigwe chini Udiwani...ni watu wenye kuendekeza matumbo na tamaa zao zaidi.
 
Hatimaye madiwani waliotimuliwa na Chadema Arusha wameandika barua kwa Mbowe na Dr Slaa kuomba radhi wasamehewe.

Mimi napendekeza wasamehewe kwa sharti la kuondoa kesi mahakamani na pia waukane muafaka bandia. Inavyoelekea kesi itakaa hadi 2015 na wananchi wa Arusha watakosa maendeleo hasa ukizingatia hakuna mbunge.

Source. Mwananchi
Nimejaribu kuitafuta habari hii kwenye gazeti la Mwananchi lakini sijaiona.

Hata kama ni habari ya kweli hawa watu si wa kuaminiwa tena. Nakumbuka walipohojiwa Dodoma walisema wanaomba radhi lakini tukasikia tena wamefungua kesi kupinga kufukuzwa. Nafikiri hii imekuja baada ya kujitahidi kukivuruga chama wakishirikiana na CCM (Pinda) bila mafanikio. CCM wameona hata wakiitisha uchaguzi na kuwatumia hao madiwani hawawezi kushinda. Hivyo lililobaki ni wao kujifanya wamejirudi wasamehewe na wapewe udiwani wao kuepusha aibu itakayoipata CCM endapo uchaguzi utarudiwa. So, CDM be careful with this trick.
 
hapo patamu ni aibu kwa mwanaume mzima kukosa msimamo hili ndilo tunaliona kwa hawa madiwani
 
Hatimaye madiwani waliotimuliwa na Chadema Arusha wameandika barua kwa Mbowe na Dr Slaa kuomba radhi wasamehewe.

Mimi napendekeza wasamehewe kwa sharti la kuondoa kesi mahakamani na pia waukane muafaka bandia. Inavyoelekea kesi itakaa hadi 2015 na wananchi wa Arusha watakosa maendeleo hasa ukizingatia hakuna mbunge.

Source. Mwananchi
Kusamehewa wanaweza kusamehewa, lkn kosa walilofanya ni la kihaini kwa Chama; msamaha lazima umaanishe kuwa wataendelea kuwa wanachama wakiishi na matokeo ya uhaini wao. Kamwe wasiruhusiwe kugombea udiwani. Wawekwe kwenye kipindi cha uangalizi wakiruhusiwa kutumika katika ngazi za chini zaidi, mpaka itakapothibitika kuwa hawatatumiwa na magamba tena.
 
Inawezekana mawazo yako ni sawa, lakini kumbuka kule Meru kata 17 zote madiwani ni CCM mbona walishindwa kuisaidia ikashinda uchaguzi? Hakuna wa kuzuia nguvu ya umma bwana. Kama ni kuwasamehe wanaweza kusamehewa lakini udiwani sijui sheria imekaaje, maana bado kesi iko mahakamani. Wanaojua sheria zetu watujuze

Waombe upya uanachama maana walishanyang'anywa kadi! Kisha wasipewe nafasi yoyote ya uongozi!
 
Back
Top Bottom