Madiwani waliofukuzwa kwa nini watetewe na serikali?

Hawa ngoja siku 30 walizopewa ziishe ni kutia timu na nyomi ya wanaArusha kwenye ofisi za mkurugenzi wa magamba kushinikiza kuondolewa kwenye list ya madiwani na uchaguzi mdogo

Naunga mkono hoja.

Wanatetewa na serikali kwa sababu haipendi kuona mtu anaonewa kwa sababu ya unyonge wake, udhaifu nk. Kitendo cha madiwani hao kufukuzwa uanachama ni kitendo cha udikteta, uonevu na udhalilishaji mkubwa sana.
Kaka Mwita25, nilidhani kwa kuwa ulizaliwa mwaka 1972 bila shaka akili imepevuka, lakini mmh; nimekosea.

Kama hao madiwani walifungua kesi kupinga maamuzi ya kuvuliwa uanachama, basi kisheria maamuzi ya cdm hayawezi kutambuliwa mpaka mahakama itoe uamuzi wa kisheria wa kadhia hiyo!
Its that simple, na tusilaumu bure!

ok kama ni hivyo wange paswa wasihuthurie vikao mpaka hapo kesi itakapo isha . mbona mfanya kazi akiwa ameshitakiwa mahakamani hata kama hana kosa kazini haendi mpaka kesi ishe . lakini leo nimesikia wata endelea kuhuthuria vikao na kupata posho kama kawaida . hapo ndo tunapo jichanganya

Hii serikali kama inataka kutaka tuwaondoe mapema ikulu wamweleza kikwete na hii strategy ya kuingilia maswala ya cdm. Mipango ya ujambazi, wizi na utawala wa mabavu na uloho wa madaraka ndio sababu za ccm kutaka kueneza ujinga. Let's see how this will unfold hapo Arusha. Chadema tumejiandaa na huu ujinga wa ccm na tutawaaibisha wote na kikwete wao, try this again. Unafikiri hatujui jinsi gani tumewaumbua ccm ndani ya cdm? Angalieni nyakati, huu sio wakati wa kuhonga wananchi, tumechoka na wizi wenu na tumeamua ku-move on despite tactics zenu! Idols wenu Gadaffi, Mubarak, Ben Ali wapo wapi leo hii?

We are moving forward na kuongoza Arusha na miji mingine kujenga Taifa letu. Tuna issues nyingi sana za kutetea hili Taifa including strategies za kuingia na kufukuza ujinga wa serikali ya kikwete.

"ccm keep try bribing wananchi na cdm mtakiona! na yeyote ndani ya cdm akikubali kununuliwa na kuharibu cdm tutakupa lesson yako"

Maishamapya,

Ni hatari kujifanya unajua wakati hujui. Nilitegemea kama nia ni njema ungeuliza kilichojiri. Kwa manufaa ya watanzania naomba nieleze ifuatavyo:

i) Kamati Kuu ya Chadema iliwafukuza uanachama madiwani 5 tarehe 7/8/2011. Tarehe 8/8 Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Arusha nilimjulisha uamuzi huo kuwa wahusika wamevuliwa uanachamana hivyo kwa mujibu wa Katiba na sheria inayotawala mamlaka za SM wamepoteza sifa ya kuwa Madiwani.

ii)Tarehe 12/8/2011 anayejiita "Meya wa Arusha" akamjulisha Waziri wa Nchi Tamisemi kuwa Madiwani hao wamevuliwa uanachama

na kuwa barua imepokelewa tarehe 12/8 wakati MD alikuwa ameipokea tarehe 8/8 kwa dispatch. Hivyo "Meya alimpotosha waziri sijui kwa lengo gani.

iii) Tarehe 10/8 Madiwani 5 walifungua, under certificate of urgency (bila main suit sijui utaratibu gani ulitumika kwa vile kwa kawaida Injunction inasimama kwenye kesi mama). Hata hivyo Injuction ilisikilizwa "ex parte" bila Chadema kujulishwa, jambo ambalo nalo ni kinyume na haki za msingi.

iii) Tarehe 11/8 katika kusikiliza ex parte mahakama ya RM ikatoa "order"- Chadema na Freeman Mbowe kuzuiwa kuzungumziia kwenye mikutano ya hadhara mambo yanayowahusu Madiwani hao 5. Pia kuwazuia washitakiwa hao kuchapisha jambo lolote linalowahusu madiwani hao 5.

Order ya mahakama haikuhusu kwa namna yeyote ile "Reinstatement" au hata amri yeyote kuhusiana na status ya madiwani hao. Hivyo Mahakama haikubadilisha wala kutengua maamuzi Katiba ya Chadema.

Hata hivyo amri hiyo ya zuio haikufikishwa kwa Chadema hadi siku 4 baadaye, na kwa maana hiyo Chadema iliendelea na mkutano wake wa hadhara wa tarehe 11/8 uliohusu madiwani hao kana kwamba hapakuwa na amri yeyote ya zuio.

iv) Siku 4 baadaye nilipokea kupitia ofisi ya Katibu wa Mkoa

a) Plaint ya Kesi mama ambapo Madiwani 5 wakiiomba Mahaka "kuwarudishia uanachama wao" kwa kile walichodai utaratibu kutofuatwa. Yaani wanaiomba mahakama iwarudishie uanachama ambao hawakuwa nao kutoka 7/8 baada ya uamuzi wa Kamati Kuu.

b) Siku hiyo hiyo nikapokea barua kutoka madiwani 5( kutoka kila mmoja) barua ya Rufaa dhidi ya uamuzi wa Kamati Kuu iliyoelekiezwa kwa Baraza Kuu-Chadema. Huu ndio utaratibu wa kawaida kwa mujibu wa Katiba ya Chadema, ambao unaelekeza uamuzi wa ngazi moja rufaa yake ni ngazi ya juu.

Ngazi ya juu ya Kamati Kuu ni Baraza Kuu na juu yake ni Mkutano Mkuu. Kwa mujibu wa Katiba ya Chadema huwezi kwenda mahakamani kama hujamaliza ngazi za rufaa ndani ya chama hasa kwa masuala ya uanachama ambayo kimsingi ni mambo ya chama.

Hata hivyo ni dhahiri mtu makini ataona kuwa madiwani hawa au walikuwa wanatumia bush lawyer au kuna ajenda mahususi iliyojificha. Huwezi kuwa na rufaa mbili kwa wakati mmoja kwa mamlaka 2 tofauti.

v) Barua ya Mkuchika inasema inatoa ufafanuzi:

a) Sijui kaombwa ufafanuzi kwa msingi na sheria ipi? sheriaziko wazi maswala ya uanachama ni maswala ya chama ufafanuzi upi unatakiwa kwa waziri ambaye kila mmoja anajua ni wa chama kingine?

b) Je waziri ni juu ya Katiba na Sheria za nchi. ZSerikali hii hii ndiyo iliyokataa hoja ya "mgombea binafsi". Sasa Chama kimewavua uanachama wanabaki kuwa madi8wani kwa udhamini wa nani?wa Waziri-na kama ni hivyo kwa sheria ipi?

c) Swala liko mahakamani na wahusika wameomba kurudishiwa na Mahakama, na hakuna ombi lolote lililoenda kwa waziri kutoka kwa Madiwani hao. Waziri anatoa ufafanuzi kwa nani? Kama alivyoandika kuwa "anayeitwa Meya Gaudence Lymo" ambaye Chadema haimtambui ni kimsingi ndiye msingi wa mgogoro waziri haoni kuna "conflict of Interest" (Waziri na Lymo ni chama kimoja na wote wanajulikana role yao katika kuchakachua uchaguzi wa Meya wa Arusha.

Hivyo, Wana JF ni vema kuweka ushabiki pembeni, tutafute kwanza facts, ndipo tuanze kuhukumu vinginevyo tutaendelea kupotoshana katika mambo ya msingi ambayo hayahitaji porojo.

Lakini Dr Msomi kwa taarifa hawa madiwani mlifukuza tarehe 7/8 na na unasema barua ulipeleka kwa MD tarehe 8/8 ambayo ni siku ya mapumziko. Ni lini mliwajulisha hawa madiwani kwa maana ya kuwapa barua zao za kuwafukuza uanachama? Pamoja na mambo mengine kama unataka kusema ukweli si uwaambie na siku madiwani walipopata barua zao rasmi kwani hawa madiwani wamekuwa kimya kila wakati, ndiyo maana kwa viongozi kama nyie wasomi na wazoefu mkawachafua hadharani na hata kuingilia maisha yao binafsi kitu ambacho kwa kweli ni siasa za maji taka. Dr. Tunakuamini Tunakuhitaji ila tuambie ukweli imani yetu izidi kwako, ila utajishushia heshima kama hutaeleza ukweli kwa watanzania.

Kama hulijui jambo kaa kimya. Mtu mjinga anayedhani anajua ni hatari sana. Kwa kukuelewesha tu kama unataka kuelewa, mtu ukifukuzwa uanachama unapoteza ubunge, urais au udiwani. Kwa hiyo wale si madiwani tena maana hawana chama. Sasa mahakama pekee ndio yenye uwezo wa kutoa zuio la muda. Sasa kama hutaki kuelewa ni sawa ila sasa kutukana watu haijengi. kwani Tumaini na RUCo kuna nini hadi unawadharau? Chuo ambacho kina vilaza ni UDOM tu ila pia si wote kuna baadhi ya wanafunzi wazuri sana UDOM.
Yeye kasoma sharia kweny Muslim University of Morogoro.. Nasikia wanatoa mabingwa wa sharia kule...teh teh tehe..!

Wanatetewa na serikali kwa sababu haipendi kuona mtu anaonewa kwa sababu ya unyonge wake, udhaifu nk. Kitendo cha madiwani hao kufukuzwa uanachama ni kitendo cha udikteta, uonevu na udhalilishaji mkubwa sana.
umejitahidi kutokana na ufinyu wa fikra zako yaani kwa mkosaji kuchukuliwa hatua wewe unasema kadhalilishwa?

Hapo ndio CHADEMA wajifunze kuwa hawako smart katika siasa za hii nchi. hivi sasa kitakachotokea ni kwamba kwa kipindi ambacho kesi inaendelea madiwani hao watakuwa on the side of CCM government. CHADEMA wamejitengenezea wenyewe minority situation. Siasa za kuonyeshana ubabe hazipaswi kupewa nafasi katika maeneo ambayo chama kimeanza kukubalika; sasa mmepoteza influence mliyojinyakulia kwa bidii kubwa!!!

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi), George Mkuchika, amedaiwa kukiuka Katiba ya nchi kutokana na kuandika barua ya kuruhusu madiwani watano waliofukuzwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuruhusiwa kuendelea kuhudhuria vikao vya baraza na kutakiwa kulipwa stahili zao zote.

Wakili Kimomogolo alisema maamuzi yaliyofikiwa na Mkuchika yalikiuka Katiba ya Muungano kwa vile mtu anayehitaji kugombea uongozi katika nafasi yoyote ni lazima awe na dhamana ya chama.
Alisema kuwa vipengele vingine vinaweka bayana kuwa katika suala la urais, ubunge na udiwani utakoma pindi chama kilichomwekea dhamana kitaondoa dhamana yake na kusema kwa kuwa tayari CHADEMA ilikwishaondoa dhamana kwa madiwani hao sasa hawana sifa. Wakili Kimomogoro alisema kuwa inashangaza kuona serikali iliyopinga mgombea binafsi mahakamani na kushinda kesi lakini inakuja kuwatambua madiwani ambao mdhamini wao amekwishawafukuza ambaye ni CHADEMA.

Nakala ya barua hiyo ambayo ilibeba kichwa cha habari kinachosema ‘Kuvuliwa uanachama hivyo kukosa sifa ya kuwa diwani’ huku mwisho wa barua hiyo ikisema kuwa ’kutokana na madiwani hao watano kufungua kesi na kuiomba mahakama kuwarejesha uanachama wataendelea kuhudhuria vikao vyote vya baraza na kulipwa stahili zote hadi mahakama itakapotoa uamuzi’.

Dr Slaa ambaye kitaaluma ni mwanasheria anasema:
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema katiba ya Chadema inasema ukishavuliwa uanachama hutakiwi kujihusisha na masuala ya kisiasa kwa sababu si mwanachama, hivyo madiwani hao wanalipwa posho za wananchi. Kwa nini wanahudhuria vikao vya Baraza la Madiwani wakati chama hakiwatambui wala mahakama haijasikiliza kesi yao ya msingi waliyoifungua?” alihoji Dk. Slaa wakati akizungumza na waandishui wa habari jijini Arusha jana.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Aliongeza kuwa inashangaza madiwani hao kufungua kesi mahakamani na kukata rufaa Baraza Kuu la Chadema kuomba warudishiwe uanachama wakati chama hakijatoa maamuzi ya rufaa waliyoikata wala mahakama haijatoa majibu, ila waziri anatoa majibu ya mahakama.[/FONT]

maamuzi ya serikali sikivu. Wao wamejipanga na hawakurupuki kwa sababu magamba yao hayaruhusu kukurupuka. nwasilisha wakuu

Hapo ndio CHADEMA wajifunze kuwa hawako smart katika siasa za hii nchi. hivi sasa kitakachotokea ni kwamba kwa kipindi ambacho kesi inaendelea madiwani hao watakuwa on the side of CCM government. CHADEMA wamejitengenezea wenyewe minority situation. Siasa za kuonyeshana ubabe hazipaswi kupewa nafasi katika maeneo ambayo chama kimeanza kukubalika; sasa mmepoteza influence mliyojinyakulia kwa bidii kubwa!!!
Ndiyo maana ile kauli maarufu ya kujivua gamba kwenu CCM haitekelezeki!! kama hao jamaa wamefukuzwa uanachama wa chadema , basi , wamefukuzwa uanachama period! hakuna CCM , mahakama wala ngedere yeyote mwenye mamlaka ya kuwarudisa tena ndani ya CDM isipokuwa CDM wenyewe.
By the way.....kwa CCM kuwatetea sana hao madiwani inaonyesha wana ubia fulani na CCM na ndiyo maana hata wana CDM hawawataki!

aa MAAMUZI MENGI YA ISSUE CRITICAL YANAYOCHUKULIWA NA MAGAMBA HUWA YANACHUKULIWA GIZANI, UMEME UKIRUDI GAFLA TU WANA REALISE KUWA WAMETOA MAAMUZI PUMBA(REFER ISHU YA LUHANJO KUMSAFISHA JAIRO). EVEN THIS UMEME UKIRUDI WATAREALISE HAAAYA TUMECHEMKA. WE SUBIRI TU YETU MACHO.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Mkuchika, ameamuru madiwani waliofukuzwa wa Chadema, kuendelea na vikao na kulipwa posho zao hadi Mahakama itakapotoa uamuzi juu ya kufukuzwa kwao.

Aidha barua ya Mkuchika yenye Kumbukumbu namba HA.23/235/01/06 iliyotolewa Agosti 23, na kumfikia Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Estomih Chang'ah, ilieleza kuwa Tamisemi bado inawatambua madiwani hao na wataendelea kulipwa posho zao hadi Mahakama itakapotoa uamuzi kama madiwani hao watano ni wanachama halali wa Chadema au la.

Barua hiyo pia ilieleza kuwa Mahakama ndiye mwamuzi wa mwisho, hivyo ni vyema suala hilo likasubiriwa kutolewa uamuzi, lakini madiwani hao ambao ni Estomii Mallah (Kimandolu), Ruben Ngowi (Themi), John Bayo (Elerai), Charles Mpanda (Kaloleni) na Diwani wa Viti Maalumu, Rehema Mohamed, kisheria wataendelea kuhudhuria vikao na kulipwa posho.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkurugenzi Chang'a alisema amepokea barua hiyo kutoka kwa Waziri Mkuchika yenye maelezo hayo kutokana na barua ya awali aliyoiandika MD/ US/101/ 1/107 Agosti 12.

Alisema suala la madiwani hao kuendelea na wadhifa, ni uamuzi utakaotolewa na Mahakama, kwani walishafungua kesi ya madai, hivyo Mahakama ndiyo itatoa uamuzi kisheria na nakala za barua hiyo wamepewa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isdore Shirima, Katibu Mkuu wa Chadema, Willibrod Slaa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Alisema Sheria ya Serikali za Mitaa namba 8 ya mwaka 1982, kifungu cha 26 (1) (e), inafafanua kuwa Waziri mwenye dhamana na serikali za mitaa, atatamka kuwa nafasi ya Diwani iko wazi, baada ya kupokea taarifa rasmi ya maandishi kutoka kwa Mwenyekiti au
Meya wa Jiji la Arusha.

Alisema suala la kuambiwa kuwa anakumbatia madiwani hao kama Mkurugenzi linamwumiza kichwa na anapokea tuhuma nyingi juu ya madiwani hao pia maendeleo ya Jiji la Arusha hafanyiki, kutokana na mgogoro huo, na Waziri ameshatoa ufafanuzi, hivyo
kutokana na uamuzi wa Waziri busara zinahitajika zaidi.

"Wengi wanadhani nawabeba madiwani hao waliovuliwa uanachama, lakini ukweli siwakumbatii, napokea malalamiko mengi lakini namwachia Mungu, ila naomba busara zaidi itumike kwa suala hili, hususan kwa viongozi wa siasa, maana Waziri ametoa majibu kwenye barua, lakini sijui itakuwaje.

“Nawaomba viongozi wa siasa kutumia busara zaidi, kwani maendeleo ya Arusha yanalala … inaumiza unapotuhumiwa kwa kitu ambacho hujakifanya, inaumiza kichwa changu sana."

Dk Slaa alisema aliwasilisha barua ya kuwavua uanachama madiwani hao kwa Mkurugenzi Agosti 8 lakini anashangaa kuwa barua ya Waziri ilimfikia Agosti 12, na si Agosti 10 kama nukushi inavyoeleza.

“Suala la Arusha inabidi liangaliwe kwa kina, kwani inavyoonekana wanapoteza muda wa maendeleo kwa vitu vya kipuuzi, wasipoangalia kuhusu uamuzi sahihi wa mgogoro wa Arusha, kitakachotokea ni kama suala la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo.

Ili kujiongezea kipato serikali yetu imeamua kuwa inaendesha shughuli za uwakili hivyo madiwani wameikodi serikali kama wakili(advocate) hivyo ukiwa na kesi ikodi serikali.

Hii serikali ya Kikwete ina wanasheria wanaojua sheria au wamekabidhiwa majukumu mazito wenzangu mimi wasiojua nini mkondo wa sheria unakoelekea? Ndio maana naelewa sasa Serikali ya CCM kumpa uwaziri wa Katiba na sheria mtu asiyejua hata sheria inaanzia wapi mwenye mafungo ya utumishi kutoka kivukoni.

aa MAAMUZI MENGI YA ISSUE CRITICAL YANAYOCHUKULIWA NA MAGAMBA HUWA YANACHUKULIWA GIZANI, UMEME UKIRUDI GAFLA TU WANA REALISE KUWA WAMETOA MAAMUZI PUMBA(REFER ISHU YA LUHANJO KUMSAFISHA JAIRO). EVEN THIS UMEME UKIRUDI WATAREALISE HAAAYA TUMECHEMKA. WE SUBIRI TU YETU MACHO.

Halafu tupo kwenye swaumu tunathubutu kusema Rais kapata taarifa ya Jairo siku moja baadaye na hivyo Ikukubatilisha maamuzi, huyu Luhanjo yuko Ikulu ya Chamwino au ya Dar? Huyu Luhanjo ni zaidi ya Rais na Waziri Mkuu mwenye dhamana ya kutolea maamuzi?

Watakapo shtukia kwenda kinyume Pinda atapindisha kwamba wamechelewesha kufikisha suala kwake na hivyo anapindisha uamuzi wa awali.

Issue ya madiwani wa Arusha ni mtego wa CCM kwa CDM lakini umefyatuliwa na CDM bila kuinasa CDM, umewanasa madiwani feki.

Wanataka udiwani huu ili wamwakilishe nani? Umma uliojitokeza siku ya mkutano wa CDM hawakuona nini ? Laiti wangeuona na waka tafakari.

aa MAAMUZI MENGI YA ISSUE CRITICAL YANAYOCHUKULIWA NA MAGAMBA HUWA YANACHUKULIWA GIZANI, UMEME UKIRUDI GAFLA TU WANA REALISE KUWA WAMETOA MAAMUZI PUMBA(REFER ISHU YA LUHANJO KUMSAFISHA JAIRO). EVEN THIS UMEME UKIRUDI WATAREALISE HAAAYA TUMECHEMKA. WE SUBIRI TU YETU MACHO.
Like father like children. Kama rais ni mkurupukaji, then mlitegemea mawaziri wangekuwaje?

Lakini Dr Msomi kwa taarifa hawa madiwani mlifukuza tarehe 7/8 na na unasema barua ulipeleka kwa MD tarehe 8/8 ambayo ni siku ya mapumziko. Ni lini mliwajulisha hawa madiwani kwa maana ya kuwapa barua zao za kuwafukuza uanachama? Pamoja na mambo mengine kama unataka kusema ukweli si uwaambie na siku madiwani walipopata barua zao rasmi kwani hawa madiwani wamekuwa kimya kila wakati, ndiyo maana kwa viongozi kama nyie wasomi na wazoefu mkawachafua hadharani na hata kuingilia maisha yao binafsi kitu ambacho kwa kweli ni siasa za maji taka. Dr. Tunakuamini Tunakuhitaji ila tuambie ukweli imani yetu izidi kwako, ila utajishushia heshima kama hutaeleza ukweli kwa watanzania.

Lago,
Maamuzi yaliyofanywa kwa hawa madiwani ni halali, lazima waelewa dhamana ya chama katika nafasi yao. Hawawezi kuwa na kiburi.

Back
Top Bottom