Madiwani waliofukuzwa kwa nini watetewe na serikali?

wale ni waasi wa chadema yaani wanunga mkono yellowgreen, serikali ndio hiyo yellowgreen ndio maana wanawatambua
 
Ngoja tutafute copy ya hilo gazeti na kuona undani wa kilichomsukuma Mkuchika kutoa uamuzi huo!!!
Mkuchika aibua mgogoro mpya Arusha
• Awarejesha madiwani waliofukuzwa CHADEMA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi), George Mkuchika, amedaiwa kukiuka Katiba ya nchi kutokana na kuandika barua ya kuruhusu madiwani watano waliofukuzwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuruhusiwa kuendelea kuhudhuria vikao vya baraza na kutakiwa kulipwa stahili zao zote.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuahirishwa kwa kesi ya viongozi wa chama hicho katika Mahakama Kuu mwanasheria, Methodi Kimomogolo, ambaye alitoa kauli hiyo baada ya Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Willibrod Slaa kuonyesha nakala ya barua iliyotoka kwa Mkuchika yenye kumb Na HA 23/235/01/16 ya Agosti 23, mwaka huu, iliyotumwa kwa Meya wa Manispaa ya Arusha, Gaudensi Lyimo, kuhusu hatma ya madiwani hao.

Nakala ya barua hiyo ambayo ilibeba kichwa cha habari kinachosema ‘Kuvuliwa uanachama hivyo kukosa sifa ya kuwa diwani' huku mwisho wa barua hiyo ikisema kuwa 'kutokana na madiwani hao watano kufungua kesi na kuiomba mahakama kuwarejesha uanachama wataendelea kuhudhuria vikao vyote vya baraza na kulipwa stahili zote hadi mahakama itakapotoa uamuzi'.

Wakili Kimomogolo alisema maamuzi yaliyofikiwa na Mkuchika yalikiuka Katiba ya Muungano kwa vile mtu anayehitaji kugombea uongozi katika nafasi yoyote ni lazima awe na dhamana ya chama.

Alisema kuwa vipengele vingine vinaweka bayana kuwa katika suala la urais, ubunge na udiwani utakoma pindi chama kilichomwekea dhamana kitaondoa dhamana yake na kusema kwa kuwa tayari CHADEMA ilikwishaondoa dhamana kwa madiwani hao sasa hawana sifa.

Wakili Kimomogoro alisema kuwa inashangaza kuona serikali iliyopinga mgombea binafsi mahakamani na kushinda kesi lakini inakuja kuwatambua madiwani ambao mdhamini wao amekwishawafukuza ambaye ni CHADEMA.

"Kwenye kesi aliyofungua Mchungaji Christopher Mtikila ambapo mahakama imeamua hakuna mgombea binafsi hivyo maamuzi yanayofanywa na madiwani hao kwenye vikao vya baraza nayo ni batili na posho wanazopokea ni wizi na anayewapa atawajibika kuzilipa, " alisema Kimomogoro.

Naye Dk. Slaa alisema alishangazwa na maamuzi hayo kwa kuwa madiwani hao walishavuliwa uanachama na kupelekea kukimbilia mahakamani ili kurejeshewa uanachama wao hivyo iwapo waziri ataendelea kuwatambua wakati chama hicho kiliondoa dhamana ni kukiuka taratibu za sheria.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Estomii Chang'a, alikiri kuipata barua hiyo anachokitekeleza ni maamuzi hayo yaliyotoka ngazi za juu.

Madiwani waliofukuzwa CHADEMA baada ya kukaidi maamuzi ya Kamati Kuu yaliyowataka kujivua nyadhifa walizopata kupitia muafaka walioingia bila baraka za chama hicho na kata zao kwenye mabano ni Naibu Meya , Estomih Mallah (Kimandolu), Charles Mpanda (Kaloleni), Ruben Ngowi (Themi) na Rehema Mohamed (Viti Maalum).
 
Haya mambo ndiyo yanapelekea serikali kuitwa kigeugeu lakini waangalie yasije kuwarudi wenyewe tusubiri ya RACHEL.
 
Mambo ya serikali ya Tz ni pasua kichwa, wameacha kazi zao za kujivua gamba wameingilia mambo ya CDM wakati kiukweli ccm ndo chanzo cha mgogoro huo. Alafu hapo ndo tunapata picha kuwa wale madiwani walikuwa corrupted ndomana wakakubali huo mwafaka sasa ccm roho inauma hela zao zimeenda bure ndomana wanapigana kufa wale madiwani warudi.
 
Pro-CDM-JF, wengi ni mbumbumbu wa sheria, wanadhani a loser Dr Slaa, ana uwezo wa kupingana na mahakama wakati ili suala ni la kisheria zaidi sio porojo.
Raia wa Tanzania haki zao wanazipata mahakamani na Madiwani wa Arusha haki zao wameona watazipata mahakamani, CDM wanatakiwa wasubiri maamuzi ya mahakama hata kama kesi itachukuwa miaka mitano
Mtoto wa loser MH.Dr Jakaya Mrisho Kikwete baba yako ni looser katika kila field hana pa kukamata , angalia hata leo kaibamiza daladala akikimbilia msoga akapata upepo wa Sangoma,fungua masikio tunakwambia baba yako hawezi kuendelea kuchezea wananchi wa Arusha kupitia madiwani majibu yake atayapata muda si mrefu
 
Serikali na CCM inahusika vipi hapo? Maana hao magwanda wenzenu wamefungua kesi mahakamani, kwa hiyo kama mnatafuta mchawi ni mahakama na si kati ya hao.


Soma taarifa ya mkuchika ndo uulize swli lako? ishu sio mahakama ishu ni ccm kuwataka wale madiwani waingie kwenye vikao na sio tamko la mahakama
 
Hivi mnategemea mahakama iwatalazimishe Chadema kurudisha uanachama wao never hata wao madiwani wanalijua hilo sijui kwa nini walikata rufaa kwenye Baraza la chama huku wamefungua kesi mahakamani.
 
Wanatetewa na serikali kwa sababu haipendi kuona mtu anaonewa kwa sababu ya unyonge wake, udhaifu nk. Kitendo cha madiwani hao kufukuzwa uanachama ni kitendo cha udikteta, uonevu na udhalilishaji mkubwa sana.
Je pia serikali hii itawatetea mapacha watatu especialy Rostam Aziz kwani pia wao wanaonewa na wanadhalilishwa na viongozi wa CCM kwa ujumla.
 
Mimi nafikiri Chadema ikae mbali na ngorogoro huu maana yenyewe imeshamaliza kazi wale si wanachama wake mgogoro huu sasa umegeuka kuwa kati ya Serikali na mahakama.
 
Maishamapya,

Ni hatari kujifanya unajua wakati hujui. Nilitegemea kama nia ni njema ungeuliza kilichojiri. Kwa manufaa ya watanzania naomba nieleze ifuatavyo:

i) Kamati Kuu ya Chadema iliwafukuza uanachama madiwani 5 tarehe 7/8/2011. Tarehe 8/8 Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Arusha nilimjulisha uamuzi huo kuwa wahusika wamevuliwa uanachamana hivyo kwa mujibu wa Katiba na sheria inayotawala mamlaka za SM wamepoteza sifa ya kuwa Madiwani.

ii)Tarehe 12/8/2011 anayejiita "Meya wa Arusha" akamjulisha Waziri wa Nchi Tamisemi kuwa Madiwani hao wamevuliwa uanachama
na kuwa barua imepokelewa tarehe 12/8 wakati MD alikuwa ameipokea tarehe 8/8 kwa dispatch. Hivyo "Meya alimpotosha waziri sijui kwa lengo gani.

iii) Tarehe 10/8 Madiwani 5 walifungua, under certificate of urgency (bila main suit sijui utaratibu gani ulitumika kwa vile kwa kawaida Injunction inasimama kwenye kesi mama). Hata hivyo Injuction ilisikilizwa "ex parte" bila Chadema kujulishwa, jambo ambalo nalo ni kinyume na haki za msingi.

iii) Tarehe 11/8 katika kusikiliza ex parte mahakama ya RM ikatoa "order"- Chadema na Freeman Mbowe kuzuiwa kuzungumziia kwenye mikutano ya hadhara mambo yanayowahusu Madiwani hao 5. Pia kuwazuia washitakiwa hao kuchapisha jambo lolote linalowahusu madiwani hao 5.

Order ya mahakama haikuhusu kwa namna yeyote ile "Reinstatement" au hata amri yeyote kuhusiana na status ya madiwani hao. Hivyo Mahakama haikubadilisha wala kutengua maamuzi Katiba ya Chadema.

Hata hivyo amri hiyo ya zuio haikufikishwa kwa Chadema hadi siku 4 baadaye, na kwa maana hiyo Chadema iliendelea na mkutano wake wa hadhara wa tarehe 11/8 uliohusu madiwani hao kana kwamba hapakuwa na amri yeyote ya zuio.

iv) Siku 4 baadaye nilipokea kupitia ofisi ya Katibu wa Mkoa

a) Plaint ya Kesi mama ambapo Madiwani 5 wakiiomba Mahaka "kuwarudishia uanachama wao" kwa kile walichodai utaratibu kutofuatwa. Yaani wanaiomba mahakama iwarudishie uanachama ambao hawakuwa nao kutoka 7/8 baada ya uamuzi wa Kamati Kuu.

b) Siku hiyo hiyo nikapokea barua kutoka madiwani 5( kutoka kila mmoja) barua ya Rufaa dhidi ya uamuzi wa Kamati Kuu iliyoelekiezwa kwa Baraza Kuu-Chadema. Huu ndio utaratibu wa kawaida kwa mujibu wa Katiba ya Chadema, ambao unaelekeza uamuzi wa ngazi moja rufaa yake ni ngazi ya juu.

Ngazi ya juu ya Kamati Kuu ni Baraza Kuu na juu yake ni Mkutano Mkuu. Kwa mujibu wa Katiba ya Chadema huwezi kwenda mahakamani kama hujamaliza ngazi za rufaa ndani ya chama hasa kwa masuala ya uanachama ambayo kimsingi ni mambo ya chama.

Hata hivyo ni dhahiri mtu makini ataona kuwa madiwani hawa au walikuwa wanatumia bush lawyer au kuna ajenda mahususi iliyojificha. Huwezi kuwa na rufaa mbili kwa wakati mmoja kwa mamlaka 2 tofauti.

v) Barua ya Mkuchika inasema inatoa ufafanuzi:

a) Sijui kaombwa ufafanuzi kwa msingi na sheria ipi? sheriaziko wazi maswala ya uanachama ni maswala ya chama ufafanuzi upi unatakiwa kwa waziri ambaye kila mmoja anajua ni wa chama kingine?

b) Je waziri ni juu ya Katiba na Sheria za nchi. ZSerikali hii hii ndiyo iliyokataa hoja ya "mgombea binafsi". Sasa Chama kimewavua uanachama wanabaki kuwa madi8wani kwa udhamini wa nani?wa Waziri-na kama ni hivyo kwa sheria ipi?

c) Swala liko mahakamani na wahusika wameomba kurudishiwa na Mahakama, na hakuna ombi lolote lililoenda kwa waziri kutoka kwa Madiwani hao. Waziri anatoa ufafanuzi kwa nani? Kama alivyoandika kuwa "anayeitwa Meya Gaudence Lymo" ambaye Chadema haimtambui ni kimsingi ndiye msingi wa mgogoro waziri haoni kuna "conflict of Interest" (Waziri na Lymo ni chama kimoja na wote wanajulikana role yao katika kuchakachua uchaguzi wa Meya wa Arusha.

Hivyo, Wana JF ni vema kuweka ushabiki pembeni, tutafute kwanza facts, ndipo tuanze kuhukumu vinginevyo tutaendelea kupotoshana katika mambo ya msingi ambayo hayahitaji porojo.


And this is the point. Kwa kifupi ni kuwa uamuzi wa kamati kuu ya CDM umepingwa mahakamani, na mahakama ikausitisha. Kama wangekata rufaa kwa kufuata ngazi za chama basi uamuzi huo ungeendelea.

Shida ni kuwa pale ambapo chombo cha juu cha chama kingeamua kubatilisha maamuzi wa kamati kuu, walalamikaji wangekuwa wameathirika tayari.

Wanakuwa hawana udiwani. Ndo maana wakakimbilia mahakamani.
Naomba nieleweke kuwa siwatetei madiwani hao, ila naelezea hali yenyewe.
 
Dr. Slaa,

Kabla sijamaliza kusoma post yako, tarehe 8/8 ni siku ya mapumziko. Sorry kama umeeleza kwani huenda aliepokea sio MD.
 
Pro-CDM-JF, wengi ni mbumbumbu wa sheria, wanadhani a loser Dr Slaa, ana uwezo wa kupingana na mahakama wakati ili suala ni la kisheria zaidi sio porojo.
Raia wa Tanzania haki zao wanazipata mahakamani na Madiwani wa Arusha haki zao wameona watazipata mahakamani, CDM wanatakiwa wasubiri maamuzi ya mahakama hata kama kesi itachukuwa miaka mitano

Umetoa darasa tosha na ni lazima tujue haki na sheria ni nini na sio nguvu na ubabe(ubishi) havisaidii! nadhani jinsi siku zinavyoenda tutafahamu umhimu wa kudai haki na kutendewa haki mahakamani! ni haki ya madiwani kudai haki yao mahakamani na ndio utawala wa sheria kwenye nchi ya demokrasia.

CHADEMA hili ni jambo la kawaida hakuna wa kumchukia kama kamati kuu ilivyo chukua maamuzi magumu lazima tuelewa na madiwani wana haki ya kwenda kwenye chombo cha kudai haki yao ambacho ni mahakama! Mahakama zitakuwepo watapita CCM na CDM watatawala wataondoka na Mahakama itabaki palepale kama chombo cha kukimbilia kudai haki! Tuache unazi na ushabiki wa vyama tujitahidi kuelewa sheria zaidi!
 
Mtoto wa loser MH.Dr Jakaya Mrisho Kikwete baba yako ni looser katika kila field hana pa kukamata , angalia hata leo kaibamiza daladala akikimbilia msoga akapata upepo wa Sangoma,fungua masikio tunakwambia baba yako hawezi kuendelea kuchezea wananchi wa Arusha kupitia madiwani majibu yake atayapata muda si mrefu

hahahhahahahhahah kwel kukariri kubaya yani umeona ID ya RITZ akili imekutuma kuwa atakua Ridhiwani! dada yangu pole sana huyu sio ridhiwani hahahahahah naumia mbavu mie!
 
Wangekuwa wanyonge wangekubali kupokea rushwa na kuukana ukweli wa mauaji ya jan. 5 ambayo wao ndo walikuwa mstari wa mbele kwenye maandamano yake?

Ngonini,

Be deep in your world. By this post, you dont seem to understand anything about anything you are trying to talk about..
 
Dr Slaa(Phd) kuna msemo wa kiswahili unasema unapo lalia siko ninako amkia! Ni kama msemo huu to every action there is equal and opposite reaction. Na inaendana na ngojera huendelezwa kwa ngojera. Ilichofanya kamati kuu kinaendelezwa na madiwani kwenda mahakani, yani zumari na mpiga chakacho msikilizaji humjua alie hodari.

Ni sawa na mamba hategemei sana maisha yake majini na nchi kavu anaweza ishi ila samaki yeye akitoka majini sekunde tu mauti humjia! na ndivyo hivyo fumbo mfumbie mjinga. Nadhani kwa Phd yako Dr Slaa utajua mchezo huu wa kamati kuu na madiwani ni nani anaefika mapema au ni nani alieanza safari mapema akchoka mapema! mwisho utajulikana lakini badae sana.
 
Back
Top Bottom