Madiwani waliofukuzwa kwa nini watetewe na serikali?

Leo nimesikia kwenye mapitio ya magazeti asbhi kuwa serikali inatambua madiwani waliofukuzwa na CDM kuendelea na vikao mpaka mahakama itakapoamua.

Wadau hii imekaaje.

Imekaaje kivipi kwani hapa ni mahakamani?, tusipende kudhani kila kitu kina amriwa ONLINE!!!

Maalim Seif, Hamis Machano, Juma Duni Haji na wengineo walitimuliwa kwenye Magamba, huko kulikuwa ni kuwatetea wanyonge? Ama kweli magamba ni kinyonga!

Mwenye CV ya naibu Meya wa Arusha Estomi Mallah, naomba aibandike humu Jamvini. Mpiganaji wetu wapenda amani

Mwenye CV ya naibu Meya wa Arusha Estomi Mallah, naomba aibandike humu Jamvini. Mpiganaji wetu wapenda amani
Mpiganaji wa mafisadi kama wewe! Ipo siku mtakimbilia Zimbabwe! You can not fool people all the time!

Mnashangaa nini mkiambiwa chama lege lege huzaa serekali lege lege huwa hamuelewi?

Wanatetewa na serikali kwasababu haipendi kuona mtu anaonewa kwasababu ya unyonge wake, udhaifu nk. Kitendo cha madiwani hao kufukuzwa uanachama ni kitendo cha udikteta, uonevu na udhalilishaji mkubwa sana.

Bw...ge kabisa... Masaburi kwa kwenda mbele...

Kwanini magamba wasiwape kadi zao ili waendelee na udiwani?
Huu ni usanii wa kitoto kabisa. Kizazi hiki kinaweka historia mbaya sana

Swali langu ni kwamba wataingia vikaoni na kukaa kambi ya nani? Chadema wamesha waona sio wa kuendelelea nao

Swali langu ni kwamba wataingia vikaoni na kukaa kambi ya nani? Chadema wamesha waona sio wa kuendelelea nao
watakuwa upande wa ccm kupitia chadema...ninacho shangaa hivi mme/mke akikupa talaka unamngangania

Mwenye CV ya naibu Meya wa Arusha Estomi Mallah, naomba aibandike humu Jamvini. Mpiganaji wetu wapenda amani

Ukibishana na mpumbavu ni kupoteza mda so mwache aende na upumbavu wake. We siku zako zinahesabika .

Hapa tunazidi kupata picha kamili.
Mkurugenz amedai hauwez kutengua uamuz wa serikal kwa uamuzi wa watu wachache.

Sikujua kua kumbe ukivuliwa uanachama unaenda mahakamani? kwa hiyo Mapacha nao wakivuliwa watakimbilia mahakamani? kazi tunayo kwa kweli

Wanatetewa na serikali kwa sababu haipendi kuona mtu anaonewa kwa sababu ya unyonge wake, udhaifu nk. Kitendo cha madiwani hao kufukuzwa uanachama ni kitendo cha udikteta, uonevu na udhalilishaji mkubwa sana.

magamba iwachukuwe wao wanapenda sana takataka watawafaa sana

Kinaachochekesha ni kwamba CCM hao hao ndiyo wamekuwa vin'gan'ganizi wa ili uwe mwakilishi inabidi uwe mwanachama wa chama cha siasa, Mtikila ameshinda mara mbili ile kesi yake ya mgombea binafsi. Lakini serikali ya CCM ikakata rufaa mara zote na kutengua ushindi.

Hii ilikuwa ni kwa fikra kwamba wagombea binafsi watakidhuru chama hicho, sasa leo hii watu walionyan'ganywa uanachama wanapata wapi uhalali wa kuwa wawakilishi wa hicho chama. Kweli CCM na serikali yake wamefilisika, wamepotoka, na historia itaendelea kuwahukumu.

Kweli CCM na serikali yake wamefilisika, wamepotoka, na historia itaendelea kuwahukumu.

Serikali na CCM inahusika vipi hapo? Maana hao magwanda wenzenu wamefungua kesi mahakamani, kwa hiyo kama mnatafuta mchawi ni mahakama na si kati ya hao.

[FONT=Georgia, 'Times New Roman', Times, serif]HABARI LEO

[/FONT]Imeandikwa na Veronica Mheta, Arusha; Tarehe: 27th August 2011

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Mkuchika, ameamuru madiwani waliofukuzwa wa Chadema, kuendelea na vikao na kulipwa posho zao hadi Mahakama itakapotoa uamuzi juu ya kufukuzwa kwao.

Aidha barua ya Mkuchika yenye Kumbukumbu namba HA.23/235/01/06 iliyotolewa Agosti 23, na kumfikia Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Estomih Chang'ah, ilieleza kuwa Tamisemi bado inawatambua madiwani hao na wataendelea kulipwa posho zao hadi Mahakama itakapotoa uamuzi kama madiwani hao watano ni wanachama halali wa Chadema au la.

Barua hiyo pia ilieleza kuwa Mahakama ndiye mwamuzi wa mwisho, hivyo ni vyema suala hilo likasubiriwa kutolewa uamuzi, lakini madiwani hao ambao ni Estomii Mallah (Kimandolu), Ruben Ngowi (Themi), John Bayo (Elerai), Charles Mpanda (Kaloleni) na Diwani wa Viti Maalumu, Rehema Mohamed, kisheria wataendelea kuhudhuria vikao na kulipwa posho.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkurugenzi Chang'a alisema amepokea barua hiyo kutoka kwa Waziri Mkuchika yenye maelezo hayo kutokana na barua ya awali aliyoiandika MD/ US/101/ 1/107 Agosti 12.

Alisema suala la madiwani hao kuendelea na wadhifa, ni uamuzi utakaotolewa na Mahakama, kwani walishafungua kesi ya madai, hivyo Mahakama ndiyo itatoa uamuzi kisheria na nakala za barua hiyo wamepewa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isdore Shirima, Katibu Mkuu wa Chadema, Willibrod Slaa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Alisema Sheria ya Serikali za Mitaa namba 8 ya mwaka 1982, kifungu cha 26 (1) (e), inafafanua kuwa Waziri mwenye dhamana na serikali za mitaa, atatamka kuwa nafasi ya Diwani iko wazi, baada ya kupokea taarifa rasmi ya maandishi kutoka kwa Mwenyekiti au
Meya wa Jiji la Arusha.

Alisema suala la kuambiwa kuwa anakumbatia madiwani hao kama Mkurugenzi linamwumiza kichwa na anapokea tuhuma nyingi juu ya madiwani hao pia maendeleo ya Jiji la Arusha hafanyiki, kutokana na mgogoro huo, na Waziri ameshatoa ufafanuzi, hivyo
kutokana na uamuzi wa Waziri busara zinahitajika zaidi.

"Wengi wanadhani nawabeba madiwani hao waliovuliwa uanachama, lakini ukweli siwakumbatii, napokea malalamiko mengi lakini namwachia Mungu, ila naomba busara zaidi itumike kwa suala hili, hususan kwa viongozi wa siasa, maana Waziri ametoa majibu kwenye barua, lakini sijui itakuwaje.

“Nawaomba viongozi wa siasa kutumia busara zaidi, kwani maendeleo ya Arusha yanalala … inaumiza unapotuhumiwa kwa kitu ambacho hujakifanya, inaumiza kichwa changu sana."

Dk Slaa alisema aliwasilisha barua ya kuwavua uanachama madiwani hao kwa Mkurugenzi Agosti 8 lakini anashangaa kuwa barua ya Waziri ilimfikia Agosti 12, na si Agosti 10 kama nukushi inavyoeleza.

“Suala la Arusha inabidi liangaliwe kwa kina, kwani inavyoonekana wanapoteza muda wa maendeleo kwa vitu vya kipuuzi, wasipoangalia kuhusu uamuzi sahihi wa mgogoro wa Arusha, kitakachotokea ni kama suala la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo.

Back
Top Bottom