Madiwani wa Makambako mvua inawaumbua

Mangandula

Senior Member
Nov 30, 2011
184
37
Hakika siasa na utaalaam ni vitu viwili tofauti, leo hii mvua imenyesha sana hapa makambako, cha ajabu barabara za mitaa walizojinasibu madiwani wetu kuwa wamezifanyia ukarabati kwa kiwango cha changalawe zimeja maji na kufanya sehemu nyingine kupasua mifereji ili kuruhusu maji kusafiri.

Cha kujiuliza ni kwamba unaweza kujenga barabara bila kuweka makaravati? Hapo madiwani mmeumbuka tatueni kero hii haraka iwezekanavyo kwani haya madimbwi yanaharibu manidhali ya mji.
 
Unaweza jenga barabara bila kuweka makaravati labda kama ulimaanisha mitaro.
Karavati litawekwa tuu mahara ambapo ni mapitio ya maji ambayo huwa collected na mitaro
Izo ni changamoto ambazo wanatakiwa zitatua kabla mvua hazijashika kasi nadhani ni uwanja wa Jah Peple huo mtu wa watu!
 
Ndiyo maana ya maji kutuama yanakuwa yamekosa mahali pa kupita. Mifereji bila makaravati unajenga mazalia ya mbu mjini! Uko sahihi huu ni uwanja wa Jah lakini hatuna shida naye kwani alikuwa diwani miaka kumi hakuna alichofanya kwa upande wa barabara hizi! Bora hawa madiwani wapya japo wamethubutu. Lakini huyu mbunge wetu kivuli hamna kitu nothing
 
****** alisema yeye siyo mvua so hawezi kunyesha ili mabwawa yajae tupate umeme hata madiwani watasema wao siyo
mungu wakuzuia mvua isilete uharibifu
 
****** alisema yeye siyo mvua so hawezi kunyesha ili mabwawa yajae tupate umeme hata madiwani watasema wao siyo
mungu wakuzuia mvua isilete uharibifu

kwa watanzania nakubaliana na wewe kwani kiongozi yeyote akitoa kauli ya kipumbavu kuhusiana na mambo yanayogusa jamii hakuna hatua yoyote inayochukuliwa iwe na wananchi au mamlaka husika. Kuhusu hili la maji kutuama ni uzembe wa madiwani wetu! Lakini wakifanya mchezo itawagalimu saaaana.
 
Kiukweli mvua ikiendelea kunyesha wiki nzima basi tutakuwa hatuna barabara ya kupita,maana hamna mifereji wala makaravati kwa ajili ya kusafirisha maji hivyo kufanya yatuame barabarani ,hata hivyo nina wasiwasi na mkandarasi aliyejenga hizi barabara uwezo wake ni mdogo sana,tafadhari rekebisheni bhana!
 
Makambako !!!!!! Kituo cha biashara Nyanda za juu kusini, eneo la Wakinga na Wabena na biashara zao.
 
Back
Top Bottom