Madiwani wa CHADEMA Arusha wagawanyika

Si zungumzii ripoti ya Marando na zungumzia kuwa lipa waandishi wa habari juzi na kuwa patia chakula na usafiri....

Hivi unajua Mallah kampeni zake kuanzia mwanzo hadi mwisho hakuchukua sent ya CHADEMA.Hivi unajua Mallah ni Accountant/Auditor anamiliki kampuni ya mahesabu tangu ajira yake ikome General Tyre miaka ya 80s.Hivi unajua Mallah ana vitega uchumi kibao vinavyomuingizia fedha nyingi?.Ikiwa Mallah ana elimu nzuri na uwezo wa kifedha unategemea ashindwe kuwaalika wanahabari wanaotafuta habari kwa udi na uvumba ?.
 
No one is perfect and no politica party is perfect. Kwenye saga ya Arusha nadhani msingi wa mtafaruku wote ni poor communications between HQ na Arusha. Binafsi sikubaliani na muafaka kwa wa 'VYEO' kwa sababu Africa nzima (sio Tanzania peke yake) kumekuwa na kasumba mbaya sana ya kugawana vyeo na hivyo kuondoa dhana nzima ya utawala wa demokrasia na uchaguzi. Na hii kasumba inachangia kwa kiasi kikubwa uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi na hasa wapiga kura maana wanajua hata wakishindwa watafanya 'makubaliano' ya amani!

Kwa maana hiyo nampongeza Nanyaro kwa kuwa na upeo juu ya utawala wa demokrasia. Arusha watu wamekufa na wengine wamepata vilema vya maisha wakitetea misingi ya utawala bora, then leo mtu asema wamefikia muafaka? In the name of those who died madiwani wa CHADEMA Arusha wanatikwa wajue huu muafaka wanaoupiginia umejaa damu - bloody muafaka!

Na nilisema huko nyuma ili madiwani wa CHADEMA wawe na uhalali wa kupokea vyeo na kusema muafaka umepatikana basi ni sharti ndugu wa marehemu wa Jan 5, pamoja na majeruhi washirikishwe. Wamekufa watu hapa wakipigania haki, kwa nini madiwani wanaona ugumu ku-demand ccm na serikali yake wakomeshe tabia ya kukiuka sheria na taratibu za uchaguzi? Kwa vipi madiwani hawa wanaweza kusema wanaamini demokrasia na utawala bora ili hali wanaishi ukiukwaji huo? Hii tabia ya 'bwana yaishe' bila ku-address chimbuko la matatizo ndiyo imetufikisha hapa.

Leo hii Mary Chitanda anatamba bungeni! utajengaje taifa kama viongozi wanakuwa na 'conscious' ya Mary Chitanda? Watoto wa Taifa hili wanakuzwa kuwa watu gani kama viongozi tulio nao ni Mary Chitanda na madiwani wasio simamia yale wanohubiri?. Huyu Mallah anaweza kusimama mbele ya umma akasema kwa nini aliandamana January 5? Kile kilichomfanya akawa barabarani kimefanyika? Kama hakusimamia alichokuwa anahubiri January 5 sisi wananchi tumwamini kwa lipi? Ni maendeleo gani hayo anatamba kuwatufutia wana-Arusha kama hakuna haki?

Mtu kama Mary Chatanda hawezi leo hii akasimama bungeni kutetea wananchi kama anachokisema 'kitawaudhi' waliomuweka hapo? Kwa maana nyingine wananchi wanakuwa wamewekwa pembeni kama karai baada ya zege kuisha! Hatuwezi kuendelea kama msingi wenyewe ndio huo. Madiwani wa Arusha inabidi mtambue hilo.

Umezungumza kitu cha msingi sana. Naomba niongeze yafuatayo kwenye mchango wako:-

Kuna suala la kuchakachuliwa kwa akili za baadhi Watanzania kuwa FIKRA SAHIHI JUU YA SUALA LO LOTE ZINATOKANA NA VIONGOZI na hasa wa CCM.

Tatizo ni kama unaloliona kwa hao waasi wa CDM hasa Mallah. Imani yake ni kuwa kwa kigezo cha muafaka tatizo la msingi la chanzo cha mgogoro limekwisha na maendeleo tayari yameingia Arusha.

Pili utegemezi kwa CCM; kuwa Mallah na wapuuzi wenziwe watafanya lo lote na CCM itawalinda; kiasi kwamba heshima kwa uongozi wa chama (CDM) hauna nafasi.

Tatu madhara ya sumu kupitia elimu duni inayotolewa nchini. Upeo wa mwanasiasa kama Mallah unaishia kuwa manipulated na akina Nepi CCM wakipewa ahadi hata kufadhiliwa kwa namna moja au nyingine.

Angalia bungeni watu wanavounga mkono mia kwa mia huku wakilalama kuwa hiki hakitoshi hakijafanyika hadi kuwatenga wabunge makini mukusudi hata kama wanazungumzia kitu cha maslahi.

Ebu mtafakari Mallah akimuagiza au kuuagiza uongozi wa chama watende anavyotaka. NI UPUNGUFU MKUBWA KIELIMU, KIMAADILI HATA KIJAMII. Ili mradi ameamua mkakati huo NITAWASHANGA CDM kutoiona fursa ya kuondoa wagonjwa wa akili kama hawa madiwani. Wapigwe chini tupate wagombea mdala wenye kukubali maudhui na mwelekeo wa CDM. Kupata au kutopata madiwani utakuwa ni uamuzi wa wananchi.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Hivi unajua Mallah kampeni zake kuanzia mwanzo hadi mwisho hakuchukua sent ya CHADEMA.Hivi unajua Mallah ni Accountant/Auditor anamiliki kampuni ya mahesabu tangu ajira yake ikome General Tyre miaka ya 80s.Hivi unajua Mallah ana vitega uchumi kibao vinavyomuingizia fedha nyingi?.Ikiwa Mallah ana elimu nzuri na uwezo wa kifedha unategemea ashindwe kuwaalika wanahabari wanaotafuta habari kwa udi na uvumba ?.
Hivi waandishi huwa wanatakiwa kulipwa kila unapotaka habari yako itolewe kwenye media....
 
hakuna jambo baya kwenye uongozi kama kukukubaliana jambo hlf badae baadhi wawasaliti wengne, hao madiwani hawana maana yyt waligombea udiwani kwa maslai yao si ya watu wao na watu km hao wanaweza wakavuruga chama kabisa afadhali kidogo hao waliotubu na MUNGU awasaidie
 
  • Thanks
Reactions: FJM

Utakuwa uanishi ughaibuni Sarawatti wa Raia Mwema alikuwa akivuta vijisenti vya Lema tangu mwaka jana ukitaka fuatilia makala za Sarawatti kuanzia mwaka jana kipindi cha uchaguzi.Binafsi niliwahi kumuuliza Sarawatti ni kwanini makala zinazomhusu Lema suala la elimu hajawahi kulizungumzia akabaki anacheka !.Raia Mwema ni gazeti langu kabla Rai haijavamiwa na mafisadi nilijaribu mara kadhaa kuwasiliana na mhariri azifuatilie habari za Arusha kwa umakini sana kwakuwa hazikuwa balanced kabisa.Nafurahi toleo jipya Sarawatti kaanza kuandika habari balanced pengine wakuu wake waligundua mauza uza ya mwandishi.


Mheshimiwa una mawazo ya kibinafi sana (kweli ni mawazo ya kidikteta) kiasi kwamba umeweza kujenda chuki kidhahili na Lema na baadhi yetu tunaokubali "uongozi" makini wa CDM. Ndiyo maana unashadidia upuuzi wa Mallah na wanaomlamba viatu.

Ebu jiulize Mallah ametoa wapi nguvu ya kuwaamuru CDM wamuombe radhi? Kwa Lipi? Mbona wewe hutuwekei hapa tuhuma za rushwa zilizotolewa na CDM dhidi ya hawa madiwani mahayawani? Pesa ni yake kweli lakini kinachotakiwa ni uongozi siyo pesa. Tabia hiyo haina tofauti na ya CCM kutumia pesa kutulubuni.

Jiulize muafaka ni wa nini? Alichokifanya Mallah bila ridhaa ya CDM ndiyo muafaka? Ninaposema bila ridhaa ya CDM nina maanisha masuala ya msingi ya mgogoro. Kukiukwa taratibu za uchaguzi wa Meya, Kuua watu, kupeleka kesi hewa mahakamani, ripoti ya Lema bungeni. nk. Kujibiwa kwa haya ndiyo muafaka siyo vyeo.

Pamoja na jitihada zako za kujaribu kutushawishi, nakushauri na wewe uangalie mantiki kwenye hoja zetu mbadala pamoja na kwamba kwa wewe NYANI HAONI KUNDULE.
 
Namsifu sana Naibu Meya Magwanda wa Arusha kuwa na msimamo kwa analolitetea na hayumbishwi na watu ka Slaa.

Slaa, wanakushinda madiwani watatu utaiweza nchi kweli? Naona saa 7:20 bado haijafika! unanchekesha!
 
Mkuu FJM, umesema yote.Nadhani chadema kuna kitu cha msingi sana hawajakifanya ambacho ni kuwaelezea wananchi haki yao ya kuiwajibisha serikali pamoja na kazi za diwani na mbunge.Watu bado wanaamini diwani na mbunge ndo wanaleta maendeleo. Wabunge wa cdm wanajua kabikuwa kazi ya kuleta maendeleo ni ya serikali na wao wabunge na madiwani ni kuisimamia serikali kwa niaba ya wananchi ili ifanye yale wanayotaka wao.Kitendo cha madiwani wa Arusha kujifanya kuwa bila kuingia kwenye mwafaka wa kugawana vyeo basi maendeleo hayatapatikana kwenye ward zao huu ni uongo na umbumbumbu wa madiwani hawa.Nadhani chadema haijafanya semina kwa madiwani wake ili wajuwe kazi zao ni nini na kazi za serikali ni zipi.Kwa mtu anayeelewa kazi ya kuleta mendeleo ni wajibu wa serikali bila kjali itikadi ya chama kwa kuwa wana nchi wote wanalipa kodi.Kzi ya diwani ni kuisimamia,kuishauri na kuiwajibisha serikali pale inapotaka kwenda kinyume na malengo ya wananchi. Siyo kazi ya diwani kwenda kuipigia magoti serikali ili ipeleke maji,barabara,au kitu chochote kwenye eneo lake.Vitu vyote hupangwa na kukubaliana na kwenye bajeti na madiwani hubaki kuhakikisha yaliyokubaliwa kwenye bajeti yao ndiyo yaliyotekelezwa.Hili la diwani kusema asipoingia mwafaka na ccm hakutakuwa na maendeleo, analitoa wapi kama si umbumbumbu wa kutaka kuendelea na fikira za kitumwa ambazo ndo zimetufikisha hapa tulipo.Badala ya kuwasidia wananchi waelewe kuwa maendeleo ni haki yao na ni wajibu wa serikali kuleta maendeleo na si kazi ya diwani au mbunge kuwapigia magoti serikali. Natamani ningekuwa na muda wa kuliingiza hili kwenye akili ya kila mtanzania. Na hiki kitu ndo kimetufanya tubaki hapa tulipo maana watu wengi hawajui hili wanadhani kuletewa maendeleo ni favour hivyo hukaa kimya wakisubiria.Watu wakielewa hili wataandamana kila mahali na watakuwa wananafatilia mipango ya serikali ya kila mwaka na kuhakikisha wanawabana pale wanaposhindwa kutimiza .Mungu tusaidie kuondoa huu umbumbumbu kwenye akili za watanzania.

Well Said Bro!
Kuna sehemu MPUUZI mmoja nimemsoma ETI barabara za mitaa za MADIWANI walioingia kwenye vikao ZINAJENGWA na zile za wengine zimedorora, Nika shindwa kuelewa hivi ni kweli Diwani akiingia kwenye vikao ndio anapeleka miradi ya barabara mtaani kwake?
Inaitajika elimu zaidi kwa watu kujua majukumu ya Viongozi wa kuchaguliwa ni yapi na serekali ni yapi.
 
Well Said Bro!Kuna sehemu MPUUZI mmoja nimemsoma ETI barabara za mitaa za MADIWANI walioingia kwenye vikao ZINAJENGWA na zile za wengine zimedorora, Nika shindwa kuelewa hivi ni kweli Diwani akiingia kwenye vikao ndio anapeleka miradi ya barabara mtaani kwake?Inaitajika elimu zaidi kwa watu kujua majukumu ya Viongozi wa kuchaguliwa ni yapi na serekali ni yapi.
Mkuu nchi hii bado kuna watu wengi wamefunikwa na gamba la ccm. N cha ajabu wengine ni wenzetu humu kwenye Jf wanashangaza sana. Hapa ndipo kwenye kiini cha haki ya watanzania na ccm wanajua watu wengi hawajui hili. Inashangaza hata madiwani wengine hawajui tena wa cdm inasikitisha sana ni vipi tutashinda hii vita.Kama watu wakiitambua haki hii ya maendeleo bila kujali wanaongozwa na chama gani, huu upuuzi wa wana siasa uchwara kama akina Nepi watapigwa mawe na hawatathubutu kusimama kwenye majukwaa kuwalaghai watu tena.Chadema wala hawahitaji kuwabemebeleza watu waingie chadema ili wawe wengi, kinachotakiwa ni umma kutambua haki zao na ndipo watu watachagua watu waliomakini kama chadema. Tukibaki na huu umbumbumbu ccm itatawala milele. Chadema waachene na malengo ya kupata wananchama mamruki kutoka ccm wao wapambane na vita ya kuondoa umbumbumbu wa watanzania na nchi hii itakuwa ya cdm bila mashaka.
 
Mkuu Mimibaba,

Mkuu naomba kutofautiana na wewe kidogo kuombwa radhi hakujalishi ni nani kakukosea.Mallah ana haki ya kudai kuombwa radhi bila kujali aliyemkosea aliwahi kugombea urais au ni mbunge.mallah anataka kuombwa radhi kwa kukashifiwa kwamba alihongwa.Pengine unadhani ni jambo dogo kwakuwa waliomtuhumu ni wakubwa zake kichama !.Haijalishi kabisa waliomtuhumu wanatawakiwa kumsafisha kwa kutumia njia zile zile walizotumia kumkashifu Radio,magazeti na TV.Nguvu ya kudai kuombwa radhii au kusafishwa ipo ndani ya katiba yetu ya JMT na viongozi wa CHADEMA wasipotekeleza matakwa ya Mallah wasimlaumu siku wakiburuzwa mahakamani.


Mkuu wangu labda umeamua kuziba masikio lakini chama kilikuwa na taarifa kwa kila jambo lililokuwa likifanyika.Mhweshimiwa Lema mbunge wakati wa utiaji saini makubaliano alitaarifiwa kwakuwa alikuwa safarini Dodoma kwenye kikao cha bunge.

Muafaka hauwezi kurejesha uhai wa wananchi waliouwawa na polisi.Wala hakuna sehemu inayozungumzia marehemu kulipwa fidia kama ilivyokuwa kwa ndugu zetu wapemba rejea muafaka wa CCM na CUF.CHADEMA na CCM hawakuweka mbele maslahi ya waathirika wa maandamano badala yake walitaka OCD afukuzwe kazi jambo ambalo lilikuwa gumu kufanywa na kamati ya muafaka chini ya mkuu wa wilaya ya Arusha.Mamlaka ya nidhamu ya OCD ni RPC na suala la kufukuzwa kazi ni IGP.




Mheshimiwa una mawazo ya kibinafi sana (kweli ni mawazo ya kidikteta) kiasi kwamba umeweza kujenda chuki kidhahili na Lema na baadhi yetu tunaokubali "uongozi" makini wa CDM. Ndiyo maana unashadidia upuuzi wa Mallah na wanaomlamba viatu.

Ebu jiulize Mallah ametoa wapi nguvu ya kuwaamuru CDM wamuombe radhi? Kwa Lipi? Mbona wewe hutuwekei hapa tuhuma za rushwa zilizotolewa na CDM dhidi ya hawa madiwani mahayawani? Pesa ni yake kweli lakini kinachotakiwa ni uongozi siyo pesa. Tabia hiyo haina tofauti na ya CCM kutumia pesa kutulubuni.

Jiulize muafaka ni wa nini? Alichokifanya Mallah bila ridhaa ya CDM ndiyo muafaka? Ninaposema bila ridhaa ya CDM nina maanisha masuala ya msingi ya mgogoro. Kukiukwa taratibu za uchaguzi wa Meya, Kuua watu, kupeleka kesi hewa mahakamani, ripoti ya Lema bungeni. nk. Kujibiwa kwa haya ndiyo muafaka siyo vyeo.

Pamoja na jitihada zako za kujaribu kutushawishi, nakushauri na wewe uangalie mantiki kwenye hoja zetu mbadala pamoja na kwamba kwa wewe NYANI HAONI KUNDULE.
 
Mkuu labda ungepitia tena kamusi ya kiswahili neno "mpuuzi' lina maana gani halafu ujitazame kati yako wewe na aliyetoa hoja nani mpuuzi.

Well Said Bro!
Kuna sehemu MPUUZI mmoja nimemsoma ETI barabara za mitaa za MADIWANI walioingia kwenye vikao ZINAJENGWA na zile za wengine zimedorora, Nika shindwa kuelewa hivi ni kweli Diwani akiingia kwenye vikao ndio anapeleka miradi ya barabara mtaani kwake?
Inaitajika elimu zaidi kwa watu kujua majukumu ya Viongozi wa kuchaguliwa ni yapi na serekali ni yapi.
 
Mlengwa mkuu ni Mallah wengine hawana cha kupoteza na ukitaka sababu nitakwambia Lema tangu mwanzo anamhofia Mallah kuliko unavyofikiri ndiyo maana kakimbilia makao makuu [~`^] kumchafua mwenzake bila sababu za msingi Mheshimiwa Slaa kwakutojua siasa za Arusha akarukia jambo kabla hajafanya utafiti vizuri kitu ambacho sijawahi kukishuhudia kwa Dr Slaa tangu aingie medani ya siasa za Tanzania.NB angalia kichwa cha habari hii utaelewa bila chenga wanaoridhika na maamuzi ya kamati kuu hawana vyeo kabisa wanatumiwa kuharibu misimamo ya madiwani wote. Naomba kukuuliza swali moja nje ya mada Lema alichaguliwa na kikao kipi kugombea ubunge ukipata jibu connect na taratibu za chama halafu jumlisha na sakata linaloendela.Kwa taarifa yako Lema alichomekwa na Mwenyekiti nje ya utaratibu wa chama walikuwapo wanachama wazuri wenye uwezo mmoja wapo mwanasheria CHADEMA wilaya na mkoa wanalijua hilo na ndio kitu kinachomsumbua Lema hataki kabisa kwakuwa wanamjua hana uwezo zaidi ya fujo.

Sijakusoma vizuri hebu wekama maelezo yako vizuri...unaiimanisha nini
 
Hivi waandishi huwa wanatakiwa kulipwa kila unapotaka habari yako itolewe kwenye media....

Crashwise hakuna mwandishi wa habari aliyelipwa ili atoe habari za Mheshimiwa Mallah upo hapo mkuu lakini unaweza kuwapatia maji ya kunywa or soda na ndicho kilichofanyika.Habari za waandishi kulipwa ni mkakati wa Lema na pro wake ili Malla aonekane hafai mbele ya jamii.
 

Crashwise hakuna mwandishi wa habari aliyelipwa ili atoe habari za Mheshimiwa Mallah upo hapo mkuu lakini unaweza kuwapatia maji ya kunywa or soda na ndicho kilichofanyika.Habari za waandishi kulipwa ni mkakati wa Lema na pro wake ili Malla aonekane hafai mbele ya jamii.


Vita ya Jimbo 2015,isije ikaharibu maslahi ya umma......! Na sisi Watanzania tuache kasumba ya zidumu fikra bora za Mwenyekiti,tuwe na ujasiri.....!Sifafanui zaidi ya hapa
 

Mkuu Ben kuna mwanajamvi mwenzagu anamwakilisha yule mnyama anayependa maziwa sana na kukamata panya kuna baadhi ya mambo alikuwa akipenda kunibishia sana lakini baada ya uchaguzi kumalizika najua kuna baadhi ya mambo niliyokuwa nikiandika na kuyatetea kwa nguvu zangu zote kaanza kuyashuhudia mwenyewe.Ukishindwa kuishi na madiwani kumi na sita utawezaje kuongoza wananchi milioni moja ?.


Vita ya Jimbo 2015,isije ikaharibu maslahi ya umma......! Na sisi Watanzania tuache kasumba ya zidumu fikra bora za Mwenyekiti,tuwe na ujasiri.....!Sifafanui zaidi ya hapa
 
Mbunge hawezi kufanya kazi yake ipasavyo bila kupata sapoti ya madiwani.Na wenzetu CCM wanatumia huo Mwanya kuhakisha shughuli za Arusha zina-paralyse ili ikifika 2015 ionekane Chadema wameshindwa kazi Arusha.Kwa kiasi kikubwa madiwani ndiyo bridge kati ya wananchi na mbunge ambaye naye huwakilisha Interest za wananchi kwa mapana na katika level ya juu.

Kwa kweli kipimo cha kiongozi ni kutafuta Diplomatic approach katika ku-solve conflict or crisis.Hili suala kwa kuwa limefikia hatua nzuri ya decision sasa,nadhani maamuzi ya busara kabisa ambayo ni diplomatic and more democratic oriented

Huwa nafika mahala nafikiria pengine uchanga wa siasa na ulimbukeni ndiyo unatufikisha hapa tulipo.
 
Mkuu Mimibaba,Mkuu naomba kutofautiana na wewe kidogo kuombwa radhi hakujalishi ni nani kakukosea.Mallah ana haki ya kudai kuombwa radhi bila kujali aliyemkosea aliwahi kugombea urais au ni mbunge.mallah anataka kuombwa radhi kwa kukashifiwa kwamba alihongwa.Pengine unadhani ni jambo dogo kwakuwa waliomtuhumu ni wakubwa zake kichama !.Haijalishi kabisa waliomtuhumu wanatawakiwa kumsafisha kwa kutumia njia zile zile walizotumia kumkashifu Radio,magazeti na TV.Nguvu ya kudai kuombwa radhii au kusafishwa ipo ndani ya katiba yetu ya JMT na viongozi wa CHADEMA wasipotekeleza matakwa ya Mallah wasimlaumu siku wakiburuzwa mahakamani.Mkuu wangu labda umeamua kuziba masikio lakini chama kilikuwa na taarifa kwa kila jambo lililokuwa likifanyika.Mhweshimiwa Lema mbunge wakati wa utiaji saini makubaliano alitaarifiwa kwakuwa alikuwa safarini Dodoma kwenye kikao cha bunge.Muafaka hauwezi kurejesha uhai wa wananchi waliouwawa na polisi.Wala hakuna sehemu inayozungumzia marehemu kulipwa fidia kama ilivyokuwa kwa ndugu zetu wapemba rejea muafaka wa CCM na CUF.CHADEMA na CCM hawakuweka mbele maslahi ya waathirika wa maandamano badala yake walitaka OCD afukuzwe kazi jambo ambalo lilikuwa gumu kufanywa na kamati ya muafaka chini ya mkuu wa wilaya ya Arusha.Mamlaka ya nidhamu ya OCD ni RPC na suala la kufukuzwa kazi ni IGP.
Mkuu mbona ni wewe tu peke yako ndo uke kinyume na waliowengi. Wewe ni mchawi?Kama unadhani wewe ni watofauti kuliko wengine basi si kwenye haya mambo ya siasa labda ungeenda kwenye physical science kule hakuna cha kubisha kwa hoja, bali ni facts zako.Kwenye siasa mkuu wengi wape huwezi kupingana na wengi hutapata kitu!Inavyoonekana na wewe ni swahiba mzuri wa Mallah ndo maana unapambana kwa ajili yake humu jamvinini. Kwa bahati mbaya sana chadema ni chama chenye watu makini na wanaheshimu haki zaidi kuliko chochote. Hawatakuwa tayari kuharibu sifa hii hata kama Mallah ni Mungu pale kimandoro. Chadema wanamuuliza Mallah je kwanini aliandamana Jan. 5? Kama anajua aliandamana kwa nini basi ajibu swali la pili je yale aliyokuwa anayadai yametekelezwa? Lakini juu ya hayo je madhara yaliyotokana na maandamano yale nani anayalipia? Je Mallah sasa anawasaliti wana Arusha walioshiriki maandamano kwa ushawishi wake na wengine wakafa na kuapata majeraha?Je ni kweli mtu kama mke wa Dr. Slaa ambaye damu ilibubujika anaweza kukubaliana na Mallah kwamba basi yameisha?Kama maswali haya na mengine mengi ambayo sikuyauliza yanaweza kujibiwa na Mallah basi anayo haki ya kuwa na kiburi anachokionyesha.Kwa kifupi watu wengi watafurahia kufukuzwa kwa huyu anayetaka kufaidika kwa mngongo wa wengi walioumia kwa ajili ya mgogoro huo!Mimi binafisi naona chadema wako very reasonable na huyu jamaa na kweli wanampenda sana la sivyo angekuwa ameshalimwa barua ya kufukuzwa zamani tu.
 

Mkuu Ben kuna mwanajamvi mwenzagu anamwakilisha yule mnyama anayependa maziwa sana na kukamata panya kuna baadhi ya mambo alikuwa akipenda kunibishia sana lakini baada ya uchaguzi kumalizika najua kuna baadhi ya mambo niliyokuwa nikiandika na kuyatetea kwa nguvu zangu zote kaanza kuyashuhudia mwenyewe.Ukishindwa kuishi na madiwani kumi na sita utawezaje kuongoza wananchi milioni moja ?.

Unazidi kunishawishi una vinasaba vya udikteta kwa kutokubali kuangalia mantiki ya mawazo bali kwa maslahi ya wewe kuendeleza chuki dhidi ya Lema. Huoni na wala huifikirii CDM kama taasisi (institution) inayoongozwa na katiba, taratibu na watu wanaoshare itikadi. NASISITIZA SI VYEO AU UBINAFSI UNAOFAGILIA.

Kuongoza watu milioni!!! Mallah anaongoza wangapi kwa upuuzi wake wa kutoheshimu chama? Mbona tumeongozwa na CCM bila tija toka 1961 na wenzetu Singapore waliopata uhuru nyuma yetu wako mbali? Haya Mallah kaingia kwenye halmashauri tusubiri maendeleo na huku mnatekeleza ilani ya CCM ambayo imeshashindwa toka ianze.

Hata hivyo naomba nikiri nimefaidika kukufahamu na hoja zako. Mimi siamini kuhusu Lema au huyo mpuuzi Mallah, mimi naamini kuhusu CDM kama chama makini. Na kwamba hii migogoro imetunufaisha kuwajua wapuuzi wasioheshimu utaratibu wa kichama iwe kwa elimu duni au kwa sababu nyingine. Maana ya hayo ni kuwa kuna tofauti za kifikra afadhali tutenganishwe.
 
1) Tulisikia kuna muafaka kati ya Mbowe na Pinda kuhusu Arusha. Si Mbowe wala Pinda waliokanusha mpaka sasa.

2) Mara tukamsikia Slaa anasema madiwani wamekula rushwa (kutokana na usemi wa Mala kupitia TV.)

3) Tukasikia Marando kapelekwa kuchunguza. Matokeo ya uchunguzi wake ni siri mpaka leo.

4) Slaa akawapa siku tatu wajiuzulu vyeo vyao lakini si udiwani. Inashangaza,mla rushwa umwache nawe ndi u mstari wa mbele kufichua mafisadi?

5) Malla akataa kujiuzulu live na ansema uchunguzi wa Marando umebaini ukweli (TV) kwa hiyo hajiuzulu mpaka uongozi umsafishe, umsafishe vipi? Kagoma kujiuzulu,

6) Siku ya pili Slaa akasema watafata katiba.

7) Mara Slaa akaacha na hoja ya kujiuzulu akawataka waombe radhi. Akasema saa 7:20 ikifika katiba itaamua. Saa hiyo haijafika bado!

8) Mala bado uzi uleule,anasema hajiuzulu wala haombi radhi na tunasikia anaongoza vikao vya manispaa huko.

9) Slaa hasikiki, mfupa mgumu!

10) Mala nampa heko.

11) Tutasikia Sloaa anajiuzulu kwa kushindwa kuongoza.
 
Back
Top Bottom