Madiwani nao Wawasha Moto Sakata la Posho

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,619
4,292
Sakata la wabunge kuongezewa posho kutoka shilingi 70'000 hadi 200'000 kwasiku sasa madiwani nao wameshtukia dili kuhusu nao pia wana haki ya kuongezewa posho, madiwani nao wanasema haiwezekani wakae kwenye vikao kupisha bajeti ya miundombinu ya mamilioni halafu mwisho wa mwezi wanaambulia shilingi 120'000 kwa mwezi! Hii sasa ngoma nzito! Souce Radio One Nipashe.
 
Nilikua na hamu yakuwatumikia wananchi wangu kwakutaka kuwania udiwani chaguzi zijazo lakini kumbe posho yenyewe kwa mwezi ni 120,000? Ngoja nisome ramani nyingine!
 
Uongozi ni kalama mkuu! huhitaji posho kuwaongoza watu. Watu wengi wanaangamia kwa (a) Kukosa maarifa (b) kukosa viongozi wa kuwatoa walipo na kuwafikisha sehemu husika kwa kuwatia moyo, kuwaelekeza na kuwapa morali ya kufanya kazi bila malipo ilimradi hiyo kazi ni kwa manufaa yao.
 
Nilikua na hamu yakuwatumikia wananchi wangu kwakutaka kuwania udiwani chaguzi zijazo lakini kumbe posho yenyewe kwa mwezi ni 120,000? Ngoja nisome ramani nyingine!

Hahahahaaaaaaa, mkuu usitishwe na posho
kuna mengine mengi yaliyofichwa ambayo huyajui,
we hushangai wakati wa kampeni huwa wanahonga
mamilioni ili waupate udiwani?...
 
Mpaka watendaji wa Kata Dodoma watahitaji nyongeza. Maisha yamepanda Dodoma!
Dodoma labda haiko Tanzania!
 
Sasa nimeshapata picha ya ule mgogoro wa umeya jiji la Arusha ni nini kilifikia wale wabunge wa Chadema kuhongwa mamilioni ya shilingi na kuupoteza udiwani wao!
 
raia yangu kwa wafanyakazi walioko dodoma,walimu ,watendaji wa kata,afisa mipango,wanafunzi wa udom st john ,mipango cbe maisha yamepanda daini haki yenu
 
jamni na sisi walimu na madakari tuwashe moto. Ila kwa sisi wengine hata perdiem zikiongezwa hata kufikia laki 2, hatutafaidika maana hatusafiri. Labda wakati wa uchaguzi 2015
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom