Madiwani Korogwe wamtimua mhasibu, DED amkingia kifua

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,148
Madiwani Korogwe wamtimua mhasibu, DED amkingia kifua
Tuesday, 29 September 2009 16:30
Na Yusuph Mussa, Korogwe

BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe wamemtimua kazi Mweka Hazina wa Halmashauri hiyo, Bw. Gofrey Kiwelu kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo halmashauri yao kupata Hati ya Mashaka.

Pamoja na kumtimua Bw. Kiwelu, pia wamewapa onyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi. Lilian Matinga, Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Rashid Said, Ofisa Elimu Wilaya (Msingi), Bw. Shaaban Shemzigwa na Ofisa Ugavi Wilaya, Bw. Mkome Salige.

Hata hivyo Bi. Matinga amekataa kutekeleza agizo hilo akisema mwenye mamlaka ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Bw. Sadick Kallaghe alisema uamuzi huo ulifikiwa
kwenye Baraza Maalumu la Madiwani lililofanyika Septemba 26, mwaka huu na wamemtaka Mkurugenzi kumwandikia barua mara moja Bw. Kiwelu kumsimamisha kazi.

Bw. Kallaghe alisema Bw. Kiwelu pamoja na makosa mengi yaliyokutwa kwenye ukaguzi wa mahesabu yanayoishia Juni 30, 2008 bado ofisi yake ilizembea kujibu hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, hivyo kuifanya halmashauri hiyo kupata Hati ya Mashaka.

Alizitaja baadhi ya hoja kati ya 11 zilizotakiwa kujibiwa lakini wakashindwa kuzijibu kwa wakati ni halmashauri kushindwa kuandaa taarifa za mwisho wa mwaka wa fedha kwa kutojumuisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, hivyo kushindwa kujua matumizi ya miradi ikiwa ni kinyume cha
kifungu namba 84 (v) cha kanuni za matumizi ya fedha za Serikali za Mitaa.

Bw. Kallaghe alisema kwa upande wa Idara ya Elimu, sh. milioni 23.1 zilitumika kama ziada wakati
makisio ya bajeti kwa ajili ya mitihani ya darasa la saba ya ilikuwa sh.milioni 109.9 lakini zikatumika sh. milioni 133.1, huku watumishi
wanaochukua masurufu kwa ajili ya safari za kikazi wakishindwa kurejesha pindi fedha zinapobaki.


Bw. Kallaghe alisema kibaya zaidi ni Bi. Matinga kuukumbatia uozo uliopo kwenye Idara ya Fedha, na yeye kudaiwa kughushi kwamba Kamati ya Uongozi, Fedha na Mipango imekaa na kutoa maoni kuwa
waandishi wa taarifa za fedha wawe makini suala hilo lisijirudie.

"Mimi kwa mujibu wa sheria pia ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango, iweje Mkurugenzi atusingizie tumekaa na kutoa maoni
yetu kwenye taarifa iliyopelekwa kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali?... Tangu Mweka Hazina huyu (Bw. Kiwelu) amekuja hatujawahi kupata
hati safi, lakini Mkurugenzi anamkumbatia," alisema Bw. Kallaghe.

Akizungumza na mwandishi wa habari, Bi. Matinga alisema hatamwandikia barua Bw. Kiwelu kwa kuwa Baraza hilo maalumu halikuwa kwa ajili ya kuhukumu watumishi bali ni kujadili hoja za mkaguzi, na kusema sheria na kanuni za halmashauri haziruhusu kikao kinachojadili jambo fulani kuingizwa jambo jingine.

"Kanuni ya 4 (4) inasema hakuna shughuli yeyote itakayojadiliwa katika mkutano maalumu wa halmashauri isipokuwa ile tu iliyoelezwa kwenye taarifa ya kuitishwa mkutano huo. Kwa maana hiyo mimi siwezi kumwandikia barua ya kumfukuza kazi mtu,
mwenye uwezo wa kufanya hivyo ni Katibu Mkuu wa TAMISEMI
 
Back
Top Bottom