Madiwani-CUF Kilwa wamzuia Mbunge Zainab Kawawa kupiga kura

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
zainabu%20kawawa.jpg

Mbunge wa Viti Maalum (CCM)
jimbo la Liwale, Zainabu Kawawa


Madiwani wa chama cha CUF wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi, wamemzuia Mbunge wa Viti Maalum (CCM) wa jimbo la Liwale, Zainabu Kawawa, kupiga kura ya kuchagua viongozi kwa maelezo kuwa kiapo alichokula ni cha nje ya Halmashauri ya Kilwa.

Tukio la kumzuia Zainabu kupiga kura lilifanyika wiki hii wakati wa kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo, kwenye mji mdogo wa Masoko.

Kawawa aliyekuwa kwenye ziara ya siku moja wilayani Kilwa, alivaa joho la madiwani na kuhudhuria kikao hicho, kilichokwenda na uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilwa na madiwani watatu kuingia vikao vya Baraza la Mji Mdogo.

Wagombea wa wadhifa huo walikuwa Abdallah Kuchao (CCM) na Mahadhi Nangona (CUF), ambapo kwa nafasi ya kuingia vikao vya Baraza la mji mdogo, wagombea walikuwa Haji Mulike, Mwanaisha Lindu, Ismaili Nalinga na Abdallah Abbasi.

Kawawa alizuiliwa wakati wa upigaji kura kumchagua Makamu Mwenyekiti, ambapo diwani wa kata ya Lihimalyao Nangoka (CUF) alisimama na kuomba mwongozo kutoka kwa mwenyekiti wa kikao hicho, Farida Kikoleka, juu ya haki ya mbunge Kawawa kupiga kura katika kikao hicho.

Kufuatia swali hilo, mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri aliyemaliza muda wake Farida Kikoleka na madiwani wengine wa CCM walijaribu kumtetea mbunge huyo aweze kupiga kura, lakini hawakufanikiwa.​
 
Hivi viti maalumu vifutwe hata Arusha mbunge wa viti maalumu alichangia kuvuruga uchaguzi wa meya,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom