Madiwani arusha watafukuzwa chadema

JOHN MADIBA

JF-Expert Member
Jan 30, 2011
251
155
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kipo tayari kuwapoteza madiwani wake watatu waliohusika kumaliza kinyemela mgogoro wa kumpata meya wa Manispaa ya Jiji la Arusha, kwa maridhiano ya kugawana madaraka.

CHADEMA imeunda kamati ya watu watatu inayoongozwa na mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho na mwanasheria mkongwe, Mabere Marando, kufanya uchunguzi wa utaratibu uliotumika kufikia maridhiano hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, alisema maridhiano yaliyofanyika kumpata meya na naibu wake hawayatambui kutokana na upungufu uliojitokeza wakati wa mchakato wa kuwapata viongozi hao.

Madiwani wa CHADEMA wanaodaiwa kukubali kufanya maridhiano ni pamoja n Diwani Estomih Mallah, ambaye atashika nafasi hiyo kuanzia sasa hadi mwaka 2014 atakapomwachia nafasi Diwani wa TLP, Michael Kivuyo, wengine ni John Bayo na Efatha Nanyaro.

Akifafanua upungufu huo, Dk. Slaa alisema kwanza maridhiano hayo hayakufikiwa na idadi ya wajumbe (madiwani) ambao wanaweza kufanya maamuzi, kwamba maridhiano hayo yalifanywa na wajumbe tisa kati ya 21 ya madiwani wote wa halmashauri hiyo.

Aliutaja upungufu mwingine kuwa mkurugenzi wa halmashauri ya jiji hilo alikubali kufanya muafaka bila ya kupata barua ya CHADEMA ya kukubali maridhiano ambayo ina majina ya walioteuliwa na chama hicho kupewa madaraka.

Aliongeza kuwa madiwani wa CHADEMA, watatu walioshiriki kwenye maamuzi husika walifanya hivyo bila kuwashirikisha viongozi wao wa wilaya, mkoa na makao makuu kwa ajili ya kupata baraka zao za kupendekeza majina ya watakaochaguliwa kuwa viongozi.

Alisema upungufu mwingine ni kuwapo kwa mianya ya rushwa ya kuwashawishi madiwani husika kushiriki kwenye maridhiano hayo pasipo kufuata taratibu zinazotakiwa.

Dk. Slaa alisema kutokana na matatizo hayo, CHADEMA haiyatambui maridhiano hayo na kudai kuwa yamefanywa kwa kupindisha kanuni na taratibu za kuwapata viongozi hao.

“CHADEMA tunasema kuwa hatuyatambui maridhiano yaliyofikiwa kumpata meya na naibu wake kwani hayakufuata kanuni na taratibu za kuwapata …uliofanyika pale ni uchakachuaji wa demokrasia,” alisema Dk. Slaa.
 
CDM kwishney
Penye ukweli tuseme kweli,kama viongozi wengine hawakushirikishwa hapo mantiki ninaipata kwamba CDM ni chama makini sana!kitapendwa na kupendeka kwa sababu watu wana sababu ya kukipenda.Pia CDM sio kama CCM wenye kukaa na kubembeleza bembeleza watuhumiwa(MAFISADI).Kama viongozi wengine hawakushikishwa,ina maana kuna jambo limejificha hapo,ndo maana katibu mkuu wa chama Dr W. Slaa atapendwa kwa misimamo yake mathubuti na siyo Mukama na Nape wenye kusema hiki leo halafu kesho wanapingana!!Kwa hiyo ndugu CDM haiwezi kufa ila CDM itazidi kupendwa.Tunajua fika kwamba CCM walishtushwa na ushindi wa CDM ndo maana sasa hivi ni wakati wa kuiwinda CHADEMA ili wawakosanishe na watu!Rushwa kwa viongozi dhaifu wa CDM ndio silaha pekee ya CCM ili CDM idhoofike mfano Shitambala yuko wapi sasa alidhani akiondoka CDM itayumba kumbe badala yake yeye ndo akawa amejizika kisiasa!Uimara wa CDM unasababishwa hasa na Uimara pamoja na umakini wa viongozi wake!hili lipo wazi hata kwa mwananchi aliyeko Dongobesh,Mwanjelwa,Mvimwa,Ulong'a,Matongo,Longalombogo,pandambili,Nyamswa,Mwitongo,Kibara,Mgogoni,Wawi,Mombo,Namtumbo,Ng'wanzugi,Lubiga,Busondo taja kote unakojua hapa nchini vijiji ,miji au majiji!wanajua kua CDM ndo tumaini pekee la Watanzania.Kwa hiyo basi jogoo hafi kwa utitiri ndugu yangu!Hata Lowassa anajua kwa nini maamuzi magumu kama ya Chadema hayafanyiki ndani ya Ccm!kwa sababu siyo utaratibu kwao!
 
Back
Top Bottom