Willegamba
Member
- Apr 14, 2011
- 44
- 5
Ktk hali ambayo siielewi ktk suala la siasa hasa ktk jiji la Arusha, leo majira ya kuanzia saa 8:30 asubuhi limepita gari la matangazo almaharufu RAHA PROMOTION la jamaa mmoja anaejulikana kwa jina la Rama akiwatangazia wananchi wa viunga vyote vya jiji la Arusha kujumuika kwa pamoja ktk ukumbi wa Manispaa ktk hafla iliyoandaliwa kuwapongeza madiwani hao kwa kumaliza tofauti zao na kuamua kufanya kazi pamoja bila kuangalia itikadi zao za vyama. Vipi uongozi wa juu wa chama cha CHADEMA mbona hamtujulishi kulikoni?