Madini ya Rubi Toka Tanzania Yaifilisi Kampuni ya Uingereza

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,112
3247718.jpg

Madini origino ya rubi toka Tanzania kama haya huwa na thamani kubwa sana Friday, October 02, 2009 7:05 AM
Kampuni moja kubwa ya ujenzi ya nchini Uingereza imefilisika na wafanyakazi wake zaidi ya 500 wamekosa kazi baada ya kampuni hiyo kuingia mkenge na kuuziwa madini feki ya rubi toka Tanzania. Kampuni ya Wrekin Construction ambayo imejenga majengo mengi ya maegesho ya magari na roundabout za nchini Uingereza imefilisika na wafanyakazi wake zaidi ya 500 kukosa kazi baada ya mmiliki wa kampuni hiyo kuuziwa madini ya rubi feki toka Tanzania.

Mmiliki wa kampuni hiyo, David Unwin, aliingiza kwenye hazina ya kampuni hiyo kilo mbili za madini ya rubi ambayo yanapatikana Tanzania pekee akisema kwamba yana thamani ya paundi milioni 15. (Takribani Tsh. Bilioni 35).

Unwin alibadilishana madini hayo kwa hisa za kampuni hiyo zenye thamani ya paundi milioni 11 akielezea kwamba madini hayo yana thamani kubwa sana kati ya paundi Milioni 11 na 15. Madini ya rubi ni maarufu nchini Uingereza kama "Gem of Tanzania".

Lakini mchezo kamili ulibumbulika baada ya wataalamu wa madini kusema kwamba madini hayo sio madini ya rubi na yana thamani ya paundi 100 (Tsh. Laki mbili) na sio Paundi Milioni 11 kama walivyokuwa wakidhania.

Madini hayo yanasemekana kuwa ni jamii ya madini yanayoitwa anyolite ambayo hupatikana kwa nadra sana katika nchi za Afrika Mashariki na hayana thamani kubwa.

Hali hiyo iliifanya kampuni hiyo ikose fedha za kuiendesha miradi yake na hatimaye kufilisika kabisa mwezi machi mwaka huu.

Polisi wa Uingereza wamejitosa kwenye kasheshe hilo na wamesema wanafanya uchunguzi baada ya kugundua kwamba nyaraka za kutathmini thamani ya madini hayo zilikuwa ni feki.

Unwin amejitetea kwamba hajafanya ujanja wowote katika dili hilo la kubadilisha hisa za kampuni kwa madini hayo ya rubi.

Uchunguzi wa polisi wa Uingereza unaendelea kubaini jinsi madini ya paundi 100 yalivyopandishwa thamani na kuwa madini ya paundi milioni 11.

http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3247718&&Cat=1
 
Utapeli sasa unatisha...
Lakini ilikuwaje kampuni kubwa namna hiyo inanunua madini ya hela nyingi hivyo bila utafiti wa kutosha juu ya genuiness ya mali?
Nadhani wabongo fulani wanahusika kufanya sanaa hii...lol!
 
WanaJf,
Je mchezo huo uliofanyika waweza kuleta madhara kwenye aina nyingine ya madini toka Tanzania yaani kuhisiwa kuwa ni feki????? au tatizo hili halina madhara yoyote kwetu??? Wachambuzi leteni elimu hapa
 
Back
Top Bottom