Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 50,956
- 22,138
Madini kwa Mzungu, mashimo kwa Mtanzania!
HATA kama isingekuwa udadisi wa vyombo vya habari, hatimaye ingejulikana tu jinsi tunavyoporwa utajiri wa madini yetu kupitia mikataba mibovu yenye kufukarisha nchi.
Ingawa Serikali imejitahidi mara nyingi kuficha, na hata kupotosha kwa makusudi, ukweli juu ya jambo hili, hila hizi zimegonga mwamba kwa sababu Mtanzania wa leo sio yule wa mwaka 1947.
Katika hali ya kufadhaika juu ya siri za ufisadi huu kuendelea kufichuliwa na vyombo vya habari, serikali ilikurupuka kuandaa muswada wa habari ambao, kama ungewasilishwa bungeni na kupita, ingekuwa ni kosa la jinai kwa mwanahabari kuandika juu ya mikataba ya kibiashara ya serikali na ufisadi ambapo adhabu yake ingekuwa ni kifungo cha muda mrefu.
Madhumuni ya muswada huo ilikuwa ni kuwalinda kwa kuwakingia kifua, wahujumu wa uchumi wa taifa letu ili waweze kuvuna na kutumbua bila ya hofu kile wasichopanda.
Lakini, wakati uporaji huu wa madini ukiendelea na serikali kuvisakama vyombo vya habari eti kwa "kununua hoja [kelele] ya Wapinzani" bungeni juu ya jambo hili, uongozi wa juu wa serikali ulijaribu kujikosha kila mara, lakini bila kuchukua hatua stahili.
Joseph Mihangwa
Julai 29, 2009HATA kama isingekuwa udadisi wa vyombo vya habari, hatimaye ingejulikana tu jinsi tunavyoporwa utajiri wa madini yetu kupitia mikataba mibovu yenye kufukarisha nchi.