madilu system ndani ya ikulu ya Gabon

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
5,139
1,139
Rais wa zamani wa Gabon marehemu Omari Bongo Ondimba alimuoa binti wa rais wa congo brazzaville mzee Dennis Sassou nguesso akiitwa Edith Lucie Bongo ambae kabla ya hapo aliitwa Edita Sassou Nguesso maarufu kama Edita mwana ya sassou au Edita mwasi ya mokonzi omari bongo.Huyu mama ambae nae kwa sasa ni marehemu alikua mdau na mpenzi mkubwa wa muziki na wanamuziki wa congo kinshasa japo yeye kwao ni congo brazzaville ambako babake ndio rais huko.Kudhihirisha upenzi wake huo kwa bana congo kinshasa aliandaa sherehe kubwa kwa ajili yake na mumewe rais omari bongo wa gabon iliyofanyika ikulu na kumualika mwanamuziki madilu system ambae nae kwa sasa ni marehemu pia kutumbuiza kwenye hafla hiyo ambayo waalikwa wengine walikua ni pamoja na babake mzee mzee dennis sassou nguesso rais wa congo brazzaa,hii maana yake ni kwamba hafla hiyo ilihudhuriwa na marais wawili,wa congo na mwenyeji wa gabon,hali ilikua hivi,hebu mtizame mamaa Edita bongo mwenye gauni la kijani alivyokuwa happy akimchezesha mumewe muziki unaoimbwa kwa lugha anayoielewa yeye-kilingala toka kwa madilu system mwana ninja,ilikua safi..



Mamaa EDITH OMARI BONGO/EDITH SASSOU NGUESSO(RIP)



 
Last edited by a moderator:
lol.. nchi za marais madikteta zina raha sana kwa rais na wateule wake,sio huku kwetu
 
he! kumbe madilu bado yupo??? mungu anisamehe nilishamzika kwenye kichwa changu cku nyingi!!!!!!!!!
 
Kweli marehemu Editha alikuwa mpenda muziki. Mungu awalaze wote mahali pema peponi Amen.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom