Madikteta wote duniani hufanana

Inaonekana watu hawashindwi kuwatambua madikteta; Kitila umesema point moja muhimu sana. Madikteta wanahofia sana intellectuals vile vile. Lakini upande mwingine kundi la wasomi hujitengeneza kama watetezi wa madikteta hao.

Mkuu naona kwa sasa unacheza na huu mziki, umejitengeneza au umetengenezwa kuwa mtetezi wao kama ulivyosema hapa. kila la kheri mkuu.

Aione BAK
 
Vyema, na Kweli kabisa. Sasa tuanze kuwaorodhesha madikteta wa dunia hii hapa. Mimi naanza na wachache ninaowafahamu. Wadau tusaidiane kutaja hadi wakamilike:

1) Gbagbo wa Ivory Coast ni Dikteta
2) Hosni Mubarak wa Egypt ni Dikteta
3) Yoweri Museveni wa Uganda ni Dikteta
4) Chama cha Mapinduzi cha Tanzania ni cha Kidikteta

5) ...
Badili no 4 uweke muhusika
 
Mbona na mimi naweza kupata shida ya huyo dikteta mwingine maridadi ambaye naye anakidhi vigezo hivyo hivyo... isije kuwa ni yale yale ya "ghaidi wako ni mpigania uhuru wa mwenzako"?
Unafiki ni mbaya sana.Kwa hiyo huko kwingine kama kuna dikteta maridadi basi udikteta wa huyu ni halali! too pathetic mwanakijiji! ni wewe kweli? ni njaa au tamaa ya kutaka kupewa vyeo vya chee?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Madikteta wote wanafanana; wawe ni wale ambao ni mtu mmoja mmoja au wawe wa chama kimoja; kufanana kwao kunatabiri vitendo vyao. Hufanana katika mambo makubwa matano:

a. Huamini kuwa wao ndio pekee wenye uwezo wa kutawala (Katika fikra zao hawaamini kama kuna mtu au chama kingine kinachoweza kutawala vizuri kuliko wao). Baadhi yao (kama ni mtu mmoja au chama) hujiaminisha kabisa kuwa ni wateule wa Mungu kutawala nchi zao.
b. Huamini kuwa wanapendwa sana kupita kiasi (hili kuelezea kwanini picha, sanamu, n.k zao huenezwa kila kona ya nchi) Hupenda kuimbiwa nyimbo za kusifiwa na kupeperushiwa maua kila wapitapo kama ishara ya "upendo" huu.
c. Hawako tayari kuamini wanaweza kukataliwa; Mara zote inapotokea mtu anawapinga au kuwakataa hutafutiwa sababu ya kuoneshwa kuwa haiwezekani awakate wao kwani (b) wao wanapendwa sana!
d. Hata siku moja hawajawahi kutengeneza mifumo itakayowaondoa wao wenyewe madarakani. Hivyo, hutumia mbinu zote kufanya mabadiliko ya kimapambo tu ambayo kwa watu wasiofuatilia huweza kuvutiwa kuwa ni mabadiliko. HIvyo aidha hujikuta wanaondoka kwa kukimbia au kwa kukimbizwa na wananchi wao au mataifa ya nje!
e. Wako tayari kufanya jambo lolote kubakia madarakani - msisitizo hapa uko kwenye neno "LOLOTE".

Kutokana na hayo matatu tabia za madikteta wote huweza kutabirika (wawe ni mtu mmoja au chama kimoja). Na ili kuhakikisha hayo matatu madikteta wote duniani (wanaovaa nguo za kiraia na wale wanaovaa nguo za kijeshi)

1. Hutumia vitisho kulazimisha kupendwa na kukubalika - silaha ya dikteta ni vitisho (terror). Wakikukamata watakasumbua sana hadi uogope. Lengo ni kukushawishi uone ni kwanini wao wanastahli kupendwa! Hupenda kujiona kama wazazi wa wananchi - nani atamchukia mzazi wake?
2. Hutengeneza masimulizi ya sifa na kuyalazimisha yaaminiwe hata kama msingi wake ni uongo. Madikteta ni mabingwa wa kuunda (manufacture) uongo. Uwezo wao mkubwa wa kufanya hivi hutokana na ukweli kuwa wao humiliki vyombo vya habari vyenye kufikia watu wengi zaidi (radio, TVs n.k)
3. Inapofikia mahali kuwa upendo wa wananchi unapungua au wanaanza kuwa na mashaka nao madikteta huanza kupoteza watu. Yaani, pole pole watu huanza kukamatwa na kuwekwa "vizuizini" ili wasimpinge sana dikteta.
4. Kisingizio pekee cha madikteta wote (wawe wa mtu mmoja au chama kimoja) kuhalalisha kuwanyanyasa, kuwanyima wananchi uhuru na hata kuwatia watu nguvuni ni "kwa ajili ya nchi". Yaani, hutumia "taifa" kama kisingizio cha wao kuendelea kutawala.

Kwanini?

Kwa sababu madikteta wote wanataka kupendwa na kukubaliwa!

Ole wao wananchi wanaposema "hapana"!!!

Na. M. M. Mwanakijiji (BGM)

Umesahau moja chadema walisherehekea Birthday ya mtoto wa lowasa ambaye siyo mwana chadema wala hajui hata historia ya chadema!
Chadema pia husherehekea ndoa ya lowasa!
Sasa hii ndiyo tabia ya Madikteta karibia wote hupenda kutukuzwa na kusujudiwa wao na familia zao kama vile fisadi lowasa anavyosujudiwa na wana chadema!
 
Umesahau moja chadema walisherehekea Birthday ya mtoto wa lowasa ambaye siyo mwana chadema wala hajui hata historia ya chadema!
Chadema pia husherehekea ndoa ya lowasa kila mwaka!

Hivi wewe umefika hata darasa la kwanza kweli?
 
Umesahau moja chadema walisherehekea Birthday ya mtoto wa lowasa ambaye siyo mwana chadema wala hajui hata historia ya chadema!
Chadema pia husherehekea ndoa ya lowasa kila mwaka!
Sasa hii ndiyo tabia ya Madikteta karibia wote hupenda kutukuzwa na kusujudiwa wao na familia zao kama vile fisadi lowasa anavyosujudiwa na wana chadema!

Unafikiri chadema wako kisiasa tuu?

Mtoto wa daktati akifariki au akiolewa madaktari hawaruhusiwi kushiriki kwasababu mtoto si daktari?

ivi kwanini mashabiki wa ccm hamtumiagi akili?
 
Unafiki ni mbaya sana.Kwa hiyo huko kwingine kama kuna dikteta maridadi basi udikteta wa huyu ni halali! too pathetic mwanakijiji! ni wewe kweli? ni njaa au tamaa ya kutaka kupewa vyeo vya chee?
Ni unafiki wa kiwango cha juu sana ndio unaomsumbua Mwanakijiji na wengine,hawana chembe ya uzaendo
 
Unafikiri chadema wako kisiasa tuu?

Mtoto wa daktati akifariki au akiolewa madaktari hawaruhusiwi kushiriki kwasababu mtoto si daktari?

ivi kwanini mashabiki wa ccm hamtumiagi akili?

Sijasema kwamba hamruhusiwi au siyo sawa husherehekea Birthday ya mtoto wa fisadi Lowasa ila nimesema madikteta wote hufanya/ hufanyiwa hivi!
 
Hakuna nguvu ya mamlaka iliyowahi kushinda nguvu ya umma duniani.
Hakuna Dikteta aliyewahi kustaafu.Siku zote anguko lao ni aibu, na sifa kuu ya dikteta ni kutokuwa na uwezo wa kujifunza kutokana na matukio au mifano.
aisee...tunatoka mbali sana
 
Hivi Mzee Mwanakijiji huu uchambuzi ni wewe uliufanya miaka mitano iliyopita? Na imekuwaje mbona inaonyesha kama wewe huamini tena maneno haya wakati ndiyo yanatokea mbele ya macho yetu?
 
Madikteta wote wanafanana; wawe ni wale ambao ni mtu mmoja mmoja au wawe wa chama kimoja; kufanana kwao kunatabiri vitendo vyao. Hufanana katika mambo makubwa matano:

a. Huamini kuwa wao ndio pekee wenye uwezo wa kutawala (Katika fikra zao hawaamini kama kuna mtu au chama kingine kinachoweza kutawala vizuri kuliko wao). Baadhi yao (kama ni mtu mmoja au chama) hujiaminisha kabisa kuwa ni wateule wa Mungu kutawala nchi zao.
b. Huamini kuwa wanapendwa sana kupita kiasi (hili kuelezea kwanini picha, sanamu, n.k zao huenezwa kila kona ya nchi) Hupenda kuimbiwa nyimbo za kusifiwa na kupeperushiwa maua kila wapitapo kama ishara ya "upendo" huu.
c. Hawako tayari kuamini wanaweza kukataliwa; Mara zote inapotokea mtu anawapinga au kuwakataa hutafutiwa sababu ya kuoneshwa kuwa haiwezekani awakate wao kwani (b) wao wanapendwa sana!
d. Hata siku moja hawajawahi kutengeneza mifumo itakayowaondoa wao wenyewe madarakani. Hivyo, hutumia mbinu zote kufanya mabadiliko ya kimapambo tu ambayo kwa watu wasiofuatilia huweza kuvutiwa kuwa ni mabadiliko. HIvyo aidha hujikuta wanaondoka kwa kukimbia au kwa kukimbizwa na wananchi wao au mataifa ya nje!
e. Wako tayari kufanya jambo lolote kubakia madarakani - msisitizo hapa uko kwenye neno "LOLOTE".

Kutokana na hayo matatu tabia za madikteta wote huweza kutabirika (wawe ni mtu mmoja au chama kimoja). Na ili kuhakikisha hayo matatu madikteta wote duniani (wanaovaa nguo za kiraia na wale wanaovaa nguo za kijeshi)

1. Hutumia vitisho kulazimisha kupendwa na kukubalika - silaha ya dikteta ni vitisho (terror). Wakikukamata watakasumbua sana hadi uogope. Lengo ni kukushawishi uone ni kwanini wao wanastahli kupendwa! Hupenda kujiona kama wazazi wa wananchi - nani atamchukia mzazi wake?
2. Hutengeneza masimulizi ya sifa na kuyalazimisha yaaminiwe hata kama msingi wake ni uongo. Madikteta ni mabingwa wa kuunda (manufacture) uongo. Uwezo wao mkubwa wa kufanya hivi hutokana na ukweli kuwa wao humiliki vyombo vya habari vyenye kufikia watu wengi zaidi (radio, TVs n.k)
3. Inapofikia mahali kuwa upendo wa wananchi unapungua au wanaanza kuwa na mashaka nao madikteta huanza kupoteza watu. Yaani, pole pole watu huanza kukamatwa na kuwekwa "vizuizini" ili wasimpinge sana dikteta.
4. Kisingizio pekee cha madikteta wote (wawe wa mtu mmoja au chama kimoja) kuhalalisha kuwanyanyasa, kuwanyima wananchi uhuru na hata kuwatia watu nguvuni ni "kwa ajili ya nchi". Yaani, hutumia "taifa" kama kisingizio cha wao kuendelea kutawala.

Kwanini?

Kwa sababu madikteta wote wanataka kupendwa na kukubaliwa!

Ole wao wananchi wanaposema "hapana"!!!

Na. M. M. Mwanakijiji (BGM)

Haya mawazo ya kipindi kile bado yanafanya kazi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom