Madhara ya unywaji wa soda kwenye afya ya Binadamu

Click_and_go

JF-Expert Member
Nov 21, 2010
451
5
Ningependa kufahamu madhara ya soda kwenye mwili wa Binadamu.

===========
Afya za mamilioni ya Watanzania wanaotumia vinywaji vya aina ya soda ipo hatarini, baada ya kugunduliwa uwepo wa chembechembe zenye kemikali za sumu ndani ya vinywaji hivyo,

Utafiti uliofanywa na Muungano wa Waandishi wa Habari za Uchunguzi Tanzania (Investigative Journalists Union of Tanzania- IJUTA) pamoja na tafiti zilizofanywa na wataalamu waliobobea katika afya ya umma duniani, umebaini kuwa vinywaji baridi aina ya soda ni hatari kuliko utumiaji wa sigara inayosababisha maradhi ya kansa katika mwili wa binadamu.

Kwa mujibu wa utafiti wa wanasayansi mbalimbali duniani, yapo madhara makubwa ya utumiaji wa vinywaji vya aina ya soda katika mwili wa binadamu.

Utafiti huo unaonyesha kuwa zipo sababu nane kuu zinazokiweka kinywaji aina ya soda kwenye kundi la vinywaji vyenye sumu ambavyo havifai kwa matumizi ya binadamu.

IJUTA imebaini kuwa makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji baridi aina ya soda yanatumia mabilioni ya dola kila mwaka kujitangaza na kutoa misaada ya kijamii kutokana na mauzo yake, bila kutaja madhara ya vinywaji hivyo kwa binadamu.

Kwamba matangazo hayo yanayogharimu mamilioni ya fedha ndiyo yanayokifanya kinywaji hicho kuwa maarufu zaidi duniani, licha ya kuwa na madhara makubwa katika mwili wa binadamu.

Aidha, utafiti huo unaonyesha kuwa umaarufu mwingine wa kinywaji aina ya soda ni utamu wa kupindukia ulio ndani ya soda.

Utafiti wa IJUTA unaonyesha kuwa utamu wa kupindukia iliomo ndani ya soda unawapumbaza wanywaji ili wasisikie ladha kali ya asidi iliyomo ndani ya soda.

IJUTA imegundua kuwa kiwango cha asidi kilicho ndani ya soda hakiwekwi wazi kwa walaji kwa sababu ya kuhofia kuwa wakibaini wataacha kikutumia kinywaji hicho.

Inaelezwa pia kuwa madini ya cola yaliyo ndani ya soda yana kilevi aina kafein kinachomteka mnywaji kuwa teja wa kinywaji hicho.

Tafiti za kitaalamu zimeonyesha kuwa soda inahusishwa na matatizo mengi ya kiafya kwa watoto na watu wazima, yakiwemo matatizo ya kuongezeka unene kupita kiasi, ugonjwa wa ini na mengineyo.

Utafiti uliofanywa nchini Marekani unaonyesha kuwa soda huwekewa ‘fructose’ (sukari) nyingi kupitia mfumo wa sirapu (fructose corn syrup) ambayo inaongoza kwa kusababisha magonjwa ya unene, kisukari, ugonjwa wa moyo na magonjwa mengine sugu yanayowakabili Wamarekani wengi hivi sasa na dunia kwa ujumla.

Dk. Mercola, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya lishe asilia na tiba mbadala nchini Marekani, amekaririwa na tafiti mbalimbali zilizofanyika nchini humo akieleza kuwa kinywaji aina ya soda ni hatari kwa binadamu, sawa na mtu anayevuta sigara au zaidi, jambo alilosisitiza kuwa siyo la kutia chumvi, bali ukweli halisi.

Watumiaji wa vinywaji aina ya soda wanaelezwa kuwa wamekuwa wakinywa kiasi kikubwa cha kaboni, kafeini (dawa ya kulevya), sukari ya kupundukia na asidi kali ambayo huvuruga afya ya mtumiaji kwa kiwango cha juu.

Soda pia imebainika kutokuwa na lishe ya aina yoyote zaidi ya maji na sukari.

Uchunguzi wa IJUTA na utafiti ya wanasayansi mbalimbali duniani, umeonyesha kuwa watu wengi hawajui kuwa unywaji wa soda huwaongezea kiasi kikubwa cha madini joto.

Chupa moja ya soda yenye ujazo wa mililita 330 husababisha unene kwa kiwango cha paundi moja kwa mwezi.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kisukari Tanzania (TDA), Ramadhan Mongi, amepata kukaririwa na vyombo vya habari hapa nchini akieleza kuwa ugonjwa wa kisukari Tanzania umeongezeka mara sita katika siku za hivi karibuni.

Alisema miaka kumi iliyopita, hali ya kisukari ilikuwa asilimia tatu (3), lakini katika miaka ya karibuni umeongezeka mara sita.

“Tunastahili kuongeza jitihada ya kupambana na gonjwa hili la kisukari kwa gharama zote kwa sababu kisukari ni moja ya magonjwa manne yanayomaliza Watanzania,” alisema.

Utafiti uliofanyika Mkoa wa Dar es Salaam ulibaini kwamba kati ya watu watano waathirika wa kisukari, mmoja tu ndiyo hupata matibabu ya serikali.

Unywaji kwa mpigo wa kabohaidrets iliyo na sukari nyingi kwenye soda hudhoofisha seli zinazozalisha vimeng’enya tofauti na vyakula vingine na pia imebainika kuwa sukari ikiingia kwa wepesi kwenye mzunguko wa damu husababisha kongosho kuzalisha vimeng’enya vingi mwilini.

Uchunguzi wa kitabibu katika Hospitali ya wanawake ya Boston nchini Marekani na katika Chuo cha Kitabibu cha Harvard umeonyesha wanawake 51,000 hawakuwa na kisukari mwanzoni mwaka wa 1991, lakini miezi minane baadaye wanawake 741 waligundulika na kisukari.

Ripoti ya utafiti huo ilionyesha kuwa wanawake waliokuwa wakitumia kinywaji aina ya soda moja ama mbili kwa siku waliongezeka uzito maradufu na walikuwa hatarini kupata ugonjwa wa kisukari.

Pia ilionyesha kuwa soda hudhoofisha mifupa na husababisha hali ya mifupa kupuputika, hali inayomuweka mtumiaji kuwa katika hatari ya kuvunjika mifupa kirahisi.

Madhara mengine yaliyobainika kusababishwa na unywaji soda ni kupukutika kwa meno na ama kuoza. Pia soda husababisha matatizo ya figo.

Soda yenye chembe ya cola husababisha figo kuwa na mawe kwa sababu ya asidi na kemikali mbalimbali zinazofichwa vipimo vyake kwa walaji.

Madaktari bingwa wa wanamichezo wanaeleza madhara yanayosababishwa na soda mwilini kuwa ni pamoja na shinikizo la damu, uharibifu wa ini, huvurugu mfumo wa kumeng’enya chakula tumboni kutokana asidi ya kiwango cha juu iliyo kwenye soda.

Wanashauri kuwa soda haistahili kutumika kama kishawishi kwenye mchezo, kwa sababu ina madhara makubwa kwa wanamichezo kwa sababu hunyonya maji kwenye mwili na kudhoofisha mwili.

Wakati utafiti huo ukidhihirisha hayo, Taasisi ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imeshindwa kutoa tamko lolote kuhusu utafiti huo, hata baada ya kupelekewa maswali kwa maandishi yanayoomba ufafanuzi wa ubora wa vinywaji vya soda katika mwili wa binadamu.

Soda yapigwa marufuku Ughaibuni
Jumatano, Mei 15, 2013 05:22 Na Fred Okoth

Yakatazwa shuleni, watoto chini ya miaka 12
Sasa yabainika kuwa ina sumu inayoua taratibu
Yagundulika kupumbaza na kusababisha uteja

SIKU chache baada ya gazeti hili kuripoti madhara yanayosababishwa na kinywaji aina ya soda, katika utafiti wake gazeti hili limebaini mengine mapya.

Kwa mujibu wa utafiti huo, imebainika kuwa soda imepigwa marufuku kutumiwa na watoto walio na umri chini ya miaka 12 na walio shuleni katika baadhi ya mataifa ya Ulaya na Marekani, kutokana na madhara ya kiafya yanayosababishwa na kinywaji hicho.

Taarifa zilizotolewa na Shirika la Habari la The Press Television Technology Advertising and Branding (Adweek) zinazonukuu taarifa ya kampuni moja kubwa duniani inayozalisha kinywaji aina ya soda, imeamua kupambana na unene (obesity), unaosababishwa na unywaji wa soda kwa kuondoa matangazo ya vinywaji vyake kwenye vyombo vya habari.

Kampuni hiyo kupitia taarifa yake hiyo iliyotolewa katika moja ya sherehe zake, ilieleza kuwa lengo la kuondoa matangazo hayo ni kuwanusuru watoto wadogo na matumizi ya vinywaji aina ya soda vilivyobainika kuwa na madhara katika mwili wa binadamu.

Nchini Marekani, tayari imekwishapitishwa sheria inayokataza watoto walio na umri wa chini ya miaka 12, kunywa kinywaji aina ya soda.

Mwenyekiti wa Kampuni hiyo, alieleza kuwa mipango ya mbeleni ya kampuni yake ni kutengeneza kinywaji hicho kikiwa na kiwango kidogo cha Kalori na kubuni kinywaji cha aina hiyo ambacho kitakuwa hakina Kalori.

Alisema mipango hiyo itatekelezwa duniani kote ambako kinywaji cha aina ya soda kinatengenezwa na nchini Marekani tayari imekwishaanza kutekelezwa.

Aidha, Kampuni hiyo imeahidi kuweka wazi virutubisho vyote vinavyotumika kutengeneza bidhaa zake na kuahidi kutoa misaada ya hali na mali kwa nchi zote 200 duniani ambako kinywaji cha soda kinauzwa.

Mbali na Marekani, kinywaji cha aina ya Soda kimekwishapigwa marufuku shuleni katika nchi za Uingereza, Ufaransa na katika majimbo ya Los Angeles, Philadelphia na Miami nchini Marekani na kwa watu wazima matumizi yake yanaelekezwa kuwa ya kiwango kidogo sana.

Vyombo vya habari vya nchini New Zealand, mwezi Machi mwaka huu viliripoti kuwa mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Natasha Harris (31), alifariki kutokana na unywaji wa soda nyingi.

Shirika la habari la AFP la Ufaransa, liliripoti tukio hilo kwa kueleza kuwa Natasha alikuwa akinywa soda nyingi kila siku, jambo ambalo liligeuka kuwa sehemu ya maisha yake kwa kipindi cha miaka mingi.

Kwamba familia ilikuwa ikimuita teja wa soda, baada ya meno yake kuoza kwa sababu ya kunywa soda, alijifungua mtoto ambaye hakuwa na fizi jambo ambalo liligundulika baadaye kuwa lilisababishwa na matumizi makubwa ya kinywaji hicho.

“Tumegundua kwamba, kwa kuzingatia ushahidi uliopo, kama sio unywaji wa soda uliopitiliza, Natasha Harris asingekufa katika muda ule na katika hali alivyokufa

“Ripoti ya Daktari aliyechunguza maiti yake (Pathologia), iligundua kwamba ini lake lilipanuka sana, likawa na mrundiko mkubwa wa mafuta kutokana na kula sukari kwa wingi. Kuwepo kwa madini aina ya ‘potasiam’ kwa kiwango kidogo sana kwenye damu yake, pia kulitokana na unywaji wa soda.” Taarifa ya kitabibu katika Hospitali aliyofia nchini New Zealand ilieleza.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kisayansi zilizo kwenye mitandao ya wanasayansi waliobobea duniani, unywaji wa soda humpumbaza mtumiaji na kumsahaulisha kula vyakula vyenye madini muhimu mwilini.

Moja ya andishi linalotahadharisha utumiaji wa kinywaji cha soda na kukitaja kuwa cha hatari kwa matumuzi ya binadamu, ni Jack Winkler, Profesa wa sera za lishe katika Chuo Kikuu cha Metropolitan nchini London, linaloeleza kuwa Soda ni bidhaa ya kishetani inayoua binadamu taratibu baada ya kinywaji hicho kumzalishia magonjwa mengi mwilini yanayomfanya kuwa tegemezi wa dawa.

Wakati msomi huyo akieleza hayo katika utafiti wake, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Dk. Raymond Wigenge, amelieleza gazeti hili soda siyo kinywaji hatari kwa matumizi ya binadamu kwa sababu kinatumiwa na mamilioni ya watu duniani kote.

Akizungumza na MTANZANIA Jumatano ofisini kwake wiki iliyopita baada ya kutoa ufafanuzi kuhusu madhara yanayosababishwa na kinywaji aina ya soda katika mwili wa binadamu, Dk. Wigenge alisema pamoja na changamoto zilizopo katika kinywaji hicho, taasisi yake haipingi uwepo wa kinywaji hicho sokoni.

“Soda haina shida kwa binadamu na hata mkiendelea kuandika suala hili, sisi tutaendelea kuueleza umma kwamba waendelee kupata kinywaji, hivyo kama ambavyo tumekuwa tukifanya,” alisema.

Alipoulizwa kama anakubaliana na tafiti za wanasayansi bingwa wa magonjwa ya binadamu walioeleza katika tafiti zao kuwa unywaji wa soda una madhara katika mwili wa binadamu, alisema hizo ni changamoto za kawaida, kwa sababu madhara yaliyomo kwenye soda hayamuathiri mtu mara moja bali huchukua muda mrefu.

Wakati Dk. Wigenge akieleza msimamo wake kuhusu kinywaji aina ya soda, nchini Mexico, taasisi ya El Poder del Consumidor inayojihusisha na kutetea walaji, inashinikiza Serikali ya nchi hiyo kuzilazimisha kampuni za soda kuorodhesha madini na chembechembe zote za kemikali zinazotumika kutengeneza kinywaji hicho.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Alejandro Calvillo, amekaririwa na vyombo vya habari vya nchi hiyo akieleza kuwa unywaji wa soda ni hatari na hilo limethibitishwa na wataalamu wa afya duniani kuwa soda ni sumu mbaya, inauwa taratibu.

Tafiti mbalimbali za wanasayansi zinaeleza kuwa soda ina asidi aina ya ‘phosphoric’ yenye uwezo wa kuvuruga madini ya ‘calcium’ yaliyoko mwilini na kusababisha mifupa na meno kudhoofika.

Aidha, asidi aina ya ‘phosphoric’ huvuruga asidi aina ya ‘hydrochloric’ iliyo tumboni mwa binadamu na hivyo kuharibu mfumo wa kusaga chakula.

Viwanda vya soda ndio watumiaji wakubwa wa sukari na wanasayansi wanasema sukari hupandisha kiwango cha ‘insulin’ ambayo husababisha kasi ya mzunguko wa damu, ugonjwa wa moyo, kupanda kwa ‘Cholesterol, kisukari, kuzeeka mapema, ongezeko la uzito na maradhi mengine.

Aidha inadaiwa kuwa viwanda vya soda pia hutumia dawa ya kulevya aina ya kafeini. Wataalamu wanasema vinywaji vyenye kafeini, husababisha kupanda kwa mapigo ya moyo, kasi ya mzunguko wa damu na matatizo ya kiza.

1580459357047.png


----

Habari wana Jf, Naomba kushiriki madhara yatokanayo na unywaji wa soda.
Soda inakiwango cha sukari, Sukari yeyote ni hatari katika mfumo wa mwili, Wataalam wanathibitisha uwepo wa takribani vijiko 10 vya sukari katika kila chupa moja ya soda, kwa maana hiyo unapokunywa soda 5 kwa siku maanake unakula vijiko 50 vya sukari iliyo kwenye maji yaliyochanganywa na sukari (soda) pamoja na kemikali inayolinda soda isiharibike, kitaalam pia kwenye soda kuna kiwango kikubwa sana cha ACID (PH 2-3). Kiwango cha kemikali kilichopo ndani ya tumbo la binadamu kinadaiwa kuwa na Ph ya 3 ambayo huweza hata kusaga mfupa uliomezwa kwa bahati mbaya,Hivyo basi, kemikali iliyopo kwenye soda ni kali zaidi ya hata iliyopo tumboni mwa mwanadamu.

INSULINI kemikali iliyoundwa katika kongosho (pancrease). Husaidia kusawazisha kiwango cha sukari mwilini,Kongoshoina kazi ya kutengenza insulin na homoni zingine za kusaidia uyeyushaji wa chakula (Mmeng’enyo).

Ikumbukwe kwamba kiwango cha sukari mwilini huchujwa sehemu ya kongosho, kongosho linapofail kuchuja ndipo sukari huanza kupanda taratibu, kiasi kwamba mtu hupata kisukari na magonjwa mengine, kongosho inapofail hapo ndipo binadamu huanza kutapata, hapo ni sawa na dreva kuambiwa apunguze speed anakaidi akitegemea BREAK, na Break inapofail hapo ndipo CHANGAMOTO huanzia.

Yamkini huenda BIA ikawa ni bora zaidi kuriko kunywa soda hizi tunazokimbilia kila siku.

Dalili za kisukari

a. Kukojoa mara kwa mara

b. Kiu Isiyoisha:

c. Njaa Kali:


d. Kuongezeka kwa uzito (unene):

e. Kupungua uzito kusiko kawaida:

f. Uchovu wa mwili:

g. Hasira:

h. Kutoona vizuri:


i. Vidonda kutopona vizuri au haraka:

j. Magonjwa ya ngozi:


k. Kuwashwa kwa ngozi:

l. Kuwa na fizi nyekundu au zilizovimba:

m.Uwezo mdogo wa kushiriki tendo la ndoa:

n. Ganzi mikononi au miguuni:

Zifuatazo ni baadhi ya Athari za sukari ;

i.Sukari huweza kuathiri ukuaji wa homoni mwilini ( kitu ambacho ni muhimu kwa kumfanya mtu kuishi na afya njema wakati wote )

ii.Sukari ndiyo chakula cha saratani mwilini.

iii.Sukari huongeza lehemu ( cholesterol ) mwilini.

iv.Sukari huweza kusababisha kizunguzungu na kudhoofisha mwili kwa watoto.

v.Sukari huweza kudhoofisha nguvu ya macho

vi.Sukari huweza kuzuia utembeaji wa protini mwilini

vii.Sukari huweza kusababisha mzio wa chakula ( Food allergies )

viii.Sukari huchangia ugonjw a wa kisukari

ix.Sukari huweza kusababisha ugonjwa wa moyo.

x.Sukari huweza kuharibu, umbo la vinasaba vya mwili ( D.N.A )

xi.Sukari huweza kusababisha utukutu, utundu na kukosa umakini kwa watoto.

xii.Sukari huweza kuchangia kupunguza n kinga ya mwili dhidi ya magonjwa yatokanayo na wadudu aina ya bacteria ( infectious diseases )


Hizo ni baadhi tu ya sababu karibu takribani 146. Je, kwa kujua sababu zote zilizo thibitishwa kuhusu madhara yatokanayo na sukari, kuna sababu gani ya kuendelea kupenda kutumia sukari jamani? Ingawa Hatuwezi kuiepuka sukari moja kwa moja kwani baadhi ya vyakula huwa havitamkwi moja kwa moja jina la kuwepo kwa sukari bali hutumia majina kama Glucose, fructose n.k Yakupasa wewe mwenyewe utokomeze ulaji wa sukari kwa kujiwekea mikakati yako, punguza matumizi ya soda, kuna watu wakipata kiu badala ya kunywa maji hukimbilia soda, Soda ni kinywaji hatari sana kuriko BIA, Hasara ya Bia ipo kwenye gharama na ulevi unaomfanya mtu asijitambue, Lakini madhara ya soda/sukari ni Makubwa sana.
unaweza punguza matumizi ya sukari kwenye chai, kwa kukamulia ndimu kwenye chai ukizoea ni taam sana.

pia kuepuka unywaji wa soda tujitahidi tunywe maji badala ya soda;

Unywaji wa soda moja kwa siku hupunguza uwezo wa mtu kuzaa

Utafiti mpya kutoka chuo cha madawa kilichopo Boston umebaini kwamba unywaji wa kinywaji kimoja au zaidi chenye sukari nyingi kwa wanawake au wanaume hupunguza uwezekano wa mwanamke kupata ujauzito au mwanaume kuzalisha.

Kiwango cha sukari kinachopatikana kwenye vinywaji mbalimbali ikiwemo soda ambapo ni sawa na theluthi moja ya sukari yote inayowekwa, kimehusishwa na hali ya kuongezeka uzito, kisukari, upungufu wa nguvu za kiume, kuwahi kupevuka kwa wasichana na kwa sasa inapunguza sana uwezo wa mtu kupata mtoto.

“Tumegundua kuna uhusiano mkubwa sana kati ya unywaji wa vimiminika vyenye sukari nyingi na uwezo mdogo wa mtu kupata mtoto, ambao mara nyingi husababishwa na vitu vingine ikiwemo, unene uliopitiliza, unywaji wa kafeini, matumizi ya vilevi, uvutaji wa sigara na matatizo ya jumla ya ulaji mbovu,’’ hayo yamesemwa na mwandishi kiongozi wa utafiti huo, Elizabeth Hatch.
Kwa wenza ambao wanapanga kupata watoto ni vizuri wakapunguza viwango vyao vya unywaji wa vimiminika hivyo, hasa kutokana na kuwa vinahusishwa pia kwenye matatizo mengine ya kiafya.

Utafiti uliochapishwa kwenye jarada la Epidemiology, watafiti walifanya uchunguzi kwa wanawake karibu 4,0000 wenye umri kati ya miaka 21 mpaka 45 na kwa wenza wao wa kiume karibu 1,000 kwa kuchunguza taarifa zao kiafya, mtindo wa maisha na mfumo wao wa ulaji – ikijumuisha idadi ya vinywaji venye sukari nyingi wanavyotumia.

Katika uchunguzi huo waligundua kwamba wanawake ambao walikunywa angalau soda moja kwa siku walikuwa wamepoteza uwezo wa kushika mimba kwa asilimia 25 na kwa wanaume uwezo ulikuwa umepungua kwa asilimia 33.

Hata hivyo unywaji wa vimiminika vya kuongeza nguvu ndio ulihusishwa na madhara makubwa zaidi kiafya kwenye uwezo wa kuzaa, lakini unywaji wa juisi za matunda na soda zisizo na sukari ulikuwa na matokeo madogo sana kwenye kusababisha ugumba au utasa.

“Kutokana na kiwango kikubwa cha sukari kinachoingia kwenye miili ya watu ambao wapo kwenye umri mzuri wa kuzaa,’’ utafiti umedai kwamba matokeo ya uchunguzi yaliyotolewa yanaweza kuleta manufaa kwenye afya za watumiaji.’’

Kuna kitu cha msingi kimesahaulika hapa. Mountain dew japo inafanana fanana kwa rangi na 7up na sprite, tofauti yake kubwa ni kwamba ina kitu inaitwa caffaine. Hi caffaine ipo pia katika Pepsi na Coka. Pia ipo kwa wingi sana katika kahawa na chai.

Madhara ya Caffaine

1. Inasababisha moyo kwenda mbio isivyo kawaida, hivyo basi ni hatar kwa watu wenye high bp.

2. Inafanya kitu inaitwa vascular constriction, kusinya kwa mishipa ya damu, inapotoke katika ubongo, watu hupata maumivu ya kichwa.

3. Inasababisha kupotea kwa maji mengi mwilini hivyo kukufanya ujisikie mchovu.

4. Kusijisikia hali ya uoga sana, kwa baadhi ya watu, inasemekana inatokana na mchakato wa akili kuwa active sana.

5.Wanawake wanokunywa caffaine kwa wingi, hupungua kwa kiwango cha nusu kutopata mimba, kulinganisha wale asiotumia.

6. Inaweza kukufany uamke ukiwa umechoka kwasababu inazuia upatikanaji wa usingizi.

7. Sina hakika, lakini nishasikia ina athari katika vinasaba, unatoa toto hamfanani kabisa.

Kama unaweza kusurf kwenye internet unaweza kupata zaidi. Mwenye hekima hajaribu sumu kama kweli ni sumu kwa kuilamba. Usisubiri ufahamu sana acha.

[h=3]Madhara ya soda ni mengi mno, kuanzia kisukari, unene na uzito kupita kiasi, kufunga choo, na magonjwa mengine mengi[/h] [h=3]MCHANGO WA SODA KATIKA UZITO NA UNENE KUPITA KIASI:[/h] [h=3]Twende pamoja.[/h] [h=3] kwa mjibu wa utafiti wake, dr.Batmanghelidj, anasema, ingawa soda hazina kalori inayoweza kuainika, zinaweza kuwa kisababisho cha kuongezeka uzito kupita kiasi kwa wale wanaozinywa kwa malengo ya kudhibiti uzito wao. [/h] Kitendawili hiki katika uelewa wetu juu ya uhusiano baina ya unywaji wa vimiminika ambavyo havichangii moja kwa moja uchukuaji wa kalori wa mwili na kuongezeka kwa uzito, kinahitaji ufafanuzi. Kwa mjibu wa utafiti huo, kuna watu wengi waliochukua uamuzi wa kunywa soda ili kudhibiti uzito, lakini matokeo yamekuwa kinyume chake.

Viwanda vya vinywaji vinakuwa kwa kasi kubwa (apace), jarida la The Nation la aprili 27, 1998 liliripoti kuwa, watoto na vijana walio wengi wanakisiwa kunywa mpaka galoni 64 za soda kwa mwaka, kiasi ambacho kiliongezeka mara tatu zaidi tangu mwaka 1978, kikaongezeka mara mbili zaidi kwa mafungu ya umri kati ya miaka 6-11 na kuongezeka kwa robo kwa watoto chini ya miaka 5(chanzo: utafiti, kitengo cha kilimo 1994, marekani).

Inavutia pia kuandika hapa kuwa, kuongezeka huku kwa matumizi ya soda kwa watoto chini ya miaka 5, kuweza kuwa ndiyo sababu ya kuongezeka mara tatu zaidi ya ugonjwa wa pumu (asthma) kwa watoto wa umri huo kati ya mwaka 1980 na 1994.

Utafiti mmoja katika kampasi ya chuo kikuu cha pennsylvania nchini marekani, ulionesha baadhi ya wanafunzi kunywa soda 14 kwa siku, msichana mmoja alitumia soda 37 kwa siku mbili. Wengi wamekiri kuwa hawataweza kuishi bila vinywaji hivi baridi.

Ikiwa vinywaji hivi vitaondolewa sokoni, watu hawa wataonesha dalili zilizosawa na zile zinazowatokea waliokuwa wategemezi kwa madawa mengine ya kulevya.

Jarida la Boys Life, liliwatafiti wasomaji wake na kugunduwa kuwa, asilimia 8 ya wasomaji wake wanakunywa soda 8 au zaidi kwa siku. Viongozi wa kambi moja ya skauti (boy scout jamboree), walikusanya chupa 200,000 tupu za soda kwa ajili ya matumizi mengine (recycling), chama cha vinywaji baridi kimefanya utafiti juu ya matumizi ya vinywaji hivi baridi mahospitalini nchini marekani na kugunduwa zaidi ya asilimia 85 wakihudumia wagonjwa chakula pamoja na vinywaji hivi baridi.

Kwa kiasi kikubwa, imeaminika kuwa vinywaji hivi vinaweza kuwa mubadala wa mahitaji ya mwili kwa maji. Imedhaniwa kuwa, kwa sababu tu vinywaji hivi vina maji, mwili utakuwa umekamilishiwa mahitaji yake ya maji. Dhana hii ni potofu.

Kuongezeka kwa matumizi ya soda zenye kafeina,kunaunda vyanzo vingi vya matatizo ya kiafya kwenye jamii zetu. Imani hii potofu kwamba vimiminika vyote ni sawa na maji kwa mahitaji ya mwili, ndiyo chanzo kikuu cha magonjwa kwa mwili wa binadamu ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa uzito kupita kiasi.

Ili kuielewa dhana hii, inatubidi kutambua baadhi ya kanuni rahisi za kianatomia na kifizioloji za ubongo ambazo huongoza hisia za kula na kunywa.

Umbile kubwa la mwili bila mpangilio kwa kusanyiko la mafuta, ni hatua ya mwanzo ya kuanguka kwa mwili wa binadamu, na kwa mjibu wa maoni ya dr.Batmanghelidj, ni matokeo ya kuchagua kusiko sahihi kwa uchukuaji wa vimiminika. Baadhi ya vinywaji vina madhara zaidi ya vingine.

Kafeina, moja ya vitu mhimu katika soda nyingi, ni dawa ya kulevya!!!.

Hii ndiyo sababu kwa wale waliozoea kunywa chai ya rangi asubuhi wasipokunywa hujisikia kichwa kuuma (they are addicted).

Ina sifa ya kumfanya mtu mtegemezi kwayo sababu ya matendo yake moja kwa moja kwenye ubongo. Inaingilia pia katika ini na kusababisha kuongezeka kwa uzarishaji wa mkojo.

Hivyo, kafeina ni kikojoshi (diuretic).

Kifiziolojia, kafeina ni wakala mkausha maji mwilini. Hii ndiyo sababu mtu analazimika kunywa soda nyingi kwa siku bila kutosheka. Maji hayabaki mwilini kwa muda mrefu.

Wakati huo huo, watu wengi wanajichanganya kwa kutokutambua hisia zao za kiu kwa kudhani kuwa wamekunywa maji ya kutosha toka katika soda, wanajihisi kuwa ni wenye njaa na kuanza kula chakula zaidi ya mahitaji yao ya mwili. Kwa hiyoupungufu wa maji (dehydration) uliosababishwa na vinywaji baridi venye kafeina, kwa muda utasababisha kuongezeka kwa uzitokutokana na kula kupita kiasi ambako ni matokeo ya moja kwa moja ya kushindwa kuzielewa hisia za njaa na kiu.

Kafeina, ni kiamsho (pick-me-up), husisimua ubongo na mwili hata wakati mtu amechoka. Inajionesha kuwa, kafeina hupunguza udhibiti wa stoo ya kwanza ya ubongo (ATP). Hifadhi hii ya kwanza hutumika kwa baadhi ya kazi ambazo kwa kawaida zisingeweza kufikiwa kunapokuwa na usawa uliosawa wa hifadhi hii.

Ikitokea soda imeongezwa sukari, walau baadhi ya mahitaji ya ubongo kwa sukari hufikiwa. Ikiwa kafeina inatoa nguvu toka stoo ya kwanza ya nguvu za ubongo kusaidia ufanyikaji kazi, walau sukari yake itarudishia baadhi ya akiba za stoo ya kwanza hata kama matokeo ya mwisho ni matumizi hasi ya ulalo (deficit) ya stoo ya kwanza kwa ubongo.

Mwanzoni mwa miaka ya 1980, kiongeza utamu cha kutengenezwa (artificial sweetener) kiitwacho 'aspartame', kilianza kutumika kwenye viwanda vya vinywaji baridi. Aspartame ina utamu mara 180 zaidi ya utamu wa sukari ya kawaida, bila nguvu yeyote (kalori) izarishwayo nayo.

Aspartame sasa inatumika kama kitu kisicho na madhara kwa sababu Taasisi ya Madawa (Federal Drug Administration ya marekani) imeitetea (deemed it) kama kitu kisicho na madhara kikitumika kama mubadala wa sukari.

Ndani ya utumbo mdogo, aspartame inabadilishwa kwenda transimita nyurolojia mbili, asidi amino aspartame na phenylalamine, vivyo hivyo methyl alikohol au formaldehyde. Inatetewa kuwa Ini huichukulia methyl alikoholi kuwa si sumu. 'Binafsi nafikiri madai haya hutolewa kunyamazisha sauti zinazopinga biashara za vyakula vilivyotengenezwa viwandani vijulikanavyo kuwa na kemikali hatari kwa binadamu - dr.Batmanghelidj'.

Kafeina huibadilisha Adenosine Triphosphate (ATP) kwenda Adenosine Monophosphate (AMP) ambayo ni nishati iliyokwishatumika (ash) na aspartate huibadilisha GuanosineTriphosphate (GTP) kwenda Guanosine Monophosphate (GMP).

Adenosine monophosphate na Guanosine monophosphate zote ni nishati zilizokwishatumika (ash) na husababisha kiu na njaa ili kuzirudishia stoo za nguvu nishati iliyopotea kwenye seli za ubongo. Kwahiyo, unywaji soda husababisha matumizi yasiyo ya busara ya hifadhi za nguvu za seli za ubongo.

Ni ukweli unaojulikana kisayansi kuwa, nishati iliyotumika AMP, huleta hisia za njaa. kafeina husababisha utegemezi (addiction), na watu wanaoitumia mara kwa mara wanatakiwa wajihesabu kama wanatembea katika soda (sodaholics).

Hivyo matumizi ya soda zenye kafeina kwa watu wasiofanya mazoezi lazima yatapelekea kuongezeka uzito, kwa kuzunguka, unywaji wa soda unasisimua kula zaidi sababu ya ubongo kulazimishwa kutumia hifadhi zake za nguvu.

Kumbuka ni baadhi tu ya thamani ya nguvu ya chakula itachukuliwa na ubongo. Sehemu kubwa ya nguvu iliyochukuliwa itahifadhiwa katika mfumo wa mafuta ikiwa haitatumika katika shughuli za mishipa (mazoezi).

Matokeo haya ya uzito kuongezeka kupita kiasi ni moja kati ya matokeo mengine mengi yatokanayo na matumizi ya soda. Kafeina hupatikana pia katika chai ya rangi, kahawa na katika vinywaji vingine vingi vya viwandani.

Tabia moja mhimu inayokuja kujiimarisha ni mwitikio wa ubongo kwa radha za utamu. Lugha ya kitaalamu inayotumika kuelezea mwitikio huu ni, 'cephalic phase response'. Mwitikio huu wa kulazimishwa unakuja kujengwa kama matokeo ya mazoea ya muda mrefu kwa radha zenye utamu zinazoambatana na utambulishaji wa nguvu mpya ndani ya mwili.

Wakati radha zenye utamu zinaposisimua katika ulimi, ubongo unaliamuru Ini kujiandaa kupokea nguvu mpya (sukari) kutoka nje. Ini nalo litasimama kutengeneza sukari toka hifadhi ya protini na wanga ya mwili, na kuanza kuhifadhi nishati ya kimetaboli inayozunguka kwenye mzunguko wa damu.

Kama Michael G Tardoff, Mark I Friedman na wanasayansi wengine, wameonesha kuwa 'cephalic phase' huwa na matokeo ya kuongeza shughuli za kimetaboli ili kuhifadhi lishe, nishati inayopatikana kwa ajili ya mabadiliko hupungua na kusababisha kuongezeka kwa njaa.

Ikiwa ni sukari hasa ndiyo inayosisimua ulimini, matokeo kwenye ini yatakuwa ni urekebishaji wa hicho kilichoingia mwilini. Ingawa ikiwa radha ya utamu haina lishe ndani yake, hisia za kutaka kula zitakuwa ndiyo matokeo yake.Ni Ini ndilo linalotengeneza hisia za kula. Kadiri radha utamu bila kalori ndani yake zinavyosisimua kionjea radha, vivyo hivyo zinavyokuja zaidi hisia za kutaka kula.

Matokeo ya 'cephalic phase' kwa radha za utamu yamethibitishwa katika majaribio kwa wanyama kwa kutumia 'saccharin' (dawa yenye utamu kama sukari). Kwa kutumia aspartame, wanasayansi kadhaa wameonesha matokeo yanayofanana ya kutaka kula kupita kiasi kwa binadamu.

Blundel na Hill wameonesha kuwa viongeza utamu visivyo na kalori hasa aspartame huongeza njaa na kuongeza uchukuaji wa chakula kwa muda mfupi. Wanaripoti, ''baada ya kunyweshwa aspartame, wapendwa waliachwa na njaa iliyobaki ikilinganishwa na walivyoachwa baada ya Glukozi. Njaa hii iliyobaki husababisha kuongezeka kwa matumizi ya chakula''.

Tardoff na Friedman wameonesha kuwa hisia hizi za kutaka kula zaidi chakula baada ya viongeza utamu vya kutengenezwa vimetumika, zinaweza kudumu mpaka dakika 90 baada ya kinywaji kitamu hata wakati majaribio yote ya damu kuonesha thamani ya kawaida. Wameonesha kuwa hata wakati usawa wa damu kwa insulini, usawa wa juu ambao unafikiriwa kuwa unasababisha njaa, umefikia usawa wa kawaida, majaribio kwa wanyama yameonesha hitaji la kutaka kula zaidi ya udhibiti.

Hii inamaanisha kwamba ubongo unashikilia kwa muda mrefu zaidi hisia za kutaka kula inapotokea tezi za kuhisia sukari zimesisimuliwa bila sukari kuwa imeingia kwenye mfumo. Radha utamu husababisha ubongo kuliamuru ini kuhifadhi ziada badala ya kuitumia toka katika akiba za mwili.

Kimsingi, mwitikio huu wa kifiziolojia kwa viongeza utamu bila kuwa na kalori ambazo mwili unazitumainia, unamlazimisha mtu kutafuta kalori hizo kokote na hatimaye kuhitaji kula.

Wakati kafeina na aspartame vimeingia mwilini, huanza kuonesha (dictates) matokeo yake ya kusisimua kwenye fiziolojia ya seli kwenye ubongo, kwenye ini, kwenye figo, kwenye kongosho, kwenye tezi mbalimbali na kadharika.

Aspartame hubadilishwa kuwa 'phenylalanine' na 'aspartate', zote huwa na matokeo ya moja kwa moja ya usisimuaji kwa ubongo. Kwa haraka matokeo ya kafeina na aspartame yanajenga namna mpya za kazi kwa ubongo, kwa sababu vinapatikana kwa kujirudia kwa kiasi kikubwa zaidi ya kile ambacho pengine kingeleta usawa wa kifiziolojia.

Transimita nyurolojia zilizo nyingi, ni mazao ya pili kutoka moja au asidi amino zingine. Hata hivyo aspartate ni moja kati ya jozi ya asidi amino za pekee ambazo hazihitaji kubadilishwa kuwa zao la pili ili kufanya kazi kwenye ubongo. Kuna nukta zinazopokea (receptors) hizi asidi amino mbili kwenye neva seli maalumu ambazo huathiri fiziolojia ya mwili haraka zaidi.

Matumizi ya viongeza utamu kwa usisimuaji wake wa kimakosa wa miishio ya neva ambayo husajili usambazaji wa kuingia wa nguvu kwenye mwili, yana matokeo mengine zaidi yasiyotarajiwa zaidi ya kusababisha kuongezeka uzito kupita kiasi.

Kwa muda wote, kemikali hizi zinaning'inia kwenye fiziolojia ya mwili kwenye mwelekeo unaoamuliwa na mfumo wa neva zinazozisisimua. Matumizi yake bila uelewa wa matokeo yake ya muda mrefu mwilini sababu tu yanasisimua tezi za radha, bado hayajaainishwa.

Utafiti umeonesha kuwa mapokezi ya aspartame yanapatikana pia kwa baadhi ya mifumo ya fahamu ambayo matokeo yake husisimua pia ogani za uzazi na matiti. Usisimuaji wa kudumu kwa tezi za matiti bila sababu nyingine zinazohusiana na ujauzito, unahusishwa kama moja ya sababu za kuongezeka kwa saratani ya matiti kwa wanawake.

Homoni iitwayo prolactini ndiyo inahusika zaidi katika mwelekeo huu. Moja ya vitu ambavyo havijafanyiwa utafiti wa kutosha juu ya madhara ya aspartame, ni matokeo yake ya madhara yanayoweza kupelekea kutokea kwa saratani ya ubongo. Majaribio kwa panya na wanyama wengine, yote yameonesha aspartame kuhusika kutengeneza uvimbe kwenye ubongo.

Dr.H.J.Roberts ameyaainisha baadhi ya matatizo ya kiafya yanayosababishwa na aspartame, na kuyaita yote kwa pamoja kama, 'magonjwa ya aspartame',katika kitabu chake; ''Breast Implants or Aspartame Diseases?'', ameyataja baadhi ya magonjwa kama vile kuumwa kichwa, kizunguzungu, kukosa usingizi, kuchanganyikiwa, kupoteza kumbukumbu, uchovu sugu, kushuka kwa damu sukari, maumivu ya maungio, nywele kupotea, na kadharika, kama ni magonjwa yasababishwayo na aspartame. Ameandika makala na vitabu vingine vingi juu ya mada hii.

Sayansi ya sasa ya kudhibiti kuongezeka uzito kupita kiasi inayohusisha ukatazaji wa baadhi ya vyakula, hata kama baadhi ya kilo zitapungua, zitaongezeka tena baada ya muda mfupi. Cha kushangaza zaidi ni fasheni mpya inayojitokeza siku hizi, mtu anakuwa mtumwa wa kuchagua chakula hiki au kile kama mbwa mnusaji hasa katika suala la helemu (cholesterol).

Usishituke!, ''tofauti na imani iliyojengeka ya kupunguza au kuondoa kabisa matumizi ya mayai katika milo yetu, mimi nakula mayai mengi nitakavyo – dr.Batmanghelidj''. Mayai yana protini nzuri iliyosawazishwa. Anasema, anaelewa pia ni namna gani utengenezwaji wa kolesteroli unavyohusiana na upungufu wa muda mrefu wa maji mwilini (prolonged dehydration).

Ikumbukwe kuwa, kafeina ni dawa ya kulevya(addictive drug) ambayo matumizi yake yamehalarishwa. Watoto wadogo kwa upande wao wanatokea kuwa wategemezi kirahisi zaidi kwa vinywaji vyenye kafeina. Hii ndiyo sababu ya kwanza watoto wengi mashuleni siku hizi hawafundishiki, tunabaki kuwalaumu bure.

Usisimuaji huu wa miili kwa vinywaji vyenye kemikali kwa watoto, hupelekea baadhi yao kuwa wategemezi wa madawa ya kulevya makubwa zaidi wakati wanapokuwa wakubwa.

Kama tulivyofafanua muda wote, mwili hutoa ishara anuwai unapokuwa na maji chini ya kiwango. Wakati huu (uzito unapozidi), mwili unakuwa unahitaji maji pekee.Mwili unaanza kuchanganya habari wakati mtu anapoamua kutumia vinywaji vya kutengenezwa kama mubadala wa mahitaji ya mwili kwa maji.

Kwa hiyo, utumiaji wa muda mrefu na wa kudumu wa soda, lazima uchukuliwe kama moja ya visababisho vya matatizo mengi ya kiafya katika jamii zetu.

"kujielimisha ni kutafuta ukweli wa mambo, kwenda shule hutusaidia tu, japo hatuwezi kwenda shule, twaweza kujielimisha – Mwl.J.k.Nyerere".

Nitarudi.
www.maajabuyamaji2.artisteer.net

Utafiti mpya kutoka chuo cha madawa kilichopo Boston umebaini kwamba unywaji wa kinywaji kimoja au zaidi chenye sukari nyingi kwa wanawake au wanaume hupunguza uwezekano wa mwanamke kupata ujauzito au mwanaume kuzalisha.

Kiwango cha sukari kinachopatikana kwenye vinywaji mbalimbali ikiwemo soda ambapo ni sawa na theluthi moja ya sukari yote inayowekwa, kimehusishwa na hali ya kuongezeka uzito, kisukari, upungufu wa nguvu za kiume, kuwahi kupevuka kwa wasichana na kwa sasa inapunguza sana uwezo wa mtu kupata mtoto.

“Tumegundua kuna uhusiano mkubwa sana kati ya unywaji wa vimiminika vyenye sukari nyingi na uwezo mdogo wa mtu kupata mtoto, ambao mara nyingi husababishwa na vitu vingine ikiwemo, unene uliopitiliza, unywaji wa kafeini, matumizi ya vilevi, uvutaji wa sigara na matatizo ya jumla ya ulaji mbovu,’’ hayo yamesemwa na mwandishi kiongozi wa utafiti huo, Elizabeth Hatch.
Kwa wenza ambao wanapanga kupata watoto ni vizuri wakapunguza viwango vyao vya unywaji wa vimiminika hivyo, hasa kutokana na kuwa vinahusishwa pia kwenye matatizo mengine ya kiafya.

Utafiti uliochapishwa kwenye jarada la Epidemiology, watafiti walifanya uchunguzi kwa wanawake karibu 4,0000 wenye umri kati ya miaka 21 mpaka 45 na kwa wenza wao wa kiume karibu 1,000 kwa kuchunguza taarifa zao kiafya, mtindo wa maisha na mfumo wao wa ulaji – ikijumuisha idadi ya vinywaji venye sukari nyingi wanavyotumia.

Katika uchunguzi huo waligundua kwamba wanawake ambao walikunywa angalau soda moja kwa siku walikuwa wamepoteza uwezo wa kushika mimba kwa asilimia 25 na kwa wanaume uwezo ulikuwa umepungua kwa asilimia 33.

Hata hivyo unywaji wa vimiminika vya kuongeza nguvu ndio ulihusishwa na madhara makubwa zaidi kiafya kwenye uwezo wa kuzaa, lakini unywaji wa juisi za matunda na soda zisizo na sukari ulikuwa na matokeo madogo sana kwenye kusababisha ugumba au utasa.

“Kutokana na kiwango kikubwa cha sukari kinachoingia kwenye miili ya watu ambao wapo kwenye umri mzuri wa kuzaa,’’ utafiti umedai kwamba matokeo ya uchunguzi yaliyotolewa yanaweza kuleta manufaa kwenye afya za watumiaji.’’

View attachment 855426


KUNA mjadala mkali unaendelea kuhusu vinywaji baridi hususan soda, baada ya utafiti wa hivi karibuni kuonesha kuwa soda inaweza kuwa na madhara zaidi kiafya kuliko hata sigara!

Hii inaweza kuwa changamoto nyingine kubwa kumkabili binadamu katika masuala ya afya, kwani makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji baridi yanatumia mabilioni ya dola kila mwaka kujitangaza na kutoa misaada ya kijamii kutokana na mauzo yake bila kutaja madhara ya vinywaji vyao.

Soda inahusishwa na matatizo mengi ya kiafya kwa watoto na watu wazima, yakiwemo matatizo ya kuongezeka unene kupita kiasi (obesity), ugonjwa wa ini (liver disease) na hata tabia za vurugu (violent behavior). Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni, unywaji wa vinywaji baridi mara kwa mara unachangia tabia ya ugomvi kwa asilimia kati 9-15!

Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa nchini Marekani, soda huwekwa ‘fructose' (sukari) nyingi ikiwa katika mfumo wa sirapu (fructose corn syrup) ambayo inaongoza kwa kusababisha magonjwa ya unene, kisukari, ugonjwa wa moyo na magonjwa mengine sugu yanayowakabili Wamarekani wengi hivi sasa na dunia kwa ujumla.

Dk. Mercola, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya lishe asilia na tiba mbadala anasema: " Ninaposema kunywa soda ni hatari sawa na mtu anayevuta sigara au pengine zaidi, siyo jambo la kutia chumvi, bali ndiyo ukweli halisi".

Dk. anaendelea kusema kuwa unywaji wa soda kwa njia nyingi ni mbaya kuliko uvutaji wa sigara, ila kutokana na kampeni kubwa ya matangazo inayofanywa na makampuni haya, inafanya vinywaji hivi vyenye sukari kuonekana havina madhara kwa watu wasio na hatia, hasa watoto wetu!

SABABU KUBWA YA KUIPIGA KIBUTI SODA
Unayesoma makala haya kuhusu madhara ya soda kwa mara ya kwanza bila shaka utakuwa unashangaa na kujiuliza; soda ina ubaya gani? Kwa mujibu wa Dk. Mercola, hakuna sababu yoyote ya kuendelea kunywa soda, labda ujikute uko katikati ya jangwa na hakuna kinywaji kingine isipokua soda!

Kiafya, unywaji wa soda au vinywaji vingine baridi vyenye ‘fructose' una madhara. Unywaji wa kiasi cha kopo moja tu la soda kila siku, utakuongezea uzito wa mwili wa kilo 10 kila mwaka na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari (diabetes) kwa asilimia 85!

‘FRUCTOSE'
‘Fructose' ni kirutubisho kilichomo ndani ya sukari na kiwango kinachowekwa wakati wa utengenezaji wa soda ni kingi kuliko kawaida. Inaelezwa kuwa miaka 100 iliyopita, Mmarekani mmoja alikuwa akitumia kiasi cha gramu 15 ya sukari (fructose) kwa siku, tena kwa kula matunda. Miaka 100 baadaye, (yaani hivi sasa), robo ya Wamarekani wote wanatumia kiasi cha gramu 135 (kutoka 15) kwa siku, tena kwa kunywa soda!

Ulaji wa sukari (fructose) kiasi cha gramu 15 kwa siku hauna madhara kiafya, labda uwe na ugonjwa wa kisukari (high uric acid levels). Hata hivyo, kwa kula sukari mara kumi zaidi ya kiwango cha gramu 15 kinachokubalika kiafya, inakuwa ndiyo chanzo cha unene wa kupindukia na magonjwa mengine hatari yanayoibuka mwilini (degenerative diseases).

Utafiti unaonesha kuwa vinywaji vingi baridi vina sukari nyingi kuliko wastani unaotakiwa. Badala ya kuwa na asilimia 55 ya ‘fructose' na asilimia 45 ya ‘glucose', vingi vina asilimia 65 ya ‘fructose', ikiwa ni karibu asilimia 20 zaidi na inavyotakiwa.

Utafiti zaidi umeonesha kuwa ‘fructose' ndiyo chanzo kikubwa cha tatizo la ugonjwa wa ini kwa watoto wengi nchini Marekani, ingawa hawatumii kilevi chochote (alcohol). Inaelezwa kuwa ‘fructose' huleta madhara kwenye ini kama inavyofanya pombe. juma: JE NI KWELI SODA INA MADHARA KULIKO SIGARA?

1001358_520283921359711_418174972_n.jpg



SODA NI SUMU KATIKA MWILI WA BINADAMU.

AFYA za mamilioni ya Watanzania na watu Duniani kwa ujumla wanaotumia vinywaji vya aina ya soda ipo hatarini, baada ya kugunduliwa uwepo wa chembechembe zenye kemikali za sumu ndani ya vinywaji hivyo,

Utafiti uliofanywa na Muungano wa Waandishi wa Habari za Uchunguzi Tanzania (Investigative Journalists Union of Tanzania- IJUTA) pamoja na tafiti zilizofanywa na wataalamu waliobobea katika afya ya umma duniani, umebaini kuwa vinywaji baridi aina ya soda ni hatari kuliko utumiaji wa sigara inayosababisha maradhi ya kansa katika mwili wa binadamu.


Kwa mujibu wa utafiti wa wanasayansi mbalimbali duniani, yapo madhara makubwa ya utumiaji wa vinywaji vya aina ya soda katika mwili wa binadamu.

Utafiti huo unaonyesha kuwa zipo sababu nane kuu zinazokiweka kinywaji aina ya soda kwenye kundi la vinywaji vyenye sumu ambavyo havifai kwa matumizi ya binadamu.

IJUTA imebaini kuwa makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji baridi aina ya soda yanatumia mabilioni ya dola kila mwaka kujitangaza na kutoa misaada ya kijamii kutokana na mauzo yake, bila kutaja madhara ya vinywaji hivyo kwa binadamu.

Kwamba matangazo hayo yanayogharimu mamilioni ya fedha ndiyo yanayokifanya kinywaji hicho kuwa maarufu zaidi duniani, licha ya kuwa na madhara makubwa katika mwili wa binadamu.

Aidha, utafiti huo unaonyesha kuwa umaarufu mwingine wa kinywaji aina ya soda ni utamu wa kupindukia ulio ndani ya soda.

Utafiti wa IJUTA unaonyesha kuwa utamu wa kupindukia iliomo ndani ya soda unawapumbaza wanywaji ili wasisikie ladha kali ya asidi iliyomo ndani ya soda.

IJUTA imegundua kuwa kiwango cha asidi kilicho ndani ya soda hakiwekwi wazi kwa walaji kwa sababu ya kuhofia kuwa wakibaini wataacha kikutumia kinywaji hicho.

Inaelezwa pia kuwa madini ya cola yaliyo ndani ya soda yana kilevi aina kafein kinachomteka mnywaji kuwa teja wa kinywaji hicho.

Tafiti za kitaalamu zimeonyesha kuwa soda inahusishwa na matatizo mengi ya kiafya kwa watoto na watu wazima, yakiwemo matatizo ya kuongezeka unene kupita kiasi, ugonjwa wa ini na mengineyo.

Utafiti uliofanywa nchini Marekani unaonyesha kuwa soda huwekewa fructose (sukari) nyingi kupitia mfumo wa sirapu (fructose corn syrup) ambayo inaongoza kwa kusababisha magonjwa ya unene, kisukari, ugonjwa wa moyo na magonjwa mengine sugu yanayowakabili Wamarekani wengi hivi sasa na dunia kwa ujumla.

Dk. Mercola, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya lishe asilia na tiba mbadala nchini Marekani, amekaririwa na tafiti mbalimbali zilizofanyika nchini humo akieleza kuwa kinywaji aina ya soda ni hatari kwa binadamu, sawa na mtu anayevuta sigara au zaidi, jambo alilosisitiza kuwa siyo la kutia chumvi, bali ukweli halisi.

Watumiaji wa vinywaji aina ya soda wanaelezwa kuwa wamekuwa wakinywa kiasi kikubwa cha kaboni, kafeini (dawa ya kulevya), sukari ya kupundukia na asidi kali ambayo huvuruga afya ya mtumiaji kwa kiwango cha juu.

Soda pia imebainika kutokuwa na lishe ya aina yoyote zaidi ya maji na sukari.

Uchunguzi wa IJUTA na utafiti ya wanasayansi mbalimbali duniani, umeonyesha kuwa watu wengi hawajui kuwa unywaji wa soda huwaongezea kiasi kikubwa cha madini joto.

Chupa moja ya soda yenye ujazo wa mililita 330 husababisha unene kwa kiwango cha paundi moja kwa mwezi.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kisukari Tanzania (TDA), Ramadhan Mongi, amepata kukaririwa na vyombo vya habari hapa nchini akieleza kuwa ugonjwa wa kisukari Tanzania umeongezeka mara sita katika siku za hivi karibuni.

Alisema miaka kumi iliyopita, hali ya kisukari ilikuwa asilimia tatu (3), lakini katika miaka ya karibuni umeongezeka mara sita.

Tunastahili kuongeza jitihada ya kupambana na gonjwa hili la kisukari kwa gharama zote kwa sababu kisukari ni moja ya magonjwa manne yanayomaliza Watanzania, alisema.

Utafiti uliofanyika Mkoa wa Dar es Salaam ulibaini kwamba kati ya watu watano waathirika wa kisukari, mmoja tu ndiyo hupata matibabu ya serikali.

Unywaji kwa mpigo wa kabohaidrets iliyo na sukari nyingi kwenye soda hudhoofisha seli zinazozalisha vimengenya tofauti na vyakula vingine na pia imebainika kuwa sukari ikiingia kwa wepesi kwenye mzunguko wa damu husababisha kongosho kuzalisha vimengenya vingi mwilini.

Uchunguzi wa kitabibu katika Hospitali ya wanawake ya Boston nchini Marekani na katika Chuo cha Kitabibu cha Harvard umeonyesha wanawake 51,000 hawakuwa na kisukari mwanzoni mwaka wa 1991, lakini miezi minane baadaye wanawake 741 waligundulika na kisukari.

Ripoti ya utafiti huo ilionyesha kuwa wanawake waliokuwa wakitumia kinywaji aina ya soda moja ama mbili kwa siku waliongezeka uzito maradufu na walikuwa hatarini kupata ugonjwa wa kisukari.

Pia ilionyesha kuwa soda hudhoofisha mifupa na husababisha hali ya mifupa kupuputika, hali inayomuweka mtumiaji kuwa katika hatari ya kuvunjika mifupa kirahisi.

Madhara mengine yaliyobainika kusababishwa na unywaji soda ni kupukutika kwa meno na ama kuoza. Pia soda husababisha matatizo ya figo.

Soda yenye chembe ya cola husababisha figo kuwa na mawe kwa sababu ya asidi na kemikali mbalimbali zinazofichwa vipimo vyake kwa walaji.

Madaktari bingwa wa wanamichezo wanaeleza madhara yanayosababishwa na soda mwilini kuwa ni pamoja na shinikizo la damu, uharibifu wa ini, huvurugu mfumo wa kumengenya chakula tumboni kutokana asidi ya kiwango cha juu iliyo kwenye soda.

Wanashauri kuwa soda haistahili kutumika kama kishawishi kwenye mchezo, kwa sababu ina madhara makubwa kwa wanamichezo kwa sababu hunyonya maji kwenye mwili na kudhoofisha mwili.

Wakati utafiti huo ukidhihirisha hayo, Taasisi ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imeshindwa kutoa tamko lolote kuhusu utafiti huo, hata baada ya kupelekewa maswali kwa maandishi yanayoomba ufafanuzi wa ubora wa vinywaji vya soda katika mwili wa binadamu.

Kwa ushauri zaidi tuwasilie, pia matatizo yakizidi muone daktari kwa matibau zaidi.
 
inategemea reaction ya mwili wako. Mi na mountain dew hatupatani maana ni kinywa tu kichwa kiagonga ile mbaya halafu huishiwa nguvu na kujisikia myonge.
 
pia kuna tetesi ya kwamba coka kola sio nzuri kwa wanawake,je?kuna ukweli wowote ktk hilo.
 
Habari wakuu!
Kwa kuelekea moja kwa moja kwenye mada juu ya mountain dew, spirite na seven up it seems they are looking the same hasa ukiangalia colour ya chupa zake ila pamoja na chemical ingeredients zake zina fanana fanana kwa namna ambayo inaleta kitu kinachoitwa SODA ila kuna utofauti ufuatao:

Mountain Dew
hii imeongezewa asilimia kubwa ya caffein hivyo inasaidia kwa wale vijana ambao wanalala lala usiku so it keep somebody too active moreover ina chemicali nyingine iitwayo TARTRAZINE hii si nzuri kwa jinsia ya kiume kwani inaambatana na kupunguza ufanisi so kilaji kinakufanya unakuwa too active but in long run i think might induce trouble. go to wikipedia for more info about TARTRAZINE

seven up and sprite
hizi hazina utofauti sana na zina fanana na Mountain dew kwa kiasi kikubwa ukiondoa hivyo vionjo nilivyovitaja hapo juu pamoja na flavor.


soda is among of junk food so let avoid it!
 
ama kweli " kusoma kuelewa kukesha mbwembwe" haya yote ningeyajuaje kama si JF?
 
kwa hiyo Mountain dew ni sawa sawa na Red Bull ila ni "Lite" ?

sina uhakika sana juu ya usawa sawa wa red-bull na mountain dew am going back for literature review then i will come, but let avoid this junks drinks kwasababu utakapopata proper dose due to frequent using it might be troublesome to you.
 
Mountain Dew ina content ya chemical inaitwa Bromide ( a drug used to calm people who are very unhappy or worried!!!!!

Mkuu kuna uhakika wowote juu ya uwepo wa bromide katika mountain dew? i guess it might be typing error or otherwise tupatie mashiko/reference juu ya uwepo wa bromide maana i have interest with this claim!
 
Kwa ujumla vinywaji vyote hivyo vya viwandani vina madhara kwa afya ukifinywa mara kwa mara, turudi kweny vinywaji vyetu vya asili kama vile Togwa, Kimpumu.nk....
 
Kwa ujumla vinywaji vyote hivyo vya viwandani vina madhara kwa afya ukifinywa mara kwa mara, turudi kweny vinywaji vyetu vya asili kama vile Togwa, Kimpumu.nk....

dont tell us to start bwiaring alcohol my take let consume large amount of fresh water and particularly spring water i will recommend it!
 
Ukweli fizzy drinks sio nzuri kwa afya yako, niliwahi kusoma article moja inayotoa maonyo kwa teenagers wa kike kua kinywaji kama coke kinaharibu mifupa, kinafanya mifupa kua dhaifu. Kuna watu hutumia soda kama sprite/7-Up kulainisha nyama iwe laini kabla ya kufanya BBQ au kupika, je ikiwa ni hivyo mwilini mwako inakuaje? Kuhakikisha kama vinywaji hivi vina madhara mwaga coke kwenye sakafu uone lile baka linaloachia. Kubwa zaidi, unaweza kusafishia choo cha kuvuta "flush"...mwaga chupa zima la coke usiku, ukiamka asubushi choo saaafi....sasa fikiria mwilini mwako inafanya nini? Hapa napenda kutoa ushauri zaidi kwa wenye watoto wajaribu sana kuwaepusha na utumiaji wa hizi fizzy drinks zote; kama hakuna juice basi bora mpe mwanao maji!
 
Back
Top Bottom