Madhara ya nguzo za simu kwa afya za watu

Boney E.M.

JF-Expert Member
Jan 22, 2007
425
35
Tanzania tunazo nguzo nyingi za simu zilizojengwa na makampuni ya simu lakini suala na madhara yake halijawekwa bayana wakati tunavyo vyombo husika kama TCRA. Inashangaza na kuona kwamba wananchi wako katika hatari kubwa ya madhara ya kiafya bila hatua za haraka kuchukuliwa. Imebainika katika utafiti uliofanywa huko Botswana na katika maeneo mengi kama nane yaliofanyiwa utafiti duniani, watu wanaokaa karibu na nguzo za simu wanapata madhara ya kiafya kama kuumwa sana na kichwa, uchovu mwingi, kutopata usingizi mzuri, matatizo ya tumbo, shinikizo la damu, mapigo ya moyo kutokuwa sawa, kiungulia, matatizo ya ngozi, kupoteza kumbukumbu, upungufu wa kinga mwilini, maungo kuuma, kizunguzungu, kansa, kifafa n.k.

Tanzania ina tabia ya kudharau tafiti kama hizi na pindi zinapoongelewa kama Bungeni utaona mazungumzo yanapotoshwa na wahusika wakati wananchi wanaendelea kudhurika. Kuna haja ya taarifa kamili kutolewa na TCRA pamoja na serikali kuhusu madhara ya nguzo za umeme karibu na makazi ya watu.

Kwa kuwa tafiti zilifanywa huko Afrika Kusini, Ujerumani, Austria na Israel zimeonyesha matokeo yanayofanana hususan magonjwa hayo serikali ionyeshe nia ya wazi ya kuwakinga wananchi wake.

Nukuu: The Guradian, 20 October 2009, page (iii)
 
Wala halinitishii.. kuna mambo mengi utaambiwa yana sababisha uliyo yataja na ndo maisha yetu ya kila siku. Bwana am tired wacha tufe tu si tunaenda kwa mola kwenye raha teleee!!
 
Tanzania tunazo nguzo nyingi za simu zilizojengwa na makampuni ya simu lakini suala na madhara yake halijawekwa bayana wakati tunavyo vyombo husika kama TCRA. Inashangaza na kuona kwamba wananchi wako katika hatari kubwa ya madhara ya kiafya bila hatua za haraka kuchukuliwa. Imebainika katika utafiti uliofanywa huko Botswana na katika maeneo mengi kama nane yaliofanyiwa utafiti duniani, watu wanaokaa karibu na nguzo za simu wanapata madhara ya kiafya kama kuumwa sana na kichwa, uchovu mwingi, kutopata usingizi mzuri, matatizo ya tumbo, shinikizo la damu, mapigo ya moyo kutokuwa sawa, kiungulia, matatizo ya ngozi, kupoteza kumbukumbu, upungufu wa kinga mwilini, maungo kuuma, kizunguzungu, kansa, kifafa n.k.

Tanzania ina tabia ya kudharau tafiti kama hizi na pindi zinapoongelewa kama Bungeni utaona mazungumzo yanapotoshwa na wahusika wakati wananchi wanaendelea kudhurika. Kuna haja ya taarifa kamili kutolewa na TCRA pamoja na serikali kuhusu madhara ya nguzo za umeme karibu na makazi ya watu.

Kwa kuwa tafiti zilifanywa huko Afrika Kusini, Ujerumani, Austria na Israel zimeonyesha matokeo yanayofanana hususan magonjwa hayo serikali ionyeshe nia ya wazi ya kuwakinga wananchi wake.

Nukuu: The Guradian, 20 October 2009, page (iii)

Uhusiano Baina ya Mionzi Itokayo Kwenye Vyombo vya Mawasiliano ya Simu na Utangazaji na Afya ya Binadamu
Miaka ya hivi karibuni hapa nchini Tanzania na seheme nyingine duniani kiwango cha matumizi ya vyombo vya habari na mawasiliano, ikiwa ni pamoja na simu,minara ya mawasiliano, radar, redio, televisheni, kompyuta na kadhalika kimeongezeka sana. Matumizi yamefanya wananchi wengi kujiuliza uhusiano wa vyombo vya mawasiliano na afya zao.

Kwa kuzingatia maoni mbali mbali yaliotolewa na wadau wa mawasiliano na wananchi kwa ujumla Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:

  1. Mionzi inayotoka kwenye vyombo vya mawasiliano kama vilivyotajwa hapo juu yapo kwenye kiwango cha chini sana kuweza kumdhuru binadamu. Kiasi cha mionzi hiyo ni sawa na kile kilichothibitishwa na mashirika mbali mbali ya kimataifa kufuatia utafiti uliochukua takriban miaka 50. Mashirika yaliyohusika katika utafiti huo ni pamoja na:
    • Shirika la Umoja wa Mataifa la Mawasiliano ya Simu (International Telecommunications Union - ITU);
    • Shirika la Afya Ulimwenguni (World Health organization - WHO);
    • Tume ya Kimataifa ya Kinga Dhidi ya Mionzi (International Commission on Non-ionizing Radiation Protection - ICNIRP)
    • Chama cha Mawasiliano ya Simu za Mikononi (GSM Association);
    • Muungano wa Watengenezaji wa Simu za Mikononi (Mobile Manufacturers Forum - MMF).
  2. Ziko taarifa nyingi sana zitokanazo na utafiti wa kisayansi juu ya athari za
    masafa (the radiofrequency-RF) kwa afya ya binadamu. Kipimo cha jinsi mionzi inavyoingia kwenye mwili wa binadamu huitwa “Specific Absorption Rate (SAR)”. Taarifa hizo zinaonyesha kuwa nguvu ya mionzi ipo chini ya kiwango fulani (threshold) hayana athari kwa mwili wa binadamu. Nguvu za mionzi hupungua toka chanzo cha mionzi hiyo (inverse sqruare law). Kutokana na utafiti wa ICNIRP na ITU, SAR ni Watt 2 kwa uzito wa kilo moja (2 W/kg kwa kichwani na kiwiliwili) na Watt 4 kwa uzito wa kilo moja (4 W/kg kwa miguuni na mikononi) kwa umma na vipimo vikubwa zaidi ya haivyo kwa wafanya kazi wa mawasiliano wakiwa kwenye mitambo ya mawasiliano.
  3. Mawimbi ya umeme na sumaku (electromagnetic waves) yako ya aina nyingi, kwa mfano: mawimbi ya radio, mawimbi ya microwave, infrared, mwanga wa kawaida, ultraviolet, X-ray, gamma rays(mawimbi yatokanayo na nuklia), na kadhalika. Kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali lililoambatanishwa na maelezo haya, nguvu ya mionzi ya redio iikiwa ni pamoja na simu ya mkononi ni kidogo ikilinganishwa na mwanga unaoonekana kwa macho. Vyanzo vya mionzi hii huweza kuwa ama vya asili au mitambo mbali mbali. Minara ya mawasiliano huwa na urefu wa mita 15 hadi 50 au kwenye majumba marefu, kwa hiyo nguvu inayomfikia binadamu ni ndogo.
  4. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekuwa ikifanya jitihada kushawishi watoa huduma za mawasiliano na utangazaji kushirikiana kutumia minara (infrastructure sharing). Hatua mojawapo iliyochukuliwa ni kutoa mfumo mpya wa leseni (Converged Licensing Framework) ambao una leseni nne: Leseni ya miundombinu (Netwwork Facility License), Leseni ya kutoa huduma (Network Service License), leseni ya matumizi (Application Service License) na leseni ya utangazaji (Content Service License). Vile vile Mamlaka imetoa kanunu za mawasiliano za 2005 ambazo zinawashawishi watoa huduma kujenga minara na kukodisha wa wengine badala ya kila mmoja kuwa na mnara wake mwenyewe.
  5. Kuna tafiti nyingi zimefanyika ambazo zimeonyesha kwamba kiwango cha
    mawimbi ya mawasiliano hakina madhara kwa afya ya binadamu. Mamlaka inashauri watumiaji wa huduma na wananchi wote kuendelea kuwa na imani na teknolojia mpya ikiwemo ya mawasiliano ya simu, utangazaji na utumiaji wa kompyuta ambazo hutumiwa ulimwenguni kote bila kuleta madhara yoyote. Maelezo haya yametokana na tafiti mbalimbali na maelezo mengine imebidi kutumia lugha ya kitaalamu. Iwapo yatahitajika maelezo zaidi au kama kuna malalamiko yoyote kuhusu mawasiliano, Mamlaka ipo tayari kutoa ufafanuzi na kuyafanyia kazi maswala yote.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania

Kwa habari zaidi tembelea www.tcra.go.tz

Ukielewa elewesha na wengine mkuu
 
Back
Top Bottom