MWILI NYUMBA
JF-Expert Member
- Jun 18, 2012
- 817
- 255
Diaspora ya Ghana inashikilia nafasi ya tatu kwa uchumi wa nchi hiyo; ya Nigeria ni ya nne kwa kuchangia uchumi wa nchi hiyo, vivyo hivyo kwa Uganda. Hapa kwetu badala ya kuweka mazingira mazuri kwa walio nje ya nchi kuchangia uchumi wa nchi yetu kama ilivyo kwa nchi za wenzetu, kwa ujuha wetu tunaziba hata kile kidogo kilichokuwa kinapatikana! Tumekwisha.
Mkuu wabongo wengi waliopo nje ni wabeba maboksi na wanafunzi,sasa unategemea bongo wafanye uwekezaji gani? Kwaninavyoiona bongo na ka experience kadogo nilikonako kakukaa nje ya nchi wengi waliopo ughaibuni elimu yao si kubwa kivilee so kazi zao ni za kuungaunga tu tofauti sana na wenzetu wa Afrika magharibi na kwingineko ambapo kwa upande wao wasomi ndiyo wanaokimbilia nje ya nchi kutokana na uhaba wa ajira.