- Thread starter
- #21
Hana mpya huyo. Kakurupuka tu na hiyo info kutoka ABC bila ku-digest. Tunamsaidia kumpiga shule analeta ubishi. Nikagundua kuwa nasomesha degree kwa mtoto wa miaka minne! Nimem-shit na elimu yake finyu ya minyoo. Isitoshe akienda lab huyo, anaweza kutwa na hiyo minyooo....
Mwanjelwa umeplay hiyo video ya ABC ukamsikia Doctor anavyoongea?, click kwenye hiyo picha ya huyo dada kama Internet yako ina-speed ya kutosha usikie Dr. Anasema nini.
Kitu unachotakiwa kufahamu ni kuwa "Nguruwe ni hatari" kwa afya yako. Sasa mimi sijahoji uhalali wa mtu kula nguruwe unapokula ujue kuwa unaweza kuwa unahatarisha maisha yako.
Ninajua pengine utakuwa na moyo mgumu kukubali hali halisi huenda kutokana na mazoea au tabia uliyojijengea ya kumla mnyama huyu, hilo usihofu huenda bado hujaathirika cha muhimu ni kuchukua tahadhari.
Unajua hii imekuwa kama vile mtu ukipima HIV ukakutwa ni positive huwa inakuwa tabu mwanzo kuamini kama vipimo vinasema kweli ila baadae unakuja kukubali kuwa ni kweli hawa jamaa wapo mwilini mwangu.
Sijasema kwamba wala kitimoto wote wana minyoo kwenye brain, la hasha ila ninachosema ni kwamba utamaduni wa kula huyu mnyama tena kwa mazingira kama ya bongo ambao hata ufugaji wake ni tata na utayarishaji wake wa kwenye ma-bar ambako order zinakuwa nyingi kuliko uwezo wa processor kuna hatari ya kujikuta unapata madhara in a long ran. Sasa kubali kataa ukweli ndiyo huo kuhusu "Pork".