Madereva wa Magari makubwa ya Mizigo yanayokwenda nje ya nchi wamegoma Siku ya Nne leo

msaragambo

Senior Member
Aug 6, 2008
127
17
Kuna mgomo baridi wa Madereva wa magari makubwa ya Mizigo yanayokwenda nje ya nchi t siku ya Nne sasa na Hakuna taarifa zozote Rasmi kutoka Vyombo husika

Mgomo huu unatokana na madai ya Madereva ya muda mrefu dhidi ya Wamiliki wa Magari,TRA,unyanyasaji wa Askari barabarani na Tanroad kwa upande wa mizani

Madera waliandika Barua Ofisi ya Waziri Mkuu kupeleka Malalamiko yao Juu ya Kero zao na kueleza dhamira yao ya Kugoma ndani ya siku 40 kama madai yao hayatasikilizwa, mpaka mgomo unaanza tarehe 17july 2011 hakuna Majibu yeyeto yaliyotoka juu ya Madai yao

Kulifanyika Mkutano jana Kati ya Mkuu wa Mkoa,Mkuu wa Wilaya,wawakilishi wa Police,TRA katika kujaribu kutafuta suluhu ya Madai ya Madereva lakini walishindwa kupata muafaka mara baada ya Mkuu wa Mkoa Mh Mwakipesile kutaka kutumia Nguvu Na Ubabe badala ya kuyatafutia Ufumbuzi Madai ya Madereva

Mkuu wa Mkoa aliwaambia Madereva anayetaka kuendesha Gari aendeshe na asiyetaka aache,Kauli hiyo iliwakasirisha madereva waliokua wanamsikiliza na kusababisha Mkutano Kuvunjika

Source Mimi mwenyewe
 
ndugu wadau! Mimi binafsi na mtaalamu wa mambo ya usafirishaji ,logistics, lakini kwa kweli hali ya madereva wa magari naweza sema yote kwa ujumla ni mbaya sana, maanake wanachukuliwa kama dei waka fulani, mtu anafanya kazi miaka kibao hakuna mkataba wala nini, na matokeo yake hakuna ppf wala nssf, hata akipata ajali matibabu ni shida na kama umevubjika kiungo hiyo ndio imekula kwako.

Huu ni wakati muafaka wasimame kidete ili haki zao zitekelezwe na haki ikipatikana naamini hata ajali zitapungua sana kwa sababu watakuwa na motivation ya kazi na future yao na familia yao


madereva mi nawasihi kazeni buti mpaka kieleweke

wananchi tupo nanyi
 
Hata mimi naungana nao ,pesa zote zinaishia mifukoni mwa wenye malori madereva wanabaki Maskini



ndugu wadau! Mimi binafsi na mtaalamu wa mambo ya usafirishaji ,logistics, lakini kwa kweli hali ya madereva wa m
agari naweza sema yote kwa ujumla ni mbaya sana, maanake wanachukuliwa kama dei waka fulani, mtu anafanya kazi miaka kibao hakuna mkataba wala nini, na matokeo yake hakuna ppf wala nssf, hata akipata ajali matibabu ni shida na kama umevubjika kiungo hiyo ndio imekula kwako.

Huu ni wakati muafaka wasimame kidete ili haki zao zitekelezwe na haki ikipatikana naamini hata ajali zitapungua sana kwa sababu watakuwa na motivation ya kazi na future yao na familia yao


madereva mi nawasihi kazeni buti mpaka kieleweke

wananchi tupo nanyi
 
Jama! Madereva hao wamefikia wapi? Ningependa nisikie wamegoma nchi nzima kwani hw jamaa wanalipwaga pesa ndogo sana. Hawa matajiri hawana utu.
 
Hakuna kinachoendelea asubuhi Police walitaka kutumia nguvu kuvusha magari ya Mafuta yaliyo Mpakani mwa Tanzania na Zambia lakini madereva wakatishia kuchoma Moto magari kama kutatokea matumizi ya nguvu wakafanikiwa kuvusha gari moja tu la Kampuni ya Asas

Serikali ya Zambia inajitahidi kumaliza mgomo kwakuwa wameanza kupata Upungufu wa Mafuta ya Diesel Na Petrol


Jama! Madereva hao wamefikia wapi? Ningependa nisikie wamegoma nchi nzima kwani hw jamaa wanalipwaga pesa ndogo sana. Hawa matajiri hawana utu.
 
Back
Top Bottom