Naambiwa kuna basi la kusini liliondoka wadau wamelifukuza wamemtandika dereva yuko hoi na vioo wamevunja
hii safi sana,huu ndio mwanzo wa kuwapo na ajira rasmi ya udereva kwenye makampuni binafsi,wamezidi kunyanyasika.pia walazimishe bei ya mafuta kushuka.
usimtishe bana, lazima watanzania tuzienzi lugha zetu
Hili la kushinikiza bei ya mafuta ishuke hawatoliweza wao peke yao. kinachotakiwa sisi sote wenye magari walau kwa hapa dar tuungane na kufanya mgomo, wa ukweli tena tukiwa na mshikamano sisi sote, tufanye mgomo wenye manufaa utakaozaa matunda.
Tatizo watu wengi japo bei imepanda, wakijiangalia wao wanauwezo wa kumudu, hivyo wakisikia kugoma wala hawajisumbui, wanaona kama haiwahusu vile, ukweli ni kuwa bei ya mafuta inaumiza sana ss 2,200, tunahitaji suluhisho la kudumu la kushusha bei hii inayoelekea kushindikana kulipika, though hadi sasa sijui ni nani atakaefanikisha hili.........
Yameanza kutoka saa saba kasoro, na madai yako yatajadiliwa zaidi siku ya jumanne! Sipati picha spidi yake huko njiani!
Umoja ni jambo la msingi kwani niliona nikisema na sisi wenye magari DSM tugome kuweka mafuta tutakuwa mimi na wewe tu,wengine wanazo za wizi hawajali kwanza watatushangaa wadanganyika hatuna nguvu hiyo tupo kwenye matabaka.Nashangaa nchi nyingine wanashirikiana sana.
Hapo sijagusa mfumuko wa bei wa vyakula na kila kitu kingine unachotakiwa kutumia hapa duniani. Halafu mtu anakuajiri anakuambia nitakulipa Shs. 400,000 gross pay, aaaaaaaah bora akae na hela yake me ntahangaika tu mtaani ntaipata hiyo, maana nikiifikiria naweza kulia bure,
Hayo mabasi ni majeneza yenye magurudumu. Mengi yake yana hali mbaya sana na hayastahili kutumika kusafirishia watu hata kidogo. Lakini kwa umaskini wa mali tulionao hiyo hali hata hatuioni. Ama tunaona ni sawa tu kuyatumia au kwa vile hatuna jinsi basi inatubidi tukubaliane tu na hali halisi.
Umaskini mbaya sana.
Kwa hali hiyo tumuombe mungu ili atuepushe na balaa manake watataka kufika mapema na huku wameumana yaani wanafukuzana!! Tuwaombee tu safari njema. Mimi nimeahirisha kusafiri
msijisahau, mtandao wa watu huu. Nyie mnazungumza lugha yetu wakati wengine hawaelewi. Mtapigwa "ban" kama ya Mchungaji Father.
Mkuu haupo sirias kabisa, medical attendant analipwa 135,000/- pm, CO anayeanza si zaidi ya 350,000/-, mwalimu? polisi?
Naamini haupo katika level hii tuliopo sisi wengine (mimi ni mwalimu) lakini hiyo laki nne usiyoitaka sisi ndio bado tunaifanyia bargain!