Madereva wa Mabasi yaendayo mikoani tokea Ubungo wamegoma!

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
May 23, 2008
1,932
985
Madereva wamegoma wakidai maslahi yao. Hali ni kizungumkuti. Hakuna usafiri kwenda mikoani. Kamanda Kova anahitajiwa Ubungo lakini bado hajafika. Vibaka nao wanaongeza juhudi za mawindo.

Souce: Ndugu yangu anayesafiri kwenda mkoa wenye vinono include ulanzi (NJOMBE)
 
Nipo kwene HOOD naenda Moro, tupo tangu saa kumi na mbili asubuhi, hakuna basi liilitoka hadi sasa!!! Hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa hadi sasa, tunauza sura tu! No Cover (Kova) no what, na hata akija sioni dalili ya hawa jamaa kulegeza msimamo wao!
 
Mambo yanazidi kuwa magumu, madereva wamekomaa hapa, hawataki kuondoka wanachotaka ni Meneja wa kituo aondoke! Kaazi kweli kweli
 
duh, naomba ajenda yao nyingine iwe kushuka kwa gharama za wese, iwe kama kenya vile 1350 Tsh
 
Mpaka sasa hakuna dalili yoyote, hakuna kiongozi yoyote wa Manispaa, wala mkuu wa wilaya aliefika hapa, hii ndio Bongo, maskini traffic leo hawataambulia hata senti tano za rushwa maana madereva wanaonekana wako more serious than ever!!!
 
Wadau mliopo ubungo Bus Terminal tupeni taarifa hao madereva wana madai gani hasa. Wameorodhesha madai yao? Tupeni update manake wengine tuna safari mida ya saa saba
 
Nipo Ubungo: Wanadai posho ndogo, hawana NSSF, wanasumbuliwa na Traffic, hawamtaki Meneja wa kituo, KIBAHA nako malori yameziba njia, nao wana mgomo
 
Wametangaza mabasi yote yaondoke, asietaka abaki!! NDIO mabasi yamewashwa!
 
Nipo Ubungo: Wanadai posho ndogo, hawana NSSF, wanasumbuliwa na Traffic, hawamtaki Meneja wa kituo, KIBAHA nako malori yameziba njia, nao wana mgomo

Wanamadai ya msingi tatizo timing (muda mwafaka) ya kuyafanya ndiyo tatizo. Impact yake kwa leo si kubwa kama ukilinganisha endapo yangefanyika jana ama siku ambayo hawa viongozi wanasafiri.
 
Yes, magari yamewashwa but dk zaidi ya kumi na tano zimepita hakuna basi lililotoka! Sijui kuna mchezo gani, ngoja kwanza niangalie kama ni foleni ya nje au ni mgomo wa kimya kimya unaendelea!!
 
Nipo Ubungo: Wanadai posho ndogo, hawana NSSF, wanasumbuliwa na Traffic, hawamtaki Meneja wa kituo, KIBAHA nako malori yameziba njia, nao wana mgomo

Haya ni madai sahihi kabisa. Hawa nao ni binadamu nao wanastahili haki na mazingira bora ya kazi
 
Poleni sana ndugu zetu wasafiri hasa wendugu unaenda kwenye ViNONO njombe umenikumbusha mbali kiongozi "miguhu,misaula,ing'owo,inyatwanga,amasebele,ing'ande nk Vahungila mbevali kwilinga na vamwibata, vamwamdeke,vamwangimba,vamwalumato,vamwakalinga,vamwamuyinga, na vasegito mbevali!!!
 
Poleni sana ila fani udereva hapa tanzania inachukuliwa kama watu ambao walikuwa hawana pa kwenda pale wamejishikiza tu!
 
Kova amefika wanazungumza, mabasi mawili yaliyolazimisha kutoka yamevunjwa vioo, kibaha nako bado kwa moto....hakuna muafaka uliofikiwa!
 
Ni ukweli usiopingika kuwa madereva wanalipwa posho kidogo. Ni kweli pia wengi wao hawajaajiriwa na hawana mikataba ya kazi. Hawana maslahi yeyote kiujumla. Hata wakiugua wengi wao huishia kufukuzwa kazi maana huna manufaa tena na mwenye gari.
wangedai:-
1. Mikataba ya ajira
2. Mazingira mazuri ya kufanya kazi
3. Pensheni
4. Huduma muhimu kama matibabu nk.

Pia nao madereva waache ujinga wa kufanya kila watakalo matajiri wao! Mfano uendeshaji kwa speed wala sio madereva peke yao ni maagizo toka kwa mabosi wao. kama hujui kukimbiza gari na kuwahi then wewe hufai! Na wao bila aibu wanafata maagizo bila kujiuliza.
Wajue kuwa hii ni taaluma kama zilivyo taaluma nyingine. Wakiiheshimu na waajiri wao watawaheshimu pia.
 
Kinachoendelea ni mazingira ya vurugu....nje kuna FFU, matangazo yamekua mengi na sasa wanatangaza wamiliki wa mabasi waende kwenye ukumbi!!!
 
Back
Top Bottom