Madenti wachangishana 2,000 kukodi walimu!

binti ashura

Senior Member
Jan 14, 2011
118
19
Madenti wachangishana 2,000 kukodi walimu!

Wakati tukiwa tunaaambiwa serikali ya JK inafanya kila jitihada ilimradi kuongeza idadi ya walimu mashuleni, hali ni tete ktk shule ya sekondari ya King'ong'o ya jijini Dsm....ambapo baada ya kukosekana kwa walimu....madenti wa skonga hilo wamefikia hatua ya kupiga doneee (kujichangisha) kiasi cha shilingi 2,000 kwa kila denti kwa mwezi ili waweze kukodi walimu wa kuwapa nondo (kuwafundisha).

Akizungumzia walimu hao wa kukodi,Diwani wa Kata ya Saranga, Ephraim Kinyafu,alisema wanawakodi walimu ambao wamemaliza kidato cha sita na wengine kutoka shule binafsi.

Hata hivyo, amesema hadi sasa walimu hao waliomaliza kidato cha sita tayari wameshaenda vyuoni na hivyo kuiweka shule hiyo kuendelea kuwasaka wengine kujaribu kutatua tatizo hilo.

“Nimelichukulia tatizo hili kama janga na ndiyo maana nimewaomba madenti kushiriki kutatua tatizo hili ambapo nimeona afadhali tuchangishane sh. 2,000 kwa kila denti kwa kila mwezi ili tuzitumie kuwakodi walimu kwa ajili ya kunusuru tatizo hili,” amesema Kinyafu.

source: Madenti wachangishana 2,000 kukodi walimu!

kwangu naona wanafunzi hao wamechukua uamuzi wa msingi ila najiuliza je kule kijijini itakuwaje?
 
Hivi kwa nini wanafunzi wa UDSM - education na wengineo wakali wa science, law & engineering wasichukue hizo part time kuokoa taifa na kujiongezea boom!

Na hii ni kwa kwa shule zote zilizo karibu na vyuo
 
una mawazo mazuri mkuu.
Tatizo Wanafunzi wengi mabishororo na wengine inawezekana hawazioni hizo fursa.
 
Wanastahiki Kupongezwa kwa jitihada zao za kukodi walimu...ni vyema wamebaini kuwa serikali yao haikerwi na ziro wanazopata.
 
Hivi kwa nini wanafunzi wa UDSM - education na wengineo wakali wa science, law & engineering wasichukue hizo part time kuokoa taifa na kujiongezea boom!

Na hii ni kwa kwa shule zote zilizo karibu na vyuo
Hofu yangu ni kuwa wanaweza wakaibuka walimu feki ambao sio wanachuo.
Watu wana mbinu bana!
 
Madenti wachangishana 2,000 kukodi walimu!

Wakati tukiwa tunaaambiwa serikali ya JK inafanya kila jitihada ilimradi kuongeza idadi ya walimu mashuleni, hali ni tete ktk shule ya sekondari ya King'ong'o ya jijini Dsm....ambapo baada ya kukosekana kwa walimu....madenti wa skonga hilo wamefikia hatua ya kupiga doneee (kujichangisha) kiasi cha shilingi 2,000 kwa kila denti kwa mwezi ili waweze kukodi walimu wa kuwapa nondo (kuwafundisha).

Akizungumzia walimu hao wa kukodi,Diwani wa Kata ya Saranga, Ephraim Kinyafu,alisema wanawakodi walimu ambao wamemaliza kidato cha sita na wengine kutoka shule binafsi.

Hata hivyo, amesema hadi sasa walimu hao waliomaliza kidato cha sita tayari wameshaenda vyuoni na hivyo kuiweka shule hiyo kuendelea kuwasaka wengine kujaribu kutatua tatizo hilo.

“Nimelichukulia tatizo hili kama janga na ndiyo maana nimewaomba madenti kushiriki kutatua tatizo hili ambapo nimeona afadhali tuchangishane sh. 2,000 kwa kila denti kwa kila mwezi ili tuzitumie kuwakodi walimu kwa ajili ya kunusuru tatizo hili,” amesema Kinyafu.

source: Madenti wachangishana 2,000 kukodi walimu!

kwangu naona wanafunzi hao wamechukua uamuzi wa msingi ila najiuliza je kule kijijini itakuwaje?

Huu ndo mtaji wa mabadiliko ya kweli 2015. Hata mtu akiwaletea usanii somo halitaeleweka. Cjui na hili watalalamikia CDM?
 
Back
Top Bottom