BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,011
Date::9/17/2009Mtoto wa Nyerere ashauri Kikwete aache kutoa muda wa mafisadi kupumuaNa Ramadhan Semtawa
Mwananchi
MADARAKA Nyerere, mtoto wa kiume wa Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere, ameonya kuwa kama uongozi wa juu wa nchi hautakuwa na msimamo, vita dhidi ya ufisadi haitakwisha na hali ya umasikini itazidi kuwa mbaya kwa Watanzania wengi.
Onyo hilo la mtoto huyo wa rais wa serikali ya awamu ya kwanza, limetolewa katika kipindi ambacho taifa liko kwenye maandalizi ya kuadhimisha miaka kumi ya kifo cha muasisi huyo wa taifa itakayokuwa Oktoba 14.
Mwalimu Nyerere alifariki Oktoba 14, 1999 akiwa Hospitali ya Mtakatifu Thomas nchini Uingereza ambako alikuwa amelazwa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana katika mahojiano maalumu na gazeti hili, Madaraka ambaye hupenda kuzungumza kwa upole na umakini, aliweka bayana kwamba, kiongozi wa juu wa nchi, lazima awe na msimamo na ajipambanue kwa marafiki zake wa karibu ili wasimchezee.
Kwanza, kabisa ingawa watu wanasema hivi na vile, lakini jambo la msingi kiongozi wa juu wa awe na msimamo, alisema Madaraka.
Mwalimu (Nyerere), alikuwa akifanya mambo ambayo wengine walikuwa wakikataa, lakini alikuwa ana maamuzi yake kichwani kama kiongozi ambayo alikuwa akiyasisimamia. Hili ni jambo la lazima.
Alifafanua kwamba katika vita ya ufisadi kumekuwa na siasa zaidi kuliko vitendo na kwamba ushahidi unaangaliwa kwa mtazamo wa kimahakama zaidi kuliko wa kimazingira.
Madaraka alisema wakati wa Mwalimu Nyerere, mtu akishukiwa kwamba ni mlarushwa, jambo la kwanza kama ni kiongozi wa serikali lilikuwa ni kungolewa katika wadhifa wake.
Mwalimu... akipata taarifa kwamba, unahusishwa na harufu ya rushwa, jambo la kwanza anakungoa au anakutaka ujiuzulu na kukwambia wewe utatuharibia serikali, alisisitiza.
Madaraka aliongeza kwamba jambo la pili ambalo lilikuwa likifanywa ni mtuhumiwa wa rushwa kuchunguzwa akiwa nje ya kazi na kufikishwa mahakamani.
Kwa hiyo, jambo la kwanza kiongozi wa juu wa nchi anapaswa kutumia mamlaka ya kuteua na pia katika kumngoa mtu ambaye hafai bila kuangalia ni rafiki au la, alisisitiza.
Tayari Rais Kikwete ameshaeleza bayana kuwa katika vita hiyo hana rafiki wala ndugu baada ya kuwepo lawama nyingi kuwa serikali inashindwa kuwashughulikia baadhi ya watuhumiwa kwa kuwa ni marafiki zake wa karibu.
Kikwete pia alisema kuwa mafisadi ni wajanja sana na hivyo inakuwa ni vigumu kuwagundua na kuwafikisha mahakamani.
Lakini Madaraka alisema wakati mwingine ushahidi wa kimahakama ni mgumu zaidi kuliko wa kimazingira.
Mfano leo hii wewe ndugu tulikuwa wote, (anamtaja rafiki yake) tumekuja Maelezo (Idara ya Habari) kuitisha mkutano bila kutoa hata soda, halafu kesho na keshokutwa uwe na gari kama (Range Rover) Vogue, katika mazingira hayo lazima uchunguzwe, alisisitiza.
Madaraka alionya kuwa hali ya kutodhibiti ipasavyo mafisadi imesababisha kuongezeka kwa pengo kubwa la masikini na matajiri wachache.
Makongoro aliweka bayana akisema: Siku hizi kuna kakundi kadogo (alitumia kidole kusisitiza udogo wake kwa mwisho wa kucha), ambako kana pesa nyingi kweli wakati Watanzania walio wengi ni masikini wa kutupa.
Kuna mtu leo hii anaweza kuja na kukuomba Sh1,500 ya kula chakula ukashangaa... hali ni mbaya huku, lakini wengine wana utajiri wa kutisha.
Alipoulizwa mtazamo wake kuhusu uongozi wa serikali ya awamu ya nne katika kupambana na ufisadi, alijibu: Bado safari ni ndefu sana.
Madaraka alisema ingawa serikali imekuwa ikichukua hatua, lakini hali bado ni mbaya kwani hakuna sababu kwa nchi kama Tanzania kuwa na umasikini wa kutisha wakati ina utajiri mkubwa.
Madaraka alisema wakati wa utawala wa baba yake, kulikuwa na uzalendo wa hali ya juu ambao alisema ulitokana na Watanzania karibu wote kuwa sawa na kukosekana matabaka.
Wananchi hawakuwa na pesa kweli na viongozi wa juu nao hawakuwa na utajiri; watu walikuwa sawa. Lakini leo hii kuna kakundi kadogo kana utajiri halafu kundi kubwa liko katika umasikini wa kutisha hii ni mbaya, alisema.
Kuhusu nia ya Rais Kikwete kuweka sheria ya kuzuia wafanyabiashara kushiriki katika siasa, Madaraka alisema: Kama ni suala la kutenganisha siasa na biashara, unasema tu hatutaki.
Sasa hivi haya mambo ya kuruhusu siasa na biashara ndiyo tunasikia mara kampuni hii ya fulani, kiongozi gani sijui. Alisema uamuzi wa kutenganisha siasa na biashara ulikuwa msingi mkuu wa Azimio la Arusha la mwaka 1967, kabla ya kuvunjwa mwaka 1990 na kuundwa Azimio la Zanzibar ambalo liliruhusu wanasiasa kufanya biashara.

Last edited by a moderator: