Madaktari wote waliogoma kufukuzwa kazi na utumishi!

Serikali imechelewa sana kufanya hayo maamuzi wakawafukuza kipindi kile sasa hivi tumeshawazoea madokta wa Wa Cuba,Kichina na Kihindi Ching Chong Wu
 
LIWALO NA LIWE ni vita kali kati ya Madaktari na Serikali...
Kwa kauli hii hapo kwenye RED serikali imeonyesha udhaifu mkubwa na failure ya wazi na tutarajie waki behave kama Al-asaad wa Syria na Ghaddafi dhidi ya raia wake simply because watu wanataka haki yao na hutaki kuwapa kisa HUTAKI TU!.
 
HUYU ALIYEANZISHA HII THREAD NADHANI ALIKUWA NA HAMU YA KUANDIKA TU.

SERIKALI HUWA HAIFANYI MAAMUZI KWA VIGEZO VIFUATAVYO:-

(a) CHUKI;
(b) PUPA;
(C) Hasira.

Serikali huangalia kila swala kwa marefu na mapana na hutoa uamuzi kwa kuzingatia maslahi ya taifa. Kamwe haiwezi kukurupuka kuwafukuza madaktari wote.

Serikali inahitaji saana kukaa mezani na madaktari wakajadiliane.

Kila Mtanzania ana wajibu wa kuchangia kuijenga TANZANIA
 
sasa hiyo hela watakayotumia kuwalipa hao madaktari wa nje si bora watumie hiyo hela kuwalipa hao madaktari wa hapa
 
:welcome:na kama watawatimua basi watakuwa wanaharakisha muda wao wa kuwepo madarakani:llama:
 
Kwa mujibu wa chanzo muhimu katika wizara ya afya, Serikali imejiandaa kuchukua hatu kali kwa madaktari wote waliogoma ifikapo kesho Ikiwa ''Ni pamoja kuwafukuza kazi na utumishi'' baada ya juhudi za Serikali na za Kimahakama ''KUTOHESHIMIWA''.

Pamoja na hatua hizo pia taratibu za kuandaa madktari mbadala toka taasisi nyingine za Serikali ikiwa ni pamoja na uwezekano wakupata msaada wa dharura wa Madaktari toka mojawapo ya Nchi za Afrika Mashariki, zinaendelea vizuri. Aidha ulinzi nao unaendelea na utaendelea kuimarishwa katika sehemu na maeneo mbalimbali.

Kauli hii bila shaka ina underline tamko la Serikali leo Bungeni kuwa '' LIWALO NA LIWE''

suala la kuwafukuza ni la utumishi kimkataba wa kazi,hilo liko kwenye uwezo wao.wanapowafukuza, matatizo ya sekta ya afya na madaktari ,ndo inakuwa imeimarishwa na kutatuliwa?Tujiulize, je gharama ya kufukuza na kupata wengine kwa msaada zinamasilahi kwa umma?pia walimu watawafukuza?na tujiulize, hawa tutakaopata kama msaada wakaa tanzania milele?serikali iache blabla na mikakati ya kuchezea pesa ya watanzania , hoja si kufukuza, jambo la msingi ni kuboresha na kuondoa matatizo ya kisekta.Nchi yetu ina matatizo mengi kiuchumi, kijamii, kifedha.wenye dhamana wajali matatizo ya wananchi , na si kukurupka kutatua matatizo.tuache siasa inabidi wapinzani watoe hatma kwa kulipeleka kwa wananchi.
 
Wacha kuota ndoto za jioni wewe! Suluhu nini kila Dr mmoja serikali imlipe milioni 13 kwa mwezi?

Ritz pamoja na jitihada za kupotosha ukweli bado, huwezi kutuaminisha kuwa Serikali ya CCM inamkakati mbadala na endelevu wa kusaidia watanzania katika sekta yoyote. Si afya, elimu wala kilimo! Endeleeni kuchumia matumbo yenu, lakini dhihaka na dhuluma mnayowafanyia wanachi hakika haiwezi kuvumiliwa miaka yote. Nanyi mjiandae kulipa maumivu haya!
 
Watendaji wakuu wa serikalini wasivyotumia akili wanawezakuwafukuza kweli lakini itakula kwaosababu mambo yataharibika zaidi wakishafanya hivyo!!
 
Wacha kuota ndoto za jioni wewe! Suluhu nini kila Dr mmoja serikali imlipe milioni 13 kwa mwezi?

ritz upo sahihi lets say kila dr anapata milioni 13 likimalizika hilo litachochewa la walimu kila mmoja kulipwa milioni saba baada ya hapo polisi ni suala lililopo wazi kuna mkakati wa makusudi kabisa wa kisiasa lakini kwa mtaji wa vifo vya watanzania
 
Dr.Chichi kumbe bado hujaona tofauti ya mgomo uliopita na huu wa sasa! Ule wa mwanzo hakukua na amri ya serikali, hivyo serikali ingewafukuza kazi ingebidi iwalipe, which is another burden to the gvt. Safari hii imecheza tricky ambayo wengi wenu hamjaijua, ukifukuzwa hupati chochote maana umedharau amri halali ya mahakama, chezeya dola weye!

Halafu mkuu mjifunze kusoma alama za nyakati. Safari hii hamna back-up ya wananchi, watu wengi hawako upande wenu kwa sababu mmekuwa too demanding and not considerate!

mkuu nakusihi usome thread moja inasema UKWELI KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI TANZANIA.... tafadhali.
 
Kwa mujibu wa chanzo muhimu katika wizara ya afya, Serikali imejiandaa kuchukua hatu kali kwa madaktari wote waliogoma ifikapo kesho Ikiwa ''Ni pamoja kuwafukuza kazi na utumishi'' baada ya juhudi za Serikali na za Kimahakama ''KUTOHESHIMIWA''. Pamoja na hatua hizo pia taratibu za kuandaa madktari mbadala toka taasisi nyingine za Serikali ikiwa ni pamoja na uwezekano wakupata msaada wa dharura wa Madaktari toka mojawapo ya Nchi za Afrika Mashariki, zinaendelea vizuri. Aidha ulinzi nao unaendelea na utaendelea kuimarishwa katika sehemu na maeneo mbalimbali. Kauli hii bila shaka ina underline tamko la Serikali leo Bungeni kuwa '' LIWALO NA LIWE''
Kwa hiyo, hao wa dharura ndio watakaokubali kufanya kazi kwenye mazingira duni (hakuna vitendea kazi, mishahara duni nk) au wataajiriwa madaktari duni pia, ambao wamekosa pa kwenda na hivyo kuiweka sekta ya afya rehani?
 
Kumbuka kuwa Tanzania ina maelfu ya Madaktari ambao bado wanategemea serikali kama ndiyo mwajiri wao. Kila daktari, wa kila ngazi, ana shida tofauti na mwengine. Wengine watastafu mwisho wa mwezi huu, wengine mwezi ujao, wengine mwaka ujao n.k. Wengine wana watoto wanaowasomesha, n.k. Kila daktari atafanya maamuzi yake yeye mwenyewe. Ninachoweza kusema ni kuwa serikali ikikaza uzi madaktari wote watarudi kazini.

jipe moyo mkuu.. idadi ya madaktari wote TZ ni chini ya 2500...hawa ndio MD, and specialist, of which for them it requires them to spend atleast 6yrs(intern inclusive)...na hawa ndio wanahitajika huko nje, unaosema wewe ni
A.M.O, C.O.. ba kunatofauti kubwa kati yao.
 
Kumbuka kuwa Tanzania ina maelfu ya Madaktari ambao bado wanategemea serikali kama ndiyo mwajiri wao. Kila daktari, wa kila ngazi, ana shida tofauti na mwengine. Wengine watastafu mwisho wa mwezi huu, wengine mwezi ujao, wengine mwaka ujao n.k. Wengine wana watoto wanaowasomesha, n.k. Kila daktari atafanya maamuzi yake yeye mwenyewe. Ninachoweza kusema ni kuwa serikali ikikaza uzi madaktari wote watarudi kazini.

mkuu kama unaweza soma thread moja inaitwa UKWELI KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI....TAFADHALI, kuna mengi pale
 
ritz upo sahihi lets say kila dr anapata milioni 13 likimalizika hilo litachochewa la walimu kila mmoja kulipwa milioni saba baada ya hapo polisi ni suala lililopo wazi kuna mkakati wa makusudi kabisa wa kisiasa lakini kwa mtaji wa vifo vya watanzania
This is erroneous reasoning/fallacy! Mtoto wako akikuomba umnunulie uniform huwezi kuanza kuorodhesha watoto wote wasio na uniform ndipo umnunulie. Kama ingekuwa hivi, hakuna tatizo ambalo lingepata ufumbuzi wowote mahali popote duniani. Hakuna mfanyakazi angepanda cheo au hata kuboreshewa maslahi yake. Ingekuwa pia kutaka kujenga hospitali moja Dar es Salaam mfano, mtu angesubiri kwanza mikoa mingine iwe na shida kama hiyo. Sasa si dunia ingekweisha kabla hata hatua moja ya maendeleo haijapatikana? Solution ni kila kitu kuangaliwa kulingana na umuhimu wake!
 
Wacha kuota ndoto za jioni wewe! Suluhu nini kila Dr mmoja serikali imlipe milioni 13 kwa mwezi?

Ritz
Hizi propaganda umezitoa wapi? Hili suala linamgusa kil mtanzania bila kujali unazi wa kichama; hao unaowatetea wana uwezo wa kwenda India; kumbuka si kila mtanzania analimudu hilo; hilo la mi. 13 umelitoa wapi? Ikiwa wanagombania kuboresha huduma za afya nalo hilo limekuwa kosa la jinai? Ritz funguka kichwa; sasa utaelewa kwa nini tuliopo mtoni hatutaki kurudi bongo maisha ya kubahatisha tulishayasahau.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Back
Top Bottom